MAFANIKIO YA KAZI MARA DUFU!
-
0:00 - 0:06Nitakuambia kwamba ikiwa Mungu angejibu maombi yangu ya kupandishwa cheo
-
0:06 - 0:09miaka michache iliyopita,
nisingekuwa nimedhatitiwa -
0:09 - 0:14kushughulikia changamoto
zinazokuja na baraka hii. -
0:14 - 0:18Kwa sababu tunapopokea baraka,
wao pia huja na changamoto. -
0:26 - 0:32Ikiwa hufanyi kazi
kulingana na wito wako, -
0:32 - 0:43kulingana na hatima yako, omba kwamba 2025
uwe mwaka wa kuhama. -
0:43 - 0:47Hata kama unapaswa kupitia
usumbufu kidogo -
0:47 - 0:52ili kufikia kazi uliyokusudiwa,
uwe tayari kwa hilo. -
0:52 - 1:00Hatuwezi kuendelea kufanya kazi tu kwa
ajili ya rasilimali za kimwili tu. -
1:00 - 1:08Hapana, lazima tufanye kazi kulingana na wito wetu.
Ni lazima tufanye kazi kulingana na hatima zetu. -
1:08 - 1:14Ni lazima tufanye kazi kulingana na yale ambayo Mungu
ameahidi na kukusudia kwa ajili yetu. -
1:14 - 1:20Ikihitajika, acha 2025 uwe
mwaka wa kuhama -
1:20 - 1:23kutoka hapo ulipo hadi pale
Anapotaka uwe. -
1:23 - 1:24Hebu tutoe maombi hayo.
-
1:27 - 1:32Jina langu ni Ian na huyu
ni mke wangu mzuri, Ashley. -
1:32 - 1:36Karibu miaka saba iliyopita, niliajiriwa
katika wilaya ya umwagiliaji -
1:36 - 1:44na cheo changu cha kazi kilikuwa Meneja wa Maji
maana yake niliwajibika -
1:44 - 1:49wakati wa kiangazi kwa ajili ya kuhakikisha
kuwa maji yanapita kwa wakulima -
1:49 - 1:54ili waweze kumwagilia mazao yao na
kuzungumza na wakulima -
1:54 - 1:59kuhakikisha kwamba wanapata wanachohitaji
na kwamba maji yapo katika kiwango kinachofaa. -
1:59 - 2:04Lakini wakati wa msimu wa baridi, wakati maji
hupungua kwa msimu, -
2:04 - 2:09asili ya kazi ingebadilika
kuwa matengenezo kwenye mfereji. -
2:09 - 2:11Wakati huo, nilihisi kama mwajiri wangu
-
2:11 - 2:15hakujua anifanye nini
kwa sababu hakukuwa na maji. -
2:15 - 2:22Nilipoanza miaka saba iliyopita, kama
mfanyakazi mwenye uzoefu mdogo wa ujenzi -
2:22 - 2:26wakati huo, kwa kawaida ningewekwa
kwenye wafanyakazi ambapo ningekuwa -
2:26 - 2:31nachimba matope kwa saa kumi kwa siku
au kukata miti siku nzima. -
2:31 - 2:37Kulikuwa na kazi nyingi sana
ngumu ambazo ningefanya. -
2:37 - 2:44Na wakati huo, sikuthamini
asili ya kazi niliyokuwa nikifanya. -
2:44 - 2:53Nilifikiri ilikuwa chini ya kile nilichopaswa kufanya
kwa sababu nilihisi kama nilikuwa na vitu vizuri zaidi vya kufanya. -
2:53 - 2:59Moyo wangu ungekuwa na kinyongo kidogo
kwa mwajiri wangu -
2:59 - 3:04na nilianza kuhisi uchungu kidogo kuhusu
kazi yangu - ambapo sikutaka kwenda. -
3:04 - 3:09Nilitambulishwa kwenye TV ya Moyo wa Mungu takriban
mwaka mmoja na nusu uliopita na mke wangu. -
3:09 - 3:15Kama vile nilivyokuwa nikihudhuria
Ibada ya Kuingiliana ya Maombi kila mwezi, -
3:15 - 3:17kitu kilibadilika moyoni mwangu.
