0:00:00.000,0:00:07.000 Nimeshaonyesha kielelezopicha hiki ambacho nilikionyesha hapa miaka miwili iliyopita kwa mara takriban 2,000 0:00:07.000,0:00:12.000 Asubuhi ya leo nitatoa kielelezopicha kifupi 0:00:12.000,0:00:15.000 ambacho ninakitoa kwa mara ya kwanza, kwa hiyo 0:00:15.000,0:00:20.000 -- sitaki wala sihitaji kupandisha matumaini; 0:00:20.000,0:00:21.000 Ninajaribu kushusha matumaini. 0:00:21.000,0:00:26.000 Kwasababu nimeisuka hii pamoja kujaribu 0:00:26.000,0:00:31.000 kukidhi changamoto la kipindi hiki. 0:00:31.000,0:00:36.000 Na nilikumbushwa na mada nzuri aliyoitoa Karen Armstrong 0:00:36.000,0:00:42.000 kwamba dini ikieleweka vizuri 0:00:42.000,0:00:45.000 cha muhimu siyo imani, bali tabia. 0:00:45.000,0:00:49.000 Labda tuseme hivyo hivyo kuhusu matarajio. 0:00:49.000,0:00:53.000 Tunawezaje kuwa na matarajio? 0:00:53.000,0:01:01.000 Matarajio wakati mwingine yanachukuliwa kama imani, mtazamo wa kisomi 0:01:01.000,0:01:04.000 Kama vile Mahatma Ghandi alivyosema, 0:01:04.000,0:01:07.000 "Inakubidi uwe mabadiliko unayopenda kuyaona katika dunia." 0:01:07.000,0:01:09.000 Na matokeo ambayo 0:01:09.000,0:01:14.000 tunatamani yawe matarajio hayawezi kutokea 0:01:14.000,0:01:19.000 kwa imani peke yake, isipokuwa kwa kiwango ambacho imani 0:01:19.000,0:01:25.000 inaleta tabia mpya. Lakini neno "tabia" 0:01:25.000,0:01:29.000 pia nadhani, wakati mwingine halieleweki katika muktadha huu. 0:01:29.000,0:01:32.000 Mimi ni mtetezi wa kubadili 0:01:32.000,0:01:35.000 taa za umeme na kununua chotara, 0:01:35.000,0:01:39.000 mimi na Tipper tuliweka vibango vya kunasa mwanga wa jua 33 katika nyumba yetu, 0:01:39.000,0:01:44.000 na ninachimba visima vya nguvujoto, na ninafanya mambo mengine mengi tu. 0:01:44.000,0:01:48.000 Lakini, kama ilivyo muhimu kubadilisha taa za umeme, 0:01:48.000,0:01:50.000 ni muhimu zaidi kubadilisha sheria. 0:01:50.000,0:01:56.000 Na tukibadili tabia zetu katika maisha yetu ya kila siku, 0:01:56.000,0:01:59.000 mara nyingine tunaacha sehemu ya uraia 0:01:59.000,0:02:06.000 na sehemu ya demokrasia. Ili tuwe na matarajio kuhusu hili, 0:02:06.000,0:02:12.000 ni lazima tuwe raia wa mstari wa mbele katika demokrasia yetu. 0:02:12.000,0:02:14.000 Ili kuweza kutatua matatizo ya mabadiliko ya hali ya hewa, 0:02:14.000,0:02:17.000 inabidi tutatue matatizo ya demokrasia. 0:02:17.000,0:02:19.000 (Makofi). Na tunalo moja. 0:02:19.000,0:02:24.000 Nimekuwa nikijaribu kuielezea habari hii kwa muda mrefu. 0:02:24.000,0:02:28.000 Nilikumbushwa kuhusu hili hivi karibuni na mwanamke 0:02:28.000,0:02:31.000 aliyepita pembeni mwa meza niliyokuwa nimekaa, 0:02:31.000,0:02:35.000 alikuwa akinishangaa wakati akinipita. Alikuwa ni wa makamo ya miaka 70 hivi, 0:02:35.000,0:02:39.000 alionekana mwenye sura ya huruma. Sikufikiria lolote kuhusu hilo 0:02:39.000,0:02:42.000 mpaka nilipoona kutoka upande mmoja wa macho yangu 0:02:42.000,0:02:44.000 alikuwa akielekea upande mwingine 0:02:44.000,0:02:48.000 huku akinishangaa. Kwa hiyo nikamwambia, "Waonaje hali?" 0:02:48.000,0:02:51.000 Na alisema, "Wajua, kama nywele zako ungeziweka rangi nyeusi, 0:02:51.000,0:02:56.000 ungefanana na Al Gore." (kicheko). 0:03:01.000,0:03:03.000 Miaka mingi iliyopita, wakati nikiwa mbunge kijana, 0:03:03.000,0:03:07.000 nilitumia muda mwingi sana kupambana na changamoto hili 0:03:07.000,0:03:10.000 la kuzuia silaha za nyuklia -- mashindano ya silaha za nyuklia. 