Return to Video

Al Gore: Mawazo mapya kuhusu tatizo la mabadiliko ya hali ya hewa

  • 0:00 - 0:07
    Nimeshaonyesha kielelezopicha hiki ambacho nilikionyesha hapa miaka miwili iliyopita kwa mara takriban 2,000
  • 0:07 - 0:12
    Asubuhi ya leo nitatoa kielelezopicha kifupi
  • 0:12 - 0:15
    ambacho ninakitoa kwa mara ya kwanza, kwa hiyo
  • 0:15 - 0:20
    -- sitaki wala sihitaji kupandisha matumaini;
  • 0:20 - 0:21
    Ninajaribu kushusha matumaini.
  • 0:21 - 0:26
    Kwasababu nimeisuka hii pamoja kujaribu
  • 0:26 - 0:31
    kukidhi changamoto la kipindi hiki.
  • 0:31 - 0:36
    Na nilikumbushwa na mada nzuri aliyoitoa Karen Armstrong
  • 0:36 - 0:42
    kwamba dini ikieleweka vizuri
  • 0:42 - 0:45
    cha muhimu siyo imani, bali tabia.
  • 0:45 - 0:49
    Labda tuseme hivyo hivyo kuhusu matarajio.
  • 0:49 - 0:53
    Tunawezaje kuwa na matarajio?
  • 0:53 - 1:01
    Matarajio wakati mwingine yanachukuliwa kama imani, mtazamo wa kisomi
  • 1:01 - 1:04
    Kama vile Mahatma Ghandi alivyosema,
  • 1:04 - 1:07
    "Inakubidi uwe mabadiliko unayopenda kuyaona katika dunia."
  • 1:07 - 1:09
    Na matokeo ambayo
  • 1:09 - 1:14
    tunatamani yawe matarajio hayawezi kutokea
  • 1:14 - 1:19
    kwa imani peke yake, isipokuwa kwa kiwango ambacho imani
  • 1:19 - 1:25
    inaleta tabia mpya. Lakini neno "tabia"
  • 1:25 - 1:29
    pia nadhani, wakati mwingine halieleweki katika muktadha huu.
  • 1:29 - 1:32
    Mimi ni mtetezi wa kubadili
  • 1:32 - 1:35
    taa za umeme na kununua chotara,
  • 1:35 - 1:39
    mimi na Tipper tuliweka vibango vya kunasa mwanga wa jua 33 katika nyumba yetu,
  • 1:39 - 1:44
    na ninachimba visima vya nguvujoto, na ninafanya mambo mengine mengi tu.
  • 1:44 - 1:48
    Lakini, kama ilivyo muhimu kubadilisha taa za umeme,
  • 1:48 - 1:50
    ni muhimu zaidi kubadilisha sheria.
  • 1:50 - 1:56
    Na tukibadili tabia zetu katika maisha yetu ya kila siku,
  • 1:56 - 1:59
    mara nyingine tunaacha sehemu ya uraia
  • 1:59 - 2:06
    na sehemu ya demokrasia. Ili tuwe na matarajio kuhusu hili,
  • 2:06 - 2:12
    ni lazima tuwe raia wa mstari wa mbele katika demokrasia yetu.
  • 2:12 - 2:14
    Ili kuweza kutatua matatizo ya mabadiliko ya hali ya hewa,
  • 2:14 - 2:17
    inabidi tutatue matatizo ya demokrasia.
  • 2:17 - 2:19
    (Makofi). Na tunalo moja.
  • 2:19 - 2:24
    Nimekuwa nikijaribu kuielezea habari hii kwa muda mrefu.
  • 2:24 - 2:28
    Nilikumbushwa kuhusu hili hivi karibuni na mwanamke
  • 2:28 - 2:31
    aliyepita pembeni mwa meza niliyokuwa nimekaa,
  • 2:31 - 2:35
    alikuwa akinishangaa wakati akinipita. Alikuwa ni wa makamo ya miaka 70 hivi,
  • 2:35 - 2:39
    alionekana mwenye sura ya huruma. Sikufikiria lolote kuhusu hilo
  • 2:39 - 2:42
    mpaka nilipoona kutoka upande mmoja wa macho yangu
  • 2:42 - 2:44
    alikuwa akielekea upande mwingine
  • 2:44 - 2:48
    huku akinishangaa. Kwa hiyo nikamwambia, "Waonaje hali?"
  • 2:48 - 2:51
    Na alisema, "Wajua, kama nywele zako ungeziweka rangi nyeusi,
  • 2:51 - 2:56
    ungefanana na Al Gore." (kicheko).
  • 3:01 - 3:03
    Miaka mingi iliyopita, wakati nikiwa mbunge kijana,
  • 3:03 - 3:07
    nilitumia muda mwingi sana kupambana na changamoto hili
  • 3:07 - 3:10
    la kuzuia silaha za nyuklia -- mashindano ya silaha za nyuklia.