-
3:17 - 3:22Kwa sababu nilikuwa nikimtafuta Mungu na
uhusiano wangu naye, -
3:22 - 3:28Nilikuwa nikijifunza kwenda kazini na
kuridhika katika hali yangu. -
3:28 - 3:35Na badala ya kuwafanyia wanadamu kazi, nilikuwa
naenda kufanya kazi na kumfanyia Bwana kazi. -
3:35 - 3:39Hili lilifanya kazi yangu iwe
ya kupendeza na ya kufurahisha zaidi. -
3:39 - 3:48Ilifanya maoni yangu juu ya bosi wangu na
watu walio karibu nami kubadilika. -
3:48 - 3:53Badala ya kuwaona kama watu
wabaya au wasionipenda, -
3:53 - 4:01Ningewaangalia kama watu waliohitaji
maombi na walimhitaji Bwana maishani mwao. -
4:01 - 4:06Ingawa uzoefu wangu katika
kazi yangu ulikuwa ukiboreka, -
4:06 - 4:12Bado nilihisi kama Bwana alikuwa na
wito mkuu kwa maisha yangu na kazi yangu. -
4:12 - 4:20Tulijiunga na Huduma ya Maombi ya Pamoja
karibu mwaka mpya wa 2025. -
4:20 - 4:24Tulikuwa tumekaa hapa kwenye kochi na kuomba.
-
4:24 - 4:31Mada ilipokuja ya kuombea
nafasi katika kazi zetu, -
4:31 - 4:38Nilikuwa nikimwomba Bwana kwa bidii na
moyoni mwangu nikimwambia Mungu, -
4:38 - 4:45'Niko tayari. Mwaka huu, najua kuwa Una
mpango kwa ajili yangu na ni mzuri - -
4:45 - 4:51iwe ni kazi nyingine au kama inanifanya
niwe na maudhui zaidi katika nafasi hii. -
4:51 - 4:58Ninaamini, Bwana, ya kwamba utanifanyia
njia na kunifungulia milango.' -
4:58 - 5:03Mwezi mmoja kabla ya ibada hiyo,
nilipigiwa simu. -
5:03 - 5:09Nilikuwa nikiomba kazini, na mmoja wa wateja wangu kutoka kazi yangu nyingine akanipigia simu.
-
5:09 - 5:15Yeye ni mkulima, na akasema, '
Unafanya nini sasa hivi, Ian?' -
5:15 - 5:22Nikasema, 'Vema, bado ninafanya kazi katika
kampuni niliyokuwa nayo hapo awali.' -
5:22 - 5:27Naye akasema, 'Ningependa utume ombi
la kazi hii hapa.' -
5:27 - 5:32Alisema, 'Sioni waombaji wowote
ambao ninafurahishwa sana nao.' -
5:32 - 5:36Hiyo ilikuwa karibu Novemba 2024.
-
5:36 - 5:41Lakini basi sikusikia ufuatiliaji wowote
baada ya kuwasilisha ombi langu. -
5:41 - 5:46Kadiri muda ulivyosonga, nilianza kukata
tamaa kidogo -
5:46 - 5:50na nilifikiri kwamba labda hii
haitatokea. -
5:50 - 5:58Kweli, mnamo Februari, nilipokea simu
kutoka kwa kampuni niliyotuma maombi, -
5:58 - 6:01na walitaka kunifanyia
mahojiano ya kazi hiyo. -
6:01 - 6:06Nilikwenda kwenye mahojiano na mimi ni
mtu ambaye anapata woga sana -
6:06 - 6:10kuhusu kuzungumza mbele ya umma au
katika mahojiano ya kazi. -
6:10 - 6:15Ukinipa gitaa na kuniuliza
niimbe wimbo wa kuabudu, hakuna shida. -
6:15 - 6:19Lakini kuzungumza mbele ya watu
sio utaalamu wangu. -
6:19 - 6:23Katika mahojiano, Bwana alinipa
maneno yote ya kusema. -
6:23 - 6:27Kazi niliyoomba ilikuwa katika
wilaya nyingine ya umwagiliaji, -
6:27 - 6:37lakini badala ya kuwa Meneja wa Maji, safari hii
mimi ni Meneja wa wilaya nzima ya umwagiliaji. -
6:37 - 6:39Niliajiriwa kuendesha kampuni.
-
6:39 - 6:43Jina langu ni Ashley na huyu ni
mume wangu mzuri, Ian. -
6:43 - 6:47Tunatoka Marekani.
