-
-
Sio mbaya kufanya mazoezi ya kutosha, kwenye video hii
-
nitafanya hesabu nyingi za
-
kugawanya njia ndefu.
-
Na kama una 2, 292 gawanya kwa 4.
-
Na sijui ni kwanini wanasema kugawanya kwa njia ndefu,
-
na tumeiona hii kidogo kwenye video iliyopita.
-
Sikuiita gawanya njia ndefu, ila nadhani sababu ni
-
kwamba inachukua muda mrefu au inachukua sehemu kubwa ya
-
kipande chako cha karatasi.
-
Kadri unavyoendelea ,unaweza ukawa na kitu hiki, huu mkia mrefu
-
ambao huleta maswali.
-
Hizi ni baadhi ya sababu nilizonazo kichwani kwanini
-
zinaitwa kugawanya njia ndefu.
-
Lakini tumeona kwenye video zilizopita kuna njia ya kukokotoa
-
hesabu ya kugawanya kwa kujua jedwali la kuzidisha
-
mpaka 10 mara 10 au 12 mara12.
-
Lakini kwa kupitia tena, hii ni sawa na
-
2, 292 gawanya kwa 4.
-
Na ni kitu kile kile, na yawezekana
-
hujaona kitu hiki kabla, kama 2, 292 gawanya kwa 4.
-
Sentensi hii na hii zote zinalingana
-
kwa viwango sawa.
-
Na unaweza sema inaonekana kama sehemu
-
ikitokea tayari umeshaiona sehemu.
-
Na hiyo ndio maana yake.
-
Ni sehemu.
-
Lakini tutaenda na mpangilio huu na baadae
-
kwenye video zijazo tutaangalia njia nyingine ya kugawanya.
-
Hebu tufanye swali hili.
-
Je 4 inaingia kwenye 2 mara ngapi?
-
Haingii kwenye 2 hata kidogo, tuendelee
-
nitabadilisha rangi.
-
Tuende kwenye 22.
-
Je 4 inaingia kwenye 22 mara ngapi?
-
Tuangalie.
-
4 mara 5 ni 20.
-
4 mara 6 ni 24.
-
Hivyo 6 inazidi.
-
Hivyo 4 inaingia kwenye 22.
-
5 mara 4 ni 20.
-
Kutakuwa na itakayobakia
-
Kisha tunatoa 22 toa 20.
-
Itakuwa 2.
-
Kisha unashusha chini hii 9.
-
Na umeona kwenye video iliyopita hii ina maanisha nini.
-
Ulipoandika hii 5 hapa juu--Kumbuka tuliandika
-
sehemu ya mamia.
-
Hivyo hii ni 500.
-
Lakini kwenye video hii nitakwenda kusisitiza zaidi kwenye
-
hatua, na unaweza kufikiria zaidi maana yake
-
kutokana na pale ninapoandika namba.
-
Ninaamini hizi hatua zote
-
utazielewa mwishoni mwa video hii
-
Hivyo tumeshusha chini 9.
-
4 inaingia mara ngapi kwenye 29?
-
Inaingia mara 6.
-
4 mara 7?
-
4 mara 7 ni 28.
-
Hivyo inangia mara saba.
-
4 mara 8?
-
4 mara 8 ni 32, hivyo haiwezi kuingia kwenye 8 hivyo
-
itaingia mara saba.
-
4 inaingia kwenye 29 mara 7.
-
7 mara 4 ni 28.
-
29 toa 28 ili kupata inayobakia
-
kwenye swali letu ambayo ni 1.
-
Na sasa tutashusha hii 2.
-
Tunakwenda kushusha chini na unapata 12.
-
4 inaingia mara ngapi kwenye 12?
-
Hii ni rahisi.
-
4 mara 3 ni 12.
-
4 inaingia kwenye 12 mara 3.
-
3 mara 4 ni 12.
-
12 toa 12 ni 0.
-
Hatuna iliyobaki.