0:03:10.000,0:03:13.000 Na mwanahistoria wa jeshi alinifundisha 0:03:13.000,0:03:18.000 katika kipindi kile kuwa migongano ya kijeshi 0:03:18.000,0:03:23.000 inawekwa katika makundi matatu: mapigano ya ndani, 0:03:23.000,0:03:28.000 mapigano ya kanda na machache lakini muhimu 0:03:28.000,0:03:33.000 ya ulimwengu, vita vya dunia. Migongano ya kimkakati. 0:03:33.000,0:03:38.000 Na kila hatua ya mgongano inahitaji mgawanyo tofauti wa rasilimali 0:03:38.000,0:03:40.000 mbinu tofauti, 0:03:40.000,0:03:44.000 uendeshaji kwa mtindo tofauti. 0:03:44.000,0:03:48.000 Changamoto za mazingira zimo katika makundi hayohayo matatu, 0:03:48.000,0:03:49.000 na kila tunachofikiria 0:03:49.000,0:03:52.000 matatizo ya mazingira yanayotukabili: uchafuzi wa hewa, uchafuzi wa maji, 0:03:52.000,0:03:56.000 majalala ya uchafu wa hatari. Lakini pia kuna 0:03:56.000,0:03:59.000 matatizo ya mazingira ya kanda, kama mvua ya tindikali 0:03:59.000,0:04:03.000 kutoka Masharikikati mpaka Kaskazinimashariki mpaka Ulaya Magharibi 0:04:03.000,0:04:07.000 mpaka Aktiki, na kutoka Magharibikati 0:04:07.000,0:04:10.000 mpaka Mississippi na hata kwenye ukanda wa ghuba ya Mexico. 0:04:10.000,0:04:12.000 Na zipo nyingi kama hizo. Lakini matatizo ya hali ya hewa 0:04:12.000,0:04:14.000 ni adimu lakini ni miongoni mwa migongano muhimu 0:04:14.000,0:04:17.000 ya ulimwengu au kimkakati. 0:04:17.000,0:04:22.000 Kila kitu kinaathirika. Na inabidi tupangilie mikakati yetu 0:04:22.000,0:04:28.000 vizuri. Tunahitaji uhamasishaji wa dunia nzima 0:04:28.000,0:04:31.000 kwa nishati mbadala, utunzaji mazingira, ufanisi 0:04:31.000,0:04:34.000 na dunia ya mapito kuelekea uchumi wa kaboni pungufu. 0:04:34.000,0:04:38.000 Tuna kazi kubwa mbele yetu. Na tunaweza kuhamasisha rasilimali 0:04:38.000,0:04:42.000 na nia ya dhati ya kisiasa. Lakini nia ya dhati 0:04:42.000,0:04:45.000 ni lazima ihamasishwe ili kuhamasisha rasilimali. 0:04:45.000,0:04:50.000 Ngoja niwaonyeshe vielelezopicha. 0:04:50.000,0:04:57.000 Nilidhani ningeanza na nembo. Kinachosekana hapa 0:04:57.000,0:04:59.000 kwa hakika ni kilele cha barafu cha Ncha ya Kaskazini. 0:04:59.000,0:05:06.000 Greenland imebaki. Miaka 28 iliyopita, hivi ndivyo 0:05:06.000,0:05:10.000 kilele cha barafu cha ncha ya kaskazini -- kilivyokuwa kinaonekana 0:05:10.000,0:05:14.000 katika mwisho wa majira ya joto wakati jua likivuka ikweta. 0:05:14.000,0:05:18.000 Msimu wa majira ya kupukutika majani uliopita, nilikwenda kwenye masijala ya takwimu za theluji na barafu 0:05:18.000,0:05:21.000 huko Boulder, Colorado, na nilikaongea na watafiti 0:05:21.000,0:05:25.000 hapa Monterey katika Naval 'Postgraduate Laboratory' 0:05:25.000,0:05:29.000 Haya ndio yaliyotokea miaka 28 iliyopita. 0:05:29.000,0:05:34.000 Kuliweka hili sawa, mwaka 2005 ulikuwa ni rekodi iliyopita. 0:05:34.000,0:05:37.000 Hiki ndicho kilichotokea msimu wa majira ya kupukutika majani uliopita 0:05:37.000,0:05:40.000 na imewashtua watafiti. 0:05:40.000,0:05:52.000 Kijiografia, kilele cha barafu cha ncha ya kaskazini kina ukubwa sawa. 0:05:52.000,0:05:53.000 Hakionekani kuwa sawa 0:05:53.000,0:05:57.000 lakini kina ukubwa sawa na Marekani, 0:05:57.000,0:06:00.000 ukiondoa sehemu iliyo takriban sawa na jimbo la Arizona. 