Hotuba ya Steve Jobs kwenye Sherehe ya Mahafali, Chuo Kikuu cha Stanford Mwaka wa 2005
-
0:06 - 0:08[Chuo Kikuu cha Stanford www.stanford.edu]
-
0:08 - 0:13Mtangazaji: Kipindi hiki kimewaletea na Chuo Kikuu cha Stanford. Tafadhali wasiliana nasi kwa stanford.edu
-
0:15 - 0:22[upigaji makofi]
-
0:22 - 0:23Steve Jobs: Asanteni
-
0:25 - 0:27[Steve Jobs - Mkurugenzi Mkuu Apple na Pixar Animation]
-
0:27 - 0:32Ni heshima kwangu kuwepo na nyinyi katika sherehe ya mahafali ya kutunuku shahada kutoka katika chuo kikuu ambacho ni kimojawapo bora katika dunia nzima.
-
0:32 - 0:35[ukelele wa kufurahia]
-
0:36 - 0:46Kusema kweli mimi sijatunukiwa shahada ya chuo kikuu na hii ni mara yangu ya kwanza kuhudhuria mahafali yoyote.
-
0:46 - 0:48[vicheko]
-
0:48 - 0:54Leo naomba niwasimulie visa vitatu vilivyotokea maishani mwangu. Vitatu tu, basi.
-
0:55 - 0:59Cha kwanza ni juu ya kuunganisha nukta.
-
1:01 - 1:08Niliacha masomo katika Chuo cha Reed baada ya muda wa miezi sita za kwanza katika mwaka wa kwanza, halafu nikakaa kama mgeni kwa muda wa miezi kumi na nane hivi kabla ya kusimamisha masomo kabisa.
-
1:09 - 1:11Kwa nini niliacha masomo?
-
1:12 - 1:14Sababu inatangulia kuzaliwa kwangu.
-
1:15 - 1:21Mama mzazi yangu alikuwa msichana hajaolewa alikuwa akitimiza shahada ya uzamili akaamua niwe mtoto wa kupanga.
-
1:22 - 1:26Alikuwa na msimamo wa dhati nilelewe na watu waliotimiza shahada ya chuo kikuu.
-
1:26 - 1:31Kwa hivyo mpango ukafanyika niasiliwe na mwanasheria na mkewe.
-
1:32 - 1:37Isipokuwa nilipoibuka mtoto wa kiume dakika la mwisho wakaamua wanataka mtoto wa kike.
-
1:38 - 1:42Kwa hivyo wazazi wangu walioandikwa katika orodha ya wanaosubiri kumwasili mtoto walipigiwa simu usiku wa manane na wakaulizwa:
-
1:43 - 1:49"Tumepata mtoto wa kiume asiyetarajiwa; mnamtaka?"
Wakajibu: "Bila shaka." -
1:51 - 1:58Baadaye mama mzazi yangu aligundua mama yangu alikuwa hajamaliza chuo kikuu huku mumewe baba yangu hajamaliza shule ya sekondari.
-
1:59 - 2:02Akakataa kutia sahihi hati maalum ya kuasiliwa.
-
2:03 - 2:12Baada ya miezi michache kupita akakubali shingo upande kutokana na ahadi ya wazazi wapya ya kuwa mimi nitasoma chuo kikuu. Hayo ndiyo yalikuwa mwanzo wa maisha yangu.
-
2:14 - 2:21Baada ya miaka kumi na saba kupita nilianza chuo kikuu lakini katika ushamba wangu nikachagua chuo ghali karibu sawa na Stanford.
-
2:22 - 2:27Pesa zote za akiba ya wazazi wangu tabaka yao ya wafanya kazi, zilitumika kulipia ada zangu za chuo kikuu.
-
2:27 - 2:30Baada ya muda wa miezi sita sikuona thamani ya masomo hayo.
-
2:30 - 2:36Sikuwa na mpango wa maisha mbali na uwezo wa chuo kunisaidia katika kufafanua mpango upi unanifaa zaidi.
-
2:37 - 2:41Huku nikitumia pesa zote za akiba ya maisha ya wazazi wangu.