  • 3:10 - 3:13
    Na mwanahistoria wa jeshi alinifundisha
  • 3:13 - 3:18
    katika kipindi kile kuwa migongano ya kijeshi
  • 3:18 - 3:23
    inawekwa katika makundi matatu: mapigano ya ndani,
  • 3:23 - 3:28
    mapigano ya kanda na machache lakini muhimu
  • 3:28 - 3:33
    ya ulimwengu, vita vya dunia. Migongano ya kimkakati.
  • 3:33 - 3:38
    Na kila hatua ya mgongano inahitaji mgawanyo tofauti wa rasilimali
  • 3:38 - 3:40
    mbinu tofauti,
  • 3:40 - 3:44
    uendeshaji kwa mtindo tofauti.
  • 3:44 - 3:48
    Changamoto za mazingira zimo katika makundi hayohayo matatu,
  • 3:48 - 3:49
    na kila tunachofikiria
  • 3:49 - 3:52
    matatizo ya mazingira yanayotukabili: uchafuzi wa hewa, uchafuzi wa maji,
  • 3:52 - 3:56
    majalala ya uchafu wa hatari. Lakini pia kuna
  • 3:56 - 3:59
    matatizo ya mazingira ya kanda, kama mvua ya tindikali
  • 3:59 - 4:03
    kutoka Masharikikati mpaka Kaskazinimashariki mpaka Ulaya Magharibi
  • 4:03 - 4:07
    mpaka Aktiki, na kutoka Magharibikati
  • 4:07 - 4:10
    mpaka Mississippi na hata kwenye ukanda wa ghuba ya Mexico.
  • 4:10 - 4:12
    Na zipo nyingi kama hizo. Lakini matatizo ya hali ya hewa
  • 4:12 - 4:14
    ni adimu lakini ni miongoni mwa migongano muhimu
  • 4:14 - 4:17
    ya ulimwengu au kimkakati.
  • 4:17 - 4:22
    Kila kitu kinaathirika. Na inabidi tupangilie mikakati yetu
  • 4:22 - 4:28
    vizuri. Tunahitaji uhamasishaji wa dunia nzima
  • 4:28 - 4:31
    kwa nishati mbadala, utunzaji mazingira, ufanisi
  • 4:31 - 4:34
    na dunia ya mapito kuelekea uchumi wa kaboni pungufu.
  • 4:34 - 4:38
    Tuna kazi kubwa mbele yetu. Na tunaweza kuhamasisha rasilimali
  • 4:38 - 4:42
    na nia ya dhati ya kisiasa. Lakini nia ya dhati
  • 4:42 - 4:45
    ni lazima ihamasishwe ili kuhamasisha rasilimali.
  • 4:45 - 4:50
    Ngoja niwaonyeshe vielelezopicha.
  • 4:50 - 4:57
    Nilidhani ningeanza na nembo. Kinachosekana hapa
  • 4:57 - 4:59
    kwa hakika ni kilele cha barafu cha Ncha ya Kaskazini.
  • 4:59 - 5:06
    Greenland imebaki. Miaka 28 iliyopita, hivi ndivyo
  • 5:06 - 5:10
    kilele cha barafu cha ncha ya kaskazini -- kilivyokuwa kinaonekana
  • 5:10 - 5:14
    katika mwisho wa majira ya joto wakati jua likivuka ikweta.
  • 5:14 - 5:18
    Msimu wa majira ya kupukutika majani uliopita, nilikwenda kwenye masijala ya takwimu za theluji na barafu
  • 5:18 - 5:21
    huko Boulder, Colorado, na nilikaongea na watafiti
  • 5:21 - 5:25
    hapa Monterey katika Naval 'Postgraduate Laboratory'
  • 5:25 - 5:29
    Haya ndio yaliyotokea miaka 28 iliyopita.
  • 5:29 - 5:34
    Kuliweka hili sawa, mwaka 2005 ulikuwa ni rekodi iliyopita.
  • 5:34 - 5:37
    Hiki ndicho kilichotokea msimu wa majira ya kupukutika majani uliopita
  • 5:37 - 5:40
    na imewashtua watafiti.
  • 5:40 - 5:52
    Kijiografia, kilele cha barafu cha ncha ya kaskazini kina ukubwa sawa.
  • 5:52 - 5:53
    Hakionekani kuwa sawa
  • 5:53 - 5:57
    lakini kina ukubwa sawa na Marekani,
  • 5:57 - 6:00
    ukiondoa sehemu iliyo takriban sawa na jimbo la Arizona.
  • 6:00 - 6:03
    Kiasi kilichopotea mwaka 2005
  • 6:03 - 6:07
    kilikuwa sawa na kila kitu mashariki ya Mississippi.
