-
Hujambo, Jina langu ni Suzan Song,
-
Mwelekezi wa Idara cha Taaluma ya Ugonjwa
wa Akili kwa Watoto, Vijana na Familia
-
ya Chuo Kikuu cha George Washington,
-
na Mshauri wa Kulinda Ubinadamu
-
kwa waathiriwa wa uhamishaji
wa lazima kote duniani na nchini.
-
Kumekuwa na ongezeko la kipekee
-
la idadi ya wakimbizi kote ulimwenguni,
-
wakiwemo wakimbizi, watafuta
makao, wahamiaji wasio halali
-
na watoto walio pweke.
-
Kote ulimwenguni, zaidi ya watu milioni 65
-
kwa sasa ni wakimbizi kutokana
na vita, mateso au mgogoro wa kivita.
-
Kufikia mwanzo mwa 2018, takribani
watoto milioni 31 kote ulimwenguni
-
walifanywa wakimbizi kutokana
na vurugu na migogoro.
-
Iwapo mitindo hii ya sasa itaendelea,
-
mtu mmoja kati ya watu mia moja
atakuwa mkimbizi hivi karibuni.
-
Kwa bahati mbaya, wakimbizi na
waathiriwa wengi wa uhamaji wa lazima
-
hawapokei huduma
inayohitajika ya afya ya akili.
-
kutokana na umakini wa huduma,
ukosefu wa kufikia huduma ya kitaalamu,
-
na shutuma dhidi ya matatizo ya akili.
-
Wakimbizi ni wale ambao
wametoroka katika nchi zao halisi
-
kutokana na wasiwasi wa
mateso yaliyopangwa
-
yanayolingana na mbari, dini,
uraia, maoni ya kisiasa
-
au uanachama katika
kikundi fulani cha jumuiya.
-
Ingawa wakimbizi huomba
ulinzi wakiwa ughaibuni
-
na wanapewa ruhusa ya kuingia Marekani,
-
Watu wanaotafuta
makao pia wana hofu ya mateso.
-
Lakini wanatafuta ulinzi wakiwa
ndani ya Marekani.
-
Wakimbizi na watu wengine
walioathiriwa na mzozo
-
waliripotiwa kuwa na
asilimia 15 hadi 30 ya
-
PTSD na mafadhaiko,
-
ikilinganishwa na asilimia 3.5 ya PTSD
miongoni mwa wasio wakimbizi.
-
Mambo thabiti
yanayoashiria afya mbovu ya akili
-
ni kupitia mateso na matukio
mengi yanayosababisha kiwewe.
-
Lakini mateso, kutenganishwa na familia, michakato ya kuchosha ya mahali pa hifadhi,
-
kutengwa na hali ngumu katika nchi unakoishi
-
zote huongeza ubaya wa afya ya akili.
-
Mazingira baada ya uhamiaji, hasa kipindi kirefu cha kuzuiliwa,
-
hali isiyo salama ya uhamiaji,
-
ufikiaji mbovu wa huduma
na vikwazo vya kazi na elimu
-
vinaweza kudhoofisha zaidi afya ya akili.
-
Haya hayatoi upeo kamili wa matatizo ya hisia
-
yanayokumbwa na watu walioathiriwa na mgogoro
-
ikiwa ni pamoja na huzuni isioelezeka, kiwewe kigumu,
-
kukata tamaa, kutengwa, hasira, na kutoamini.
-
Watu wengi wanakumbana na hatua za kawaida
-
kwa matukio yasiyo ya kawaida kabisa.
-
Baada ya muda, wakimbizi wengi huonyesha dalili chache au hawaonyeshi dalili zozote.
-
Idadi ndogo huonyesha mtindo wa kupona
-
na idadi ndogo ingine huendelea kutatizika.
-
Kwa hivyo tunahitaji kutathmini tofauti kati ya hali za tukio za dhiki
-
na hali dhahiri ya ugonjwa wa akili kwa wakimbizi.
-
Tunafanya hili kwa kulenga kushirikisha
-
hali za awali za kiwewe,
-
mambo ya kila siku ya kusababisha mzongo,
-
na mifumo mikuu ya ushirikiano wa kijamii ambayo mtu anahusika.
-
Wataalamu wa akili wanaweza kusaidia watu hawa
-
kupitia shughuli za kliniki zinazofaa kwa wakimbizi na wanaotafuta makao.
-
Kwa kiwango cha sera kwa kufanya tathmini za makao
-
na kwa kiwango cha utetezi kwa kuhimiza usawa wa kufikia,
-
uwezo wa huduma kuwahifadhi wakimbizi na watu waliohamishwa kwa lazima,
-
na kwa kushirikiana na wanachama wa jumuiya ya masomo mbalimbali
-
kama vile mawakili, walimu na watengenezaji wa sera
-
kutoa mfumo salama ambao wakimbizi
-
na walionusurika kuhamishwa lazima wanaweza kutegemea.