-
2:42 - 2:47Basi nikakata shauri kuachana na masomo nikiamini mambo yatakuwa shwari.
-
2:47 - 2:52Wasiwasi ilinikumba wakati huohuo lakini sasa nikilitafakari shauri hilo ni miongoni mwa yale bora katika maisha yangu.
-
2:53 - 2:54[vicheko]
-
2:54 - 2:59Pindi tu nilipoachana sikulazimishwa kuchukua madarasa yale ambayo hayakunivutia.
-
3:00 - 3:04Nikaenda kwa yale yaliyovutia kwangu.
-
3:05 - 3:14Sikuwa na maisha ya starehe. Sikuwa na chumba katika bweni. Ilibidi nilale sakafuni katika vyumba vya marafiki. Nilikuwa nikiokota chupa kupata senti za kununulia chakula.
-
3:14 - 3:21Kila Jumapili mimi hutembeza maili saba ili nipata lishe maalum katika hekalu ya Wahindi wafuasi wa dini ya Hare Krishna.
-
3:22 - 3:23Niliipenda mno.
-
3:24 - 3:30Mengi niliyowahi kutokana na upekuzi wangu pamoja na uwezo wangu kuelewa yakawa adimu nyakati za baadaye.
-
3:30 - 3:31Hebu, nitoe mfano mmoja:
-
3:33 - 3:38Wakati huo Chuo cha Reed kilikuwa na ufundisho bora wa utaalamu wa maandiko kuliko vyuo vyote vingine nchini.
-
3:38 - 3:45Kwenye eneo la chuo kila tangazo, kila kitambulisho kwenye mitoto ya meza kilichorwa vizuri sana.
-
3:45 - 3:52Kwa sababu nimeshajitoa masomoni sikulazimishwa kuchukua madarasa yanayotakiwa na nikaamua kuchukua darasa la utaalamu wa maandiko nijifunze jinsi ya kufanya.
-
3:53 - 3:59Nilijifunza aina za chapa mifano ni serif na sans serif, juu ya upimaji nafasi katikati ya michanganyiko tofauti ya herufi,
-
4:00 - 4:02na juu ya ukamilifu wa utaalamu wa maandiko, kitu gani kinaleta ukamilifu.
-
4:03 - 4:11Kujifunza huko kulikuwa kuzuri, kwenye usanaa usio na kujivuna mbali na mazingira ya kisayansi, kwangu mimi nilivutiwa kupindukia.
-
4:12 - 4:16Sikuwa na matumaini ya kuyatumia masomo hayo katika kazi nitakayofanya,
-
4:17 - 4:23Lakini baada ya muda wa miaka kumi kupita tulipokuwa tunabunia tarakilishi ya kwanza aina ya Mactintosh nikafikiria upya mafundisho hayo.
-
4:23 - 4:29Tulitumia kabisa katika ubunaji wa Mac ambayo ilikuwa tarakilishi ya kwanza kuwa na utaalamu mzuri wa maandiko.
-
4:29 - 4:32Nisingeli kuwa mgeni katika darasa hilo nilipokuwa ninahangaika kwenye chuo,
-
4:32 - 4:37tarakilishi iitwayo Mac haikungali kuwa na aina nyingi za herufi wala herufi zenye uwiano wa nafasi za katikati zao.
-
4:37 - 4:42Na kwa sababu Windows iliiga Mac haielekei tarakilishi za kibinafisi zozote zingekuwa nazo kamwe.
-
4:42 - 4:49[vicheko na upigaji makofi]
-
4:50 - 4:54Nisipongeliachana na masomo singalipitia darasa lile la utaalamu wa maandiko.
-
4:54 - 4:58matokeo yake tarakilishi ya kibinafsi hazingekuwa na vivutio kiasi zinazokuwa nazo.
-
4:58 - 5:02Bila shaka ilikuwa haiwezekani kuunganisha nukta zitakazokuja mambo ya usoni nilipokuwa chuoni.