  • 6:07 - 6:11
    Kiasi cha ziada kilichotoweka msimu uliopita wa majira ya kupukutika majani
  • 6:11 - 6:14
    kilikuwa sawa na hiki. Kinarudi tena wakati wa majira ya baridi,
  • 6:14 - 6:18
    lakini sio kama barafu ya kudumu: bali barafu nyembamba.
  • 6:18 - 6:24
    Dhaifu. Kiasi kilichobaki kinaweza kutoweka chote
  • 6:24 - 6:25
    wakati wa majira ya joto katika muda mfupi wa miaka takriban mitano.
  • 6:25 - 6:30
    Hii inaleta mgandamizo mkubwa huko Greenland.
  • 6:31 - 6:37
    Tayari, katika mzunguko wa Aktiki --
  • 6:39 - 6:43
    hiki ni kijiji maarufu huko Alaska. Ni kitongoji
  • 6:43 - 6:52
    cha Newfoundland. Antaktika. Utafiti wa NASA hivi karibuni
  • 6:52 - 6:55
    Kiasi cha kuyeyuka barafu kwa kiwango cha kawaida mpaka kikubwa kabisa.
  • 6:55 - 6:59
    kwenye sehemu yenye ukubwa sawa na California.
  • 6:59 - 7:02
    “Zilikuwepo nyakati nzuri,
  • 7:02 - 7:05
    Ilikuwa ni wakati mbaya”: kifungua sentensi maarafu sana
  • 7:05 - 7:08
    katika fasihi ya Kiingereza. Ningependa kuwahadithia kwa ufupi
  • 7:08 - 7:11
    "Hadithi ya Sayari Mbili". Dunia na Zuhura
  • 7:11 - 7:14
    Zina ukubwa sawa. Kipenyo cha dunia
  • 7:14 - 7:19
    ni takriban kilometa 400 zaidi, lakini ni ukubwa sawa.
  • 7:19 - 7:21
    Zina kiasi sawa cha kaboni
  • 7:21 - 7:26
    Lakini tofauti ni, duniani, karibu kaboni yake yote
  • 7:26 - 7:29
    imefyonzwa kwa miaka mingi kutoka kwenye anga
  • 7:29 - 7:33
    imekusanyika katika ardhi kama makaa ya mawe, mafuta,
  • 7:33 - 7:36
    gesi asilia, nk. Katika Zuhura, kaboni nyingi
  • 7:36 - 7:41
    bado iko angani. Tofauti ni hali yetu ya hewa
  • 7:41 - 7:44
    ni nyuzi 59 kwa wastani. Kwenye Zuhura
  • 7:44 - 7:48
    ni 855. Hii ina maana zaidi kwa mkakati wetu wa sasa
  • 7:48 - 7:50
    wa kuondoa kaboni nyingi ardhini haraka tuwezavyo
  • 7:50 - 7:51
    na kuiweka katika anga.
  • 7:54 - 7:57
    Sio kwasababu Zuhura iko karibu zaidi ya jua.
  • 7:57 - 7:59
    Ni ya moto mara tatu zaidi ya Zebaki,
  • 7:59 - 8:02
    ambayo iko karibu kabisa na jua. Sasa, kwa ufupi
  • 8:02 - 8:04
    hii hapa ni picha ambayo mmeiona kama moja ya picha za zamani,
  • 8:04 - 8:08
    lakini ninaionyesha kwasababu ninataka kuwapa CSI: Hali ya hewa.
  • 8:08 - 8:14
    Jumuiya ya wanasayansi duniani inasema,
  • 8:14 - 8:18
    uchafuzi wa mazingira unaosababishwa na mwanadamu, ukiwekwa kwenye anga,
  • 8:18 - 8:20
    unaongeza utando, unaozuia miale inayotoka.
  • 8:20 - 8:21
    Wote mnajua kwamba, angalau
  • 8:21 - 8:25
    Muhtsari wa IPCC, wanasayansi walitaka kusema,
  • 8:25 - 8:28
    “Mna uhakika gani?” Walitaka kujibu kwamba ni "asilimia 99.”
  • 8:28 - 8:30
    Wachina walipinga, kwa hiyo muafaka ulikuwa
  • 8:30 - 8:32
    “zaidi ya asilimia 90.”
  • 8:32 - 8:35
    Naam, wenye mashaka walisema, “Oh, subiri kidogo,
  • 8:35 - 8:39
    hii inaweza kuwa mabadiliko kwenye – hii nishati
  • 8:39 - 8:42
    kutoka kwenye jua. “Kama hii ni kweli,
  • 8:42 - 8:46
    basi anga za juu zingekuwa za moto sana sawa na
  • 8:46 - 8:49
    anga za chini, iwapo joto zaidi litakuwa linaingia.
  • 8:49 - 8:52
    Iwapo litakuwa linazuiwa wakati wa kutoka, kwa hiyo
  • 8:52 - 8:58
    tungetegemea kuwe na joto kidogo hapa na baridi kidogo pale. Hapa ni anga za chini.