-
Hivyo 4 inaingia mara 573 kwenye 2, 292.
-
Hivyo hii 2, 292 gawanya kwa 4 ni sawa na 573.
-
Au tunasema hiki kitu hapa ni sawa na 573.
-
Tufanye mifano mingine zaidi.
-
Tufanye mifano zaidi.
-
Nitatumia rangi nyekundu.
-
Tuseme tulikuwa na 7 inayoingia kwenye 6, 475.
-
Labda inaitwa njia ndefu kwasababu unaiandika vizuri na
-
kwa urefu na unapata huu mstari.
-
Sijui.
-
Kuna sababu nyingi za kwanini inaitwa njia ndefu.
-
Hivyo unasema 7 inaingia kwenye 6 mara sifuri.
-
Hivyo tunahitaji kuendelea mbele.
-
Hivyo tunakwenda kwenye 64.
-
7 inaingia kwenye 64 mara ngapi?
-
Tuangalie.
-
7 mara 7 ni?
-
Hii ni ndogo sana.
-
Ngoja niifikirie kidogo.
-
7 mara 9 ni 63.
-
Hii iko karibu zaidi.
-
Na kisha 6 mara 10 itakuwa kubwa sana.
-
7 mara 10 ni 70.
-
Hii ni kubwa sana.
-
Hivyo 7 inaingia kwenye 64 mara 9.
-
9 mara 7 ni 63.
-
64 toa 63 kupata inayobaki ambayo ni 1.
-
Shusha 7 chini.
-
7 inaingia mara ngapi kwenye 17?
-
7 mara 2 ni 14.
-
KIsha saba mara 3 ni 21.
-
Hivyo 3 inazidi
-
Hivyo 7 inaingia mara mbili kwenye 17.
-
2 mara 7 ni 14.
-
17 toa 14 ni 3.
-
Kisha tunashusha 5.
-
-
Na 7 inaingia mara ngapi kwenye 35?
-
Hii 7 kwenye jedwali la kuzidisha mara 5.
-
5 mara 7 ni 35.
-
-
Unaendelea.
-
Hivyo inabaki 0.
-
Hivyo mifano yote niliyofanya mpaka sasa sina niliyobakiza.
-
Hebu tufanye nyingine ambayo labda inaweza ikawa na inayobakia.
-
Na kuhakikisha tuna itakayobakia
-
nitatengeneza swali.
-
Ni rahisi kutengeneza swali la itakayobakia
-
kuliko swali lisilo na itakayobakia.
-
Tuchukulie ninataka kuigawa tatu kwenye ---
-
1, 735092.
-
Hii itakuwa nzuri.
-
Kama tunaweza kufanya swali hili basi hakuna kitakachotushinda.
-
Hivyo 1, 735,092.
-
Hii ndio tunaigawanya kwa 3.
-
-
Sina uhakika kama hii tutapata itakayobakia.
-
Kwenye video zijazo nitakuonyesha namna ya kujua kama
-
kitu kinaweza gawanywa kwa 3.
-
Tunaweza kuifanya sasa.
-
Tunaweza kujumlisha hizi tarakimu zote.
-
1 jumlisha 7 ni 8.
-
8 jumlisha 3 ni 11.
-
11 jumlisha 5 ni 16.
-
16 jumlisha 9 ni 25.
-
25 jumlisha 2 ni 27.
-
Hivyo namba hii inagawanyika kwa 3.
-
Ukijumlisha tarakimu zote unapata 27.
-
Na kisha unaweza kujumlisha ---2 jumlisha 7 ni 9.
-
Hivyo hii inagawanyika kwa 9.
-
Hii ndio mbinu ambayo inafanya kazi kwa 3 tu.
-
Hivyo namba hii inagawanyika kwa 3.
-
Ngoja nibadilishe kidogo, ili
-
isigawanyike kwa 3.
-
Ngoja niifanye kwenye 1.
