-
Hapa tuna mchoro unaovutia sana.
-
Hebu tuangalie vitu kadhaa kuhusu huu mchoro.
-
Tunajua mstari MK
-
ni msambamba na mstari NJ.
-
Kwa hiyo mstari huu ni msambamba na mstari huu.
-
Huu ni mstari MK, na huu ni mstari NJ.
-
Sasa, kwa taarifa hizo
-
katika huu mchoro,
-
nategemea kuthibitisha kuwa kipimo cha pembe LMK
-
ni sawa na kipimo cha hii pembe hapa
-
na hii pembe ni LNJ.
-
Njia nyingine ya kuandika hii ni;
-
kipimo cha LMK ni b na kipimo cha LNK ni a.
-
Kwa hiyo tunataka kuthibitisha kuwa b ni sawa na a
-
kwa kutumia hizi taarifa zote tunazozijua.
-
Nakushauri ufanye mwenyewe
-
kabla sijaanza kufanya.
-
Vizuri, sasa hebu tufanye.
-
Kitu cha kwanza unachoweza kuona ni nina pembetatu hapa,
-
pembetatu MLK.
-
Tunafahamu nini kuhusu kipimo cha pembe za ndani za pembetatu?
-
Kipimo cha pembe za ndani za pembetatu
-
ni nyuzi 180.
-
Tunafahamu kuwa b, ambayo ni kipimo cha pembe
-
jumlisha pembe hii, c
-
jumlisha pembe hii, ambayo ni nyuzi 90
-
itakuwa sawa na nyuzi 180.
-
Na kama tukitoa nyuzi 90 kutoka pande zote
-
tutapata b jumlisha c ni sawa na nyuzi 180 toa nyuzi 90.
-
Itakuwa nyuzi 90.
-
Au kama tukitaka kutafuta thamani ya b kwa wazi
-
tunaweza kutoa c pande zote,
-
na tunaweza kuandika b ni sawa na nyuzi 90 toa c.
-
Hivyo, hiyo ni njia mojawapo ya kuifafanua b.
-
Je tunaweza kuifafanua kwa njia hiyo hiyo?
-
Kwa mara nyingine, kama unatamani kufanya mwenyewe
-
nakushauri ufanye hivyo.
-
Kama tukiangalia kwa makini tutaona tuna pembetatu NLJ,
-
hii ni pembetatu kubwa, takribani ni kama mchoro wote.
-
Kinachovutia zaidi kuhusu NLJ ni kuwa J ni pembe mraba nyingine,
-
c ni moja ya pembe za ndani,
-
na a ni pembe nyingine ya ndani.
-
Tunaweza kuandika kitu ambacho kinafanana,
-
tunaweza kuandika a jumlisha c jumlisha nyuzi 90
-
ni sawa na nyuzi 180.
-
Kwa hiyo tutafanya nini hapa?
-
Tuafanya hatua ile ile kutafuta a.
-
Kama tukitoa 90 pande zote na tukitoa c pende zote
-
tutapata nini?
-
Tutapata a ni sawa na nyuzi 90 na kama tukitoa c kutoka pande zote
-
tutapata nyuzi 90 toa c.
-
Hii inavutia,
-
b ni sawa na nyuzi 90 toa c na a ni sawa na nyuzi 90 toa c.
-
Kwa hiyo nyuzi 90 toa c ni sawa na a, na pia ni sawa na b.
-
Au, sasa tunaweza kusema kuwa a ni sawa na b,
-
kwamba kipimo cha pembe LMK ambacho ni b
-
ni sawa na kipimo cha pembe LNJ ambacho ni a.