  • 8:58 - 9:01
    Hapa ni anga za kati: baridi zaidi.
  • 9:01 - 9:02
    CSI: Hali ya hewa
  • 9:02 - 9:09
    Naam, hapa kuna habari njema. 68% ya Wamarekani wanaamini
  • 9:09 - 9:12
    kwamba shughuli za binadamu ndizo zinasababisha
  • 9:12 - 9:17
    matatizo ya ongezeko la joto. Asilimia 69 wanaamini kuwa joto la dunia linaongezeka
  • 9:17 - 9:20
    kwa kiasi kikubwa. Kumekuwa na maendeleo,
  • 9:20 - 9:27
    lakini hapa kuna ufunguo: ukipewa orodha
  • 9:27 - 9:36
    kati ya changamoto za kukabiliana nazo, uchafuzi wa hali ya hewa ulimwenguni umewekwa mwishoni kabisa mwa orodha
  • 9:36 - 9:39
    Kinachokosekana hapa ni umuhimu wa dharura hii.
  • 9:39 - 9:44
    Kama utakubaliana na mchanganuo wa hali halisi,
  • 9:44 - 9:47
    lakini huoni umuhimu wa wito huu,
  • 9:47 - 9:48
    upo upande gani?
  • 9:48 - 9:51
    Naam, Umoja wa Ulinzi wa Hali ya Hewa, ambao ninauongoza
  • 9:51 - 9:55
    kwa kushirikiana na CurrentTV – ambao wameandaa muswaada huu,
  • 9:55 - 9:59
    walifanya mashindano dunia nzima ya jinsi ya kutangaza hili.
  • 9:59 - 10:01
    Huyu ndiye mshindi.
  • 10:48 - 10:55
    NBC – Nitawaonyesha hapa vituo vyote vya televisheni – na waandishi mahiri
  • 10:55 - 10:59
    wa NBC waliuliza maswali 956 mwaka 2007
  • 10:59 - 11:02
    miongoni mwa wagombea urais: mawili kati yao yalikuwa kuhusu
  • 11:02 - 11:09
    matatizo ya hali ya hewa. ABC: maswali 844, mawili kuhusu matatizo ya hali ya hewa.
  • 11:09 - 11:19
    Fox: mawili. CNN: mawili. CBS: sifuri.
  • 11:19 - 11:23
    Kuanzia vicheko mpaka machozi. Hili ni mojawapo ya
  • 11:23 - 11:24
    matangazo ya zamani ya tumbaku.
  • 11:25 - 11:27
    Kwa hiyo hiki ndicho tunachofanya.
  • 11:27 - 11:37
    Haya ni matumizi ya petroli katika nchi zote hizi. Na sisi.
  • 11:37 - 11:43
    Lakini siyo nchi zilizoendelea peke yake.
  • 11:43 - 11:47
    Nchi zinazoendelea zinatufuata kwa sasa
  • 11:47 - 11:49
    na wanakaza mwendo. Na kwa hakika,
  • 11:49 - 11:52
    jumla ya utoaji wa hewa chafu kwa mwaka huu ni sawa
  • 11:52 - 11:55
    na tulivyokuwa mwaka 1965. Na wanatukaribia
  • 11:55 - 11:59
    kwa haraka sana. Jumla ya kiasi chote:
  • 11:59 - 12:05
    ifikapo mwaka 2025, itakuwa sawa na tulivyokuwa mwaka 1985
  • 12:05 - 12:10
    Kama nchi tajiri wasingekuwepo kabisa
  • 12:10 - 12:13
    hapa, tungekuwa bado na tatizo hili.
  • 12:13 - 12:17
    Lakini tumewapa nchi zinazoendelea
  • 12:17 - 12:19
    teknolojia na njia za kufikiria
  • 12:19 - 12:25
    ambazo zinaongeza tatizo. Hii hapa ni Bolivia.
  • 12:25 - 12:28
    Kwa miaka zaidi ya 30.
  • 12:47 - 12:51
    Hapa ni unyakuaji wa sekunde chache. Miaka ya 60.
  • 12:51 - 13:00
    70, 80, 90. Ni lazima tusimamishe hili. Na habari njema ni kwamba tunaweza.
  • 13:00 - 13:04
    Teknolojia tunazo.
  • 13:04 - 13:09
    Inabidi tuwe na msimamo wa pamoja wa jinsi gani tutakabiliana na hili:
  • 13:09 - 13:13
    mapambano dhidi ya umaskini duniani
  • 13:13 - 13:17
    na changamoto la kupunguza utoaji wa hewa chafu kwa nchi tajiri,
  • 13:17 - 13:21
    zote zina utatuzi mmoja rahisi.