0:06:00.000,0:06:03.000 Kiasi kilichopotea mwaka 2005 0:06:03.000,0:06:07.000 kilikuwa sawa na kila kitu mashariki ya Mississippi. 0:06:07.000,0:06:11.000 Kiasi cha ziada kilichotoweka msimu uliopita wa majira ya kupukutika majani 0:06:11.000,0:06:14.000 kilikuwa sawa na hiki. Kinarudi tena wakati wa majira ya baridi, 0:06:14.000,0:06:18.000 lakini sio kama barafu ya kudumu: bali barafu nyembamba. 0:06:18.000,0:06:24.000 Dhaifu. Kiasi kilichobaki kinaweza kutoweka chote 0:06:24.000,0:06:25.000 wakati wa majira ya joto katika muda mfupi wa miaka takriban mitano. 0:06:25.000,0:06:30.000 Hii inaleta mgandamizo mkubwa huko Greenland. 0:06:31.000,0:06:37.000 Tayari, katika mzunguko wa Aktiki -- 0:06:39.000,0:06:43.000 hiki ni kijiji maarufu huko Alaska. Ni kitongoji 0:06:43.000,0:06:52.000 cha Newfoundland. Antaktika. Utafiti wa NASA hivi karibuni 0:06:52.000,0:06:55.000 Kiasi cha kuyeyuka barafu kwa kiwango cha kawaida mpaka kikubwa kabisa. 0:06:55.000,0:06:59.000 kwenye sehemu yenye ukubwa sawa na California. 0:06:59.000,0:07:02.000 “Zilikuwepo nyakati nzuri, 0:07:02.000,0:07:05.000 Ilikuwa ni wakati mbaya”: kifungua sentensi maarafu sana 0:07:05.000,0:07:08.000 katika fasihi ya Kiingereza. Ningependa kuwahadithia kwa ufupi 0:07:08.000,0:07:11.000 "Hadithi ya Sayari Mbili". Dunia na Zuhura 0:07:11.000,0:07:14.000 Zina ukubwa sawa. Kipenyo cha dunia 0:07:14.000,0:07:19.000 ni takriban kilometa 400 zaidi, lakini ni ukubwa sawa. 0:07:19.000,0:07:21.000 Zina kiasi sawa cha kaboni 0:07:21.000,0:07:26.000 Lakini tofauti ni, duniani, karibu kaboni yake yote 0:07:26.000,0:07:29.000 imefyonzwa kwa miaka mingi kutoka kwenye anga 0:07:29.000,0:07:33.000 imekusanyika katika ardhi kama makaa ya mawe, mafuta, 0:07:33.000,0:07:36.000 gesi asilia, nk. Katika Zuhura, kaboni nyingi 0:07:36.000,0:07:41.000 bado iko angani. Tofauti ni hali yetu ya hewa 0:07:41.000,0:07:44.000 ni nyuzi 59 kwa wastani. Kwenye Zuhura 0:07:44.000,0:07:48.000 ni 855. Hii ina maana zaidi kwa mkakati wetu wa sasa 0:07:48.000,0:07:50.000 wa kuondoa kaboni nyingi ardhini haraka tuwezavyo 0:07:50.000,0:07:51.000 na kuiweka katika anga. 0:07:54.000,0:07:57.000 Sio kwasababu Zuhura iko karibu zaidi ya jua. 0:07:57.000,0:07:59.000 Ni ya moto mara tatu zaidi ya Zebaki, 0:07:59.000,0:08:02.000 ambayo iko karibu kabisa na jua. Sasa, kwa ufupi 0:08:02.000,0:08:04.000 hii hapa ni picha ambayo mmeiona kama moja ya picha za zamani, 0:08:04.000,0:08:08.000 lakini ninaionyesha kwasababu ninataka kuwapa CSI: Hali ya hewa. 0:08:08.000,0:08:14.000 Jumuiya ya wanasayansi duniani inasema, 0:08:14.000,0:08:18.000 uchafuzi wa mazingira unaosababishwa na mwanadamu, ukiwekwa kwenye anga, 0:08:18.000,0:08:20.000 unaongeza utando, unaozuia miale inayotoka. 0:08:20.000,0:08:21.000 Wote mnajua kwamba, angalau 0:08:21.000,0:08:25.000 Muhtsari wa IPCC, wanasayansi walitaka kusema, 0:08:25.000,0:08:28.000 “Mna uhakika gani?” Walitaka kujibu kwamba ni "asilimia 99.” 0:08:28.000,0:08:30.000 Wachina walipinga, kwa hiyo muafaka ulikuwa 0:08:30.000,0:08:32.000 “zaidi ya asilimia 90.” 0:08:32.000,0:08:35.000 Naam, wenye mashaka walisema, “Oh, subiri kidogo, 0:08:35.000,0:08:39.000 hii inaweza kuwa mabadiliko kwenye – hii nishati 0:08:39.000,0:08:42.000 kutoka kwenye jua. “Kama hii ni kweli, 0:08:42.000,0:08:46.000 basi anga za juu zingekuwa za moto sana sawa na 0:08:46.000,0:08:49.000 anga za chini, iwapo joto zaidi litakuwa linaingia. 