Kizazi kipya cha wasanifu majengo na wabuifu wa Africa.
-
0:01 - 0:04Safari ndefu ambayo nimewahi kusafiri,
-
0:04 - 0:06Ilikuwa ni mwaka 2002
-
0:07 - 0:08Nilikuwa na miaka 19
-
0:09 - 0:12Ilikuwa ni mara ya kwanza kupanda ndege
-
0:12 - 0:15na mara ya kwanza kutoka nje ya nchi.
-
0:15 - 0:16Rwanda,
-
0:17 - 0:21Ilibidi niende umbali wa maelfu ya kilometa
-
0:21 - 0:22kufwata ndoto zangu.
-
0:22 - 0:25Ndoto niliyokuwa nayo tangu utotoni,
-
0:26 - 0:30Na hiyo ndoto ilikuwa ni kuwa msanifu majengo.
-
0:31 - 0:34Kipindi hicho ilikuwa haiwezekani nchini mwangu.
-
0:34 - 0:36Kulikuwa hamna shule za usanifu majengo.
-
0:36 - 0:39Kwahiyo nilivyopata msaada wa kwenda kusoma china,
-
0:40 - 0:42niliacha maisha yangu na familia nyuma
-
0:42 - 0:44nikahamia Shanghai.
-
0:45 - 0:47Ilikuwa ni wakati mzuri
-
0:47 - 0:52Nchi ilikuwa inapitia mlipuko wa majengo.
-
0:52 - 0:53Shanghai nyumbani kwangu kupya
-
0:53 - 0:56ilikuwa inabadilika kuwa mji wenye maghorofa mengi.
-
0:57 - 0:59China ilikuwa inabadilika
-
0:59 - 1:03Mipango mji mipya ilijengwa ili kuleta muonekano mpya wa maendeleo.
-
1:04 - 1:10Majengo mapya ya kustaajabisha yalikuwa yanajengwa kila sehemu,
-
1:10 - 1:13Lakini nyuma ya hii yote,
-
1:13 - 1:17utumikwishaji wa wafanyakazi wengi wa kigeni,
-
1:17 - 1:21utenganeshwaji wa maelfu ya watu
-
1:21 - 1:23uliifanya hii miradi ifanikiwe.
-
1:23 - 1:25Na haya maendeleo ya haraka
-
1:25 - 1:28yalichangia kuchafua mazingira kwa kiasi kikubwa.
-
1:28 - 1:30amabayo ina hatarisha China leo.
-
1:31 - 1:33Mnamo mwaka 2010
-
1:33 - 1:35nilivyorudi nyumbani Rwanda
-
1:35 - 1:40Kule, nikakuta maendeleo yanayofanina na China.
-
1:40 - 1:46Nchi ilikuwa na bado ina pitia ukuaji wake wa kiuchumi na kijamii,.
-
1:47 - 1:50Msukumo wa kujenga miji , miundombini na majengo.
-
1:50 - 1:52upo kwenye ukubwa wake
-
1:52 - 1:53na matokeo yake,
-
1:53 - 1:55kuna mlipuko wa majengo pia.
-
1:56 - 2:01Huu ndo uhalisia ulioko kwenye bara zima la Africa,
-
2:01 - 2:02Na hii ndo sababu.
-
2:03 - 2:06Ifikapo mwaka 2050, idadi ya watu Africa itakuwa mara mbili.
-
2:06 - 2:10Kufikia watu billioni 2.5.
-
2:10 - 2:12Ifikapo hapo
-
2:12 - 2:17Idadi ya watu wa Africa itakuwa pungufu kidogo kuzidi ilivyo sasa
-
2:17 - 2:21ya China na India.
-
2:23 - 2:28Miundombinu na majengo yanayohitajika kuhimili watu wengi kiasi hiki
-
2:28 - 2:31haijategemewa kwenye historia ya binadamu.
-
2:32 - 2:35Tumekisia kwamba ifikapo mwaka 2050
-
2:35 - 2:41inabidi tujenge zaidi ya nyumba 700,000,000
-
2:41 - 2:44shule takribani 300,000
-
2:44 - 2:48na sehemu za huduma za kiafya zisizopungua 100,000.
