-
♪ (muziki) ♪
-
Kabla ya kuibuka kwa mtandao
kila mtu aliona habari zinazofanana.
-
Zilitoka kwenye televisheni, redio na
magazeti.
-
Walinzi wa taarifa walikuwa watu,
-
huku wahariri wakikagua habari zote
-
na kuamua zitakazoonyeshwa kwa umma.
-
Leo, mashirika ya zamani ya habari
-
yameungwa na
vyanzo vingine vingi mtandaoni;
-
na kwenye intaneti
-
mara nyingi ni programu ya kompyuta
inayoamua kitakachotazamwa na watu.
-
Unapotafuta kwenye wavuti
au kutembelea tovuti ya mtandao jamii,
-
Kuna maudhui mengi zaidi kiasi kwamba
mfumo unahitajika kuchuja matokeo.
-
Ili kutabiri mtumiaji angependa
kuona nini,
-
mifumo ya mtandaoni hutumia algoriti.
-
Algoriti ni kundi la maagizo
-
yanayoambia kompyuta
jinsi ya kutekeleza majukumu fulani
-
kama vile jinsi ya kupanga maelezo.
-
Algoriti hubaini maudhui utakayoonyeshwa
-
kulingana na mseto
wa kilicho maarufu
-
na kinachojua kuhusu
mtazamo na mambo yanayokuvutia.
-
Unapofungua akaunti kwenye mtandao jamii
-
kuna uwezekano utatoa
maelezo ya msingi
-
kama vile jina, jinsia na umri wako.
-
Huenda ukashiriki maelezo mengine
bila hata kugundua.
-
Kila wakati unapopenda, kushiriki,
au kutoa maoni kwenye chapisho
-
maelezo hayo huhifadhiwa
na kutumiwa kubuni wasifu wako.
-
Kwenye wavuti pana,
vitendo vingi unavyofanya
-
hufuatiliwa na vinaweza kufikiwa
na algoriti za mtandao jamii.
-
Inaweza kushangaza
-
kiasi ambacho algoriti inaweza
kujifunza kukuhusu kupitia vitendo vyako.
-
Data hii unayoweka ni muhimu
-
kwa sababu mifumo ya mtandaoni
hupata pesa kwa kuuza matangazo.
-
Watangazaji watalipa ili kuwafikia watu
-
wenye uwezekano mkubwa wa kuvutiwa
na ujumbe wao.
-
Kadri mfumo unavyokujua
-
ndivyo unaweza kukuonyesha maudhui
na matangazo yaliyowekewa mapendeleo.
-
Algoriti zinaweza kukuhimiza
uendelee kubofya, kupitia au kutazama
-
kwa kuonyesha maudhui
yaliyo maarufu, yanayovutia au mapya
-
kwa sababu lengo
ni kushikilia umakini wako
-
Algoriti zinaweza kufadhili maudhui
ya ajabu, ya uongo au yanayopotosha.
-
Kuna nyakati ambapo algoriti
zinaweza kuwa muhimu, kwa mfano,
-
wakati huduma ya kutiririsha muziki
inapendekeza wimbo mpya
-
kulingana na ulichosikiliza awali.
-
Lakini wakati algoriti zinabaini
habari au taarifa tunazoona
-
huenda athari zikawa kubwa zaidi.
-
Wakati maelezo
yamebadilishwa ili kutufaa sisi tu,
-
tunaweza kuishia katika hali ya
mapendeleo.
-
Mapendeleo hutokea
wakati tunaonyeshwa tu maelezo
-
ambayo tuna uwezekano wa kuyakubali.
-
Kuwa katika hali ya kupendelea kunaweza
kutufanya tusikubali maoni
-
ambayo ni tofauti na yetu binafsi.
-
Hili linaweza kuwa na athari mbaya
kwa demokrasia
-
ambayo inawahitaji raia kuwasikiliza
wengine na kuelewana.
-
Kufahamu ni kwa nini tunaona
tunachoona mtandaoni
-
kunaweza kutusaidia kuwa
watumiaji makini zaidi wa maelezo.
-
Mipasho yetu kamwe haitupi picha kamili
-
kwa hivyo tunahitaji kujenga desturi ya
kutafuta habari
-
na maelezo kutoka kwa vyanzo mbalimbali.
-
♪ (muziki) ♪