  • 13:21 - 13:25
    Watu wanasema, “Utatuzi ni upi?” Huu hapa.
  • 13:25 - 13:31
    Weka bei kwenye kaboni. Tunahitaji kodi ya CO2, mapato
  • 13:31 - 13:39
    yatakayoondoa ushuru kwenye ajira, ambao ulivumbuliwa na Bismark --
  • 13:39 - 13:40
    na mambo mengine yamebadilika
  • 13:40 - 13:41
    toka karne ya 19.
  • 13:41 - 13:48
    Katika ulimwengu maskini, inatubidi tuunganishe mikakati yetu
  • 13:48 - 13:52
    juu ya umaskini na utatuzi wa matatizo ya hali ya hewa.
  • 13:52 - 13:55
    Mpango wa kupambana na umaskini Uganda
  • 13:55 - 13:59
    utaathiriwa iwapo hatutatatua tatizo la hali ya hewa.
  • 13:59 - 14:07
    Lakini muitikio unaweza kuleta tofauti kubwa sana
  • 14:07 - 14:12
    katika nchi maskini. Hili ni pendekezo
  • 14:12 - 14:16
    ambalo limezungumzwa sana huko Ulaya.
  • 14:16 - 14:20
    Hii ni kutoka kwenye jarida la Nature Magazine. Hizi zinazingatia
  • 14:20 - 14:27
    nishati mbadala ya jua, iliyounganishwa kwenye umeme wa gridi
  • 14:27 - 14:30
    kusambaza umeme
  • 14:30 - 14:38
    Ulaya kote, zaidi kutoka kwenye nchi zinazoendelea. Umeme wa DC.
  • 14:38 - 14:41
    Hii sio “chapati angani,” hii inawezekana.
  • 14:41 - 14:44
    Tunahitaji kufanya hili kwa ajili ya uchumi wetu wenyewe.
  • 14:44 - 14:47
    Takwimu za hivi karibuni zinaonyesha kuwa muundo wa zamani
  • 14:47 - 14:51
    haufanikiwi. Kuna fursa kubwa ya uwekezaji
  • 14:51 - 14:55
    ambayo mnaweza kufanya. Kama unawekeza kwenye udongo wa lami
  • 14:55 - 15:01
    au mafuta, basi una kibindo
  • 15:01 - 15:05
    ambacho kina raslimali za kaboni.
  • 15:05 - 15:09
    Na kiko katika muundo wa zamani.
  • 15:09 - 15:12
    Walevi wa madawa haramu wanaona mishipa kwenye vidole vyao wakati zile za
  • 15:12 - 15:17
    kwenye mikono na miguu yao hazionekani. Kutengeneza lami
  • 15:17 - 15:23
    na makaa ni sawa. Hii hapa ni baadhi ya mifano ya uwekezaji
  • 15:23 - 15:26
    ambayo nafikiri inaleta maana.
  • 15:26 - 15:29
    Nina maslahi katika hizi, kwa hiyo nina udhuru hapa.
  • 15:29 - 15:32
    Lakini joto la ardhini, kukusanya nishati ya jua,
  • 15:32 - 15:38
    betri za miali ya jua za teknolojia ya hali ya juu, ufanisi na uhifadhi.
  • 15:39 - 15:42
    Mmewahi kuona hiki kielelezopicha, lakini kuna mabadiliko.
  • 15:42 - 15:46
    Nchi mbili pekee ambazo hazikuridhia
  • 15:46 - 15:51
    --na sasa iko moja tu. Australia ilifanya uchaguzi.
  • 15:51 - 15:54
    Na kulikuwa na kampeni huko Australia
  • 15:54 - 15:59
    ambayo ilihusisha luninga na mtandao na matangazo ya redio
  • 15:59 - 16:01
    kuhamasisha uzito wa dharura hii kwa watu wa huko.
  • 16:01 - 16:05
    Na tuliwafunza watu 250 jinsi ya kuonyesha kielelezopicha hiki
  • 16:05 - 16:10
    katika vitongoji na vijiji na miji huko Australia.
  • 16:10 - 16:12
    Vitu vingine vingi vilichangia kwenye hilo,
  • 16:12 - 16:15
    lakini Waziri Mkuu mpya alitangaza kwamba
  • 16:15 - 16:19
    Jambo lake la muhimu kwanza ni kubadili msimamo wa Australia
  • 16:19 - 16:24
    kuhusu Kyoto, na amefanya hivyo. Sasa wameelewa
  • 16:24 - 16:28
    sababu mojawapo ikiwa ni ukame mkubwa uliowakumba.
  • 16:28 - 16:32
    Hili ni Ziwa Lanier. Rafiki yangu Heidi Cullins
  • 16:32 - 16:36
    kama tungekuwa tunatoa majina kwa ukame kama tufanyavyo kwa vimbunga,
  • 16:36 - 16:39
    tungeuita ukame wa kusini mashariki Katrina,
  • 16:39 - 16:41
    na tungesema kuwa unaelekea Atlanta.