-
2:49 - 2:52Ngoja nikupe muelekeo
-
2:53 - 2:57Kila siku kwa miaka 35 ijayo
-
2:57 - 3:00inabidi tujenge sehemu saba za huduma za afya.
-
3:00 - 3:01shule 25
-
3:01 - 3:06na karibia uniti 60000 za nyumba kila siku,
-
3:06 - 3:07kila siku
-
3:10 - 3:13Tutawezaje kujenga hivi vyote?
-
3:14 - 3:18Je tutafwata mfano wa ujenzi usio salama
-
3:18 - 3:20kama ule wa China?
-
3:20 - 3:24Au tutaweza kutengeneza wa kwetu wa kipekee wa Africa.
-
3:24 - 3:27Ambao utakuwa wa kuridhisha na wa faida kwa maendeleo?
-
3:28 - 3:30Nina amini tunaweza.
-
3:30 - 3:33Nawajua Wa Africa ambao tayari wanaufanya.
-
3:33 - 3:36Mfano msanifu majengo wa Nigeria Kunlé Adeyemi,
-
3:36 - 3:40Na kazi zake kwenye mitaa ya Pwani za miji mikubwa.
-
3:40 - 3:43Sehemu kama Makoko Lagos
-
3:43 - 3:48Ambapo mamia maelfu ya watu wanaishi kwenye vijijumba vya kushona
-
3:48 - 3:49vilivyo juu ya maji,
-
3:49 - 3:51bila miundo mbinu ya serikali wala huduma za kijamii.
-
3:52 - 3:58Jamii iliyo katika hatari ya muongezeko wa maji na mabadiliko ya tabia nchi.
-
3:58 - 4:03Lakini bado watu wanaoishi hapo ni mfano wa wapambanaji
-
4:03 - 4:05na wenye nia ya kuishi.
-
4:05 - 4:08Kunlé na timu yake wametengeneza shule ya mifano.
-
4:08 - 4:11Ambayo inavumilia maji ya bahari yanyoongezeka.
-
4:11 - 4:13Hii ni shule ya Makoko.
-
4:15 - 4:19Ni mfano wa jengo linaloeleya ambalo linaweza kutumika kwenye kliniki,
-
4:19 - 4:21nyumba na masoko
-
4:22 - 4:24na miundombinu mingine ambayo hii jamii inahitaji.
-
4:24 - 4:26Ni moja la jibu la kipekee
-
4:26 - 4:31amabalo linaweza hakikisha maisha ya hii jamii ambayo inaishi kwenye maji ya Lagos.
-
4:32 - 4:34Huyu ni Francis Kéré.
-
4:35 - 4:37Anafanya kazi kwenye nchi anayotokea.
-
4:37 - 4:38Burkina Faso.
-
4:38 - 4:44Kéré na timu yake wametengeneza miradi ambayo inatumia njia za kitamaduni za ujenzi.
-
4:44 - 4:47Kéré na timu yake wanafanya kazi kwenye jamii
-
4:47 - 4:50na wametengeneza shule za mifano
-
4:50 - 4:51ambazo jamii nzima.
-
4:51 - 4:55zinafanana na kila mradi kwenye vijiji vya nchi hii
-
4:55 - 4:57inakuja pamoja kujenga.
-
4:58 - 5:01Watoto wanaleta mawe kwa ajili ya msingi,
-
5:01 - 5:04wanawake wanaleta maji kwa ajili ya upauaji wa matofali,
-
5:04 - 5:08na kila mtu anafanya kazi kubonda sakafu za udongo
-
5:09 - 5:10pamoja na jamii,
-
5:10 - 5:14Kéré na timu yake wametengeneza miradi inayofanya kazi vizuri
-
5:14 - 5:17kwa mwanga na uingizaji hewa wa kutosha.
-
5:17 - 5:20Zinafaa kwenye huu mstakabali
-
5:20 - 5:22na ni nzuri mno mno.
