MUUJIZA USIOWEZEKANA KITABIBU!
-
0:00 - 0:06Tulikwenda kwenye vipimo vingine
na kwa utukufu wa Mwenyezi Mungu. -
0:06 - 0:12hakukuwa na virusi hata kidogo mwilini mwake,
jambo ambalo kitabibu haliwezekani. -
0:12 - 0:18Kwa Mungu hakuna lisilowezekana.
Kwa hiyo, huo ulikuwa muujiza kwetu. -
0:19 - 0:22USHUHUDA
TV YA MOYO WA MUNGU -
0:24 - 0:27Neema na amani kwenu nyote.
-
0:27 - 0:30Jina langu ni Fernando. Mimi ni mwalimu wa muziki.
-
0:30 - 0:34Na kando yangu ni mke wangu, Gina,
ambaye ni daktari. -
0:34 - 0:38Na hapa kuna mtoto wetu msichana, Gianna.
-
0:38 - 0:42Tunatoka Honduras,
umbali mrefu kutoka Kaskazini mwa Wales -
0:42 - 0:44lakini tuna furaha kuwa hapa pamoja nanyi nyote.
-
0:44 - 0:49Yote ilianza tulipotaka
kuanzisha familia. -
0:49 - 0:55Ilikuwa mwaka mmoja baada ya ndoa yetu, kwa hiyo tuliamua kuanza uchunguzi wetu wa kimatibabu.
-
0:55 - 1:04Uchunguzi wa kwanza wa kimatibabu uliripoti uchunguzi wa mke wangu.
-
1:04 - 1:09Ilikuwa ni virusi vinayoitwa HPV,
-
1:09 - 1:14ambayo ni virusi vinavyoweza kusababisha
saratani kwenye uterasi. -
1:14 - 1:16Na havitibiki.
-
1:16 - 1:23Kwa hivyo baada ya hapo, tulitaka
kumuona mtaalamu mwingine. -
1:23 - 1:28Kwa hivyo tuliendesha vipimo vingine, kama
biopsy na ultrasounds, -
1:28 - 1:34na iliripoti kidonda kikubwa
kwenye tumbo la uzazi la mke wangu. -
1:34 - 1:42Kwa hivyo hiyo ilisababisha athari kubwa sana
mioyoni mwetu. -
1:42 - 1:49Chaguo moja la matibabu ambalo tulikuwa nalo ni utaratibu unaoitwa conization,
-
1:49 - 1:57ambayo inajaribu kuondoa vidonda vyote
vilivyo kwenye uterasi. -
1:57 - 2:02Wakati mchakato huu ukifanyika,
tulianza kumlilia Mungu pia -
2:02 - 2:08na tukaanza kuutafuta uso wa Mungu kuhusu hali hii.
-
2:08 - 2:14Kwa hiyo, tulifanya utaratibu na pia tuliifikia TV ya Moyo wa Mungu.
-
2:14 - 2:19Kwa upande wangu, sauti ya hofu ilianza kunisemesha.
-
2:19 - 2:22Na pia, nilikuwa na wasiwasi sana juu ya afya ya mke wangu.
-
2:22 - 2:26Lakini tulisimama imara katika
Bwana wakati huo huo -
2:26 - 2:30na tulijua kwamba Mungu
angefanya jambo fulani. -
2:30 - 2:31Lakini ilikuwa ngumu sana.
-
2:31 - 2:39Nadhani, kwa upande wangu, hiyo ilikuwa moja ya changamoto ngumu sana katika maisha yangu.
-
2:39 - 2:46Tuliifikia TV ya Moyo wa Mungu, tukatuma ombi la maombi na timu ikawasiliana nasi
-
2:46 - 2:52wiki chache baadaye, na tukapokea
simu kutoka kwa Ndugu Chris. -
2:52 - 2:58Kwa hiyo wakati ukafika, na Ndugu Chris akatuombea kupitia simu.
-
2:58 - 3:05Na ninakumbuka kwamba nilihisi kutapika,
kwa hiyo nilianza kupokea ukombozi. -
3:05 - 3:09Na pia, nilikuwa nalia.
-
3:09 - 3:14Na mke wangu alihisi joto kwenye eneo la tumbo lake.