-
5:02 - 5:06Lakini mambo yakadhihirika kweupe nikirudia nyuma baada ya muda wa miaka kumi kupita.
-
5:07 - 5:12Kutia mkazo kauli hiyo, huwezi kuunganisha nukta za mambo ya usoni; ni zile tu zilizokwisha fanyika ambazo zinaweza kuzingatiwa ziunganishwe,
-
5:12 - 5:16Lazima uamini nukta za baadaye zitaunganika katika maisha yako ya baadaye.
-
5:16 - 5:21Sharti uwe na uaminifu wa huenda moyo wako, majaliwa, maisha, hulka zako, na kadhalika.
-
5:21 - 5:27Kwa sababu kuamini nukta zitaunganika baadaye kutakutilia moyo na imani kupiga njia uliyoinyoshea wewe mwenyewe.
-
5:27 - 5:32Hata ukifuata njia isiyo ya kawaida, uaminifu ndio utakunyoshea.
-
5:38 - 5:42Kisa changu cha pili ni juu ya upendo na kukosa upendo.
-
5:43 - 5:48Mimi nilibahatika - nilipata kujua ninavyopenda kufanya nikiwa bado mvulana.
-
5:48 - 5:51Mimi pamoja na rafiki yangu jina lake Woz tulianzisha kampuni la Apple kwenye kibanda cha gari nyumbani kwao wazazi wangu na mimi nikiwa na umri wa miaka ishirini.
-
5:51 - 5:59Tulifanya kazi kwa bidii na baada ya muda wa miaka kumi kampuni ya Apple iliyoanzia na watu wawili sisi tukiwa kwenye kibanda, ilikua kupata thamani ya dola bilioni mbili ikiwa na waajiriwa zaidi ya elfu nne.
-
6:00 - 6:05Tulikuwa tumetoa maumbile yetu bora - Macintosh, mwaka mmoja kabla, nami nikipata umri wa miaka thelathini.
-
6:06 - 6:07Kisha nikafukuzwa kazini.
-
6:09 - 6:11Je, inawezaje kufukuzwa kutoka kampuni uliyoanzisha wewe mwenyewe?
-
6:12 - 6:18Basi kama kampuni ya Apple ilivyoendelea kukua tukaajiri mtu mwenye kipaji kizuri kuongoza kampuni akiwa na mimi,
-
6:18 - 6:21na mwaka wa kwanza mambo yakawa shwari.
-
6:21 - 6:25Halafu baada ya hapo mitazamo yetu ikaanza kutengana hatimaye tukafarakana.
-
6:25 - 6:28Tulipofarakana baraza letu la wakurugenzi wakamuunga mkono yeye.
-
6:28 - 6:32Kwa hivyo nikiwa na umri wa miaka thelathini nilifukuzwa kazi bayana ikatangazwa kwenye magazeti.
-
6:33 - 6:37Kitu kilichokuwa kitovu cha maisha yangu nikiwa mtu mzima kimekwisha, nami nikadhoofika.
-
6:38 - 6:40Kwa muda wa miezi michache, kweli nilikuwa sikujua la kufanya.
-
6:41 - 6:47Niliona nimewasikitisha wale wajasiriamali wa kizazi kilichotangulia - nikashindwa kubeba amali ilyonipasa niibebe.
-
6:48 - 6:53Tulikutana na David Packard pamoja na Bob Noyce nikaomba radhi kwa kuharibu mambo.
-
6:54 - 6:58Kushindwa kwangu kulijulikana na wengi hata nilifikiri kukimbia Bonde.
-
6:58 - 7:03Lakini katika mwendo polepole nilitanabahi ya kuwa bado niliipenda kazi yangu.
-
7:04 - 7:11Mambo yaleyale ya mabadiliko pale Apple hayajaubadilisha upendo wangu hata kidogo.
-
7:12 - 7:13Kwa hivyo basi nikaamua kuanzia upya.
-
7:14 - 7:20Sikufahamu wakati huohuo mambo yakawa kufukuzwa kwangu Apple kulinifanyia mema kwa kiwango cha juu.
