Je, unahangaika na MSONGO WA MAWAZO? USHUHUDA huu utakutia moyo!
-
0:00 - 0:02Sina msononeko tena.
-
0:02 - 0:09Kwa kweli, msononeko uliniacha siku hiyo baada ya kumaliza Maombi ya Pamoja.
-
0:09 - 0:12Nilihisi amani sana.
-
0:15 - 0:23Je, ni eneo gani la maisha yako unapitia, unakumbana na utumwa?
-
0:23 - 0:28Leo ni siku yako ya uhuru.
Pokea uhuru sasa hivi! -
0:28 - 0:40Uhuru katika familia yako, afya, kazi, fedha, biashara - pokea uhuru!
-
0:42 - 0:46Naitwa Tumpale,
nikishuhudia kutoka Tanzania. -
0:46 - 0:53Mwaka jana tarehe 2 Machi 2024,
nilijiunga na Maombi ya Pamoja. -
0:53 - 0:57Nilikuwa na matatizo matatu makubwa maishani mwangu.
-
0:57 - 1:05Niligunduliwa na ugonjwa wa uvimbe anuai kwenye ovari (Polycystic Ovarian Syndrome) , ambao nilikuwa nao kwa zaidi ya miaka kumi.
-
1:05 - 1:12Kwa muda wote huo, nilikuwa nikipambana na hedhi isiyo ya kawaida.
-
1:12 - 1:17Kulikuwa na nyakati ambapo
mwaka mzima ungepita bila ya mimi -
1:17 - 1:22kupata hedhi yangu,
na hilo liliniathiri sana. -
1:22 - 1:31Nchini Tanzania, mimi na mama yangu tulijaribu kutafuta matibabu kutoka kwa madaktari tofauti.
-
1:31 - 1:36Nilitumia dawa nyingi tofauti
bila mafanikio -
1:36 - 1:44na utambuzi niliopewa hapa ni kwamba nilikuwa na ukosefu wa usawa wa homoni.
-
1:44 - 1:52Shida iliendelea hadi nikalazimika kusafiri kwenda India kwa ajili ya Shahada yangu ya Kwanza.
-
1:52 - 1:58Nikiwa India, nilijiambia, 'Acha nitafute matibabu hapa.
-
1:58 - 2:02Ngoja nione kama naweza kupata msaada
wa kuliondoa tatizo hili'- -
2:02 - 2:07kwa sababu ilikuwa ikiniathiri kiakili
na nilikuwa na wasiwasi. -
2:07 - 2:12Wanawake wengi walio na ugonjwa wa uvimbe anuai kwenye ovari (Polycystic Ovarian Syndrome) wana shida
-
2:12 - 2:15katika kupata watoto katika ndoa zao.
-
2:15 - 2:24Kwa hiyo nikiwa India, nilienda hospitalini
na nilipewa vipimo tofauti. -
2:24 - 2:28Hao ndio walionigundua
na ugonjwa wa uvimbe anuai kwenye ovari (Polycystic Ovarian Syndrome) . -
2:28 - 2:31Lakini kwa Tanzania, niliambiwa kwamba
nilikuwa na ukosefu wa usawa wa homoni. -
2:31 - 2:38Baada ya utambuzi huo, nilipewa
dawa ambazo nilitumia, -
2:38 - 2:41lakini bado shida yangu haikutatuliwa.
-
2:41 - 2:49Niliizoea lakini iliniathiri -
ningejiona sijakamilika. -
2:49 - 2:52Ukiwa msichana, unatarajia kuwa 'wa kawaida'
kama wenzako. -
2:52 - 2:55Niliiona kama sehemu ya maisha yangu.
-
2:55 - 3:02Wakati huo mnamo Machi 2024,
pia nilikuwa na maambukizi ya njia ya mkojo. -
3:02 - 3:08Matatizo hayo mawili hayakuwa matatizo yaliyonileta kwenye
-
3:08 - 3:10Huduma ya Maombi ya Pamoja.
-
3:10 - 3:14Tatizo kubwa lililoniletea
ni msononeko. -
3:14 - 3:18Niliporudi Tanzania
kwa ajili ya mafunzo yangu ya vitendo, -
3:18 - 3:23Niligundua kuwa mfumo hapa ni tofauti.
