-
Sasa tumechanganya vitu kidogo:
-
upande wa kushoto wa mizani, sio tu tuna
-
hivi vitu vitatu vya bluu vinavyofanana vyenye uzito usiofamika kila kimoja kikiwa na uzito x,
-
pia tuna vitu vya uzito wa kg 1 hapa,
-
tunavyo viwili.
-
Sasa, tunaenda kutafuta X ni ngapi.
-
Lakini kabla hata hatujafanya hivyo, nataka ufikirie mlinganyo wa kihesabu
-
utakaowakilisha kinachoendelea, tulichonacho upande wa kushoto kikilinganishwa na
-
tulichonacho upande wa kulia katika mizani.
-
Nitakupa sekunde chache ufukirie...
-
Hebu tufikirie tulichonacho upande wa kushoto:
-
tuna vitu vitatu vyenye uzito X, kwa hiyo unaweza sema tuna 3x
-
na halafu tuna vitu viwili vya uzito wa kilogramu 1, kwa ujumla tuna kg 2. Kwa hiyo + 2.
-
Kwa hiyo njia moja ya kufikiria kuhusu uzito wa upande wa kushoto ni 3x + 2.
-
Vitu vitatu vyenye uzito X jumlisha kilogram mbili.
-
Hicho ndicho tulichonacho upande wa kushoto.
-
Sasa, hebu tufukirie kuhusu tulichonacho upande wa kulia.
-
Tunaweza kuvihesabu.
-
Viko 14.
-
Vipande 14, kila kimoja kina uziti wa kg 1, kwa hiyo jumla ya uzito ni kg 14.
-
Na tunaona kwamba mizani iko sawa, haijapinda chini au juu.
-
Kwa huu uzito wa hapa lazima uwe sawa na huu uzito wa jumla.
-
Mizani iko sawa, kwa hiyo tunaweza kuandika alama ya sawa sawa.
-
ngoja niandike kwa rangi ya kijivu.
-
Sasa, ninachotaka ufikiri,
-
na unaweza kufikiria ama kwa kutumia alama au mizani, ni:
-
utafanyaje -- hebu tufikirie vitu vichache:
-
utafanyaje kwanza ili uondoe hivi vipande vidogo vya kg 1?
-
Nakupa muda ufilirie kuhusu hilo..
-
Kitu kirahisi ni:
-
unaweza kuondoa hivi vipande vya kg 1 upande wa kushoto,
-
lakini kumbuka, ukiviondoa hivi vipande upande wa kushoto,
-
na mizani ilikuwa sawa, sasa upande wa kushoto utakuwa mwepesi
-
na utapanda juu. Lakini tunataka kuuweka sawa ili tuendelee kusema
-
Uzito huu ni sawa na uzito huo.
-
Kwa hiyo tukiondoa vipande viwili upande wa kushoto, tunatakiwa pia tuondoe vipande viwili upande wa kulia.
-
Kwa hiyo, tutaondoa viwili pale, na halafu tutaondoa viwili pale.
-
Kihesabu, tunachokifanya, tunatoa kilogramu 2 kila upande.
-
Tunatoa 2 upande huu,
-
Kwa hiyo upande wa kushoto sasa tuna 3x + 2, kutoa 2
-
tunatakiwa na 3x,
-
na upande wa kulia tuna 14 na tumetoa 2
-
kwa hiyo tutaenda kubakiwa na vipande 12.
-
Na unaweza kuona nilizozikata, nimebakiwa na 12,
-
na hapa bloku 3 za X.
-
Kwa vile tumeondoa kiwango kile kile pande zote,
-
mizani yetu bado iko sawa. Na mlinganyo wetu: 3x ni sawa na 12.
-
Sasa , hii imekuwa sawa na hesabu tulioiona katika video ya mwisho.
-
sasa ninakuukiza: tufanye nini tuitenge x moja,
-
kuwa na X moja tu upande wa kushoto wa mizani,
-
wakati tunaendelea kuifanya mizani sawa?
-
Njia rahisi ya kufikiria hii ni:
-
Kama nikitaka X moja upande wa kushoto, hiyo ni theluthi ya jumla ya X hapa.
-
Kwa hiyo vipi kama nikizidisha upande wa kushoto na theluthi --
-
-- lakini kama nataka kuufanya mzani sawa, natakiwa kuzidisha upande wa kulia na theluthi.
-
Kama tunaweza kufanya hilo kihesabu,
-
Hapa naweza kuzidisha upande wa kushoto kwa 1/3,
-
na kama nikitaka mzani wangu kuwa sawa pia natakiwa kuzidisha upande wa kulia kwa 1/3.
-
Kuzidisha kwa uhalisia inamaanisha; baki na 1/3 ya kiasi ulichokuwa nacho mwanzo
-
Tutaondoa hizi mbili.
-
Kama tukitaka kunakuwa na theluthi ya kiasi tulichokuwa nacho mwanzo,
-
-- kuna vipande 12 vimebaki baada ya kuondoa viwili vya mwanzo --
-
kwa hiyo, 1/3 ya 12: tutaenda kubakiwa na vipande vinne vya kg 1.
-
Hebu niondoe vyote nibakishe vinne
-
Na nimebakiwa na 4 hapa.
-
Na kwa hiyo ukichobakiwa nacho,
-
ni hii 'X'. - Nitaiwekea kivuli kuonyesha hii moja ndiyo tuliyobakiwa nayo -
-
na halafu tuna hivi vipande vya kg 1.
-
Unaweza kuona kihesabu hapa: 1/3 * 3x
-
-- au unaweza kusema 3x gawanya kwa 3 -- kwa njia yoyote hii inatupa
-
-- hizi tatu zinakwisha, kwa hiyo hiyo inakupa X
-
na upande wa kulia 12 * 1/3 - ambayo ni sawa na 12/3, ni sawa na 4.
-
Na kwa vile tumefanya kitu kile kile kwa pande zote, mizani yetu bado iko sawa.
-
Kwa hiyo unaona uzito wa kitu hiki unatakiwa uwe sawa na uzito wa vioande hivi 4.
-
x ni sawa na kilogramu 4.