-
7:20 - 7:27Uzito ulionitwisha wa kufaulu kwangu ulichukuliwa na urahisi wa kuwepo mwanzoni kwa mara nyingine, nikiwaza na kuwazua.
-
7:28 - 7:30Niliachiliwa huru kuanzisha muda wa ubunaji ulionufaika zaidi katika maisha yangu yote.
-
7:31 - 7:35Katika miaka mitano iliyofuata nilianzisha kampuni jina lake, NeXT, nyingine jina lake Pixar,
-
7:36 - 7:39nikampenda kwa dhati mwanamke wa aina yake akawa mke wangu.
-
7:39 - 7:48Kampuni Pixar ikabunia sinema ya tarakilishi ya katuni hai ya kwanza katika dunia iitwao Toy Story halafu sasa Pixar imefaulu kushinda kampuni za katuni hai zote katika dunia.
-
7:48 - 7:49[upigaji makofi na ukelele wa kufurahia]
-
7:49 - 7:55Katika mabadiliko hayo ya matukio yasiyo na kifani, kampuni ya Apple ilinunua kampuni ya NeXT nami nikarudia Apple,
-
7:55 - 7:59huku teknolojia iliyoundwa kampuni ya NeXT ikawa chimbuko la mvuvumko wa Apple wa leo hii.
-
7:59 - 8:03Isitoshe mimi pamoja na mke wangu tumebarikiwa na familia nzuri mno.
-
8:03 - 8:07Nina hakika mambo hayo yote hakungalifanikiwa endapo mimi nisipongelifukuzwa kazi Apple.
-
8:08 - 8:11Ilikuwa dawa chungu kabisa lakini nakisia mimi nikiwa mgonjwa niliihitaji.
-
8:12 - 8:16Wakati mwingine unapigwa kichwani na maisha.
-
8:16 - 8:21Usipoteze imani. Mimi ninaamini ndio upendo wa kazi yangu ulionisukuma niendelee nayo.
-
8:22 - 8:27Huna budi kutafuta lile unayolipenda ama ni kazi au wapenzi wako.
-
8:28 - 8:34Kazi yako hula sehemu kubwa sana ya maisha yako, njia pekee kuridhika nayo ni kufanya ile unayoamini ni kazi muhimu mno.
-
8:35 - 8:38Pia njia ya pekee katika kufanya kazi muhimu mno ni kupenda unayoifanya.
-
8:39 - 8:43Endapo bado hujaikuta, endelea kuitafuta usikubali kwa shingo upande.
-
8:43 - 8:47Kama yalivyo katika mambo ya mapenzi, utafahamu ndipo utakapoikuta.
-
8:47 - 8:52Na kama yalivyo katika uhusiano wa kimapenzi kila ukipita wakati, nao unaendelea kuboreka.
-
8:52 - 8:54Kwa hivyo endelea kuitafuta usikubali kwa shingo upande.
-
8:57 - 9:04[Upigaji makofi]
-
9:05 - 9:08Kisa changu cha tatu ni juu ya kifo.
-
9:09 - 9:12Nilipokuwa na umri wa miaka kumi na saba nilisoma kidondoa kilichoeleweka kama:
-
9:13 - 9:18"Ukiishia kila siku kama ni siku yako ya mwisho, siku moja ndipo itakuwepo."
-
9:18 - 9:20[vichekesho]
-
9:20 - 9:28Kidonda hicho kiliniathiri sana na tangu siku hiyo na kuendelea kwa muda wa miaka thelathini na mitatu, nimekuwa ninajitazama kwenye kioo nikijiuliza:
-
9:28 - 9:33"Ikiwa leo ni siku ya mwisho maishani mwangu, ningefanya kama nimeshapanga nifanye leo hii?"
-
9:33 - 9:39Wakati wowote jibu likiwa "hapana" kwa siku nyingi zaidi mfululizo, najua sina budi kubadilisha kitu fulani.
-
9:40 - 9:47Nikikumbuka karibu nitakuwa nimeshakufa, ni kifaa muhimu kuliko vifaa vyote vingine nimekuwa navyo katika kunisaidia kufanya uchaguzi mkubwa katika maisha.