-
6:47 - 6:54Niliigundua TV ya Moyo wa Mungu kwa mara ya kwanza
zaidi ya mwaka mmoja na nusu uliopita. -
6:54 - 7:00Wakati huo, nilikuwa na vilio katika maisha yangu.
sikuwa nikifanya kazi hata kidogo; Sikuwa na kazi. -
7:00 - 7:03Hapo awali niliishi maisha ya dhambi sana
-
7:03 - 7:10lakini Bwana alikuwa amenikomboa kutoka kwenye
shughuli za uhalifu na uraibu wa dawa za kulevya. -
7:10 - 7:16Ilikuwa vigumu kwangu kupata kazi
kwa sababu ya rekodi yangu ya uhalifu. -
7:16 - 7:23Kulikuwa na nyakati chache ambapo nilikuwa
nimeajiriwa na kisha baadaye pale -
7:23 - 7:28walipochunguza historia yangu, na
kuona mashtaka ambayo yalikuwa kwenye rekodi yangu, -
7:28 - 7:33hawakutaka niwe sehemu ya
kampuni, jambo ambalo linaeleweka. -
7:33 - 7:40Na kwa hivyo Bwana alinipa mstari wa
'kutotegemea akili yangu mwenyewe -
7:40 - 7:44bali kumkiri yeye katika
njia zangu zote, naye atayanyosha mapito yangu. -
7:44 - 7:50Na kwa hivyo ningeendelea kuhudhuria
Huduma za Maombi za TV ya Moyo wa Mungu, -
7:50 - 7:53na nilianza kuona mafanikio
katika maisha yangu. -
7:53 - 8:01Nilikuwa nikiomba na kumwomba Bwana
anifungulie fursa ya kazi -
8:01 - 8:05ambapo naweza kushiriki jinsi Mungu
amebadilisha maisha yangu. -
8:05 - 8:09Na nilipokuwa nikitafuta mtandaoni,
nilipata jina la kazi. -
8:09 - 8:14Inaitwa Mtaalamu wa Usaidizi wa Rika
na hii ni nzuri sana. -
8:14 - 8:21Ilisema kwamba tunataka kuajiri mtu
ambaye anauzoefu wa kimaisha juu ya -
8:21 - 8:26maatizo ya matumizi ya dawa za kulevya au ambaye amepitia
changamoto za afya ya akili -
8:26 - 8:32na tunataka watumie simulizi lao kama
motisha ya matumaini ya kuwasaidia wengine -
8:32 - 8:36na kuwatia moyo na kuwafahamisha
kuwa haimanishi hakuna tumaini -
8:36 - 8:40na kwamba wanaweza kutoka
katika mitego ya uraibu. -
8:40 - 8:46Kwa hivyo niliishia kusali, na kuomba
kazi hii katika kampuni ya afya, -
8:46 - 8:49na niliishia kuajiriwa kwa ajili yake.
-
8:49 - 8:56Na kwa hivyo nilikuwa nikifanya kazi katika kazi yangu
kwa karibu mwaka na nusu na hivyo -
8:56 - 9:01ilikuwa muda mfupi baada ya kuanza kuhudhuria
Ibada ya Maombi ya Pamoja. -
9:01 - 9:05Nilikuwa nimeajiriwa kwa muda katika kazi yangu.
-
9:05 - 9:09Na jambo lingine, pia, ni kwamba sikuwa
na uwezo wa kudumisha kazi -
9:09 - 9:12kwa zaidi ya mwaka mmoja, na nimevuka
alama hiyo sasa. -
9:12 - 9:16Kuwa na uwezo wa kufanya vizuri katika eneo langu la kazi
imekuwa nzuri sana -
9:16 - 9:19na nisiwe na vizuizi hivi maishani mwangu.
-
9:19 - 9:26Katika Utumishi wa Mwaka Mpya, Desemba 28,
tulikuwa tukisali kwa bidii -
9:26 - 9:29kwa ajili ya kupandishwa vyeo na mafanikio
katika taaluma zetu. -
9:29 - 9:35Miezi michache baadaye, msimamizi wangu
aliniita ofisini kwake. -
9:35 - 9:41Kwanza, aliniteua kuwa mfanyakazi bora wa
mwezi kutoka kwa timu yangu na akasema, -
9:41 - 9:49'Tunaona jinsi wateja wetu wanavyokujibu vizuri
na unaendelea vizuri sana.' -
9:49 - 9:50Utukufu wote kwa Mungu!