  • 16:41 - 16:45
    Hatuwezi kusubiri ukame kama huu
  • 16:45 - 16:47
    ili tubadili utamaduni wetu wa kisiasa.
  • 16:47 - 16:56
    Hii hapa habari njema. Miji inayounga mkono mkataba wa Kyoto nchini Marekani
  • 16:56 - 16:59
    imefikia 780 -- na nadhani niliuona mmoja ukipita pale,
  • 16:59 - 17:05
    ukirahisisha hii. Hii ni habari njema.
  • 17:05 - 17:11
    Sasa kwa kumalizia, tulisikia siku chache zilizopita
  • 17:11 - 17:20
    kuhusu thamani ya kufanya ujasiri uonekane kitu cha kawaida
  • 17:20 - 17:23
    ili iwe jambo la kawaida.
  • 17:23 - 17:32
    Tunachohitaji sasa ni kizazi kipya cha majasiri. Sisi tulio hai
  • 17:32 - 17:34
    ndani ya Marekani
  • 17:34 - 17:36
    hasa leo, na hata kwa dunia nzima,
  • 17:37 - 17:42
    inabidi waelewe kuwa historia
  • 17:42 - 17:52
    imetupa uchaguzi -- kama vile ambavyo Jill Bolte Taylor alipojaribu
  • 17:52 - 17:57
    kuokoa maisha yake wakati alipokuwa amekinzwa
  • 17:57 - 18:01
    na hali ya kushangaza iliyomkumba.
  • 18:01 - 18:04
    Sasa tuna utamaduni wa ukinzani.
  • 18:04 - 18:09
    Lakini tuna dharura ya kidunia.
  • 18:09 - 18:13
    Inabidi tutafute njia ya kujenga,
  • 18:13 - 18:19
    katika kizazi cha walio hai leo, wito wa dhamira
  • 18:19 - 18:22
    Natamani ningepata maneno muafaka ya kuelezea hili.
  • 18:25 - 18:27
    Hiki kilikuwa ni kizazi kingine shupavu
  • 18:27 - 18:30
    kilicholeta demokrasia katika dunia.
  • 18:30 - 18:37
    Ambacho kiliondoa utumwa. Na kuwapa wanawake haki ya kupiga kura.
  • 18:37 - 18:44
    Tunaweza kulifanya hili. Usiniambie kuwa hatuna uwezo wa kulifanya.
  • 18:44 - 18:48
    Iwapo tukiwa na wiki moja tu ya gharama tunaitumia kwenye vita vya Iraki,
  • 18:48 - 18:51
    tungekuwa tunakaribia kutatua changamoto hili.
  • 18:51 - 18:55
    Tuna uwezo wa kutenda.
  • 19:01 - 19:14
    Jambo la mwisho. Nina matumaini, kwasababu nina amini
  • 19:14 - 19:18
    tuna uwezo, katika wakati huu wa changamoto kubwa,
  • 19:18 - 19:24
    kuweka pembeni ukinzani na kujikwamua kwenye changamoto hili.
  • 19:24 - 19:27
    ambalo historia imetuwekea.
  • 19:29 - 19:41
    Wakati mwingine nasikia watu wakiongelea kuhusu hali tete ya matatizo ya mabadiliko ya hali ya hewa
  • 19:41 - 19:43
    kwa kusema, "Oh, hii mbaya sana.
  • 19:43 - 19:49
    Mzigo mkubwa tunao." Ningependa kuwaomba
  • 19:49 - 19:53
    mbadilishe hilo. Ni vizazi vingapi
  • 19:53 - 19:58
    katika historia ya mwanadamu wamekuwa na fursa
  • 19:58 - 20:07
    ya kupambana na changamoto lenye kuhitaji juhudi zetu kubwa?
  • 20:07 - 20:13
    Changamoto ambalo litatukamua
  • 20:13 - 20:21
    kuliko uwezo wetu wa kutenda? Nafikiri inabidi tukabiliane
  • 20:21 - 20:25
    na changamoto hili kwa furaha kubwa
  • 20:25 - 20:30
    na shukrani kuwa sisi ni kizazi
  • 20:30 - 20:34
    ambacho, miaka elfu ijayo,
  • 20:34 - 20:43
    waghani wa muziki na washairi watasheherekea
  • 20:43 - 20:50
    kwa kusema, kuwa sisi tulifanikiwa kujitafuta ndani mwetu
  • 20:50 - 20:55
    kutatua tatizo hili na kuweka msingi
  • 20:55 - 20:57
    kwa maisha ya baadae ya mwanandamu yenye matumaini.
  • 20:57 - 21:00
    Tufanye hivyo. Asanteni sana.
