MAJIBU YA BIBLIA YALIYOFICHIKA | INGIA KATIKA ROHO - SEHEMU YA 2
-
0:17 - 0:20Karibu katika Chuo Kikuu cha Mungu.
-
0:20 - 0:25Tunataka kuwashukuru ninyi nyote mliotuma maswali yenu kwetu.
-
0:25 - 0:28Kama mshauri wetu Nabii TB Joshua alivyotuambia:
-
0:28 - 0:33Ikiwa una nia ya somo na una hamu ya kujifunza,
-
0:33 - 0:35utajitahidi kukaa mbele kila wakati,
-
0:35 - 0:39uliza maswali na ushirikiane na mwalimu.
-
0:39 - 0:42Kumbuka katika Chuo Kikuu cha Mungu,
-
0:42 - 0:45moyo, roho ya mtu ni warsha,
-
0:45 - 0:47na Roho Mtakatifu, Mwalimu wa Kimungu.
-
0:47 - 0:49Ndiyo, na hiyo ndiyo ahadi ya Mungu
-
0:49 - 0:52ambayo Yesu alitupa katika Kitabu cha Mathayo 7:7
-
0:52 - 0:55kwamba ukimtafuta, utampata.
-
0:55 - 0:58Ukimtafuta kwa moyo wako wote.
-
0:58 - 1:00Kumbuka, kuutafuta Ufalme wa Mungu
-
1:00 - 1:02ni kuwa na Ufalme wa Mungu.
-
1:02 - 1:05Ndiyo, Mungu hajali shaka au maswali,
-
1:05 - 1:08ilimradi maswali hayo yanatufanya tumtafute,
-
1:08 - 1:12tumkaribie Yeye zaidi, kutafuta Neno Lake.
-
1:12 - 1:14Neno la Mungu ndilo mamlaka ya mwisho suluhu
-
1:14 - 1:18ya maswali na matatizo yote.
-
1:18 - 1:21Leo, chini ya uongozi wa Roho Mtakatifu,
-
1:21 - 1:24tutachunguza baadhi ya maswali yako
-
1:24 - 1:27katika nuru ya Neno la Mungu.
-
1:27 - 1:31Ndiyo, kabisa, na miongoni mwa maswali yaliyotumwa kwetu
-
1:31 - 1:33ni kutoka kwa Anthony anayetokea Kanada
-
1:33 - 1:35Anauliza swali hili la kuvutia, anasema,
-
1:35 - 1:42"Ikiwa hisia zetu ni pazia linatotutenganisha sisi na Mungu, je, kazi ya hizi hisia ni zipi sasa?
-
1:42 - 1:44Kwa nini Mungu alitupatia hizi hisia?
-
1:44 - 1:48Je, hisia hizi zinaweza kutumika kumtafuta Mungu?"
-
1:48 - 1:52Ahsante Anthony kwa kututumia maswali haya.
-
1:54 - 1:57Anthony, ahsante kwa maswali yako.
-
1:58 - 2:00Acha nikupeleke kwenye Biblia.
-
2:00 - 2:06Kitabu cha Zaburi 115:4-7 katika kuonyesha sanamu,
-
2:06 - 2:10kinatupatia picha ya mchoro wa hizi hisia tano.
-
2:11 - 2:16"4 Sanamu zao ni fedha na dhahabu, kazi ya mikono ya wanadamu.
-
2:17 - 2:245 Zina vinywa lakini hazisemi, zina macho lakini hazioni,
-
2:24 - 2:306 Zina masikio lakini hazisikii, zina pua lakini hazisikii harufu,
-
2:30 - 2:387 zina mikono lakini hazishiki...Ahsante.
-
2:38 - 2:42Mungu alitupa fahamu kuu tano
-
2:42 - 2:45ambazo hutuwezesha kuingiliana na ulimwengu wa mwili
-
2:45 - 2:50ambamo tunaishi kama wanadamu.
-
2:50 - 2:55Kazi ya msingi ya hisia hizi tano ni kutusaidia kuwasiliana
-
2:55 - 2:59vya kutosha na watu wanaotuzunguka.
-
2:59 - 3:03Pia hutusaidia kupata tunachodhamiria, kutambua
-
3:03 - 3:08na kukamata vitu vinavyotuzunguka na kutembea kwa usalama
-
3:08 - 3:12katika mazingira yetu.
-
3:12 - 3:14Hisia hizi zote zimeunganishwa.
-
3:14 - 3:17Ninamaanisha, zinafanya kazi pamoja
-
3:17 - 3:21na kutuma kwenye ubongo ishara pokezi
-
3:21 - 3:25au habari kutoka kwenye mazingira,
-
3:25 - 3:28ubongo wetu, ambao ni maabara ya maarifa ya hisia
-
3:28 - 3:30huchakata taarifa hizi zote,
-
3:30 - 3:35hutambua ishara hizo kupitia hifadhidata ya kumbukumbu zetu
-
3:35 - 3:38na hutoa majibu sahihi.
-
3:38 - 3:42Haya yote hutokea katika wakati halisi.
-
3:42 - 3:44Basi hebu tuiangalie milango hiyo mitano ya fahamu.
-
3:44 - 3:49Kwa mlango wa fahamu wa kuona, tunaweza kuona na kutambua vitu
-
3:49 - 3:52ambavyo Mungu aliviumba, vitu na watu wanaotuzunguka.
-
3:52 - 3:54Kuona ndio hisia kuu katika
-
3:54 - 3:56kusafiri kwa usalama katika mazingira yetu,
-
3:56 - 3:59kuendesha gari, kutembea, kusoma.
-
3:59 - 4:00Kwa mlango wa fahamu wa kusikia,
-
4:00 - 4:03hata bila mawasiliano ya kuona, tunaweza kuwa na maarifa wazi
-
4:03 - 4:05ya mazingira yetu ya sasa
-
4:05 - 4:09kwa kutofautisha sauti maalum ambazo hutoa.
-
4:09 - 4:14Kwa mfano, sauti ya ndege au kutambua sauti ya rafiki.
-
4:14 - 4:15Kwa hisia ya harufu
-
4:15 - 4:18tunaweza kujua harufu, manukato,
-
4:18 - 4:22na kuangalia ikiwa kitu ni kizuri au labda chakula kimeharibika.
-
4:22 - 4:24Kwa hisia ya ladha,
-
4:24 - 4:27tunaweza kutathmini utamu au uchungu wa chakula
-
4:27 - 4:29kabla ya kukitumia.
-
4:29 - 4:32Kwa hisia ya kuhisi au kugusa,
-
4:32 - 4:35tunaweza kuhisi halijoto iliyoko
-
4:35 - 4:39kujua mavazi sahihi ya kuvaa ili kulinda miili yetu ipasavyo.
-
4:39 - 4:43Pia,tunaweza kuhisi uzito au ugumu wa kitu.
-
4:43 - 4:46Kwa mfano, chakula hiki kina harufu nzuri.
-
4:46 - 4:48Je, ni chakula gani unachopenda zaidi, Racine?
-
4:48 - 4:50Mchele wa Jollof.
-
4:50 - 4:54Chakula hiki kina harufu nzuri - ndio, nataka kukionja.
-
4:54 - 4:56Au, nguo hizi ni nzuri -
-
4:56 - 4:57nataka kuzinunua.
-
4:57 - 5:00Au, ni baridi sana na kuna upepo leo -
-
5:00 - 5:03sitaki kwenda ufukweni tena.
-
5:03 - 5:06Unaweza kuona jinsi hisia zetu zinavyoweza
-
5:06 - 5:11kuwa na ushawishi kwenye chaguzi na matendo yetu.
-
5:11 - 5:12Zingatia matumizi ya hisi zetu.
-
5:12 - 5:15Kwa mfano, unaendesha gari.
-
5:15 - 5:18ghafla, mtembea kwa miguu anavuka barabara.