-
5:23 - 5:25Kwa miaka saba iliyopita,
-
5:25 - 5:28nimekuwa nikifanya kazi kama msanifu majengo wa MASS Design Group.
-
5:28 - 5:31Ni kampuni ya ubunifu iliyoanzishwa Rwanda.
-
5:32 - 5:36Tumefanya kazi na nchi nyingi Africa,
-
5:36 - 5:40Tukilenga huu mpango wa kukidhi na wenye faida,
-
5:40 - 5:42wa usanifu majengo.
-
5:42 - 5:44Na Malawi ni moja ya hizo nchi.
-
5:45 - 5:48Ni nchi yenye mazingira mazuri yaliyojificha.
-
5:48 - 5:51yenye milima yenye vilele virefu na ardhi yenye rutuba.
-
5:51 - 5:55Lakini pia ina idadi kubwa za vifo vya kina mama duniani.
-
5:57 - 6:01Mwanamke mwenye mimba Malawi huzalia nyumbani au
-
6:01 - 6:05hutembea safari ndefu kuelekea kliniki ya karibu.
-
6:06 - 6:11Na moja kati ya kina mama 36 anafariki wakati wakujifungua.
-
6:13 - 6:14Malawi
-
6:14 - 6:16na timu yetu ya MASS Design Group
-
6:16 - 6:18Tumetengeneza kijij cha kina mama cha kusubiria kujifungua.
-
6:19 - 6:23Hii ni sehemu ambayo wanawake wanakuja wiki 6 kabla ya kujifungua.
-
6:24 - 6:26Hapa wanapata matunzo ya uzazi
-
6:26 - 6:29na kujifunza kuhusu lishe na uzazi wa mpango.
-
6:30 - 6:32Wakati huo huo wanatengeneza umoja
-
6:32 - 6:35na wakina mama wengine wanaosubiria kujifungua na familia zao.
-
6:37 - 6:39Muundo wa kijiji cha kusubiria kujifungulia cha Kasungu
-
6:40 - 6:44inaazima ukienyeji wa vijiji vya Malawi
-
6:44 - 6:48na imejengwa kutumia nyenzo na mbinu rahisi .
-
6:48 - 6:53Matofali tunayotumia yametengenezwa na udongo wa kwenye eneo hili hili
-
6:54 - 6:57Hii inapunguza matumizi ya cabon kwenye jengo hili,
-
6:57 - 6:59lakini kabla ya yote.
-
6:59 - 7:05Inaleta sehemu safi na inayofaa kwa ajili ya akina mama.
-
7:05 - 7:08Hii mifano inaonesha kuwa majengo na miundo
-
7:08 - 7:14ina nguvu na uwezo wa kutatua matatizo yanayotukabiri.
-
7:16 - 7:19Lakini la umuhimu zaidi
-
7:19 - 7:22tunaweza tengeneza mifano ya kutatua matatizo
-
7:22 - 7:24kwenye jamii zetu.
-
7:24 - 7:27Lakini mifano hii mitatu haitoshi
-
7:28 - 7:31Mifano mingine 300 haitotosha.
-
7:32 - 7:38Tunahitaji jamii nzima ya waasnifu majengo na wabunifu wa ki Afrika.
-
7:38 - 7:41Waongoze kwa mifano mingi zaidi
-
7:41 - 7:43Mnamo Mei mwaka huu
-
7:43 - 7:47tulifanya mkutano wa wasanifu majengo wa Africa, Kigali,
-
7:47 - 7:50na tukawaalika wabunifu wengi wa Africa
-
7:50 - 7:54na waalimu wa usanifu majengo wanaofanya kazi ndani ya bara hili
-
7:55 - 7:57Sote tulikuwa na jambo moja la kufanana
-
7:58 - 8:03Sote tulisoma shule ulaya
-
8:03 - 8:04na nje ya Africa
-
8:04 - 8:06Hii inabidi ibadilike.