  • 21:24 - 21:30
    Chris Anderson: Kwa watu wengi wa TED, kuna uchungu mkubwa
  • 21:30 - 21:32
    ambao ni wa ubunifu tu -- lakini mwishowe,
  • 21:32 - 21:34
    ubunifu kwenye karatasi ya uchaguzi --
  • 21:34 - 21:38
    ubunifu mbaya ni kwamba sauti yako haikusikika
  • 21:38 - 21:39
    kama ile ya miaka nane iliyopita katika nafasi
  • 21:39 - 21:41
    ambayo ungeweza kufanya kweli.
  • 21:41 - 21:43
    Hii inauma.
  • 21:43 - 21:50
    Al Gore: Hamuelewi ninyi. (Kicheko).
  • 21:53 - 21:54
    CA: Ukiangalia wagombea wanaoongoza
  • 21:54 - 21:56
    katika chama chako wanachokifanya kwa sasa – Namaanisha, kuna --
  • 21:56 - 22:01
    unafurahia mipango yao kuhusu matatizo ya hali ya hewa?
  • 22:10 - 22:14
    AG: Jibu la swali hilo ni gumu kwangu
  • 22:14 - 22:18
    kwasababu, kwa upande mwingine, nadhani kwamba
  • 22:18 - 22:22
    ni lazima tuone fahari kwa ukweli kwamba
  • 22:23 - 22:29
    mgombea wa Republican – mgombea wa uhakika--
  • 22:29 - 22:33
    John McCain, na wagombea wote
  • 22:33 - 22:38
    wa Democratic – wote watatu wana tofauti
  • 22:38 - 22:40
    ya mitazamo ya namna ya kusonga mbele
  • 22:40 - 22:45
    juu ya matatizo ya hali ya hewa. Wote watatu wameahidi kutoa mwongozo,
  • 22:45 - 22:49
    na wote watatu wana mitazamo tofauti kutokana na msimamo
  • 22:49 - 22:52
    wa uongozi wa sasa. Na ninadhani
  • 22:52 - 22:56
    kuwa wote watatu wamewajibika katika
  • 22:56 - 23:07
    kupitisha mipango na mapendekezo. Lakini mazungumzo ya kampeni --
  • 23:07 - 23:08
    kama yalivyofafanuliwa kwa maswali --
  • 23:08 - 23:09
    ambayo yalitayarishwa na
  • 23:09 - 23:12
    Umoja wa Wapiga Kura Watunzaji wa Mazingira, mchanganuo wa maswali yote --
  • 23:12 - 23:14
    na, mathalani, midahalo yote
  • 23:16 - 23:18
    imedhaminiwa na nembo ya Orwellian,
  • 23:18 - 23:22
    “Makaa Safi.” Kuna mtu yeyote ameliona hilo?
  • 23:22 - 23:26
    Kila mdahalo ulidhaminiwa na “Makaa Masafi.”
  • 23:26 - 23:28
    “Naam, kupunguza zaidi hewa chafu!”
  • 23:28 - 23:32
    Ukubwa na uzito wa mazungumzo
  • 23:32 - 23:35
    katika demokrasia yetu haujaweka msingi
  • 23:35 - 23:39
    katika mikakati thabiti inayohitajika.
  • 23:39 - 23:42
    Kwa hiyo wanasema maneno muafaka na itabidi wafanye --
  • 23:42 - 23:45
    yeyote atakayechaguliwa – jambo la muhimu,
  • 23:45 - 23:49
    lakini ngoja niwaeleze: niliporudi kutoka Kyoto
  • 23:49 - 23:56
    mwaka 1997 nikiwa na hisia za furaha kubwa
  • 23:56 - 23:58
    kwamba tumewezakupata utatuzi huko,
  • 23:58 - 24:00
    na nililikabili bunge la Marekani,
  • 24:00 - 24:04
    lakini mbunge mmoja kati ya 100 alikuwa tayari kupiga kura
  • 24:04 - 24:11
    kupitisha, kuridhia mkataba huo. Chochote watakachosema wagombea
  • 24:11 - 24:16
    lazima kiwe sambamba na watakachosema watu.
  • 24:16 - 24:20
    Changamoto hili ni sehemu ya mfumo
  • 24:20 - 24:22
    wa ustaarabu wetu wote.
  • 24:22 - 24:25
    CO2 ni pumzi ya ustaarabu wetu.
  • 24:26 - 24:29
    Na sasa tumeutengeneza mlolongo huu bandia. Kubadilisha mwelekeo
  • 24:29 - 24:36
    kunahitaji upeo, kipimo, mwelekeo wa mabadiliko
  • 24:36 - 24:39
    ambayo ni zaidi ya tulivyofanya huko nyuma.
