-
-
Kwenye hii video, nitakufundisha
-
njia mpya ya kukokotoa gawanya,
-
hususani kwa namba ndefu.
-
Pia tutaona ni jinsi gani inavyofanya kazi.
-
Hivyo, hebu tukokotoe 96 gawanya kwa 4.
-
Nitaandika kitu tofauti kidogo.
-
Nitaandika 96 gawanya kwa ... Hivyo
-
naandika alama ngeni kidogo
-
kwa hapa, hiki kinachoifunika 96.
-
Lakini utaisoma hii kama 96 gawanya kwa 4.
-
Na nitakuonyesha kwa nini tunaiandika hivi.
-
Hii ndiyo njia inayotumika kukokotoa hesabu hii.
-
Hivyo, kitu cha kwanza tutakachokifanya hapa ni,
-
kujiuliza 4 inaingia kwa 9 mara ngapi?
-
Vizuri, tunafahamu kuwa 4 mara 2 ni sawa na 8, 4 mara 3
-
ni sawa na 12.
-
Hivyo, 3 itazidi.
-
Tutaivuka 9.
-
Hivyo, tunahitaji kuwa chini ya 9 lakini siyo namba ya chini zaidi.
-
Tunahitaji namba itakayotufikisha
-
kwenye 9 bila ya kuzidi.
-
Hivyo, itakuwa ni mara mbili.
-
4 mara 2 inakaribia 9.
-
Hivyo, 2 mara 4 tunapata?
-
vizuri, 2 mara 4 ni 8.
-
4 mara 2 ni 8.
-
au 2 mara 4 ni 8.
-
Na sasa, tunatoa.
-
Tunatoa 9 kwa 8.
-
Na tunapata 1.
-
Kisha tunashusha chini tarakimu nyingine ambayo ni 6.
-
Na kisha tunajiuliza ni ngapi mara
-
4 inaingia kwa 16?
-
Vizuri, tunaelewa kuwa 4 inaingia kwa 16
-
mara 4.
-
4 mara 4 ni 16.
-
Hivyo, 4 mara 4 tunapata 16.
-
Kisha tunazidisha 4 mara 4 tunapata 16.
-
Tunatoa.
-
Na 16 toa kwa 16, hatubakiwi na kitu.
-
Na hilo hapo juu ni jibu letu.
-
Bado inaonekana kushangaza.
-
Lakini hivi punde tutaona
-
ni jinsi gani inavyofanya kazi.
-
Tumepata 96 gawanya kwa 4 ni sawa na
-
natumia rangi tufauti.. ni sawa na 24.
-
Hebu simamisha video,
-
na utafakari ni jinsi gani inavyofanya kazi.
-
Ni kivipi muujiza huu ulete jibu sahihi hapa?
-
Unaweza kuihakiki.
-
4 mara 24, unapata 96.
-
Vizuri, nafikiri umeelewa hapo.
-
Kitu cha msingi hapa ni
-
kuzingatia thamani ya namba .
-
Na inakujulisha nini kinachoendelea
-
wakati tunapofanya hesabu yetu.
-
Tukiingalia 9 hapa,
-
hii 9 ni nafasi ya makumi.
-
Kwa hakika hii inawakilisha 90.
-
Inawakilisha makumi 9.
-
Hivyo, tunaweza kusema, ni ngapi mara
-
4 tunapata 90 kama tunazingatia vigawe vya 10?
-
Vizuri, inakwenda mpaka mara 20.
-
4 mara 20 ni 80.
-
Hivyo, tumesema 4 mara 20 ni 80.
-
Lakini bado tumebakiwa na 16.
-
Ukichukua 96 kutoa 80.
-
Unabakiwa na 16 gawanya kwa 4.
-
4 mara nne tunapata 16.
-
Vizuri sana,
-
mwanzo tulizidisha mara 20.
-
Kisha tukasema, hiyo haiwezi kutupatia
-
96.
-
Tukazidisha 4 kwa namba nyingine.
-
Na hiyo ikatupatia jawabu.
-