-
5:18 - 5:21Kama dereva, unajikuta mara moja
-
5:21 - 5:24na uamuzi, jibu la kuchukua, unaweza kuvuta breki,
-
5:24 - 5:27au kama kasi yako ni kubwa sana,
-
5:27 - 5:30inabidi uende mbali na mtu huyo.
-
5:30 - 5:33Unaweza kuona hisia zote zikifanya kazi pamoja;
-
5:33 - 5:37ninaona, ninavuta breki; ninageuza gurudumu.
-
5:37 - 5:41Kwa hivyo vitendo hivi vyote hufanyika wakati huo huo kwa wakati halisi.
-
5:41 - 5:43Vyote vimeunganishwa.
-
5:43 - 5:46Vinafanya kazi pamoja.
-
5:46 - 5:49Unaweza kuona ni ushawishi kiasi gani
-
5:49 - 5:54hisia zetu zinaweza kuwa kwenye chaguzi na matendo yetu.
-
5:54 - 6:02Tunachoona, kusikia, kunusa, kuonja, kuhisi kinaweza kuathiri mawazo yetu.
-
6:02 - 6:04Ninamaanisha nini kwa kushawishi mawazo yetu?
-
6:04 - 6:10Ninamaanisha, vina ushawishi juu ya tamaa na mapenzi yetu.
-
6:10 - 6:14Mawazo yetu yanaweza kuathiri matendo yetu au kutotenda.
-
6:14 - 6:15Kwa nini?
-
6:15 - 6:19Kwa sababu mwanadamu hufanya mapenzi yake kupitia akili yake.
-
6:19 - 6:23Hiyo ndiyo maana ya busara au kufikiri.
-
6:23 - 6:26Binadamu ni tofauti na wanyama.
-
6:26 - 6:28Binadamu sio roboti.
-
6:28 - 6:32Yeye ni wakala huru wa maamuzi.
-
6:32 - 6:36Kwa sababu ya ushawishi kutokana na mwingiliano na mazingira
-
6:36 - 6:40ambayo yanahitaji majibu au mtazamo sahihi,
-
6:40 - 6:45Mungu anamtaka mtu kuwa na akili huru -
-
6:45 - 6:49akili inayofikiri yenyewe.
-
6:49 - 6:51Mungu amempa mwanadamu
-
6:51 - 6:55uwezo wa kufikiria na kuchagua kati ya kile kinachofaa au la -
-
6:55 - 6:57hiyo ni akili ya kawaida,
-
6:57 - 7:00kuchagua kati ya mema au mabaya,
-
7:00 - 7:02hiyo ni hisia ya hukumu,
-
7:02 - 7:06kuchagua kati ya mema na mabaya - hiyo ni hisia ya maadili.
-
7:06 - 7:10Hayo ni matokeo ya hisia za kufikiri na uwajibikaji -
-
7:10 - 7:15ambazo ni muhimu kwa maisha katika jamii au kikundi.
-
7:15 - 7:20Mwanadamu kulingana na urefu wa maisha yake, hukua kimwili
-
7:20 - 7:24kutoka katika kiinitete hadi kuwa mtoto mchanga,
-
7:24 - 7:30kupitia utoto, ujana, utu uzima na uzee.
-
7:30 - 7:35Tunaweza kuona kwamba kukua kimwili ni kazi ya wakati.
-
7:35 - 7:37Tunapokua katika umri,
-
7:37 - 7:42tunapitia hatua za maisha ya mwanadamu.
-
7:42 - 7:45Mwanadamu si mtu wa kimwili tu
-
7:45 - 7:49bali mtu mwenye akili na maadili.
-
7:49 - 7:52Hasa! Na ni muhimu kukumbuka kwamba
-
7:52 - 7:56kwa sababu maisha na majukumu yake yako katika hatua,
-
7:56 - 8:00mwanadamu pia lazima akue katika ukomavu wa kiakili.
-
8:00 - 8:02Kivipi?
-
8:02 - 8:05Ukuaji wa kiakili ni kazi ya kujifunza -
-
8:05 - 8:07kujifunza kutokana na kile tunachofanya.
-
8:07 - 8:10Kujifunza kutoka kwa kile tunachojifunza, kile kinachotokea karibu nasi
-
8:10 - 8:14na kujifunza kile kinachotokea kwetu.
-
8:14 - 8:17Umewahi kujiuliza kila mtu anapokutana na mtu mpya
-
8:17 - 8:19katika uhusiano mpya?
-
8:19 - 8:22Maswali ya kwanza watakayojiuliza wenyewe
-
8:22 - 8:28yatahusu historia yao, elimu, kazi katika maisha.
-
8:28 - 8:32Wachache sana watashughulikia maisha yao ya kiroho.
-
8:32 - 8:36Na hilo ndilo linaloleta tofauti kati ya mtazamo wa mwanadamu
-
8:36 - 8:40na mtazamo wa Mungu.
-
8:40 - 8:44Ndiyo, katika Wagalatia 5,
-
8:44 - 8:49Mungu asingetuamuru tuenende katika Roho
-
8:49 - 8:54kama hakututengeneza sisi kufanya kazi katika Roho.
-
8:54 - 8:57Biblia inasema kwamba Mungu alimuumba mwanadamu,
-
8:57 - 9:02wanadamu, kwa sura na mfano wake.
-
9:02 - 9:04Kitabu cha Ayubu 33:4 kinasema
-
9:04 - 9:08mwanadamu ni zao kuu la Roho Mtakatifu;
-
9:08 - 9:12mwanadamu ni kazi ya kiungu ya sanaa.
-
9:12 - 9:13Kwa nini?
-
9:13 - 9:17Kwa sababu wanadamu wamekusudiwa kufikiri, kuzungumza,
-
9:17 - 9:22kutenda na kupanga na Mungu.
-
9:22 - 9:26Kwa hiyo mwanadamu amekusudiwa kuishi katika kupatana na Mungu.
-
9:26 - 9:28Je, tunaishi sambamba na Mungu?
-
9:28 - 9:32Siku zote kumbuka Mungu ni Roho.
-
9:32 - 9:36Kwa hiyo swali ambalo tunapaswa kujiuliza ni:
-
9:36 - 9:39mwanadamu ni nani?
-
9:39 - 9:41Hilo ndilo swali.
-
9:41 - 9:48Biblia ni hifadhidata ya mwamini kwa maoni yake binafsi.
-
9:48 - 9:54Je, Biblia inasema nini kuhusu mwanadamu, kuhusu wewe na mimi?
-
9:55 - 10:00Biblia inasema katika kitabu cha 1Wathesalonike 5:23
-
10:00 - 10:04kwamba, mtu ni kiumbe wa kiroho
-
10:04 - 10:08ambaye ana roho na mwili.
-
10:08 - 10:15Kwa maneno mengine, mwanadamu ana asili ya kimwili na ya kiroho.
-
10:15 - 10:19Mwanadamu sio tu mtu wa kimwili, kiakili;
-
10:19 - 10:25yeye pia ni mtu wa maadili na mtu wa kiroho,
-
10:25 - 10:28kwa sababu tumeumbwa kuwa kama Mungu
-
10:28 - 10:33ndani ya mioyo yetu na Mungu ni Roho.
-
10:33 - 10:34Kwa hivyo zingatia.
-
10:34 - 10:38Kila mara Biblia inaporejelea moyo wa mwanadamu,
-
10:38 - 10:43inazungumzia roho ya mtu - roho ya mwanadamu.
-
10:43 - 10:50Ndio maana katika Kitabu cha 1 Samweli 16:7, na Mathayo 15:8,
-
10:50 - 10:53Biblia inakazia kwamba
-
10:53 - 10:57inapokuja kwa hukumu ya haki, mtazamo wa Mungu,
-
10:57 - 11:02kuhusu mwanadamu daima huelekea kwenye moyo wa mwanadamu, roho ya mwanadamu.
-
11:02 - 11:06Hii ina maana kwamba Mungu humwona mwanadamu kama kiumbe cha roho,
-
11:06 - 11:10anayeishi katika mwili wa kawaida.
