-
Je, ni ukweli,
-
au ni maoni?
-
Je, ni muhimu?
-
Ndiyo.
-
Zote ni muhimu.
-
Lakini kufahamu jinsi ya kutenganisha
kati ya ukweli na maoni
-
kunaweza kutusaidia kufahamu vyema
tunachosoma na kusikia,
-
na jinsi tunabuni maoni yetu.
-
Hebu tuangalie.
-
Ukweli ni kauli ambayo
inaweza kuthibitishwa kuwa ni kweli.
-
Ukweli haupendelei,
-
inayomaanisha kuwa haushawishiwi
na imani au mafikira ya mtu.
-
Ukweli hauwezi kupingwa wala kubadilishwa.
-
Yafuatayo ni baadhi ya maswali muhimu
ya kubaini ukweli.
-
1. Inaweza kupimwa au kuthibitishwa
kupitia hesabu au data?
-
Kwa mfano, mbili ukiongeza mbili inakua
nne.
-
Tunaweza kuongeza nambari
na kuonyesha kuwa kauli hii ni ya kweli.
-
2. Inaweza kuangaliwa?
Tunaweza kuiona ikifanyika?
-
Kwa mfano, asilimia 99 ya watu
hawawezi kuramba kiwiko.
-
Huu ni kweli.
-
Huu ni ukweli unaoweza kuangaliwa.
-
Utafiti umebaini
-
kuwa mtu mmoja tu kati ya 100
anaweza kufanya hivyo.
-
3. Je, inaweza kuthibitishwa
na vyanzo vya msingi,
-
kama vile utafiti, picha,
magazeti na vitu vilivyobuniwa?
-
Ufuatao ni mfano.
-
Nintendo ilianzishwa mnamo 1889.
-
Huu ni ukweli, kwa sababu unaweza
kuthibitishwa na vyanzo vingi.
-
Mtu aliyefahamika kama Fusajiro Yamauchi
kutoka Japani
-
alianzisha Nintendo kama kampuni
ya kucheza kadi mnamo 1889,
-
na sasa ni mojawapo ya kampuni
kubwa zaidi za michezo duniani.
-
Sasa hebu tuangalie maoni,
-
ambayo mara nyingi yanaweza
kuwa magumu zaidi.
-
Maoni ni kauli ya imani au uamuzi.
-
Maoni huwakilisha
kile ambacho mtu anafikiri au kuhisi.
-
Maoni yanaweza kubadilika.
-
Hebu tuangalie baadhi ya mifano.
-
Aiskrimu ni tamu.
-
Watu wengi wanaamini hili,
lakini baadhi ya watu hawaamini.
-
Ni uamuzi, na kwa hivyo ni maoni.
-
Tunapotathmini mtu au kitu
-
mara nyingi tunatumia vivumishi kama vile
muhimu, mrembo, kufana au ngumu.
-
Kivumishi kinachoturuhusu
kufanya uamuzi kuhusu kitu
-
ni dalili kuwa kauli ni maoni.
-
Neno lingine la ishara za maoni
ni neno "paswa".
-
Ufuatao ni mfano.
-
Kila mtu anapaswa kujifunza
zaidi ya lugha moja.
-
Ingawa huenda kuna sababu nyingi nzuri
za kujifunza zaidi ya lugha moja,
-
si kila mtu atakubaliana
na thamani ya kibinafsi ya kufanya hivyo.
-
Mitazamo ya kisiasa ni maoni.
-
Watu tofauti watakuwa na maoni tofauti
kuhusu matatizo ya jamii
-
na jinsi ya kuzishughulikia vyema.
-
Kwa kuwa maoni hayawezi
kuthibitishwa au kutothibitishwa,
-
hama jibu sahihi na lisilo sahihi:
-
mitazamo tofauti tu.
-
Ingawa maoni yanaweza kuungwa
na ukweli na ushahidi,
-
suala tunalojali bado linaweza kujadiliwa.
-
Kwa mfano, ninaweza kusema
-
kuwa kwenda shuleni mwaka mzima
ni kuzuri kwa wanafunzi.
-
Sasa kuna sababu za kuunga mtazamo huu,
-
wengine wanaweza kusema
kuwa kipindi kifupi cha mapumziko
-
kinaweza kuwazuia wanafunzi
kusahau walichojifunza,
-
au kusema kuwa wanafunzi mara nyingi
huchoshwa katika majira ya joto,
-
au kuwa nchi nyingine duniani
hutumia mfumo wa mwaka mzima.
-
Hata hivyo, hatuwezi kuthibitisha
kuwa kauli hiyo ni kweli.
-
Kuna sababu nyingi za kufikiri
kuwa kalenda ya miezi 10 ni bora zaidi.
-
Unaweza kusema wanafunzi
wanahitaji mapumziko zaidi
-
na wanapaswa kuruhusiwa kushiriki kwa
shughuli za kambi na za msimu wa joto,
-
au kuwa ukosefu wa kiyoyozi unamaanisha
-
hawapaswi kuwa katika
jengo la shule katika msimu wa joto.
-
Tukirejelea kauli,
-
tunaweza pia kubaini
neno lingine la ishara la maoni:
-
neno "bora".
-
Wakati tunalinganisha vitu tofauti
-
au tunapoona maneno kama vile
"kubwa zaidi", "bora zaidi" au "bora"'
-
inaweza kupendekeza
kuwa tunatafuta kauli ya maoni.
-
Aina nyingine ya maoni ni utabiri.
-
Mara nyingi utabiri hulingana
na uzoefu, maarifa au utafiti,
-
lakini kwa sababu yanategemea
siku za baadaye,
-
hatuwezi kuyathibitisha leo.
-
Hebu tuangalie mfano.
-
Magari yanayojiendesha yatawakilisha
10% ya magari barabarani kufikia 2026.
-
Hilo ni nzuri na la kutisha.
-
Ingawa waundaji wengi wa magari wanabuni
teknolojia ya magari ya kujiendesha,
-
hatuna njia ya kuthibitisha
kauli hiyo leo.
-
Kwa hivyo, ni maoni.
-
Jambo moja la kukumbuka ni kwamba kwa
sababu tu tunaamini jambo kuwa kweli,
-
hilo halilifanyi kuwa ukweli.
-
Hebu tutoe muhtasari wa tulichojifunza.
-
Ukweli ni kauli ambayo
inaweza kuthibitishwa kuwa kweli.
-
Inaweza kupimwa au kuthibitishwa na data?
-
Je, inaweza kuangaliwa?
-
Tunaweza kuthibitisha ukweli wake
kupitia vyanzo vingine?
-
Je, haibadiliki?
-
Tukijibu "ndiyo"
kwa mojawapo ya maswali haya,
-
basi inamaanisha kuwa ni kweli.
-
Maoni ni kauli ya imani au uamuzi
-
ambayo haiwezi kuthibitishwa kuwa kweli.
-
Je, inatathmini mtu au kitu?
-
Tunaweza kuijadili?
-
Je, inatoa utabiri?
-
Inaweza kubadilika?
-
Ukijibu "ndiyo" kwa maswali haya,
-
Hayo ni maoni.
-
Kujua jinsi ya kutenganisha
kati ya ukweli na maoni
-
hutusaidia kuelewa maelezo
-
na kubadili imani zetu binafsi kuhusu
dunia.
-
Ijaribu na uone iwapo unaweza
kutumia maswali haya
-
kubainisha tofauti katika maisha yako.
-
Manukuu ni ya Carol Wang
Ukaguzi ni wa llona vd Tang