0:08:49.000,0:08:52.000 Iwapo litakuwa linazuiwa wakati wa kutoka, kwa hiyo 0:08:52.000,0:08:58.000 tungetegemea kuwe na joto kidogo hapa na baridi kidogo pale. Hapa ni anga za chini. 0:08:58.000,0:09:01.000 Hapa ni anga za kati: baridi zaidi. 0:09:01.000,0:09:02.000 CSI: Hali ya hewa 0:09:02.000,0:09:09.000 Naam, hapa kuna habari njema. 68% ya Wamarekani wanaamini 0:09:09.000,0:09:12.000 kwamba shughuli za binadamu ndizo zinasababisha 0:09:12.000,0:09:17.000 matatizo ya ongezeko la joto. Asilimia 69 wanaamini kuwa joto la dunia linaongezeka 0:09:17.000,0:09:20.000 kwa kiasi kikubwa. Kumekuwa na maendeleo, 0:09:20.000,0:09:27.000 lakini hapa kuna ufunguo: ukipewa orodha 0:09:27.000,0:09:36.000 kati ya changamoto za kukabiliana nazo, uchafuzi wa hali ya hewa ulimwenguni umewekwa mwishoni kabisa mwa orodha 0:09:36.000,0:09:39.000 Kinachokosekana hapa ni umuhimu wa dharura hii. 0:09:39.000,0:09:44.000 Kama utakubaliana na mchanganuo wa hali halisi, 0:09:44.000,0:09:47.000 lakini huoni umuhimu wa wito huu, 0:09:47.000,0:09:48.000 upo upande gani? 0:09:48.000,0:09:51.000 Naam, Umoja wa Ulinzi wa Hali ya Hewa, ambao ninauongoza 0:09:51.000,0:09:55.000 kwa kushirikiana na CurrentTV – ambao wameandaa muswaada huu, 0:09:55.000,0:09:59.000 walifanya mashindano dunia nzima ya jinsi ya kutangaza hili. 0:09:59.000,0:10:01.000 Huyu ndiye mshindi. 0:10:48.000,0:10:55.000 NBC – Nitawaonyesha hapa vituo vyote vya televisheni – na waandishi mahiri 0:10:55.000,0:10:59.000 wa NBC waliuliza maswali 956 mwaka 2007 0:10:59.000,0:11:02.000 miongoni mwa wagombea urais: mawili kati yao yalikuwa kuhusu 0:11:02.000,0:11:09.000 matatizo ya hali ya hewa. ABC: maswali 844, mawili kuhusu matatizo ya hali ya hewa. 0:11:09.000,0:11:19.000 Fox: mawili. CNN: mawili. CBS: sifuri. 0:11:19.000,0:11:23.000 Kuanzia vicheko mpaka machozi. Hili ni mojawapo ya 0:11:23.000,0:11:24.000 matangazo ya zamani ya tumbaku. 0:11:25.000,0:11:27.000 Kwa hiyo hiki ndicho tunachofanya. 0:11:27.000,0:11:37.000 Haya ni matumizi ya petroli katika nchi zote hizi. Na sisi. 0:11:37.000,0:11:43.000 Lakini siyo nchi zilizoendelea peke yake. 0:11:43.000,0:11:47.000 Nchi zinazoendelea zinatufuata kwa sasa 0:11:47.000,0:11:49.000 na wanakaza mwendo. Na kwa hakika, 0:11:49.000,0:11:52.000 jumla ya utoaji wa hewa chafu kwa mwaka huu ni sawa 0:11:52.000,0:11:55.000 na tulivyokuwa mwaka 1965. Na wanatukaribia 0:11:55.000,0:11:59.000 kwa haraka sana. Jumla ya kiasi chote: 0:11:59.000,0:12:05.000 ifikapo mwaka 2025, itakuwa sawa na tulivyokuwa mwaka 1985 0:12:05.000,0:12:10.000 Kama nchi tajiri wasingekuwepo kabisa 0:12:10.000,0:12:13.000 hapa, tungekuwa bado na tatizo hili. 0:12:13.000,0:12:17.000 Lakini tumewapa nchi zinazoendelea 0:12:17.000,0:12:19.000 teknolojia na njia za kufikiria 0:12:19.000,0:12:25.000 ambazo zinaongeza tatizo. Hii hapa ni Bolivia. 0:12:25.000,0:12:28.000 Kwa miaka zaidi ya 30. 0:12:47.000,0:12:51.000 Hapa ni unyakuaji wa sekunde chache. Miaka ya 60. 0:12:51.000,0:13:00.000 70, 80, 90. Ni lazima tusimamishe hili. Na habari njema ni kwamba tunaweza. 0:13:00.000,0:13:04.000 Teknolojia tunazo. 0:13:04.000,0:13:09.000 Inabidi tuwe na msimamo wa pamoja wa jinsi gani tutakabiliana na hili: 0:13:09.000,0:13:13.000 mapambano dhidi ya umaskini duniani 0:13:13.000,0:13:17.000 na changamoto la kupunguza utoaji wa hewa chafu kwa nchi tajiri, 0:13:17.000,0:13:21.000 zote zina utatuzi mmoja rahisi. 