-
11:10 - 11:15Roho ya mwanadamu ni sehemu ya mwanadamu ambayo ina ufahamu wa kiroho.
-
11:15 - 11:18Ninamaanisha, uelewa wa kiroho.
-
11:18 - 11:21Roho ya mwanadamu ni sehemu ya mwanadamu
-
11:21 - 11:24ambayo imeunganishwa na ulimwengu wa kiroho
-
11:24 - 11:30na hupokea miongozo na ufunuo kutoka kwa Mungu, ambaye ni Roho.
-
11:30 - 11:33Hebu tumfikirie sasa mtu kutoka kwenye kibiblia
-
11:33 - 11:37ambaye alikuwa hasa katika maelewano na Mungu katika Roho.
-
11:37 - 11:38Tunapaswa kumkumbuka Musa.
-
11:38 - 11:40Fikiria mtazamo wa Musa
-
11:40 - 11:43pale yeye na watu wake walipokuwa wamenaswa
-
11:43 - 11:48katikati ya Bahari Nyekundu na majeshi ya Misri yanayowafuata.
-
11:48 - 11:52Hakika watu wa Israeli walikuwa na kila sababu ya
-
11:52 - 11:56kufikiri kwamba mwisho ulikuwa umefika
-
11:56 - 12:00ukizingatia ukubwa na nguvu za kijeshi za majeshi ya Misri.
-
12:00 - 12:03Tunaweza kusoma kuhusu hili katika Kitabu cha Kutoka 14:10.
-
12:03 - 12:07"Basi Waisraeli wakalia si kwa hofu tu,
-
12:07 - 12:12bali pia katika uasi na hasira iliyoelekezwa dhidi ya Musa na Mungu wake."
-
12:12 - 12:17Waliruhusu hisia zao kuamuru mwelekeo wa imani yao
-
12:17 - 12:20na kuingiwa na hofu
-
12:20 - 12:25na kusahau kabisa miujiza yote ambayo Mungu alikuwa amewafanyia
-
12:25 - 12:28na kufanya kwa niaba yao.
-
12:28 - 12:33Badala ya kukasirishwa na mwitikio wa watu wake - ukosefu wa imani,
-
12:33 - 12:37Musa alikuwa mtulivu, makini na dhabiti.
-
12:37 - 12:41Hata katikati ya uchochezi mkali,
-
12:41 - 12:45Biblia inasema alikuwa mtulivu sana, mwenye kujiamini na mwenye amani.
-
12:45 - 12:46Kwa nini?
-
12:46 - 12:49Kwa sababu mtazamo wa roho yake ulikuwa kwa Mungu.
-
12:49 - 12:53Ninamaanisha, roho yake ilikuwa imeunganishwa na Mungu.
-
12:53 - 12:57Na ndio maana aliweza kushinda kile ambacho akili zake zilikuwa zikimwambia.
-
12:57 - 13:01Kweli - mtu wa kiroho na mtu wa imani - Musa.
-
13:01 - 13:04Mafunzo ni mengi ya kujifunza kutoka kwake.
-
13:04 - 13:10Swali ni kwa nini mwanadamu hawezi kutumia hisia zake kumtafuta Mungu?
-
13:10 - 13:12Hilo ndilo swali.
-
13:12 - 13:15Jibu la swali hili ni la moja kwa moja.
-
13:15 - 13:18Mungu ni Roho.
-
13:18 - 13:22Kwa hiyo, hatuwezi kumjua Mungu kwa hisia na
-
13:22 - 13:25ufahamu au uwezo wa nje wa binadamu
-
13:25 - 13:31kwa sababu Mungu haonekani, ni wa kiroho, si wa kimwili.
-
13:31 - 13:35Yeye ni kiumbe mkuu anayeishi katika ulimwengu juu ya hisia.
-
13:35 - 13:38Anaishi katika Roho.
-
13:38 - 13:45Kwa hiyo, ili kumtafuta Mungu, ni lazima uwe katika roho.
-
13:45 - 13:48Na unaweza tu kumuona na kuhusiana Naye
-
13:48 - 13:52katika ulimwengu wa roho kupitia ufunuo.
-
13:52 - 13:54Je, tunamaanisha nini kwa ufunuo?
-
13:54 - 13:58Ufunuo huleta katika hisia zetu za kiroho
-
13:58 - 14:03ukweli wa mambo ya kiroho ambayo hayawezi kutambulika
-
14:03 - 14:08kwa hisiai zetu za asili za kibinadamu.
-
14:08 - 14:14Kama vile tulivyo na viungo vya asili vilivyowekwa katika miili yetu ya kimwili
-
14:14 - 14:18ambazo hulisha hisia zetu za kibinadamu kwa habari
-
14:18 - 14:20kutoka kwenye mazingira
-
14:20 - 14:26kama macho yetu, masikio yetu, mikono yetu, nk
-
14:26 - 14:31Mungu pia ametujalia hisia za kiroho
-
14:31 - 14:36vile vile, zilizounganishwa katika roho zetu.
-
14:36 - 14:40Hisia kuu ya kiroho ambayo Mungu ameiweka ndani ya roho zetu
-
14:40 - 14:43ni dhamiri zetu.
-
14:43 - 14:50Dhamiri ni kiungo cha roho cha kutambua mambo ya kiroho.
-
14:50 - 14:55Hiyo ndiyo maana Nabii TB Joshua anaiita hali ya haki.
-
14:55 - 15:11Hebu tumsikilize Mtume Paulo alivyosema katika kitabu cha Warumi 8:16.
-
15:12 - 15:14Paulo alisema,
-
15:17 - 15:2516 "Ni Roho mwenyewe anayeshuhudia pamoja na roho zetu kwamba sisi ni wana wa Mungu."
-
15:25 - 15:28Hii ina maana gani?
-
15:28 - 15:31Hii ina maana kwamba hisia ya haki
-
15:31 - 15:34huleta mwamko wa kujijua.
-
15:34 - 15:40Ninaamaanisha, ufahamu wa wewe ni nani katika Kristo Yesu.
-
15:40 - 15:44Swali ni: Je, ufahamu huu unakujaje?
-
15:44 - 15:47Ufahamu huo unakuja kwa njia ya ufunuo
-
15:47 - 15:52wakati Roho Mtakatifu anaposhuhudia rohoni mwetu.
-
15:52 - 15:56Roho Mtakatifu anashuhudiaje rohoni mwetu?
-
15:56 - 15:59Kupitia dhamiri zetu.
-
15:59 - 16:05Paulo alielezea zaidi katika Warumi 9:1.
-
16:05 - 16:07Anasema,
-
16:07 - 16:249 "Ninasema kweli katika Kristo na dhamiri yangu inanishuhudia kwa njia ya Roho Mtakatifu kuwa sisemi uongo."
-
16:26 - 16:34Kwa hiyo, 1 Wakorintho 2:9-15 inatufundisha kwamba hisia zetu za asili
-
16:34 - 16:39haziwezi kufahamu wala kujua mambo ya Mungu au mambo ya Roho
-
16:39 - 16:43kwa sababu yanaweza tu kutambulika kiroho.
-
16:43 - 16:46Na ikiwa haya yote yanaonekana kuwa mengi kwako, usijali.
-
16:46 - 16:50Katika safu ya msingi tunapoendelea, haya yote yatanyambulishwa.
-
16:50 - 16:52ili kwamba uweze kuelewa kweli
-
16:52 - 16:56jinsi tunavyoweza kuhusiana na Mungu kupitia roho zetu
-
16:56 - 17:00na mtu ni nini hasa - roho yake, mwili wake, nafsi yake.
-
17:00 - 17:04Kwa hivyo subiri unapopata zaidi juu ya haya kwenye safu ya msingi
-
17:04 - 17:05inayokuja hivi karibuni.