-
Sasa namba hii haita gawanyika kwa 3.
-
Ninataka namba ambayo mwishoni
-
nitakuwa na itakayobaki.
-
Ili uone itakavyokuwa.
-
Hebu tufanye hii.
-
3 inaingia kwenye 1 mara sifuri.
-
Tunaweza kuendelea.
-
Unaweza kuandika 0 hapa, na kuizidisha, lakini hiyo
-
inaweza kukuchanganya.
-
Hivyo tunasongeza moja upande wa kulia.
-
3 inaingia mara ngapi kwenye 17?
-
3 mara 5 n i 15.
-
3 mara 6 ni 18 hii ni kubwa.
-
Hivyo 3 inaingia kwenye 17 mara 5.
-
5 mara 3 ni 15.
-
Tunatoa.
-
17 toa 15 ni 2.
-
Tunashusha 3 chini.
-
3 inaingia mara ngapi kwenye 23?
-
3 mara 7 ni 21.
-
3 mara 8 ni kubwa.
-
Ni sawasawa na 24.
-
Hivyo 3 inaingia kwenye 23 mara 7.
-
7 mara 3 ni 21.
-
Tunatoa.
-
23 toa 21 ni 2.
-
Tunashusha chini namba inayofuata.
-
Tunashusha 5.
-
Nadhani unaelewa kwanini inaitwa gawanya njia ndefu.
-
Tunashusha 5.
-
3 inaingia mara ngapi kwenye 25?
-
3 mara 8 inakaribia lakini 3 mara 9 inazidi sana.
-
Inaingia mara 8.
-
8 mara 3 ni 24.
-
Ninaishiwa nafasi sasa.
-
Unatoa unapata 1.
-
25 toa 24 ni 1.
-
Tunaweza kushusha chini hii 0.
-
-
Na unapata 3 ambayo inaingia mara ngapi kwenye 10?
-
Hii ni rahisi.
-
Inaingia mara 3.
-
3 mara 3 ni 9.
-
Hii inakaribia 10.
-
3 mara 3 ni 9.
-
10 toa 9, nitakuwa nikivuta kwenda juu
-
na kushuka chini kidogo.
-
10 toa 9 ni 1, kisha tunashusha namba inayofuata.
-
Ninaishiwa rangi.
-
Ninaweza kuishusha hii 9.
-
3 inaingia mara ngapi kwenye 19?
-
6 ndio inayokaribia.
-
Inatupa 18.
-
3 inaingia mara 6 kwenye 19.
-
6 mara 3-- ngoja nishushe chini.
-
6 mara 3 ni 18.
-
19 toa 18--hii pia tunatoa.
-
19 toa 18 ni 1 na tunakaribia kumaliza.
-
Nitarudia kutumia rangi ya pinki .
-
Tunashusha chini hii 1.
-
3 inaingia mara ngapi kwenye 11?
-
Hii ni mara 3 kwa sababu 3 mara 4 ni kubwa.
-
3 mara 4 ni 12, hivyo hii ni kubwa.
-
Hivyo inaingia mara 3.
-
Hivyo 3 inaingia mara 3 kwenye 11.
-
3 mara 3 ni 9.
-
Kisha tunatoa tunapata 2.
-
Na hakuna kilichobakia kushusha chini.
-
Tukiangalia hapa juu hakuna kilichobakia
-
kushusha chini, hivyo tumemaliza.
-
Tumebakiwa na 2 baada ya
-
kufanya hesabu nzima.
-
Hivyo jibu, 3 inaingia kwenye 1, 735,091--
-
mara 578,363 na kubaki 2.
-
Na hii 2 iliyobakia ni ile tuliyoipata huku chini.
-
Ninaamini umeelewa na unaweza kukokotoa
-
hesabu zaidi za kugawanya.
-
Na pia kupitia zoezi hili, unaweza kukubali kwanini
-
inaitwa kugawanya njia ndefu.
-