-
Msingi wa hesabu za sehemu.
-
Kwenye hii video tutazungumzia
-
hesabu za sehemu.
-
Tunaweza kuizungumzia sehemu kwa njia nyingi.
-
Kwanza tutaanza na msingi mama.
-
Tuchukulie nina mraba.
-
Mzima hapa.
-
Hebu! tuandike.
-
Huu hapa ni,
-
Mraba mzima.
-
Nitachokifanya ni kuugawa kwenye vipande vinne vilivyo sawa.
-
Kwanza nagawa kwa sehemu mbili zilizo sawa,
-
ninapokata kwa mara ya pili,
-
Naugawa kwenye sehemu nne zilizo sawa.
-
Hivyo kuna vipande vinne vilivyo sawa.
-
Na sasa nitakwenda
-
kuchagua kipande kimoja,
-
ambacho ni hiki hapa.
-
Ninachokichagu.
-
Swali ni kwamba, Je, ni sehemu gani ya mraba
-
kwa kipande nilicho weka kivuli chekundu?
-
Vizuri, ni kimoja kwa vipande vinne vilivyo sawa, tupo sawa?
-
Nimetia kivuli kimoja kati ya vipande vinne.
-
Hivyo tutaiandika kama.
-
Kipande hiki kinawakilisha 1/4 ya umbo zima.
-
Pia tunaweza kufanya kwa kutumia njia mbili.
-
Chukulia hiki ni kimoja miongoni mwa vipande vinne vilivyo sawa,
-
pia unaweza kuchukua umbo zima gawa kwa 4
-
itakupa kiasi hiki.
-
Hebu! tufanye nyingine.
-
Tutafute namna ya
-
kuwakilisha 1 juu ya 8, hivyo 1 juu ya 8.
-
Tutaligawanya lote hili,
-
ambalo ni mstatili.
-
Tutaugawa kwenye vipande 8 vilivyo sawa.
-
Hebu! tuanze.
-
Hapa nagawa kwa vipande viwili vilivyo sawa.
-
Unaweza kuona vizuri hapo.
-
Kisha navigawa kwenye vipande viwili vilivyo sawa,
-
ilikupata vipande vinne vilivyo sawa.
-
Na ninapogawa vipande vyote hivi
-
kuwa vipande viwili vilivyo sawa, nitakuwa na vipande 8 vilivyo sawa.
-
Inaonekana haviko sawa.
-
Kwa sababu nimechora kwa mkono,
-
lakini natumai umeona lengo.
-
Sasa nina vipande 8 vilivyo sawa.
-
Nakwenda kuchagua kimoja.
-
Hiyo itawakilisha 1/8.
-
Nachagua kipande chochote kile,
-
Naanza na hiki hapa,
-
na siyo lazima kuanza na cha kwanza.
-
Kimraba hiki,
-
nachokiwekea kivuli chekundu kinawakilisha 1/8 ya umbo .
-
Hebu! tuangalie mifano ifuatayo;
-
nimetia vivuli hapo.
-
Hebu! simamisha video.
-
unaweza ukatumia karatasi,
-
ilikutambua kwenye umbo la zambarau, je
-
ni sehemu gani inayowakilishwa na kipande chekundu?
-
Unapotazama kipande cha bluu kwenye hili umbo,
-
je, kipande chekundu kinawakilisha sehemu gani ya umbo?
-
Unapoitazama hii pembe tatu,
-
je, kipande hiki chekundu ni sehemu gani ya umbo?
-
Hebu! simamisha video kwanza.
-
Hebu tuangalie sasa.
-
Tukianza na huu mstatili,
-
tunavipande vitatu sawa, tulichotia kivuli ni kimoja .
-
Mstatili huu,
-
unawakilisha 1/3 ya umbo.
-
Sasa,
-
Hili linalofuatia hapa
-
ni duara, tunavipande 1, 2, 3, 4, 5
-
vilivyo sawa.
-
Na tulichotia kivuli ni kimoja kati ya vipande vitano.
-
Hivyo kipande hiki kidogo kinawakilisha 1/5.
-
Hiki hapa ni 1/5 ya umbo zima.
-
Na hili hapa linavutia.
-
Unaweza kusema nina vipande vinne,
-
kisha nikatia kivuli kimoja.
-
Hivyo kitawakilisha 1/4.
-
Lakini kumbuka, linapaswa kuwa na vipande vinne vilivyo sawa.
-
Tunaliona vizuri kabisa ,
-
kipande hiki hapa
-
hakina ukubwa sawa, tukilinganisha na kipande hiki na hata hiki
-
hapa.
-
Hivi siyo sipande vinne vilivyo sawa.
-
Hivyo, hatuwezi kusema hii ni 1/4 ya pembe tatu.
-
Huwezi kusema hivyo.
-