-
17:05 - 17:07Kwa hivyo inapokuja kwenye maarifa ya mwanadamu,
-
17:07 - 17:10hisia zetu haziwezi kuona moyo au roho ya mwanadamu.
-
17:10 - 17:13Vinaweza tu kuona mwili wa mwanadamu kwa sababu ndiyo
-
17:13 - 17:18sehemu ya mwanadamu ambayo imeunganishwa na ulimwengu huu unaoonekana.
-
17:18 - 17:20Eneo la hisia.
-
17:20 - 17:25Mwili na hisi za mwanadamu haziwezi kuunganishwa na ulimwengu wa kiroho.
-
17:25 - 17:30Ni roho ya mwanadamu pekee ambayo ni sehemu ya kiroho ya mwanadamu
-
17:30 - 17:35ambayo inaweza kuunganishwa na makao ya roho, ambayo ni mahala pa Mungu.
-
17:35 - 17:37Kweli, ndivyo hivyo.
-
17:37 - 17:41Swali ni: Je, tunaangaliaje katika mwelekeo huo?
-
17:41 - 17:45Ili kuingia kwenye ulimwengu huo wa roho,
-
17:45 - 17:50mwanadamu lazima awe katika roho akiongozwa na Roho Mtakatifu.
-
17:50 - 17:53Roho zetu, mioyo yetu ndio sehemu ya mawasiliano,
-
17:53 - 17:56mahali pa kuwasiliana na Roho Mtakatifu.
-
17:56 - 17:58Roho Mtakatifu anatumia mioyo yetu
-
17:58 - 18:01kuwasiliana nasi.
-
18:01 - 18:08Na Mungu anazungumza na mioyo yetu, na roho zetu, sio masikio yetu.
-
18:08 - 18:13Ninakushauri usome Kitabu cha Matendo 17 -
-
18:13 - 18:17wakati watu wa Athene walipokuwa wakimtafuta Mungu
-
18:17 - 18:20kwa akili zao na maarifa ya hisia
-
18:20 - 18:25ili kumtafuta na kumwabudu Mungu.
-
18:25 - 18:26Acha nisome
-
18:33 - 18:39Matendo ya Mitume 17:23
-
18:39 - 18:5823 "Kwa kuwa nilipokuwa nikitembea mjini niliona sehemu nyingi za kuabudia. Niliona pia madhabahu moja iliyoandikwa, ‘Kwa Mungu asiyejulikana.’ Huyo Mungu mnayemwabudu bila kumfahamu, ndiye ninayemtangaza kwenu."
-
18:58 - 19:0924 Mungu aliyeumba dunia na vitu vyote vilivyomo, ambaye pia ni Bwana wa mbingu na nchi, haishi katika mahekalu yaliyojengwa na wanadamu.
-
19:09 - 19:2025 Wala hahudumiwi kwa mikono ya wanadamu kana kwamba anahitaji cho chote; kwa sababu yeye ndiye anayewapa watu wote uhai na pumzi na kila kitu.
-
19:21 - 19:3526 Yeye aliumba mataifa yote ya wanadamu waishi juu ya nchi kutokana na mtu mmoja. Pia amepanga muda wa maisha ya watu wote, akaweka na mipaka ya mahali watakapoishi
-
19:35 - 19:4727 ili wamtafute Mungu na wamfahamu. Lakini Yeye hayuko mbali nasi kwa maana
-
19:47 - 20:0028 ‘Tunaishi na kuenenda na kuwa na uhai ndani yake,’ na kama mtunga mashairi wenu alivyosema, ‘Sisi ni uzao wa Mungu.’
-
20:00 - 20:2129 Kwa kuwa sisi ni wa uzao wa Mungu hatupaswi kudhani kuwa yeye ni kama sanamu ya dhahabu au fedha au jiwe iliyotengenezwa kwa akili na ufundi wa mwanadamu.
-
20:23 - 20:27Kwa kuwa watu wote wana roho, tunapaswa kujiuliza swali
-
20:27 - 20:36Kwa nini inaonekana kwamba wanadamu wengi hawana uhusiano wowote na Mungu?
-
20:36 - 20:40Ukweli ni kwamba Mungu amewaumba wanadamu
-
20:40 - 20:45kufanya kazi katika ulimwengu wa asili na wa kiroho.
-
20:45 - 20:51Lakini wengi wetu tunaishi katika hisia, ninamaanisha katika asili.
-
20:51 - 20:56Na sisi tuko butu inapokuja kwa mambo ya Roho.
-
20:56 - 21:00Kwa sababu kama Maandiko yanavyosema katika Kitabu cha 1 Wakorintho 2:9
-
21:00 - 21:03mambo ya Rohoni si dhahiri.
-
21:03 - 21:05Hatuwezi kuyaona.
-
21:05 - 21:12Na Biblia inasema zaidi katika 1 Wakorintho 15:46-47,
-
21:12 - 21:15Ngoja nisome.
-
21:16 - 21:381 Wakorintho 15:46.
-
21:38 - 21:4646 Lakini si yule wa kiroho aliyekuja kwanza; bali ni yule wa mwili, na kisha yule wa kiroho.
-
21:47 - 22:0147 Mtu wa kwanza alitoka katika nchi, alifanywa kwa mavumbi; mtu wa pili ni Bwana kutoka mbinguni.
-
22:01 - 22:1448 Na kama alivyokuwa yule wa ardhini, ndivyo walivyo wale walio wa ardhini; na alivyo mtu wa mbinguni, ndivyo walivyo wale walio wa mbinguni.
-
22:15 - 22:21Maandiko haya tuliyosoma hivi punde yanabainisha aina mbili za wanaume.
-
22:21 - 22:25Mtu wa asili na mtu wa kiroho.
-
22:25 - 22:31Mwanadamu wa asili ni kipofu wa kiroho na ni butu katika ufahamu
-
22:31 - 22:34katika ulimwengu usioonekana.
-
22:34 - 22:40Ulimwengu wa roho umefungwa kabisa nje ya maono yake ya kiroho.
-
22:40 - 22:44Ni wakati tu Roho Mtakatifu anaangaza macho yake ya kiroho
-
22:44 - 22:50ili aweze kuona na kuelewa mambo ya Rohoni.
-
22:50 - 22:55Waefeso 1:7-18 inasema kwamba Bwana Mungu wetu Yesu Kristo,
-
22:55 - 22:58Baba wa Utukufu, anaweza kutupa Roho wa Ufunuo
-
22:58 - 23:02na hekima katika kumjua Yeye
-
23:02 - 23:06ili macho ya ufahamu wetu yafumbuliwe
-
23:06 - 23:10Ili tuweze kujua tumaini la mwito wake ni nini
-
23:10 - 23:13na utajiri wa utukufu wake ukoje
-
23:13 - 23:17katika urithi wake wa watakatifu.
-
23:17 - 23:32Ninatumaini mna Biblia zenu hapo, twende sasa kwenye 1 Wakorintho 2:9 na tusome pamoja kuanzia mstari wa 9 mpaka ule wa 12.
-
23:32 - 23:439 Lakini, kama Maandiko yasemavyo, Hakuna aliyeona, hakuna aliyesikia, hakuna aliyewaza, kile ambacho Mungu amekiandaa kwa ajili ya watu wampendao.
-
23:43 - 23:5310 Lakini Mungu amejidhihirisha kwetu kwa njia ya Roho wake. Roho huchunguza kila kitu, hata mambo ya ndani ya Mungu.
-
23:53 - 24:0611 Kwa maana ni nani anajua mawazo ya mtu isipo kuwa roho aliye ndani ya huyo mtu? Vivyo hivyo hakuna mtu anayeelewa mawazo ya Mungu isipokuwa Roho wa Mungu.
-
24:06 - 24:1512 Sisi hatukupokea roho ya dunia hii bali Roho aliyetoka kwa Mungu ili tuweze kuelewa yale ambayo Mungu ametupatia bure
-
24:15 - 24:20Kwa hiyo swali ni: Je, tunaunganishwaje na Roho?