  • 24:39 - 24:41
    Na ndio maana ninaanza kwa kusema,
  • 24:41 - 24:47
    muwe na matumaini kwa mnachokifanya, lakini muwe raia wenye shauku
  • 24:48 - 24:50
    Mahitaji – badilisha taa za umeme,
  • 24:50 - 24:53
    lakini pia badilisha sheria. Badilisha mikataba ya kimataifa.
  • 24:53 - 24:59
    Ni lazima tuongelee hili. Tutatue hii demokrasia – hii--
  • 25:00 - 25:06
    Tuna sclerosis kwenye demokrasia yetu. Na inabidi tubadili hili.
  • 25:07 - 25:08
    Tumia mtandao. Nenda kwenye mtandao.
  • 25:08 - 25:12
    Ungana na watu. Muwe raia wenye shauku
  • 25:12 - 25:14
    Muweze kuzuia -- hatuwezi
  • 25:14 - 25:16
    kuwa na mitambo mipya ya kutengeneza nishati ya makaa
  • 25:16 - 25:21
    ambayo haiwezi kuchuja na kutunza CO2. Hii ina maana kwamba inatulazimu
  • 25:21 - 25:23
    tujenge haraka vyanzo hivi vya nishati mbadala.
  • 25:23 - 25:27
    Kwa sasa, hakuna mtu anaongelea kwenye kiwango hicho. Lakini naamini
  • 25:27 - 25:31
    kwamba kati ya sasa na Novemba, inawezekana.
  • 25:31 - 25:32
    Huu Mshikamano wa Kutunza Mazingira
  • 25:33 - 25:36
    utazindua kampeni ya nchi nzima --
  • 25:36 - 25:39
    uhamasishaji kuanzia shina, matangazo ya luninga, matangazo ya mtandaoni,
  • 25:39 - 25:42
    radio, magazeti – kwa kushirikiana na kila mtu
  • 25:42 - 25:45
    Kutoka Maskauti wa Kike mpaka wawindaji na wavuvi.
  • 25:45 - 25:49
    Tuna hitaji msaada. Tunahitaji msaada.
  • 25:49 - 25:53
    CA: Kwa wajibu wako binafsi kusonga mbele,
  • 25:53 - 25:55
    Al, kuna kitu kingine zaidi ya hicho
  • 25:55 - 25:56
    ambacho utapenda kufanya?
  • 25:56 - 26:04
    AG: Nimekuwa nikisali ili niweze kupata jibu
  • 26:04 - 26:09
    la swali hilo. Nifanyaje?
  • 26:09 - 26:13
    Buckminster Fuller aliandika, "Kama maisha ya baadae ya
  • 26:13 - 26:18
    ya ustaarabu yangenitegemea mimi, ningefanya nini?
  • 26:18 - 26:23
    Nitakuwaje? Itatutegemea sisi sote,
  • 26:23 - 26:25
    hata hivyo, sio kwa taa za umeme tu.
  • 26:25 - 26:33
    Wengi wetu hapa, ni Wamarekani. Tuna demokrasia.
  • 26:33 - 26:39
    Tunaweza kubadili mambo, lakini tunatakiwa tuhamasike kubadili.
  • 26:39 - 26:44
    Kinachotakiwa hasa ni ufahamu zaidi.
  • 26:44 - 26:46
    Na hii ni ngumu ku --
  • 26:46 - 26:50
    ni ngumu kuijenga -- lakini inakuja.
  • 26:50 - 26:53
    Kuna methali ya zamani ya Kiafrika ambayo baadhi yenu mnaijua
  • 26:53 - 26:57
    ambayo inasema, "iwapo unataka kwenda haraka, nenda peke yako;
  • 26:57 - 27:05
    iwapo mnataka kwenda mbali, nendeni pamoja. "Inabidi twende mbali haraka.
  • 27:05 - 27:09
    Kwahiyo inatubidi tuwe na mabadiliko katika ufahamu.
  • 27:09 - 27:13
    Mabadiliko katika malengo. Nia mpya ya dharura.
  • 27:13 - 27:16
    Utambuzi mpya wa fursa hii
  • 27:16 - 27:19
    tuliyonayo katika kukabiliana na changamoto hili.
  • 27:19 - 27:23
    CA: Al Gore, asanteni sana kwa kuja TED
  • 27:23 - 27:27
    AG: Asante. Asante sana. (Makofi)
Title:
Al Gore: Mawazo mapya kuhusu tatizo la mabadiliko ya hali ya hewa
Speaker:
Al Gore
Description:

Katika kielelezopicha hiki kipya (kinachozinduliwa kwenye TED.com), Al Gore anatoa ushahidi kwamba kasi ya mabadiliko ya hali ya hewa yaweza kuwa mbaya kuliko wanasayansi walivyobashiri hivi karibuni. Anatupa changamoto tuchukue hatua.

more » « less
Video Language:
English
Team:
closed TED
Project:
TEDTalks
Duration:
27:31
TED added a translation

Swahili subtitles

Revisions