-
9:50 - 9:54Na akasema, 'Tunataka kubadilisha
mkataba wako ufanye kazi muda wote.' -
9:54 - 10:00Na zaidi ya hayo, watu ambao tunafanya kazi
nao katika kampuni yangu ya afya, -
10:00 - 10:03ni mpango madhubuti wa
matibabu ya jamii y, -
10:03 - 10:09na hivyo watu tunaowasaidia ni watu
walio na uwezekano mkubwa wa kufungwa, -
10:09 - 10:12ambao wana changamoto za afya ya akili.
-
10:12 - 10:16Tuna takriban watu tisini katika mzigo wetu
na kila mmoja wao -
10:16 - 10:20amepata uzoefu akitoka katika
hospitali ya magonjwa ya akili. -
10:20 - 10:26Na kwa hivyo tunapata kuwajumuisha tena katika
jamii na kuwasaidia kwa zana za ustawi. -
10:26 - 10:32Na msimamizi wangu alisema kwamba alitaka
niongoze makundi mawili yanayosimamia ustawi -
10:32 - 10:37wa urejesho kwa sababu ya jinsi
wateja wanavyonijibu vizuri. -
10:37 - 10:42Nilijifunza kuwa shida yetu
ni ya kiroho katika maisha hivyo -
10:42 - 10:47Ninaingia kwenye mikutano hii
na kabla ya kukutana na wateja wangu, -
10:47 - 10:53Ninasali na kuwaombea ili
Mungu aende kwa nguvu katika maisha yao. -
10:53 - 10:58Na sehemu ya kundi,
ninao kama kumi na tano kati yao, -
10:58 - 11:03na karibu wote sasa
ama wanaenda kanisani -
11:03 - 11:06au kusoma Biblia au
kwenda kwenye mafunzo ya Biblia. -
11:06 - 11:11Na sehemu ya ajabu kuhusu
kazi yangu ni kuruhusiwa kushiriki -
11:11 - 11:14kwamba Yesu alibadilisha maisha yangu
kwa sababu ni ushuhuda wangu. -
11:14 - 11:19Aligeuza fujo yangu kuwa ujumbe na
akageuza vipimo hivyo kuwa ushuhuda! -
11:19 - 11:24Na wateja wangu, ingawa wana
changamoto hizo za afya ya akili, -
11:24 - 11:29na wanahangaika na mambo hayo,
wanaona kwamba kuna kitu -
11:29 - 11:34tofauti kuhusu mimi na kupata kuwatia moyo
na kuona maendeleo -
11:34 - 11:40ambayo Bwana amefanya katika
maisha yao ni yenye thawabu kubwa sana. -
11:40 - 11:46Sikuwahi kufikiria kuwa ingewezekana
kuwa na kazi kama hii -
11:46 - 11:51kwa sababu adui angeingia na kujaribu
kuleta hatia na aibu kutoka kwenye maisha yangu ya zamani -
11:51 - 11:58kwamba Bwana alikuwa amenisamehe tangu nilipotubu
na kuziacha kabisa njia zangu. -
11:58 - 12:05Hayo ni mafanikio ya ajabu ambayo Mungu
ameniletea mimi na mume wangu katika maisha -
12:05 - 12:08baada ya kujiunga na Maombi ya Pamoja
ya ukombozi. -
12:08 - 12:12Na pia kuwa na furaha tu ya Bwana.
-
12:12 - 12:16Sijawahi kuona maisha
kwa njia ya ajabu kama hii, -
12:16 - 12:23na ninashukuru sana kwa
huduma hii hai ya ajabu. -
12:23 - 12:27Ninashukuru na kuthamini sana!
-
12:27 - 12:31Ushauri wangu ni kwamba haijalishi
uko katika hali gani, -
12:31 - 12:38na haijalishi jinsi mwonekano wa kimwili
wa vitu vinavyokuzunguka unavyoweza kuonekana, -
12:38 - 12:45Mungu ni mkuu kuliko shida zetu zote
au hali zetu zote, -
12:45 - 12:55na ametuweka katika nafasi fulani ya
ukuaji ili aweze kukuza tabia zetu. -
12:55 - 13:03Ingawa huwezi kuona Mungu akifanya kazi katika
maisha yako na kusikiliza maombi yako, -
13:03 - 13:05ingawa huwezi
kumsikia kwa sasa, -
13:05 - 13:10Yeye anasikiliza kila wakati na anakutazama
na anajali, -
13:10 - 13:13na anataka kujibu maombi yako.