-
24:20 - 24:22Je, unaunganaje na Roho?
-
24:22 - 24:25Kwa imani.
-
24:25 - 24:31Kumwamini Kristo Yesu - huo ndio muunganiko wetu pekee.
-
24:31 - 24:34Kwa hiyo tunaishije kwa imani?
-
24:34 - 24:37Kumbuka, tunaishi kwa imani
-
24:37 - 24:45tunapotambua muungano wetu na Yesu Kristo katika roho.
-
24:45 - 24:46Kuishi kwa imani,
-
24:46 - 24:51roho zetu lazima zitawale hisia zetu,
-
24:51 - 24:53na ili roho zetu zitawale hisia zetu,
-
24:53 - 24:57mawazo yetu lazima yafanywe upya kwa kulijua Neno
-
24:57 - 25:00na kulifanyia kazi.
-
25:00 - 25:05Kwa hiyo tunajuaje kwamba akili zetu zimefanywa upya?
-
25:05 - 25:07Swali zuri.
-
25:07 - 25:10Akili zetu zinafanywa upya
-
25:10 - 25:14tunapoanza kufikiria sio juu ya udhaifu wetu
-
25:14 - 25:21na mapungufu, bali haki yetu katika Kristo Yesu.
-
25:21 - 25:262 Wakorintho 12:7-10
-
25:26 - 25:32Yote ni kuhusu uzoefu wa Mtume Paulo na mwiba.
-
25:35 - 25:547 Na ili nisijione bora kuliko nilivyo, kutokana na mafunuo haya makuu, nilipewa mwiba katika mwili wangu, mtumishi wa shetani, ili anitese.
-
25:54 - 26:008 Nilimsihi Bwana mara tatu aniondolee mwiba huu.
-
26:01 - 26:219 Lakini aliniambia, “Neema yangu inakutosha, kwa kuwa uwezo wangu unakamilika katika udhaifu.” Kwa hiyo nitajisifu kwa furaha zaidi kuhusu udhaifu wangu ili uwezo wa Kristo ukae juu yangu.
-
26:22 - 26:27Unaona, wakati Paulo alipoteswa na mwiba katika mwili wake.
-
26:27 - 26:31alimwomba Mungu mara nyingi ili Mungu aondoe mwiba huo.
-
26:31 - 26:35Lakini Mungu akamwambia: “Neema yangu yakutosha.”
-
26:35 - 26:36Kwa nini?
-
26:36 - 26:42Maana nguvu zangu hukamilishwa katika udhaifu.
-
26:42 - 26:46Mara, ufunuo wa mapenzi ya Mungu ulippomjia,
-
26:46 - 26:49Paulo hakulalamika tena.
-
26:49 - 26:53Akasema badala yake, ninapokuwa dhaifu, nina nguvu.
-
26:53 - 26:57Akili yake ilifanywa upya na akaacha kuwa na wasiwasi
-
26:57 - 27:00kuhusu mwiba katika mwili wake.
-
27:00 - 27:05Kwa hivyo, hebu tufanye muhtasari wa majibu ya maswali haya yote.
-
27:05 - 27:11Mtu wa asili - mtu wa hisia anaufahamu kuhusu mwili wake tu.
-
27:11 - 27:13na hana ufahamu wa ulimwengu wa roho.
-
27:13 - 27:16Kwa nini iko hivyo?
-
27:16 - 27:18Biblia inasema tangu kuanguka kwa mwanadamu,
-
27:18 - 27:22mwanadamu amepoteza fahamu zake za roho
-
27:22 - 27:26kwa sababu ya dhambi na hufanya kazi katika asili tu.
-
27:26 - 27:29Tunaweza kusoma kuhusu hili katika Mwanzo 6:3.
-
27:29 - 27:33Roho ya mwanadamu wa asili imekufa kwa Mungu kwa sababu ya dhambi
-
27:33 - 27:35tangu Adamu,
-
27:35 - 27:39mwili wa mwanadamu, ambao Biblia inauita utu wa nje,
-
27:39 - 27:44mtu wa nje au mzee ni sehemu ya mwili ya mwanadamu
-
27:44 - 27:48iliyoundwa na Mungu kuingiliana na ulimwengu unaoonekana au wa mwili.
-
27:48 - 27:50Hiyo ni kweli.
-
27:50 - 27:52Wakati roho ya mwanadamu
-
27:52 - 27:56ni sehemu ya kiroho ya mwanadamu iliyoundwa na Mungu
-
27:56 - 28:00kuingiliana au kuwasiliana na yasiyoonekana
-
28:00 - 28:05au ulimwengu wa kiroho ambapo Mungu anakaa.
-
28:05 - 28:07Kwa hiyo mtu wa kiroho ni,
-
28:07 - 28:11yule ambaye roho yake imeumbwa upya au kufanywa upya
-
28:11 - 28:16kwa nguvu za Mungu katika hatua ya kuzaliwa upya kiroho kwa imani
-
28:16 - 28:18katika Kristo Yesu.
-
28:18 - 28:21Hivyo ndivyo Yesu alimaanisha alipomwambia Nikodemo
-
28:21 - 28:23katika kitabu cha Yohana 3:3.
-
28:23 - 28:25Unahitaji kuzaliwa mara ya pili.
-
28:25 - 28:28Yesu akajibu, akamwambia, Hakika,
-
28:28 - 28:32Nawaambia, Mtu asipozaliwa mara ya pili,
-
28:32 - 28:36hawezi kuuona ufalme wa Mungu” (Yohana 3:3).
-
28:37 - 28:40Tuko hapa leo kuutafuta Ufalme wa Mungu
-
28:57 - 29:05Unamaanisha nini unaposema kwa nje?
-
29:07 - 29:12Kwa hivyo unamaanisha nini unaposema kwa "nje"?
-
29:12 - 29:18Kwa "nje", tunamaanisha kile kinachoonekana, nyenzo, kimwili -
-
29:18 - 29:22vitu unavyoweza kuona kwa macho yako ya asili,
-
29:22 - 29:24kusikia kwa masikio yako,
-
29:24 - 29:29mambo ambayo unaweza kuhisi au kuyajua kiakili.
-
29:29 - 29:31Kinyume chake, 'ndani' inarejelea
-
29:31 - 29:36mambo ambayo hatuwezi kuyaona, kama moyo wa mwanadamu, roho ya mwanadamu,
-
29:36 - 29:41ambayo ni hali ya kiroho ya mwanadamu ambayo ni Mungu pekee anaweza kuona.
-
29:41 - 29:44Ndiyo maana, kuhusu wanadamu,
-
29:44 - 29:46mtu anahitaji kuongozwa na ufunuo wa kiungu
-
29:46 - 29:51ili kupata kiini cha jambo linapokuja suala la hukumu.
-
29:51 - 29:53Tunapolijua hili.
-
29:53 - 29:56Tunajua kwamba hatupaswi kumhukumu mtu yeyote kwa sura
-
29:56 - 29:59kwa sababu Mungu pekee ndiye anayejua hali halisi
-
29:59 - 30:03ya moyo wa mwanadamu.
-
30:03 - 30:08Inapokuja kwa mambo ya Mungu asiyeonekana,
-
30:08 - 30:10tunahitaji kuwa katika roho
-
30:10 - 30:13kwa sababu imani pekee ndiyo impendezayo Mungu.
-
30:13 - 30:17Waebrania 11:6
-
30:17 - 30:22Pasipo imani haiwezekani kumpendeza;
-
30:22 - 30:27kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba Mungu yuko
-
30:27 - 30:32na kwamba Yeye ndiye Mlipaji wa wale wanaomtafuta kwa bidii.
-
30:32 - 30:37Tunamtafuta kwa bidii, kama tulivyosema leo, kwa imani.
-
30:37 - 30:41Kumbuka, imani inamlenga Mungu asiyeonekana,
-
30:41 - 30:45wakati maono ya asili yanalenga nje, kinachoonekana,
-
30:45 - 30:49kile kinachoonekana, ambacho ni halisi.