-
3:14 - 3:21Kwa hiyo, baada ya maombi, tulijihisi wepesi
na tukawa na amani ya moyo. -
3:21 - 3:25Kwa hiyo tulijua kwamba Mungu alikuwa ameanza
kufanyia kazi hali yetu. -
3:25 - 3:36Tulikwenda kwa vipimo vingine wa kufuatilia na tulipata matokeo wiki chache baadaye,
-
3:36 - 3:46na kwa ajili ya utukufu wa Mungu, hapakuwa na virusi katika mwili wake, jambo ambalo kimatibabu haliwezekani.
-
3:46 - 3:49Kwa Mungu hakuna lisilowezekana.
-
3:49 - 3:55Kwa hiyo huo ulikuwa muujiza kwetu;
hilo lilikuwa jibu la maombi yetu. -
3:55 - 4:01Hii ni ripoti ya kwanza ya matibabu
ambayo ilitolewa mnamo Juni 2021. -
4:01 - 4:08Kama unavyoona, kuna
jina la mke wangu, Gina. -
4:08 - 4:15Kuna maneno machache ya kiufundi, ya matibabu.
-
4:15 - 4:21Lakini ukiona karibu kwenye picha inayofuata,
-
4:21 - 4:27unaweza kuona virusi vimewekwa alama nyekundu.
-
4:27 - 4:37Kisha kwenye ripoti iliyofuata, ambayo ilitolewa mnamo Agosti 2021, miezi michache baadaye,
-
4:37 - 4:51inasema kwamba kuna utambuzi katika Kihispania wa 'Displasia Moderada/ NIC II'
-
4:51 - 4:55ambayo ina maana kwamba kulikuwa na uharibifu mkubwa katika uterasi yake.
-
4:55 - 4:57Hii ilikuwa kabla ya maombi.
-
4:57 - 5:04Lakini baada ya maombi, kama unavyoona sasa, hii ni ripoti ya tatu.
-
5:04 - 5:08Na ilitolewa mnamo Septemba 2022.
-
5:08 - 5:11Ilikuwa ni mchakato wa mwaka mmoja, kama unaweza kuona.
-
5:11 - 5:17Na utambuzi unasema kwa Kihispania 'negativo' ambayo ni hakuna ugonjwa.
-
5:17 - 5:24Sasa, unaweza kuona kwamba hakuna tiki kwenye kisanduku chochote, ambayo ina maana kwamba yuko huru kutokana na hilo.
-
5:24 - 5:34Baada ya sala hiyo, karibu miezi mitano baadaye, mke wangu alipata mimba.
-
5:34 - 5:41Na kwa kweli ilikuwa baraka kwa sababu ilikuwa maombi yetu, ndoto ya kuanzisha familia.
-
5:41 - 5:49Na sasa tuna mtoto wetu wa kike,
na sasa ana umri wa miezi 19. -
5:49 - 5:54Kila siku nauona mkono wa Mungu ninapomwona, ninapomtazama usoni.
-
5:54 - 5:57Na sasa naona ndoto hii ilitimia.
-
5:57 - 6:06Na bado ninashughulikia. Ninamaanisha, ana umri wa miezi 19 tu lakini ninahisi furaha sana, nimebarikiwa sana.
-
6:06 - 6:13Neema na amani kwenu nyote. Jina langu ni Gina na hapa kuna mume wangu Fernando
-
6:13 - 6:18na huyu ni binti yetu, Gianna.
Tunatoka Honduras. -
6:18 - 6:36Mnamo Juni 2021, nilifanya uchunguzi wa pap smear na matokeo yakaonyesha nilikuwa na virusi vya HPV.
-
6:36 - 6:42Na miezi miwili baadaye, nilifanya tena vipimo vilevile
-
6:42 - 6:48na matokeo yalionyesha sio
tu uwepo wa virusi hivi -
6:48 - 6:54lakini tatizo lilikuwa limeongezeka
na kusababisha vidonda vikali zaidi. -
6:54 - 7:00Vidonda vinavyosababishwa na virusi hivi
vilibeba hatari kubwa ya saratani. -
7:00 - 7:06Habari hizi ziligusa sana
maisha na ndoa zetu. -
7:06 - 7:12Kuzungumza kibinafsi, nilianza kuhoji.
-
7:12 - 7:16Ningejiuliza,
‘Kwa nini jambo hili linatupata? -
7:16 - 7:22Ikiwa sisi ni Wakristo, watoto wa Mungu,
kwa nini tunapita katika haya?' -
7:22 - 7:29Mimi ni daktari kitaaluma.