-
13:13 - 13:19Nitakuambia kwamba ikiwa Mungu angejibu
maombi yangu ya kupandishwa cheo -
13:19 - 13:22miaka michache iliyopita, nisingekuwa
nimezatitiwa -
13:22 - 13:27kushughulikia changamoto zinazokuja
na baraka hii. -
13:27 - 13:31Kwa sababu tunapopokea baraka,
wao pia huja na changamoto. -
13:31 - 13:36Utukufu wote kwa Yesu kwamba, kupitia njia ya
mapambano na majaribu -
13:36 - 13:41ambayo nilipaswa kupitia ili kufikia hatua hii
ya maisha yangu, sasa nimezatitiwa zaidi -
13:41 - 13:47na kujitayarisha kushughulikia hali
zinazotokea mbele yangu, na pia -
13:47 - 13:53kuwa baraka kwa wale wanaonizunguka
na kuwasaidia kuwaelekeza kwa Yesu. -
13:53 - 13:59Kwa ujumla, weka tu imani yako kwa Yesu na
usiwe na wasiwasi kuhusu jinsi mambo yanavyoonekana -
13:59 - 14:05na itachukua muda gani kwa sababu
wakati kamili wa Mungu utakuja -
14:05 - 14:09fanya kila kitu kiwe sawa kwako.
-
14:09 - 14:16Neno langu la ushauri lingekuwa, baada ya ukombozi
kufuatia Huduma za Maombi ya Pamoja, -
14:16 - 14:22ni muhimu kudumisha ukombozi wako
kwa kukaa katika Neno la Mungu -
14:22 - 14:25na kuyatafakari mchana na usiku.
-
14:25 - 14:30Moja ya mistari ninayoipenda zaidi ni pale
Mfalme Daudi katika kitabu cha Zaburi aliposema, -
14:30 - 14:35'Bwana, ufiche Neno lako moyoni mwangu,
nisije nikakutenda dhambi.' -
14:35 - 14:40Kwa hivyo hilo lingekuwa neno langu la ushauri
- kupata mkate wetu wa kila siku. -
14:40 - 14:43Unajua hatuwezi kuishi bila
Neno la Mungu. -
14:43 - 14:47Neno lake hutuhuisha.
Linatupa uzima. -
14:47 - 14:52Linatusaidia kufanya upya akili zetu.
Kwa hivyo hilo lingekuwa neno langu la ushauri.
- Title:
- MAFANIKIO YA KAZI MARA DUFU!
- Description:
-
Ian na Ashley kutoka Marekani wote walipata mafanikio ya ajabu ya kazi baada ya kujiunga na Mkesha wa Maombi ya Mwaka Mpya mtandaoni pamoja na Ndugu Chris. Ubarikiwe na kutiwa moyo unapotazama shuhuda zao, ukijifunza kwamba wakati wa Mungu ni mkamilifu na baraka Zake ni nyingi!
"Ikiwa hufanyi kazi inayoendana na wito wako, kulingana na hatima yako, omba kwamba 2025 uwe mwaka wa kuhama. Hata kama itabidi upitie usumbufu kidogo ili kufikia kazi unayokusudiwa, uwe tayari kwa hilo!"
Ili kupokea maombi bila malipo kutoka kwa Ndugu Chris kupitia Zoom, tuma ombi lako la maombi hapa - https://www.godsheart.tv/zoom - na Timu ya God's Heart TV itawasiliana nawe kupitia barua pepe kwa info@godsheart.tv
➡️ Pata Kutiwa Moyo Kila Siku kwenye WhatsApp - https://godsheart.tv/whatsapp/
➡️ Kuwa Mshirika wa TV wa Moyo wa Mungu - https://godsheart.tv/partnership
➡️ Habari kuhusu Maombi ya Pamoja - https://godsheart.tv/interactive-prayer/
➡️ Jitolee kama Mtafsiri wa TV ya Moyo wa Mungu - https://godsheart.tv/translate/
➡️ Shirikisha ushuhuda wako - https://godsheart.tv/testimony
➡️ Jiunge na Ibada yetu ya Maombi ya Moja kwa Moja Jumamosi ya kwanza ya kila mwezi - https://www.youtube.com/godshearttv/live - Video Language:
- English
- Team:
God's Heart TV
- Duration:
- 15:23
![]() |
georgejbudeba edited Swahili subtitles for DOUBLE JOB BREAKTHROUGH! | |
![]() |
georgejbudeba edited Swahili subtitles for DOUBLE JOB BREAKTHROUGH! | |
![]() |
georgejbudeba edited Swahili subtitles for DOUBLE JOB BREAKTHROUGH! |