-
30:49 - 30:52Kwa hiyo mtu wa kiroho, ninamaanisha, mtu wa imani
-
30:52 - 30:56haridhiki na ujuzi wa akili bali hutazama zaidi ya hayo,
-
30:56 - 31:00kwa sababu Biblia inasema katika 2 Wakorintho 5:7,
-
31:00 - 31:02tunaenenda kwa imani, si kwa kuona.
-
31:02 - 31:05Ndiyo, imani ni kutoka katika roho ya mwanadamu.
-
31:05 - 31:08Ninamaanisha ulimwengu usioonekana au ulimwengu wa kiroho.
-
31:08 - 31:11Na kuona ni kutoka katika mwili wa mwanadamu,
-
31:11 - 31:15ulimwengu unaoonekana au ulimwengu wa asili.
-
31:16 - 31:22Na sasa, hebu tutazame tena katika kitabu cha 2 Wakorintho 4 kuanzia mstari wa 18.
-
31:22 - 31:23Hebu tusome pamoja.
-
31:23 - 31:272 Wakorintho 4:18
-
31:28 - 31:4218 Kwa maana hatuweki mawazo yetu kwenye vitu vinavyoonekana bali kwenye vitu visivyoonekana. Maana vile vinavyoonekana ni vya muda mfupi, lakini vile visivyoonekana vinadumu milele.
-
31:42 - 31:50Na Biblia inasema zaidi katika 1 Samweli 16:6-13, unaweza kusoma zaidi kwa undani katika wakati wako.
-
31:50 - 31:55yote ni kuhusu Samweli na Daudi, mfalme wa pili wa Israeli.
-
31:55 - 32:00Samweli, nabii alitumwa kwenye nyumba ya Yese huko Bethlehemu
-
32:00 - 32:05kumtia mafuta mfalme mpya aliyewekwa rasmi wa Israeli.
-
32:05 - 32:10Alipofika, alimtazama mwana wa Yese mwenye sura nzuri zaidi
-
32:10 - 32:15kama mfalme mteule lakini Mungu alimkataa
-
32:15 - 32:17na akamchagua aliyepuuzwa.
-
32:17 - 32:23mvulana wa kawaida mdogo na mchungaji, Daudi
-
32:23 - 32:27Muulize Nabii Samweli katika Kitabu cha 1 Samweli 16:7
-
32:27 - 32:30na angekufundisha kwamba
-
32:30 - 32:33tunapaswa kujifunza kutozingatia nje.
-
32:33 - 32:39Ninamaanisha, sio juu ya sifa za nje za mwanadamu zinazoonekana.
-
32:39 - 32:42Lakini tunapaswa kuzingatia ndani kwa kuangalia ndani
-
32:42 - 32:45moyoni kwa msaada wa Roho Mtakatifu.
-
32:45 - 32:51Ikiwa tunataka kuona mambo jinsi Mungu anavyoyaona juu ya mwanadamu.
-
32:51 - 32:53Kwa hiyo asante sana.
-
32:53 - 32:57Ndio, huo ulikuwa mtazamo mfupi wa maana yake - 'nje' na 'ndani'.
-
32:57 - 33:02Na ndio, sote tunahitaji kuukuza utu wetu wa ndani, mtu wetu wa kiroho.
-
33:02 - 33:06Na kwa msaada wa Roho Mtakatifu kila siku, kila wakati tunaweza.
-
33:11 - 33:18Mtu anawezaje kukuza imani kwa Mungu, kwa dhati?
-
33:18 - 33:24Kwanza, kuna haja ya kujua imani ni nini.
-
33:24 - 33:28Tatizo la imani linafanywa kuwa rahisi kueleweka pale tu
-
33:28 - 33:31tunapojua kwamba imani ni kutenda tu
-
33:31 - 33:34juu ya kile ambacho Mungu amesema.
-
33:34 - 33:40Suala kuu la imani yetu ni ukweli wa imani hiyo.
-
33:40 - 33:44Ili imani iwe ya kweli, lazima itegemee Neno la Mungu,
-
33:44 - 33:52ambalo ni Roho na Uzima. ( Yohana 6:63 )
-
33:52 - 33:55Mwanadamu huongea maneno ya kawaida
-
33:55 - 34:02bali Mungu hunena Maneno ambayo ni Roho na Uzima.
-
34:02 - 34:05Lakini ili neno la mwanadamu liwe Neno la Mungu,
-
34:05 - 34:09lazima liathiriwe na Roho Mtakatifu kwa uzima.
-
34:09 - 34:14Swali ni: Je, mwanadamu anaweza kusema Maneno ya Uzima?
-
34:14 - 34:16Mwanadamu huongea maneno ya kawaida
-
34:16 - 34:21lakini mwanadamu anaweza kunena Maneno ya Uzima ambayo ni Roho na Uzima
-
34:21 - 34:25yanapoathiriwa na Roho Mtakatifu.
-
34:25 - 34:31Maneno hayo lazima yaathiriwe na Roho Mtakatifu kwa uzima.
-
34:31 - 34:34Ninamaanisha nini ninaposema kuna uzima katika Neno?
-
34:34 - 34:36Neno la Mungu ni Roho na Uzima
-
34:36 - 34:41kwa sababu lina uwezo wa kuzalisha nguvu ya kiroho
-
34:41 - 34:47ambayo hukua na kustawi ndani ya mioyo yetu iitwayo imani.
-
34:47 - 34:52Imani hiyo ndiyo inayosukuma maneno yetu kufanya maajabu.
-
34:52 - 34:55Hiyo ni imani ya Biblia.
-
34:55 - 35:14Imani ya Biblia inaitwa Imani ya Kiroho, katika kitabu cha 2 Wakorintho 4:13
-
35:14 - 35:3713 Na kwa kuwa tuna roho ile ile ya imani; kama ilivyoandikwa, niliamini, na kwa sababu hiyo nilinena; sisi nasi twaamini, na kwa sababu hiyo twanena
-
35:37 - 35:43Kwa hivyo imani hufanyika katika sehemu mbili:
-
35:43 - 35:45Kwa mioyo yetu tunaamini;
-
35:45 - 35:52Kwa vinywa vyetu tunakiri, na imani ni yote mawili.
-
35:52 - 35:56Unajua, mfano wa wana saba wa Skeva unaonyesha hivyo
-
35:56 - 35:59imani ya kweli si kuiga.
-
35:59 - 36:03Imani lazima itokee katika moyo wa kila mtu
-
36:03 - 36:07au katika usadikisho, ambao unaongoza kwenye harakati halisi
-
36:07 - 36:10au maungamo halisi ya imani.
-
36:10 - 36:15Ili imani iwe ya kweli, moyo na kinywa havipaswi kupingana kamwe.
-
36:15 - 36:19Kwa maneno mengine, tunapaswa kumaanisha kile tunachosema.
-
36:19 - 36:22Hii ina maana kwamba tunapaswa kuamini kile tunachokiri.
-
36:22 - 36:24Je, unaamini unachokiri?
-
36:24 - 36:26Unamaanisha unachosema?
-
36:26 - 36:29Kwa sababu imani ya kimaandiko au imani ya kibiblia imeonyeshwa
-
36:29 - 36:35kwa kuamini kwenye moyo na kukiri kwa kinywa.
-
36:35 - 36:39Kinywa lazima kiwe na makubaliano kamili ya moyo
-
36:39 - 36:42kabla ya kuwa na maungamo ya imani yanayokubalika au ya kweli.
-
36:42 - 36:45Kweli kabisa.
-
36:45 - 36:47Huo ndio ufunguo, makubaliano.
-
36:47 - 36:52Swali ni: Imani inaweza kusitawije?
-
36:52 - 36:56Ukuaji wa Neno la Mungu moyoni mwako,
-
36:56 - 37:01huzaa imani ndani ya moyo wako.