Kutokana na hili, hofu na mashaka viliongezeka -
7:29 - 7:35kwa sababu nilijua uzito wa utambuzi huu
-
7:35 - 7:44na jinsi hii ilivyoweka hatarini hamu yangu ya kuwa mama na ndoto yetu ya kupata watoto.
-
7:44 - 7:54Tulipokuwa tukitayarisha habari hizi, mimi na mume wangu tulianza kumlilia Mungu atuhurumie.
-
7:54 - 8:05Pia tulianza kutembelea madaktari, wataalamu kufanya vipimo zaidi vya matibabu - ultrasound, biopsy.
-
8:05 - 8:10Daktari pia alifanya utaratibu wa matibabu unaojulikana kama conization.
-
8:10 - 8:20Wakati wa mchakato huu, tuliendelea kuomba na kumlilia Mungu kwa muujiza.
-
8:20 - 8:26Kisha, tuliwasiliana na TV ya Moyo wa Mungu
na kutuma ombi letu la maombi. -
8:26 - 8:31Tulipokea simu kutoka kwa Ndugu Chris ambapo alituombea.
-
8:31 - 8:37Nakumbuka wazi siku hiyo.
Tulikuwa tumekaa chumbani kwetu. -
8:37 - 8:43Tulipokuwa tukipokea maombi,
nilihisi joto kali tumboni mwangu -
8:43 - 8:47na nilipata mguso kutoka kwa
Roho Mtakatifu moyoni mwangu. -
8:47 - 8:54Baada ya maombi, nilipata
amani isiyoelezeka -
8:54 - 9:02pamoja na imani na hakikisho kwamba Mungu alikuwa ameanza kufanya kazi katika mwili wangu na maisha yetu.
-
9:02 - 9:08Hakukuwa na woga tena au mawazo ya mashaka - amani tu mioyoni mwetu.
-
9:08 - 9:13Wiki chache baadaye, nilifanya mtihani wa smear tena.
-
9:13 - 9:19Na matokeo - kwa utukufu na heshima ya Yesu - yalikuwa hakuna ugonjwa.
-
9:19 - 9:29Tumbo langu lilikuwa safi! Hakukuwa na virusi tena na vidonda vya precancerous vilikuwa vimetoweka.
-
9:29 - 9:32Kitabibu, hii haiwezi kuelezewa.
-
9:32 - 9:38Virusi vya HPV, havina tiba –
lakini kwa Mungu hakuna lisilowezekana! -
9:38 - 9:45Matibabu tofauti ambayo mara nyingi hupewa mwanamke aliye na shida hii
-
9:45 - 9:48huhatarisha uwezo wa kupata mtoto.
-
9:48 - 10:00Katika kisa changu, utaratibu wa tiba ulihusisha kuondoa sehemu ya mlango wangu wa uzazi(cervix)
-
10:00 - 10:05ili kuondoa sehemu kubwa ya vidonda.
-
10:05 - 10:10Kwa sababu hiyo, hatari ya
kuharibika kwa mimba iliongezeka. -
10:10 - 10:16Miezi mitano baadaye baada ya Mungu
kutushangaza kwa muujiza huu, -
10:16 - 10:21Alitubariki zaidi kwa
habari kwamba nilikuwa mjamzito. -
10:21 - 10:29Hii ilithibitisha kwa mara nyingine kwamba
Mungu alikuwa amefanya kazi tumboni mwangu. -
10:29 - 10:34Nilikuwa na mimba ya kawaida kwa utukufu wa Mungu bila matatizo yoyote.
-
10:34 - 10:38Ulikuwa msimu ambao tungeweza kufurahia
tukiwa wenzi wa ndoa. -
10:38 - 10:44Na kwa utukufu wa Yesu, huyu hapa binti yetu Gianna, miezi 19 baadaye.
-
10:44 - 10:49Nilijifungua kawaida bila matatizo.
-
10:49 - 10:54Kwa hiyo, tunamshukuru sana Mungu kwa sababu
amekuwa mwema sana kwetu. -
10:54 - 11:06Ushauri wangu kwa kila anayetazama ni kutozingatia matatizo yako; mzingatie Yesu.
-
11:06 - 11:13Hali hii ilinitoa katika
hali ya faraja niliyokuwa nayo kiroho -
11:13 - 11:15na kunivuta karibu na Yesu.
