-
[Mchafuko wa Maelezo]
-
Mtandao unampa kila mtu katika jamii
sauti katika mazingira ya umma.
-
Lakini wakati yeyote anaweza kuchapisha
chochote mtandaoni, maelezo huwa mengi.
-
Baadhi ya maelezo haya yanaaminika,
lakini mengi hayaaminiki.
-
Kwenye mtandao jamii na mifumo ya
kutafuta, maelezo yote hufanywa kuwa sawa.
-
Inaweza kuwa vigumu kubaini
kinachotoka kwa chanzo kinachoaminika,
-
kama vile shirika la kitaalamu la habari,
-
na kisichoaminika.
-
Mitandao ya jamii hufanya iwe rahisi
maelezo mabaya kuenea,
-
inayomaanisha tunasikia zaidi
kuhusu tatizo hili za habari bandia.
-
Lakini, habari bandia ni nini, haswa?
-
Kauli hiyo hutumiwa kufafanua
aina zote za maelezo yasiyo sahihi,
-
kuanzia kwa makala yanayonuiwa
kuwahadaa watu,
-
hadi meme zinazopotosha
na mada za chambo cha kubofya,
-
hadi nadharia za uongo.
-
Baadhi ya watu huita ripoti za habari
wasizopenda kuwa "habari bandia",
-
kama njia ya kufedhehesha vyanzo
vinavyoaminika,
-
hali inayozidisha tu kuchanganyikiwa.
-
Ili kufahamu tatizo la
maelezo yasiyo sahihi mtandaoni,
-
ni muhimu kuyabainisha na kuyapambanua.
-
Maelezo yasiyo ya kweli yanaweza
kubainishwa kwa aina mbili:
-
maelezo ya kupotosha na maelezo ya uongo.
-
Maelezo ya kupotosha si ya kweli,
-
lakini mtu anayeyashiriki
anayaamini kuwa ya kweli.
-
Ingawa maelezo ya kupotosha yanaweza
kudhuru,
-
lengo lake si kusababisha madhara.
-
Mifano inaweza kujumuisha hitilafu ya
ukweli
-
inayosababishwa na kutoelewa,
-
picha iliyobadilishwa,
-
au picha halisi inayoonekana
na hadithi iliyotungwa.
-
Maelezo ya uongo, upande mwingine,
-
ni maelezo ya kimakusudi yasiyo ya kweli
-
yanayobuniwa na kushirikiwa ili
kusababisha madhara.
-
Yana lengo la kuwachanganya
watu kuhusu kilicho kweli,
-
na kuathiri jinsi wanavyofikiri
na kutenda.
-
Kwa mfano, uvumi usio wa kweli
uliosambaa kuhusu mgombeaji wa kisiasa
-
ambao unawafanya wengine
kushuku uaminifu wake.
-
Kwa pamoja, maelezo yote haya ya
kupotosha na uongo
-
yanaweza kufikiriwa
kama mchafuko wa maelezo.
-
Hadithi au machapisho yasiyoaminika
yanaweza kuvutia au kufana,
-
au kuchochea hisia inayotufanya tutake
kuamini na kuyashiriki kwa marafiki.
-
Watu huchangia mchafuko wa maelezo kwa
kushiriki maelezo ya uongo na kupotosha.
-
Kabla ya kuamini au kushiriki
kitu, subiri na ujiulize,
-
"Nani alibuni hili, na kwa nini?"
-
Hii ni hatua ya kwanza katika
kukabili mchafuko wa maelezo
-
ili kuwa raia anayefahamu zaidi.
-
[Imeletwa kwako na CIVIX]
-
[Kwa usaidizi wa Kanada]