-
9:47 - 9:54Kwa sababu karibu vitu vyote vinavyotarajiwa kutoka katika dunia, heshima zote, woga zote zu kutiliwa aibu au kushindwa
-
9:54 - 10:00mambo hayo hutoweka yakiwa ana kwa ana na kifo, yanayobaki ni yale yenye umuhimu wa kweli.
-
10:00 - 10:07Ukikumbuka hilo utakufa pasi na wasiwasi ya kufikiri kitu adimu kimekupotea.
-
10:07 - 10:12Umeshaonekana bayana mtupu. Hakuna sababu kutofuatilia moyo wako.
-
10:13 - 10:17Muda wa mwaka mmoja hivi uliopita nilipimwa nina saratani.
-
10:18 - 10:23Nilipimwa mnamo saa moja u nusu asubuhi ikaonyesha bayana uvimbe wa kongosho.
-
10:23 - 10:25Hata mimi sikujua kongosho ndicho kitu gani.
-
10:26 - 10:35Madaktari walinieleza bila shaka saratani ya aina hii haina tibu ninatarajiwa kuishi muda usiozidi miezi mitatu hadi sita.
-
10:35 - 10:43Daktari yangu alinishauri kwenda nyumbani nipange mambo yangu muhimu. Ndiyo mawaidha ya daktari kifo kinakuja.
-
10:43 - 10:51Ndio maana kuwashauri watoto wako yote ya busara kawaida ungewaeleza katika muda wa miaka kumi sasa muda ndio miezi michache.
-
10:51 - 10:56Ina maana kupanga utaratibu wa mambo yote ilimradi umewaepusha familia na matatizo na shida.
-
10:57 - 10:59Ina maana ya kuwaaga wote wapendwa.
-
11:01 - 11:03Nilikaa na utambuaji huo siku nzima.
-
11:03 - 11:10Baadaye jioni ya siku hiyo nilipata uchunguzi wa tishu iliyokatwa kutoka katika uvimbe wa kongosho kwa kutumia endoscopu iliyopitishwa kwenye koo, kupitia tumbo hadi utumbo.
-
11:10 - 11:14Kongosho ilipigwa sindano na seli chache zilivutwa kutoka katika uvimbe.
-
11:15 - 11:23Mimi nilitulizwa na dawa lakini mke wangu naye alikuwepo akaniambia madaktari walipotazama seli kwa kutumia hadobini wakaanza kulia machozi,
-
11:23 - 11:28kwa sababu ikagunduliwa aina ya saratani iliyoniumiza ni adimu sana na tibu inawezekana kutokana na upasuaji.
-
11:28 - 11:32Nilipata upasuaji nashukuru Mungu sasa nimeshapoa.
-
11:32 - 11:40[upigaji makofi]
-
11:40 - 11:46Mara hiyo ndiyo ilinikaribisha na kifo zaidi. Nami matumaini ni hakitanikaribia tena kwa muda mrefu sana.
-
11:46 - 11:54Kwa sababu nimeivumilia naweza kutamka kwa dhati zaidi kuliko wakati kifo kilikuwa wazo linalotumika bali likiwa dhana tupu.
-
11:55 - 12:01Hakuna mtu anayetaka kufa. Hata wale wanayo hamu kwenda mbinguni hawataki kufa ili wapafike.
-
12:01 - 12:07Hata hivyo kifo ni mwisho wa safari ya maisha tuliyonayo sisi sote. Hakuna mtu aliyejiepusha nacho.
-
12:07 - 12:14Ndivyo yalivyo yawe yafaa kwani kifo kimebuniwa bora kuliko vitu vyote vingine maishani.
-
12:14 - 12:18Ni kifaa kinachobadilisha maisha. Kinafutilia mbali yale yaliyokwisha zeeka huku kikikaribisha yale mapya.
-
12:19 - 12:27Sasa yale mapya ndiyo ya nyinyi ingawaje siku moja si muda mrefu kutoka leo katika mwendo wa polepole mtakuwa waliozeeka mtafutiliwa mbali.