-
3:23 - 3:31Sifa zinazohitajika ili mtu ajiandikishe kwa Shahada ya Kwanza
-
3:31 - 3:35katika unusukaputi(anesthesia) hapa katika nchi yangu ni tofauti
-
3:35 - 3:41na zile ambazo mtu anatakiwa kuwa nazo
ili ajiandikishe nchini India. -
3:41 - 3:46Kwa hivyo katika nchi yangu sifa zinakuwa tofauti, ili uweze kwenda kwa digrii ya Shahada ya utaalamu wa unusukaputi(anesthesia).
-
3:46 - 3:53inabidi uwe muuguzi mwenye uzoefu wa kufanya kazi usiopungua miaka miwili.
-
3:53 - 3:56Hiyo ilikuwa changamoto kwangu
kwa sababu niliporudi, -
3:56 - 4:03Ilinibidi nianze kufanya kazi kama
muuguzi na mtaalamu wa unusukaputi. -
4:03 - 4:10Kwa hiyo ilikuwa vigumu kwa sababu sikuwahi kuwa muuguzi; kila kitu kilikuwa kipya kwangu.
-
4:10 - 4:16Tofauti na wenzangu, hata mimi sikuwa na uzoefu. Nilikuwa sina uzoefu kabisa.
-
4:16 - 4:21Ilikuwa mbaya sana kiasi
kwamba nilikuwa nikidhihakiwa. -
4:21 - 4:28Nilichukuliwa kuwa mtu asiye na uzoefu zaidi. Nilikuwa najiona sina maana.
-
4:28 - 4:35Ilikuwa mbaya sana - hadi nilikuwa
na msongo huu. -
4:35 - 4:43Kwa hivyo nilikuwa nikipitia Facebook na YouTube, kisha nikakutana na TV ya Moyo wa Mungu.
-
4:43 - 4:51Kisha nikatuma ombi la maombi. Hivyo ndivyo nilivyojiunga na Maombi ya Pamoja tarehe 2 Machi 2024.
-
4:51 - 4:56Maombi yalipokuwa yakiendelea,
nilihisi nguvu za Roho Mtakatifu -
4:56 - 4:58kwa sababu miguu yangu ilianza kutetemeka.
-
4:58 - 5:06Nilianza kutetemeka na nilihisi maumivu makali ya kichwa na maumivu katika eneo la nyonga.
-
5:06 - 5:11Mwishoni mwa maombi,
nilihisi amani sana. -
5:11 - 5:17Kabla ya maombi, moyo wangu ulikuwa
mzito sana. Nilikuwa nimepoteza matumaini. -
5:17 - 5:22Nilitaka hata kuacha. Sikutaka
kwenda kazini tena. -
5:22 - 5:29Sikutaka kuendelea na kitu chochote kinachohusu unusukaputi (anesthesia) au mafunzo yangu ya kazi.
-
5:29 - 5:34Lakini mwisho wa maombi, nilihisi amani.
-
5:34 - 5:40Siwezi hata kuielezea lakini ilikuwa ni amani hii ambayo sijawahi kuhisi hapo awali.
-
5:40 - 5:46Na mwisho wa Machi, nilipata hedhi.
-
5:46 - 5:56Na kisha tangu wakati huo hadi sasa, sijawahi kukosa hedhi na ni kawaida.
-
5:56 - 6:02Nilifurahi sana lakini nilijiambia,
'Labda ni kama miaka hiyo -
6:02 - 6:06ambapo ningeiona mara tatu
au labda mara mbili kwa mwaka. -
6:06 - 6:10Acha nione kama nitapata kila mwezi.'
-
6:10 - 6:13Na ilikuwa kama Mungu akisema,
'Hii ni ya kudumu!' -
6:13 - 6:20Kwa hiyo mwaka mzima hadi leo,
sijawahi kukosa kipindi changu. -
6:20 - 6:26Kwa maambukizi ya njia ya mkojo,
nilipona kwa sababu tangu wakati huo, -
6:26 - 6:30Sijapata maambukizi hayo mpaka leo.
-
6:30 - 6:36Na kwa upande wa masomo yangu...
-
6:36 - 6:41Kama nilivyosema, nilipoteza tumaini langu
na hata nilitaka kuacha. -
6:41 - 6:47Kulikuwa na siku ambapo, asubuhi, sikutaka kuamka na kwenda kazini
-
6:47 - 6:51kwa sababu ilikuwa mbaya sana.
-
6:51 - 6:55Sikutarajia kupata alama nzuri
-
6:55 - 6:59kwa sababu mwisho wa mafunzo,
wanakutahini . -
6:59 - 7:07Na ukifaulu, utastahiki kufanya mtihani wa leseni kwa leseni yako ya kufanya kazi.