-
37:01 - 37:02Warumi 10:17
-
37:02 - 37:08Imani hukua tunaposikia na kutii Neno la Mungu.
-
37:16 - 37:30Je, mtu anahamaje kutoka kwenye ujuzi wa hisia hadi ujuzi wa ufunuo?
-
37:37 - 37:42Je, mtu anahamaje kutoka kwenye ujuzi wa hisia hadi ujuzi wa ufunuo?
-
37:42 - 37:47Ndiyo, hilo ndilo jambo ambalo sisi sote waumini tunapaswa kujiuliza.
-
37:47 - 37:51Hebu tukumbuke kilichompata mtumishi wa Elisha.
-
37:51 - 37:53Kwa macho yake ya kimwili,
-
37:53 - 37:58mtumishi wa Elisha aliona hatari ya papo hapo na hofu ikamshika.
-
37:58 - 38:03Bwana wake alipomwomba Mungu amfungue macho ya rohoni.
-
38:03 - 38:08Macho yake yakafunguliwa na katika roho,
-
38:08 - 38:11aliona malaika wakimzunguka.
-
38:11 - 38:12Na nini kilitokea?
-
38:12 - 38:14Hofu yake ikatoweka.
-
38:14 - 38:15Ndiyo.
-
38:15 - 38:20Kwa hiyo kuhama kutoka maarifa ya hisia hadi maarifa ya ufunuo
-
38:20 - 38:26ni suala la kuukabidhi moyo wako kwa Roho Mtakatifu.
-
38:26 - 38:30Roho Mtakatifu ndiye anayefungua macho ya imani yetu
-
38:30 - 38:34kuona ukweli uliofichwa katika Neno la Mungu.
-
38:34 - 38:38Kutafakari katika Neno la Mungu huleta ufunuo.
-
38:38 - 38:40Huo ndio ufunguo.
-
38:40 - 38:47Tunatafakari hadi Mungu atupe nuru iliyo wazi, ufahamu wa wazi.
-
38:47 - 38:49Kwa hiyo unapotafakari Neno la Mungu,
-
38:49 - 38:55kumruhusu Roho Mtakatifu kuchukua uongozi, ufunuo utakuja
-
38:55 - 38:58na ufunuo utakapokuja , utakubeba
-
38:58 - 39:02juu ya ulimwengu wa hisia hadi katika uwepo wa Mungu
-
39:02 - 39:06katika roho na huko utaona waziwazi;
-
39:06 - 39:10hapo ndipo ufahamu wa kiroho unakuja.
-
39:10 - 39:24Ngoja tusome katika kitabu cha 2 Wafalme 6 kuanzia mstari wa 15
-
39:25 - 39:3815 Kesho yake asubuhi na mapema, mtumishi wa mtu wa Mungu alipoamka na kutoka nje, jeshi, pamoja na farasi na magari ya vita, likawa limeuzunguka mji. Mtumishi wake akasema, “Ole wetu, bwana wangu! Tutafanya nini?
-
39:38 - 39:4716 Nabii akajibu, “Usiogope. Wale walio pamoja nasi ni wengi zaidi kuliko wale walio pamoja nao.”
-
39:47 - 39:51Jiweke katika Maandiko na umsikie Mungu akikuambia,
-
39:51 - 39:55Walio pamoja nawe ni wengi kuliko wale walio kinyume chako.
-
39:55 - 40:1017 Kisha Elisha akaomba, “Ee Bwana, mfumbue macho huyu mtumishi ili apate kuona.” Ndipo Bwana akayafumbua macho ya yule mtumishi, naye akatazama na kuona vilima vimejaa farasi na magari ya moto, yamemzunguka Elisha pande zote.
-
40:10 - 40:14Nakipenda sana hiki kipande cha maandiko.
-
40:14 - 40:19Ni mfano mzuri wa swali lako kuhusu kuhama kutoka kwenye maarifa ya hisia kwenda kwenye maarifa ya ufunuo.
-
40:19 - 40:23Hiki ndicho hasa kilichomtokea mtumishi wa Elisha.
-
40:23 - 40:26Na hiki ndicho hasa kinachotokea kwa wengi wetu leo.
-
40:26 - 40:29Wengi leo katika nyumba zao wameelemewa na hali zao
-
40:29 - 40:31kwa sababu tunazitazama kwa asili
-
40:31 - 40:35na unazidiwa na hofu inakuja na shaka inakuja.
-
40:35 - 40:37Kwa hivyo kuna haja ya sisi kubadili mtazamo wetu
-
40:37 - 40:41kutoka asili hadi kwenda rohoni.
-
40:41 - 40:44Kwa hivyo kuhama kutoka maarifa ya hisia kwenda kwenye ufunuo
-
40:44 - 40:47ni kwa neema.
-
40:47 - 40:50Unachohitaji kufanya ni kujinyenyekeza
-
40:50 - 40:57chini ya uongozi wa Roho Mtakatifu - Roho wa Ufunuo.
-
40:57 - 41:01Mabadiliko hayo, hatua hiyo ni kidogo kidogo,
-
41:01 - 41:04kila siku, kidogo kidogo, kila dakika, kidogo kidogo.
-
41:04 - 41:09Ni safari na safari ya maili elfu moja huanza na hatua moja.
-
41:09 - 41:11Kwa hivyo tuna furaha sana leo
-
41:11 - 41:14kwamba ulijiunga nasi kuchukua hatua hiyo, hatua hiyo kuelekea rohoni
-
41:14 - 41:16kwa kuungana nasi kwenye programu leo,
-
41:16 - 41:20ambayo ni 'KATIKA NURU YA NENO LA MUNGU'
-
41:20 - 41:24Kwa hivyo safari hiyo leo imeanza na hatua hii ambayo umechukua.
-
41:24 - 41:28Na kumbuka MFULULIZO WA MSINGI - MIHADHARA YA KIMUNGU
-
41:28 - 41:30ambayo umekuwa ukiona kwenye Chuo Kikuu cha Mungu -
-
41:30 - 41:31huhitaji tu kutazama mara moja
-
41:31 - 41:33unajua, Neno la Mungu halifungwi na wakati.
-
41:33 - 41:35Kila Neno la Mungu ni Roho na Uzima.
-
41:35 - 41:38Chukua muda kutazama tena na tena,
-
41:38 - 41:43pitia vifungu vya Biblia, tafakari ukweli uliofichwa hapo
-
41:43 - 41:46na ukitaka kutafuta mahali mafundisho hayo yalipo,
-
41:46 - 41:48unaweza kuangalia katika maelezo hapa chini.
-
41:48 - 41:52Kuna kiunga na ikiwa una maswali zaidi, kumbuka,
-
41:52 - 41:56unapotafakari mafundisho haya, maswali yatatokea moyoni mwako
-
41:56 - 41:59na unaweza kutuma maswali yako kwetu kwa kwenda
-
41:59 - 42:03kwenye tovuti yetu - theuog.org - kwenda kwenye sehemu ya mawasiliano
-
42:03 - 42:05na kututumia ujumbe.
-
42:05 - 42:09Na tutapitia maswali yako yote na kwa neema ya Mungu,
-
42:09 - 42:13yatajibiwa chini ya uongozi wa Roho Mtakatifu.
-
42:13 - 42:17Hakuna njia ya mkato ya ukomavu wa kiroho.
-
42:17 - 42:24Ufahamu wetu wa kidunia lazima utoe nafasi kwa ufahamu wa kiroho au ufunuo, kufikia ukomavu. ” – Nabii TB Joshua
-
42:24 - 42:27Mafundisho yote tunayokupa hayana mpaka wa muda.
-
42:27 - 42:30Tafadhali pitia, tafakari juu yake,
-
42:30 - 42:34na umwombe Roho Mtakatifu akusaidie kuwa na uelewa mzuri juu yake.
-
42:34 - 42:38Hiyo ndiyo njia pekee imani inaweza kukua katika maisha yetu.