0:13:21.000,0:13:25.000 Watu wanasema, “Utatuzi ni upi?” Huu hapa. 0:13:25.000,0:13:31.000 Weka bei kwenye kaboni. Tunahitaji kodi ya CO2, mapato 0:13:31.000,0:13:39.000 yatakayoondoa ushuru kwenye ajira, ambao ulivumbuliwa na Bismark -- 0:13:39.000,0:13:40.000 na mambo mengine yamebadilika 0:13:40.000,0:13:41.000 toka karne ya 19. 0:13:41.000,0:13:48.000 Katika ulimwengu maskini, inatubidi tuunganishe mikakati yetu 0:13:48.000,0:13:52.000 juu ya umaskini na utatuzi wa matatizo ya hali ya hewa. 0:13:52.000,0:13:55.000 Mpango wa kupambana na umaskini Uganda 0:13:55.000,0:13:59.000 utaathiriwa iwapo hatutatatua tatizo la hali ya hewa. 0:13:59.000,0:14:07.000 Lakini muitikio unaweza kuleta tofauti kubwa sana 0:14:07.000,0:14:12.000 katika nchi maskini. Hili ni pendekezo 0:14:12.000,0:14:16.000 ambalo limezungumzwa sana huko Ulaya. 0:14:16.000,0:14:20.000 Hii ni kutoka kwenye jarida la Nature Magazine. Hizi zinazingatia 0:14:20.000,0:14:27.000 nishati mbadala ya jua, iliyounganishwa kwenye umeme wa gridi 0:14:27.000,0:14:30.000 kusambaza umeme 0:14:30.000,0:14:38.000 Ulaya kote, zaidi kutoka kwenye nchi zinazoendelea. Umeme wa DC. 0:14:38.000,0:14:41.000 Hii sio “chapati angani,” hii inawezekana. 0:14:41.000,0:14:44.000 Tunahitaji kufanya hili kwa ajili ya uchumi wetu wenyewe. 0:14:44.000,0:14:47.000 Takwimu za hivi karibuni zinaonyesha kuwa muundo wa zamani 0:14:47.000,0:14:51.000 haufanikiwi. Kuna fursa kubwa ya uwekezaji 0:14:51.000,0:14:55.000 ambayo mnaweza kufanya. Kama unawekeza kwenye udongo wa lami 0:14:55.000,0:15:01.000 au mafuta, basi una kibindo 0:15:01.000,0:15:05.000 ambacho kina raslimali za kaboni. 0:15:05.000,0:15:09.000 Na kiko katika muundo wa zamani. 0:15:09.000,0:15:12.000 Walevi wa madawa haramu wanaona mishipa kwenye vidole vyao wakati zile za 0:15:12.000,0:15:17.000 kwenye mikono na miguu yao hazionekani. Kutengeneza lami 0:15:17.000,0:15:23.000 na makaa ni sawa. Hii hapa ni baadhi ya mifano ya uwekezaji 0:15:23.000,0:15:26.000 ambayo nafikiri inaleta maana. 0:15:26.000,0:15:29.000 Nina maslahi katika hizi, kwa hiyo nina udhuru hapa. 0:15:29.000,0:15:32.000 Lakini joto la ardhini, kukusanya nishati ya jua, 0:15:32.000,0:15:38.000 betri za miali ya jua za teknolojia ya hali ya juu, ufanisi na uhifadhi. 0:15:39.000,0:15:42.000 Mmewahi kuona hiki kielelezopicha, lakini kuna mabadiliko. 0:15:42.000,0:15:46.000 Nchi mbili pekee ambazo hazikuridhia 0:15:46.000,0:15:51.000 --na sasa iko moja tu. Australia ilifanya uchaguzi. 0:15:51.000,0:15:54.000 Na kulikuwa na kampeni huko Australia 0:15:54.000,0:15:59.000 ambayo ilihusisha luninga na mtandao na matangazo ya redio 0:15:59.000,0:16:01.000 kuhamasisha uzito wa dharura hii kwa watu wa huko. 0:16:01.000,0:16:05.000 Na tuliwafunza watu 250 jinsi ya kuonyesha kielelezopicha hiki 0:16:05.000,0:16:10.000 katika vitongoji na vijiji na miji huko Australia. 0:16:10.000,0:16:12.000 Vitu vingine vingi vilichangia kwenye hilo, 0:16:12.000,0:16:15.000 lakini Waziri Mkuu mpya alitangaza kwamba 0:16:15.000,0:16:19.000 Jambo lake la muhimu kwanza ni kubadili msimamo wa Australia 0:16:19.000,0:16:24.000 kuhusu Kyoto, na amefanya hivyo. Sasa wameelewa 0:16:24.000,0:16:28.000 sababu mojawapo ikiwa ni ukame mkubwa uliowakumba. 