President Obama Speaks on the Death of Nelson Mandela - captioned
-
0:02 - 0:09Akishtakiwa mahakamani mnamo mwaka wa1964, Nelson Mandela alifunga kauli yake akisema
-
0:10 - 0:17"Nimepigana dhidi ya utawala usio na haki wa watu weupi pia dhidi ya utawala usio na haki ya watu weusi."
-
0:18 - 0:23Nimetunza maadili ya jamii huria na ya kidemokrasia
-
0:23 - 0:29ambapo watu wote wanaishi pamoja wakisikilizana katika amani wakiwa na fursa iliyo na haki kujiendeleza.
-
0:29 - 0:36Ni maadili yenye matumaini ya kuendesha maisha yangu ili yatekelezwe. Lakini vinginevyo ni maadili ambayo
-
0:36 - 0:40mimi niko tayari kufa kwa ajili yake.
-
0:40 - 0:47Naye Marehemu Mheshimiwa Nelson Mandela akaishi katika harakati zenye kutekeleza maadili hayo akayafanya kuwa wa ukweli.
-
0:47 - 0:51Alitimiza zaidi ya yanayo tarajiwa na mtu yeyote yule.
-
0:51 - 0:53Leo ameenda nyumbani kwa Mola Wetu.
-
0:53 - 0:58Mtu mheshimiwa shujaa, mashuhuri, ametuacha
-
0:58 - 1:00naye mtu mzuri kwa dhati mfano kwa watu wote
-
1:00 - 1:04ambaye tutapaswa kushirikiana naye duniani humu.
-
1:04 - 1:10ametuacha si mmojawetu tena yupo na wahenga.
-
1:10 - 1:12Kwa heshima zake za kishujaa ikiwa na nia yake imara
-
1:12 - 1:17kujitolea mhanga kwa ajili ya uhuru wa wengine pasi na uhuru wake mwenyewe,
-
1:17 - 1:22Madiba alibadilisha Afrika Kusini akitusukuma sisi sote tuendelee kutafuta haki.
-
1:22 - 1:27Safari yake ya kwenda katika uraisi ilipoanza akiwa mfungwa ilijumuisha ahadi ya kuwa
-
1:27 - 1:33binadamu wote pamoja na nchi zote zinaweza kubadilika ziwe bora zaidi.
-
1:33 - 1:36Ahadi yake kuhamisha utawala kutoka kwa wabeberu kwa watu wote wa Afrika Kusini
-
1:36 - 1:37akipatana na wale walimofunga jela
-
1:37 - 1:43ikawa mfano kwa watu wote kuutamani
-
1:43 - 1:46ama ukiwa katika maisha ya mataifa au maisha kibinafsi.
-
1:46 - 1:51Tusisahu hulka zake za adabu, uungwana na uchangamfu
-
1:51 - 1:54akijikosoa
-
1:54 - 1:58ndio awe mtu wa kusifika.
-
1:58 - 1:58Kama alivyosema mara,
-
1:58 - 2:05"Mimi si mtakatifu isipokuwa umembunia mtakatifu kama mwenye dhambi ambaye daima anajaribu awe mtii.
-
2:08 - 2:09Mimi ni mmojawapo wa wale wasiohesabika
-
2:09 - 2:13aliyetiliwa moyo na maisha ya Marehemu Nelson Mandela.
-
2:13 - 2:16Kitendo changu cha kwanza cha kisiasa
-
2:16 - 2:23cha kwanza kilichohusika na masuala ya sera ama siasa
-
2:24 - 2:26kilikuwa kupinga sera za kugawanya watu kutokana na rangi ya ngozi inayoitwa apartheid.
-
2:26 - 2:32Nilisoma kwa makini maneno na maandishi yake.
-
2:32 - 2:35Siku alipoachiliwa huru
-
2:35 - 2:37ilinipa mimi uelewano wa uwezo wa binadamu
-
2:37 - 2:41wanapoongozwa na matumaini yao si uwoga wao.
-
2:41 - 2:44Na kama wengine wengi duniani kote, siwezi kujifikiria katika maisha yangu
-
2:44 - 2:49pasi na mfano uliowekwa na Marehemu Mheshimiwa Nelson Mandela.
-
2:49 - 2:55Katika maisha yangu yote nitafanya kadiri niwezavyo kujifunza kutoka kwake.
-
2:55 - 2:59Kwa Graca Machel na jamaa zake
-
2:59 - 3:04mimi pamoja na mke wangu Michelle tunatoa pole pole sana ikiwa na shukrani mno
-
3:04 - 3:08kwa kumshirikisha mtu asiye na kifani na sisi.
-
3:08 - 3:13Kazi yake ya maisha ilimtenga siku nyingi ndefu na wapendwa wake wa moyo.
-
3:13 - 3:16Tumaini la pekee langu ni muda huu mfupi mliokuwa naye
-
3:16 - 3:20ulileta amani na utulivu kwa jamaa zake wote.
-
3:20 - 3:22Kwa raia wa Afrika Kusini,
-
3:22 - 3:28sisi tunanufaika kutoka kwa mfano wa ufanyaji upya ukiwa na usuluhisho na unyumbukaji
-
3:28 - 3:30mliofanya kuwa ukweli.
-
3:30 - 3:37Afrika Kusini huria ikiwa na usalama wa wenyewe kwa wenyewe ndiyo mfano kwa dunia nzima.
-
3:37 - 3:44Ndio urithi wa Madiba kwa talifa alilolipenda.
-
3:44 - 3:49Huenda hatutawahi kumpata mfano wake Marehemu Mheshimiwa Nelson Mandela kwa mara nyingine.
-
3:49 - 3:56Ndio sisi tuliovalishwa njuga kadiri tuwezavyo kusogeza mbele mfano uliowekwa naye:
-
3:56 - 3:59Kukata shauri zikiongozwa na upendo si chuki;
-
3:59 - 4:03kutompunguzia umuhimu wa mchango wa mtu mmoja;
-
4:03 - 4:09kujitashidi kutengeneza mambo ya usoni yanayostahiki kujitolea mhanga kwake.
-
4:09 - 4:16Sasa hivi, tusite tukishukuru ukweli wa maisha yake Mheshimiwa Marehemu Nelson Mandela
-
4:16 - 4:23mtu ambaye alishika mambo ya kale mikononi mwake akipinda tao la ulimwengu wa maadili iielekee kwa haki ya binadamu
-
4:24 - 4:27Mungu ibariki kumbukumbu yake Amwekee mahali pema upeponi.
- Title:
- President Obama Speaks on the Death of Nelson Mandela - captioned
- Description:
-
Original video: http://youtu.be/eIbwXCbiklY
Transcript: http://www.whitehouse.gov/the-press-office/2013/12/05/statement-president-death-nelson-mandela - Video Language:
- English
- Team:
- Captions Requested
- Duration:
- 04:38
PETE MHUNZI edited Swahili subtitles for President Obama Speaks on the Death of Nelson Mandela - captioned |