-
8:07 - 8:11Kama tunataka kutengeneza mipango inayoendana na sisi
-
8:11 - 8:14kulikoni kutaka kuibadilisha Kigali iwe Beijing
-
8:14 - 8:17au Lagos iwe Shenzen
-
8:17 - 8:18tunahitaji jamii
-
8:18 - 8:22itakayojenga miundo ya kujiamini ya jamii inayokuja
-
8:22 - 8:24ya wasanifu majengo na wabunifu wa ki Africa.
-
8:25 - 8:32(Makofi)
-
8:33 - 8:34Mnamo September mwaka jana,
-
8:34 - 8:37tulianzisha kituo cha ubunifu cha Africa
-
8:37 - 8:40tuanze kujenga hii jamii
-
8:42 - 8:45Tuliwaweka wanafunzi 11 kutoka kwenye bara zima.
-
8:46 - 8:50Ni kozi inayodumu kwa miezi 20
-
8:51 - 8:54Hapa wanajifunza kukabiliana na vikwazo vikubwa
-
8:54 - 8:57kama mabadiliko ya tabia hewa na mipango miji
-
8:57 - 8:58kama ambavyo Kunlé na timu yake wamefanya.
-
8:59 - 9:01Wanafanya kazi na jamii
-
9:01 - 9:05kuendeleza mipango ya ujenzi na miundo mbinu
-
9:05 - 9:07kama ambavyo Kéré na timu yake wamefanya.
-
9:08 - 9:12Wanajifunza kuelewa umuhimu wa kiafya wa majengo mazuri
-
9:12 - 9:16kama ambavyo sisi wa MASS Design Group tumekuwa tukifanya uchunguzi
-
9:16 - 9:17kwa miaka kadhaa iliyopita.
-
9:18 - 9:20Muda wa sifa wa huu ushirika
-
9:20 - 9:24ni mradi walio sanifu na kujenga.
-
9:24 - 9:27Hii ni shule ya msingi ya Ruhehe,
-
9:27 - 9:28mradi walio usanifu.
-
9:28 - 9:33Walijikita kwenye jamii ili waelewe matatizo yanayoikabili.
-
9:33 - 9:35Lakini pia kuzindua njia mpya,
-
9:35 - 9:39kama vile kutumia ukuta uliotengenezwa na mawe ya volkano.
-
9:39 - 9:43kubadilisha mazingira mazima ya chuo kuwa sehemu ya kucheza na kujifunza.
-
9:45 - 9:47Walitathimini hali ya mazingira,
-
9:48 - 9:51na kutengeneza mfumo wa paa ambao unaongeza mwanga wa jua
-
9:51 - 9:53na unaongeza utendaji wa sauti.
-
9:53 - 9:57Ujenzi wa shule ya msingi ya Ruhehe utaanza mwaka huu.
-
9:59 - 10:05(Makofi)
-
10:05 - 10:06Na kwenye miezi inayofuatia
-
10:06 - 10:10wasomi wa chuo cha ubunifu cha Afrika watafanya kazi moja kwa moja
-
10:10 - 10:12na jamii ya Ruhehe kuijenga.
-
10:13 - 10:15Tulivyowauliza wanafunzi
-
10:15 - 10:19wanataka kufanya nini baada ya kukamilisha fellowshipu yao ya Ubunufu wa kiAfrica,
-
10:19 - 10:21Tsepo kutoka South Africa alisema,
-
10:21 - 10:24anataka kutambulisha hii namna mpya ya kujenga nchini kwake.
-
10:24 - 10:27Kwa hivyo ana mpango wa kufungua kampuni yake binafsi Johannesburg,
-
10:28 - 10:32Zani anataka kutanua nafasi kwa wanawake wawe wahandisi.
-
10:33 - 10:35kabla ya kujiunga na kituo cha Ubunifu cha Afrika.
-
10:35 - 10:37alisaidia kuanzisha, Nairobi,
-
10:37 - 10:42shirika la kusaidia kuziba pengo la wanawake kwenye sekta ya uhandisi,
-
10:42 - 10:45na anategemea kupeleka huu msimamo Afrika nzima.
-
10:45 - 10:46mwishowe dunia nzima.