-
7:07 - 7:11Na kulikuwa na idara
ambazo zilinitisha sana, -
7:11 - 7:15kama vile ICU (Kitengo cha Wagonjwa Mahututi)
na Idara ya Dharura. -
7:15 - 7:17Haya ni maeneo muhimu sana.
-
7:17 - 7:23Kwa utukufu wa Mungu, nilimaliza
mafunzo yangu ya kazi kwa alama nzuri. -
7:23 - 7:31Nilipata A katika idara hizo ambazo
nilikuwa na matumaini kidogo ya kufuzu. -
7:31 - 7:38Nilijiambia, 'Nikipata C katika idara hii, nitakushukuru, Mungu.'
-
7:38 - 7:39Lakini Mungu alinipa A.
-
7:39 - 7:43Kwa hivyo nilipata A na B.
-
7:43 - 7:47Haya ni matokeo yangu.
-
7:47 - 8:03Alama ya jumla ya mafunzo yangu - nilipata 92.9%.
-
8:03 - 8:05Sina msononeko tena.
-
8:05 - 8:12Kwa kweli, msononeko uliniacha siku hiyo baada ya kumaliza Maombi ya Pamoja.
-
8:12 - 8:15Nilihisi amani sana.
-
8:15 - 8:24Ushauri wangu ungekuwa - hakuna kitu ambacho Mungu hawezi kukufanyia ukimkimbilia.
-
8:24 - 8:31Kwa kila suluhu, kila jibu, kimbilia Kwake, na hatakuangusha kamwe.
-
8:31 - 8:35Watu wanaweza kukukatisha tamaa, lakini Mungu
hawezi kamwe kukukatisha tamaa. -
8:35 - 8:39Na kwa wanafunzi - usikate tamaa.
-
8:39 - 8:48Kama mimi, watu waliniambia, 'Huna akili. Hutakiwi kuwa hapa.
-
8:48 - 8:50Ulichagua njia mbaya ya kazi.'
-
8:50 - 8:54Usiruhusu mawazo hasi kichwani mwako.
-
8:54 - 8:58Kuna kitu kizuri ambacho
Mungu anasema juu yako. -
8:58 - 9:01Ukimkimbilia Yeye, atakuonyesha
wewe ni nani hasa.
- Title:
- Je, unahangaika na MSONGO WA MAWAZO? USHUHUDA huu utakutia moyo!
- Description:
-
more » « less
Je, unapigana vita kichwani mwako na mawazo hasi yanayoendelea? Ushuhuda wa Tumpale kutoka Tanzania hakika UTAKUTIA MOYO! Baada ya kupokea maombi mtandaoni, hakupata tu uhuru kutoka kwenye mfadhaiko bali kuponywa kutokana na ugonjwa wa ovari ya poly-cystic na ukosefu wa usawa wa homoni, pamoja na mafanikio ya kitaaluma. Utukufu wote uwe kwa Mungu!
Ili kupokea maombi bila malipo kutoka kwa Ndugu Chris kupitia Zoom, wasilisha ombi lako la maombi hapa - https://www.godsheart.tv/zoom
➡️ Pata Kutiwa Moyo Kila Siku kwenye WhatsApp - https://godsheart.tv/whatsapp/
➡️ Kuwa Mshirika wa TV wa Moyo wa Mungu - https://godsheart.tv/partnership
➡️ Habari kuhusu Maombi ya Pamoja - https://godsheart.tv/interactive-prayer/
➡️ Jitolee kama Mtafsiri wa TV ya Moyo wa Mungu - https://godsheart.tv/translate/
➡️ Shirikisha ushuhuda wako - https://godsheart.tv/testimony
➡️ Jiunge na Ibada yetu ya Maombi ya Moja kwa Moja Jumamosi ya kwanza ya kila mwezi - https://www.youtube.com/godshearttv/live - Video Language:
- English
- Team:
God's Heart TV
- Duration:
- 09:32
| georgejbudeba edited Swahili subtitles for Struggling with DEPRESSION? This TESTIMONY will inspire you! | ||
| georgejbudeba edited Swahili subtitles for Struggling with DEPRESSION? This TESTIMONY will inspire you! | ||
| georgejbudeba edited Swahili subtitles for Struggling with DEPRESSION? This TESTIMONY will inspire you! | ||
| georgejbudeba edited Swahili subtitles for Struggling with DEPRESSION? This TESTIMONY will inspire you! | ||
| georgejbudeba edited Swahili subtitles for Struggling with DEPRESSION? This TESTIMONY will inspire you! |