-
12:27 - 12:31Naomba radhi nimetia chumvi lakini nimesema kweli.
-
12:32 - 12:37Muda wenu una mwisho wake msije kuupoteza katika kuishi maisha ya mtu mwingine.
-
12:37 - 12:42Usinaswe na porojo ambayo mfumo wake ni kuishi ukiwa na matokeo ya dhana za watu wengine.
-
12:42 - 12:46Usiruhusu makelele ya maoni ya watu wengine kumeza sauti yako inayotokea moyoni mwako.
-
12:46 - 12:50Na iliyo muhimu zaidi, uwe na ujasiri kufuatilia moyo wako welekevu wako.
-
12:51 - 12:55Hisia hizo zimeshafahamu ukamilifu wa njia yako ya kimaisha.
-
12:55 - 12:58mambo yote mengine hushika kiwango cha pili katika maisha.
-
12:59 - 13:09[upigaji makofi]
-
13:09 - 13:17Nilipokuwa kijana palikuwa na jarida la maajabu liitwalo "The Whoe Earth Catalog", ambalo lilikuwa kitabu muhimu mno kwa kizazi changu.
-
13:17 - 13:25Kilibuniwa na mtu jina lake Stewart Brand aliyefanya kazi hiyo karibu kiasi na chuo hiki, naye alikijaza maana akiwa na kipaji cha utungaji mashairi.
-
13:25 - 13:34Enzi hizo za sitini kabla ya tarakilishi ya kibinafsi na uchapishaji ofisini kwa hivyo lilitengenezwa na mashine ya chapa, mikasi, na kamera za kutoa picha mara moja.
-
13:34 - 13:44Lilikuwa kama Google katika maumbile ya kitabu chenye jalada la karatasi muda wa miaka thelathini na tano kabla ya kuibuka kwa Google: Lilikuwa na maadili likimiminika na vifaa na madokezo mazuri sana.
-
13:45 - 13:48Stewart akiwa na timu yake walitoa matoleo machache ya Whole Earth Catalog,
-
13:48 - 13:52hatimaye lilipokaribu kwisha walitoa toleo la mwisho.
-
13:52 - 13:56Wakati ulikuwa katikati ya enzi za sabini nami umri wangu sawa na wa nyinyi.
-
13:58 - 14:07Juu ya jalada la mwisho ilikuwa foto ya njia sehemu za mashamba majira ya asubuhi ambako kuomba kuchukuliwa na gari hawatishi wasio na wasiwasi.
-
14:08 - 14:16Chini ya foto palikuwa na maneno: "Endeleza njaa ya elimu." Ndio ujumbe wao wa mwisho wakitilia nanga uchapishaji. wa "Whole Earth Catalog".
-
14:16 - 14:22Endeleza njaa ya elimu. Nami nimejiombea maneno hayo mwenyewe.
-
14:23 - 14:28Sasa hivi mkihitimu tayari kuanzia upya, nawatakieni nyinyi maneno hayo.
-
14:28 - 14:31Endeleza njaa ya elimu.
-
14:31 - 14:32Asanteni sana
-
14:33 - 14:49[upigaji makofi]
-
14:54 - 14:57[Chuo Kikuu cha Stanford - www.stanford.edu]
-
14:57 - 15:00Mtanganzaji: Kipindi hicho kimeidhiniwa na Chuo Kikuu cha Stanford.
-
15:00 - 15:03Karibuni! Wasiliana nasi kwa stanford.edu
- Title:
- Hotuba ya Steve Jobs kwenye Sherehe ya Mahafali, Chuo Kikuu cha Stanford Mwaka wa 2005
- Description:
-
Hii ni hotuba nyeti yenye mengi ya busara hasa kwa wanafunzi wa chuo kikuu wanaokabiliwa na uchaguzi wa masomo hatimaye ajira au ujasiriamali.
- Video Language:
- English
- Team:
- Captions Requested
- Duration:
- 15:05
PETE MHUNZI edited Swahili subtitles for Steve Jobs' 2005 Stanford Commencement Address |