0:16:28.000,0:16:32.000 Hili ni Ziwa Lanier. Rafiki yangu Heidi Cullins 0:16:32.000,0:16:36.000 kama tungekuwa tunatoa majina kwa ukame kama tufanyavyo kwa vimbunga, 0:16:36.000,0:16:39.000 tungeuita ukame wa kusini mashariki Katrina, 0:16:39.000,0:16:41.000 na tungesema kuwa unaelekea Atlanta. 0:16:41.000,0:16:45.000 Hatuwezi kusubiri ukame kama huu 0:16:45.000,0:16:47.000 ili tubadili utamaduni wetu wa kisiasa. 0:16:47.000,0:16:56.000 Hii hapa habari njema. Miji inayounga mkono mkataba wa Kyoto nchini Marekani 0:16:56.000,0:16:59.000 imefikia 780 -- na nadhani niliuona mmoja ukipita pale, 0:16:59.000,0:17:05.000 ukirahisisha hii. Hii ni habari njema. 0:17:05.000,0:17:11.000 Sasa kwa kumalizia, tulisikia siku chache zilizopita 0:17:11.000,0:17:20.000 kuhusu thamani ya kufanya ujasiri uonekane kitu cha kawaida 0:17:20.000,0:17:23.000 ili iwe jambo la kawaida. 0:17:23.000,0:17:32.000 Tunachohitaji sasa ni kizazi kipya cha majasiri. Sisi tulio hai 0:17:32.000,0:17:34.000 ndani ya Marekani 0:17:34.000,0:17:36.000 hasa leo, na hata kwa dunia nzima, 0:17:37.000,0:17:42.000 inabidi waelewe kuwa historia 0:17:42.000,0:17:52.000 imetupa uchaguzi -- kama vile ambavyo Jill Bolte Taylor alipojaribu 0:17:52.000,0:17:57.000 kuokoa maisha yake wakati alipokuwa amekinzwa 0:17:57.000,0:18:01.000 na hali ya kushangaza iliyomkumba. 0:18:01.000,0:18:04.000 Sasa tuna utamaduni wa ukinzani. 0:18:04.000,0:18:09.000 Lakini tuna dharura ya kidunia. 0:18:09.000,0:18:13.000 Inabidi tutafute njia ya kujenga, 0:18:13.000,0:18:19.000 katika kizazi cha walio hai leo, wito wa dhamira 0:18:19.000,0:18:22.000 Natamani ningepata maneno muafaka ya kuelezea hili. 0:18:25.000,0:18:27.000 Hiki kilikuwa ni kizazi kingine shupavu 0:18:27.000,0:18:30.000 kilicholeta demokrasia katika dunia. 0:18:30.000,0:18:37.000 Ambacho kiliondoa utumwa. Na kuwapa wanawake haki ya kupiga kura. 0:18:37.000,0:18:44.000 Tunaweza kulifanya hili. Usiniambie kuwa hatuna uwezo wa kulifanya. 0:18:44.000,0:18:48.000 Iwapo tukiwa na wiki moja tu ya gharama tunaitumia kwenye vita vya Iraki, 0:18:48.000,0:18:51.000 tungekuwa tunakaribia kutatua changamoto hili. 0:18:51.000,0:18:55.000 Tuna uwezo wa kutenda. 0:19:01.000,0:19:14.000 Jambo la mwisho. Nina matumaini, kwasababu nina amini 0:19:14.000,0:19:18.000 tuna uwezo, katika wakati huu wa changamoto kubwa, 0:19:18.000,0:19:24.000 kuweka pembeni ukinzani na kujikwamua kwenye changamoto hili. 0:19:24.000,0:19:27.000 ambalo historia imetuwekea. 0:19:29.000,0:19:41.000 Wakati mwingine nasikia watu wakiongelea kuhusu hali tete ya matatizo ya mabadiliko ya hali ya hewa 0:19:41.000,0:19:43.000 kwa kusema, "Oh, hii mbaya sana. 0:19:43.000,0:19:49.000 Mzigo mkubwa tunao." Ningependa kuwaomba 0:19:49.000,0:19:53.000 mbadilishe hilo. Ni vizazi vingapi 0:19:53.000,0:19:58.000 katika historia ya mwanadamu wamekuwa na fursa 0:19:58.000,0:20:07.000 ya kupambana na changamoto lenye kuhitaji juhudi zetu kubwa? 0:20:07.000,0:20:13.000 Changamoto ambalo litatukamua 0:20:13.000,0:20:21.000 kuliko uwezo wetu wa kutenda? Nafikiri inabidi tukabiliane 0:20:21.000,0:20:25.000 na changamoto hili kwa furaha kubwa 0:20:25.000,0:20:30.000 na shukrani kuwa sisi ni kizazi 0:20:30.000,0:20:34.000 ambacho, miaka elfu ijayo, 0:20:34.000,0:20:43.000 waghani wa muziki na washairi watasheherekea 0:20:43.000,0:20:50.000 kwa kusema, kuwa sisi tulifanikiwa kujitafuta ndani mwetu 0:20:50.000,0:20:55.000 kutatua tatizo hili na kuweka msingi 0:20:55.000,0:20:57.000 kwa maisha ya baadae ya mwanandamu yenye matumaini. 