-
10:48 - 10:50Moses kutoka sudan ya kusini
-
10:50 - 10:52nchi mpya duniani
-
10:52 - 10:55anataka kufungua shule mpya ya ufundi wa teknolojia.
-
10:55 - 11:00ambayo itafundisha watu ujenzi kwa kutumia malighafi zilizoko nchini mwao
-
11:02 - 11:05Moses alitamani kuwa msanifu majengo.
-
11:06 - 11:11Vita za wenyewe kwa wenyewe nchini kwao ziliingilia masomo yake.
-
11:12 - 11:16Wakati anajiaandaa kuanza kusoma kwenye kituo cha Ubunifu cha Afrika
-
11:16 - 11:21tulikuwa tunasikia bunduki zikilia nyuma ya simu yake ya mahojiano.
-
11:22 - 11:25Lakini katikati ya vita ya wenyewe kwa wenyewe
-
11:25 - 11:27Moses alishikilia wazo lake
-
11:27 - 11:32la kwamba usanifu majengo unaweza kuwa njia ya kufanya jamii ziwe pamoja.
-
11:33 - 11:36Imani za mwanafunzi huyu zinatoa msukumo
-
11:36 - 11:39wa kwamba usanifu majengo unaleta tofauti,
-
11:39 - 11:41wa jinsi ambavyo Afrika inajengwa.
-
11:43 - 11:46Ukuaji wa Afrika hauwezi kusahauliwa
-
11:47 - 11:51Waza miji mipya ya Afrika,
-
11:51 - 11:53lakini sio kama makazi duni
-
11:53 - 11:55lakini zenye uvumulivu
-
11:55 - 11:59na zenye jamii za kushabihiana zaidi duniani.
-
11:59 - 12:01Hili linawezekana
-
12:02 - 12:06Na tuna uwezo wa kulifanya litokee.
-
12:06 - 12:10Lakini safari ya kuandaa vipaji vya yajayo mbeleni
-
12:10 - 12:12kama safari yangu,
-
12:12 - 12:13ni ndefu sana.
-
12:15 - 12:19Kwa vizazi vijavyo vya wabunifu wa Ki Africa
-
12:19 - 12:23inabidi tufupishe hii safari.
-
12:23 - 12:24Lakini la umuhimu zaidi--
-
12:25 - 12:27na siwezi kuliwekea msisitizo wa kutosha--
-
12:27 - 12:29tunahitaji kujenga kujiamini kwao kiubunifu
-
12:29 - 12:33na kuwapa nguvu kutengeneza majibu ya ki Africa
-
12:33 - 12:36lakini yafae kwa dunia nzima.
-
12:36 - 12:37Asante sana.
-
12:37 - 12:44(Makofi)
- Title:
- Kizazi kipya cha wasanifu majengo na wabuifu wa Africa.
- Speaker:
- Christian Benimana
- Description:
-
Christian Benimana anataka kujenga mtandao wa wasanifu majengo watakaoweza kusaidia mlipuko wa miji mipya ya Afrika kukua na kuwa yenye manufaa--ikizingatia ukuaji na thamani ambazo ni za ki Africa. Kutoka Nigeria mpaka Burkina Faso na kuendelea mbele, anatoa mifano ya usanifu majengo unavyoleta jamii pamoja. Harakati za wasanifu majengo, wabunifu na wahandisi kwenye bara hili na diaspora wanajifunza na wanatiana hamasa, Benimana ana tualika tuwaze mbele jinsi ambavyo miji ya Afrika itakavyokuwa ya kushabihiana zaidi duniani.
- Video Language:
- English
- Team:
- closed TED
- Project:
- TEDTalks
- Duration:
- 12:57
Joachim Mangilima approved Swahili subtitles for The next generation of African architects and designers | ||
Julieth Mbeyella accepted Swahili subtitles for The next generation of African architects and designers | ||
Julieth Mbeyella edited Swahili subtitles for The next generation of African architects and designers | ||
Julieth Mbeyella edited Swahili subtitles for The next generation of African architects and designers | ||
Neria-Neema Kwayu edited Swahili subtitles for The next generation of African architects and designers |