-
11:15 - 11:23Kwa hivyo ushauri wangu ni - katikati ya
hali yako, ugonjwa au shida, -
11:23 - 11:29mkimbilie Mungu na ichukue kama fursa
ya kukua katika maisha yako ya kiroho. -
11:29 - 11:37Kwanza kabisa, nataka kutoa
ushauri kwa ndoa. -
11:37 - 11:42Nitakushauri kwamba unapokumbana na tatizo, jaribu au hali fulani,
-
11:42 - 11:46kukaa pamoja na kumkimbilia Mungu pamoja.
-
11:46 - 11:53Sio wakati wa kunyoosheana vidole,
kujisikia hatia au kufikiria, 'Itakuwaje kama?' -
11:53 - 11:56Hapana, mkaribie Mungu tu na mkae pamoja.
-
11:56 - 12:04Kwa sababu ukifanya hivi, basi baada ya jaribu, ndoa yako itaimarika, kama tulivyo sasa.
-
12:04 - 12:10Kwa hiyo, hilo lilitusaidia kukua kiroho na kunisaidia kuwa karibu zaidi na mke wangu.
-
12:10 - 12:14Kwa hiyo huo ni ushauri ambao ningetoa
kwa wanandoa. -
12:14 - 12:22Kwa neema ya Mungu, tumekuwa tukijitolea na God's Heart TV kama watafsiri katika Kihispania.
-
12:22 - 12:28Kwa hivyo, imekuwa baraka kwa kweli kwetu kuwa sehemu ya timu ya kujitolea.
-
12:28 - 12:34Na nitawatia moyo watazamaji wote wanaozungumza Kiingereza na lugha nyingine
-
12:34 - 12:41kutoa talanta zao kwa Mungu na kufanya kazi katika miradi yake, kwa sababu hii ni baraka kweli.
-
12:41 - 12:46Pia tumekuwa tukijitolea katika miradi ya kutoa misaada nchini Honduras.
-
12:46 - 12:50Hii inatusaidia katika maisha yetu ya kiroho.
-
12:50 - 12:56Imani yetu inakua na kuinuliwa kila tunapofanya kazi hii.
-
12:56 - 13:03Unapotafsiri, unatazama video na kusoma mahubiri mara nyingi,
-
13:03 - 13:05na hii inakusaidia wewe pia.
-
13:05 - 13:11Pia unasoma
Neno la Mungu hata zaidi. -
13:11 - 13:14Kwa hivyo, nadhani hii ni baraka kweli.
-
13:14 - 13:18Nitawahimiza watazamaji wote walio na talanta hii kutafsiri
-
13:18 - 13:23ili tu kutoa talanta zao kwa Mungu na
kufanya hivi kwa utukufu wa Mungu.
- Title:
- MUUJIZA USIOWEZEKANA KITABIBU!
- Description:
-
more » « less
Mungu aliwabariki Fernando na Gina kutoka Honduras kwa muujiza wa ajabu wa uponyaji, ukifuatwa na zawadi ya mtoto wa kike! Tunaomba ushuhuda wao utakutia moyo na kukuhamasisha kuamini kwamba kwa Mungu, HAKUNA lisilowezekana.
Ili kupokea maombi bila malipo kutoka kwa Ndugu Chris kupitia Zoom, wasilisha ombi lako la maombi hapa - https://www.godsheart.tv/zoom
➡️ Pata Kutiwa Moyo Kila Siku kwenye WhatsApp - https://godsheart.tv/whatsapp/
➡️ Kuwa Mshirika wa TV wa Moyo wa Mungu - https://godsheart.tv/partnership
➡️ Habari kuhusu Maombi ya Pamoja - https://godsheart.tv/interactive-prayer/
➡️ Jitolee kama Mtafsiri wa TV ya Moyo wa Mungu - https://godsheart.tv/translate/
➡️ Shirikisha ushuhuda wako - https://godsheart.tv/testimony
➡️ Jiunge na Ibada yetu ya Maombi ya Moja kwa Moja Jumamosi ya kwanza ya kila mwezi - https://www.youtube.com/godshearttv/live - Video Language:
- English
- Team:
God's Heart TV
- Duration:
- 13:53
| georgejbudeba edited Swahili subtitles for MEDICALLY IMPOSSIBLE MIRACLE! | ||
| georgejbudeba edited Swahili subtitles for MEDICALLY IMPOSSIBLE MIRACLE! |