-
42:38 - 42:42Kwamba tuna ufunuo haimaanishi tunaweza kukulazimisha kuamini;
-
42:42 - 42:44lazima uwe na ufunuo na usadikisho wako mwenyewe.
-
42:44 - 42:45Inakujaje?
-
42:45 - 42:47Soma, tafakari.
-
42:47 - 42:52Ruhusu Roho wa Mungu akuongezee ufahamu wako.
-
42:52 - 42:54Tunahitaji kuwa wakristo wakomavu
-
42:54 - 42:57kwa sababu tuko katika mazingira yenye changamoto nyingi
-
42:57 - 42:58na Mungu anataka uishi kwa imani, uwe hodari katika imani.
-
42:58 - 43:01Unaweza kufanya hivyo jinsi gani?
-
43:01 - 43:04Unaweza kufikia hilo tu kwa kuendeleza uhusiano wako
-
43:04 - 43:08pamoja na Mgeni wa ajabu asiyeonekana - Roho Mtakatifu.
-
43:08 - 43:11Vipi? Vutia umakini wake.
-
43:11 - 43:15Na unaweza kufanya hivyo tu unapotafakari Neno na kuomba
-
43:15 - 43:19na atakuja na kuboresha mipaka yako ya kiroho.
-
43:19 - 43:20katika jina la Yesu.
-
43:20 - 43:23Kwa hiyo, ahsante kwa kujiunga nasi kwenye kipindi hiki cha leo,
-
43:23 - 43:26'KATIKA NURU YA NENO LA MUNGU'
-
43:26 - 43:30Kama vile Nikodemo alivyomwendea Yesu usiku ili kuuliza maswali,
-
43:30 - 43:34kujua na kukuza imani katika Yesu,
-
43:34 - 43:39wewe pia unaweza kutazama hili na kuuliza maswali moyoni mwako kwa Mungu
-
43:39 - 43:40na Roho Mtakatifu,
-
43:40 - 43:44Msaidizi, Mshauri atakuja na kujibu maswali yako
-
43:44 - 43:46kupitia Neno la Mungu.
-
43:46 - 43:50Ndiyo, ndiyo maana kila kitu kiko katika nuru ya Neno la Mungu.
-
43:50 - 43:54Amina. Watakatifu, ndugu, dada, waumini duniani kote,
-
43:54 - 43:58tunaenda kukuombea.
-
43:58 - 44:00Tumeona barua pepe nyingi sana.
-
44:00 - 44:02Tulipitia maswali na majibu yote.
-
44:02 - 44:05Tumeona watu wengi wakipitia uchungu,
-
44:05 - 44:07maumivu na matatizo.
-
44:07 - 44:11Kwa hiyo tunaenda kuomba pamoja, mwamini Mungu
-
44:11 - 44:15kwamba Mungu Mwenyezi atakutana nawe katika sehemu ya hitaji lako muhimu,
-
44:15 - 44:17kwa maana Yesu hafanyi neno lolote pasipo Neno lake.
-
44:17 - 44:21Usisahau, Neno la Mungu lina kipaumbele kuliko jina.
-
44:21 - 44:23Ndio maana tunakupa mafundisho haya.
-
44:23 - 44:27Lakini tunasimama mbele za Mungu tukiwaombea,
-
44:27 - 44:31na Mungu atakuweka katika rehema zake, katika jina la Yesu.
-
44:31 - 44:35Kwa hivyo, endelea kuungana nasi hapa kwenye Chuo Kikuu cha Mungu.
-
44:35 - 44:38Ujuzi wa hisia hukoma pale ufunuo uwadiapo.
- Title:
- MAJIBU YA BIBLIA YALIYOFICHIKA | INGIA KATIKA ROHO - SEHEMU YA 2
- Description:
-
more » « less
Je, umepata ukweli uliofichika kutoka kweye Sehemu ya 1 ya Mfululizo wa Msingi, ‘Pga Hatua Katika Roho’? Jiunge na Racine na Ruth wanapochukua muda kujibu baadhi ya maswali yako.
Kama vile Nikodemo alivyomjia Yesu usiku kuuliza maswali yaliyokuwa yakisumbua imani yake, wengi wametuma maswali yao. Jibu la kila swali letu liko katika Neno la Mungu. Fungua moyo wako kwa Roho Mtakatifu, Mwalimu wa Kimungu na kuruhusu majibu ya maswali haya yaimarishe imani yako, katika programu hii maalum, ‘KATIKA NURU YA NENO LA MUNGU’.
Je! una swali kwa Racine & Ruth katika Chuo Kikuu cha Mungu?
Tutuma ujumbe kwenye https://theuog.org/contact/SURA:
00:00 - Utangulizi
01:26 - Ni matumizi gani ya kweli ya hisia zetu?
28:53 - Unamaanisha nini usemapo kwa 'nje'?
37:19 - Je, mtu anahamaje kutoka kwenye ujuzi wa hisia kwenda kwenye ujuzi wa ufunuo?
41:19 - Safari yako imeanza
43:54 - Jitayarishe kwa maombi...#Racine #Ruth #TheUOG #Teaching
-----------------------------------------
Mfululizo wa Msingi wa Chuo Kikuu cha Mungu: "PIGA HATUA KATIKA ROHO!" ni mfululizo wa mafundisho chini ya uongozi wa Roho Mtakatifu utakaopatikana kwa wote, akifunua hazina iliyofichwa katika Neno la Mungu ambayo huchochea roho zetu kupiga hatua katika roho…. maana hapo ndipo Mungu alipo. Ni dhana potofu kwamba kweli za kiroho zinaweza kutambulika kiakili. Tunahitaji kuwa wabichi; yaani tunahitaji kuwa katika Roho - ulimwengu wa maarifa ya ufunuo, tukiikabidhi mioyo yetu kwa uvuvio wa Roho Mtakatifu, Roho yule yule wa Ufunuo (Waefeso 1:17-18). Ufunuo huleta usadikisho na usadikisho huleta harakati za kweli katika safari yetu na Yesu, safari yetu ya Umilele.------------------------------------------
Tufuate kwenye mitandao ya kijamii @theuogofficial:
https://facebook.com/theuogofficial
https://instagram.com/theuogofficial
https://twitter.com/theuogofficial
https://tiktok.com/theuogofficial------------------------------------------
➡️ Tuma Ombi Lako la Maombi: https://theuog.org/contact/
➡️ Kuwa Mjitoleaji: https://theuog.org/contact/volonteer/
➡️ Toa: https://theuog.org/?form=give - Video Language:
- English
- Team:
The University of God
- Duration:
- 44:49
| fatinakatisha edited Swahili subtitles for HIDDEN ANSWERS OF THE BIBLE | STEP INTO THE SPIRITUAL - PART 2 | ||
| fatinakatisha edited Swahili subtitles for HIDDEN ANSWERS OF THE BIBLE | STEP INTO THE SPIRITUAL - PART 2 | ||
| fatinakatisha edited Swahili subtitles for HIDDEN ANSWERS OF THE BIBLE | STEP INTO THE SPIRITUAL - PART 2 | ||
| fatinakatisha edited Swahili subtitles for HIDDEN ANSWERS OF THE BIBLE | STEP INTO THE SPIRITUAL - PART 2 | ||
| fatinakatisha edited Swahili subtitles for HIDDEN ANSWERS OF THE BIBLE | STEP INTO THE SPIRITUAL - PART 2 | ||
| fatinakatisha edited Swahili subtitles for HIDDEN ANSWERS OF THE BIBLE | STEP INTO THE SPIRITUAL - PART 2 | ||
| fatinakatisha edited Swahili subtitles for HIDDEN ANSWERS OF THE BIBLE | STEP INTO THE SPIRITUAL - PART 2 | ||
| fatinakatisha edited Swahili subtitles for HIDDEN ANSWERS OF THE BIBLE | STEP INTO THE SPIRITUAL - PART 2 |