0:20:57.000,0:21:00.000 Tufanye hivyo. Asanteni sana. 0:21:24.000,0:21:30.000 Chris Anderson: Kwa watu wengi wa TED, kuna uchungu mkubwa 0:21:30.000,0:21:32.000 ambao ni wa ubunifu tu -- lakini mwishowe, 0:21:32.000,0:21:34.000 ubunifu kwenye karatasi ya uchaguzi -- 0:21:34.000,0:21:38.000 ubunifu mbaya ni kwamba sauti yako haikusikika 0:21:38.000,0:21:39.000 kama ile ya miaka nane iliyopita katika nafasi 0:21:39.000,0:21:41.000 ambayo ungeweza kufanya kweli. 0:21:41.000,0:21:43.000 Hii inauma. 0:21:43.000,0:21:50.000 Al Gore: Hamuelewi ninyi. (Kicheko). 0:21:53.000,0:21:54.000 CA: Ukiangalia wagombea wanaoongoza 0:21:54.000,0:21:56.000 katika chama chako wanachokifanya kwa sasa – Namaanisha, kuna -- 0:21:56.000,0:22:01.000 unafurahia mipango yao kuhusu matatizo ya hali ya hewa? 0:22:10.000,0:22:14.000 AG: Jibu la swali hilo ni gumu kwangu 0:22:14.000,0:22:18.000 kwasababu, kwa upande mwingine, nadhani kwamba 0:22:18.000,0:22:22.000 ni lazima tuone fahari kwa ukweli kwamba 0:22:23.000,0:22:29.000 mgombea wa Republican – mgombea wa uhakika-- 0:22:29.000,0:22:33.000 John McCain, na wagombea wote 0:22:33.000,0:22:38.000 wa Democratic – wote watatu wana tofauti 0:22:38.000,0:22:40.000 ya mitazamo ya namna ya kusonga mbele 0:22:40.000,0:22:45.000 juu ya matatizo ya hali ya hewa. Wote watatu wameahidi kutoa mwongozo, 0:22:45.000,0:22:49.000 na wote watatu wana mitazamo tofauti kutokana na msimamo 0:22:49.000,0:22:52.000 wa uongozi wa sasa. Na ninadhani 0:22:52.000,0:22:56.000 kuwa wote watatu wamewajibika katika 0:22:56.000,0:23:07.000 kupitisha mipango na mapendekezo. Lakini mazungumzo ya kampeni -- 0:23:07.000,0:23:08.000 kama yalivyofafanuliwa kwa maswali -- 0:23:08.000,0:23:09.000 ambayo yalitayarishwa na 0:23:09.000,0:23:12.000 Umoja wa Wapiga Kura Watunzaji wa Mazingira, mchanganuo wa maswali yote -- 0:23:12.000,0:23:14.000 na, mathalani, midahalo yote 0:23:16.000,0:23:18.000 imedhaminiwa na nembo ya Orwellian, 0:23:18.000,0:23:22.000 “Makaa Safi.” Kuna mtu yeyote ameliona hilo? 0:23:22.000,0:23:26.000 Kila mdahalo ulidhaminiwa na “Makaa Masafi.” 0:23:26.000,0:23:28.000 “Naam, kupunguza zaidi hewa chafu!” 0:23:28.000,0:23:32.000 Ukubwa na uzito wa mazungumzo 0:23:32.000,0:23:35.000 katika demokrasia yetu haujaweka msingi 0:23:35.000,0:23:39.000 katika mikakati thabiti inayohitajika. 0:23:39.000,0:23:42.000 Kwa hiyo wanasema maneno muafaka na itabidi wafanye -- 0:23:42.000,0:23:45.000 yeyote atakayechaguliwa – jambo la muhimu, 0:23:45.000,0:23:49.000 lakini ngoja niwaeleze: niliporudi kutoka Kyoto 0:23:49.000,0:23:56.000 mwaka 1997 nikiwa na hisia za furaha kubwa 0:23:56.000,0:23:58.000 kwamba tumewezakupata utatuzi huko, 0:23:58.000,0:24:00.000 na nililikabili bunge la Marekani, 0:24:00.000,0:24:04.000 lakini mbunge mmoja kati ya 100 alikuwa tayari kupiga kura 0:24:04.000,0:24:11.000 kupitisha, kuridhia mkataba huo. Chochote watakachosema wagombea 0:24:11.000,0:24:16.000 lazima kiwe sambamba na watakachosema watu. 0:24:16.000,0:24:20.000 Changamoto hili ni sehemu ya mfumo 0:24:20.000,0:24:22.000 wa ustaarabu wetu wote. 0:24:22.000,0:24:25.000 CO2 ni pumzi ya ustaarabu wetu. 0:24:26.000,0:24:29.000 Na sasa tumeutengeneza mlolongo huu bandia. Kubadilisha mwelekeo 0:24:29.000,0:24:36.000 kunahitaji upeo, kipimo, mwelekeo wa mabadiliko 0:24:36.000,0:24:39.000 ambayo ni zaidi ya tulivyofanya huko nyuma. 0:24:39.000,0:24:41.000 Na ndio maana ninaanza kwa kusema, 0:24:41.000,0:24:47.000 muwe na matumaini kwa mnachokifanya, lakini muwe raia wenye shauku 0:24:48.000,0:24:50.000 Mahitaji – badilisha taa za umeme, 0:24:50.000,0:24:53.000 lakini pia badilisha sheria. Badilisha mikataba ya kimataifa. 0:24:53.000,0:24:59.000 Ni lazima tuongelee hili. Tutatue hii demokrasia – hii-- 0:25:00.000,0:25:06.000 Tuna sclerosis kwenye demokrasia yetu. Na inabidi tubadili hili. 0:25:07.000,0:25:08.000 Tumia mtandao. Nenda kwenye mtandao. 0:25:08.000,0:25:12.000 Ungana na watu. Muwe raia wenye shauku 0:25:12.000,0:25:14.000 Muweze kuzuia -- hatuwezi 0:25:14.000,0:25:16.000 kuwa na mitambo mipya ya kutengeneza nishati ya makaa 0:25:16.000,0:25:21.000 ambayo haiwezi kuchuja na kutunza CO2. Hii ina maana kwamba inatulazimu 0:25:21.000,0:25:23.000 tujenge haraka vyanzo hivi vya nishati mbadala. 0:25:23.000,0:25:27.000 Kwa sasa, hakuna mtu anaongelea kwenye kiwango hicho. Lakini naamini 0:25:27.000,0:25:31.000 kwamba kati ya sasa na Novemba, inawezekana. 0:25:31.000,0:25:32.000 Huu Mshikamano wa Kutunza Mazingira 0:25:33.000,0:25:36.000 utazindua kampeni ya nchi nzima -- 0:25:36.000,0:25:39.000 uhamasishaji kuanzia shina, matangazo ya luninga, matangazo ya mtandaoni, 0:25:39.000,0:25:42.000 radio, magazeti – kwa kushirikiana na kila mtu 0:25:42.000,0:25:45.000 Kutoka Maskauti wa Kike mpaka wawindaji na wavuvi. 0:25:45.000,0:25:49.000 Tuna hitaji msaada. Tunahitaji msaada. 0:25:49.000,0:25:53.000 CA: Kwa wajibu wako binafsi kusonga mbele, 0:25:53.000,0:25:55.000 Al, kuna kitu kingine zaidi ya hicho 0:25:55.000,0:25:56.000 ambacho utapenda kufanya? 0:25:56.000,0:26:04.000 AG: Nimekuwa nikisali ili niweze kupata jibu 0:26:04.000,0:26:09.000 la swali hilo. Nifanyaje? 0:26:09.000,0:26:13.000 Buckminster Fuller aliandika, "Kama maisha ya baadae ya 0:26:13.000,0:26:18.000 ya ustaarabu yangenitegemea mimi, ningefanya nini? 0:26:18.000,0:26:23.000 Nitakuwaje? Itatutegemea sisi sote, 0:26:23.000,0:26:25.000 hata hivyo, sio kwa taa za umeme tu. 0:26:25.000,0:26:33.000 Wengi wetu hapa, ni Wamarekani. Tuna demokrasia. 0:26:33.000,0:26:39.000 Tunaweza kubadili mambo, lakini tunatakiwa tuhamasike kubadili. 0:26:39.000,0:26:44.000 Kinachotakiwa hasa ni ufahamu zaidi. 0:26:44.000,0:26:46.000 Na hii ni ngumu ku -- 0:26:46.000,0:26:50.000 ni ngumu kuijenga -- lakini inakuja. 0:26:50.000,0:26:53.000 Kuna methali ya zamani ya Kiafrika ambayo baadhi yenu mnaijua 0:26:53.000,0:26:57.000 ambayo inasema, "iwapo unataka kwenda haraka, nenda peke yako; 0:26:57.000,0:27:05.000 iwapo mnataka kwenda mbali, nendeni pamoja. "Inabidi twende mbali haraka. 0:27:05.000,0:27:09.000 Kwahiyo inatubidi tuwe na mabadiliko katika ufahamu. 0:27:09.000,0:27:13.000 Mabadiliko katika malengo. Nia mpya ya dharura. 0:27:13.000,0:27:16.000 Utambuzi mpya wa fursa hii 0:27:16.000,0:27:19.000 tuliyonayo katika kukabiliana na changamoto hili. 0:27:19.000,0:27:23.000 CA: Al Gore, asanteni sana kwa kuja TED 0:27:23.000,0:27:27.000 AG: Asante. Asante sana. (Makofi)