< Return to Video

MAJIBU YA BIBLIA YALIYOFICHIKA | INGIA KATIKA ROHO - SEHEMU YA 2

  • 0:17 - 0:20
    Karibu katika Chuo Kikuu cha Mungu.
  • 0:20 - 0:25
    Tunataka kuwashukuru ninyi nyote mliotuma maswali yenu kwetu.
  • 0:25 - 0:28
    Kama mshauri wetu Nabii TB Joshua alivyotuambia:
  • 0:28 - 0:33
    Ikiwa una nia ya somo na una hamu ya kujifunza,
  • 0:33 - 0:35
    utajitahidi kukaa mbele kila wakati,
  • 0:35 - 0:39
    uliza maswali na ushirikiane na mwalimu.
  • 0:39 - 0:42
    Kumbuka katika Chuo Kikuu cha Mungu,
  • 0:42 - 0:45
    moyo, roho ya mtu ni warsha,
  • 0:45 - 0:47
    na Roho Mtakatifu, Mwalimu wa Kimungu.
  • 0:47 - 0:49
    Ndiyo, na hiyo ndiyo ahadi ya Mungu
  • 0:49 - 0:52
    ambayo Yesu alitupa katika Kitabu cha Mathayo 7:7
  • 0:52 - 0:55
    kwamba ukimtafuta, utampata.
  • 0:55 - 0:58
    Ukimtafuta kwa moyo wako wote.
  • 0:58 - 1:00
    Kumbuka, kuutafuta Ufalme wa Mungu
  • 1:00 - 1:02
    ni kuwa na Ufalme wa Mungu.
  • 1:02 - 1:05
    Ndiyo, Mungu hajali shaka au maswali,
  • 1:05 - 1:08
    ilimradi maswali hayo yanatufanya tumtafute,
  • 1:08 - 1:12
    tumkaribie Yeye zaidi, kutafuta Neno Lake.
  • 1:12 - 1:14
    Neno la Mungu ndilo mamlaka ya mwisho suluhu
  • 1:14 - 1:18
    ya maswali na matatizo yote.
  • 1:18 - 1:21
    Leo, chini ya uongozi wa Roho Mtakatifu,
  • 1:21 - 1:24
    tutachunguza baadhi ya maswali yako
  • 1:24 - 1:27
    katika nuru ya Neno la Mungu.
  • 1:27 - 1:31
    Ndiyo, kabisa, na miongoni mwa maswali yaliyotumwa kwetu
  • 1:31 - 1:33
    ni kutoka kwa Anthony anayetokea Kanada
  • 1:33 - 1:35
    Anauliza swali hili la kuvutia, anasema,
  • 1:35 - 1:42
    "Ikiwa hisia zetu ni pazia linatotutenganisha sisi na Mungu, je, kazi ya hizi hisia ni zipi sasa?
  • 1:42 - 1:44
    Kwa nini Mungu alitupatia hizi hisia?
  • 1:44 - 1:48
    Je, hisia hizi zinaweza kutumika kumtafuta Mungu?"
  • 1:48 - 1:52
    Ahsante Anthony kwa kututumia maswali haya.
  • 1:54 - 1:57
    Anthony, ahsante kwa maswali yako.
  • 1:58 - 2:00
    Acha nikupeleke kwenye Biblia.
  • 2:00 - 2:06
    Kitabu cha Zaburi 115:4-7 katika kuonyesha sanamu,
  • 2:06 - 2:10
    kinatupatia picha ya mchoro wa hizi hisia tano.
  • 2:11 - 2:16
    "4 Sanamu zao ni fedha na dhahabu, kazi ya mikono ya wanadamu.
  • 2:17 - 2:24
    5 Zina vinywa lakini hazisemi, zina macho lakini hazioni,
  • 2:24 - 2:30
    6 Zina masikio lakini hazisikii, zina pua lakini hazisikii harufu,
  • 2:30 - 2:38
    7 zina mikono lakini hazishiki...Ahsante.
  • 2:38 - 2:42
    Mungu alitupa fahamu kuu tano
  • 2:42 - 2:45
    ambazo hutuwezesha kuingiliana na ulimwengu wa mwili
  • 2:45 - 2:50
    ambamo tunaishi kama wanadamu.
  • 2:50 - 2:55
    Kazi ya msingi ya hisia hizi tano ni kutusaidia kuwasiliana
  • 2:55 - 2:59
    vya kutosha na watu wanaotuzunguka.
  • 2:59 - 3:03
    Pia hutusaidia kupata tunachodhamiria, kutambua
  • 3:03 - 3:08
    na kukamata vitu vinavyotuzunguka na kutembea kwa usalama
  • 3:08 - 3:12
    katika mazingira yetu.
  • 3:12 - 3:14
    Hisia hizi zote zimeunganishwa.
  • 3:14 - 3:17
    Ninamaanisha, zinafanya kazi pamoja
  • 3:17 - 3:21
    na kutuma kwenye ubongo ishara pokezi
  • 3:21 - 3:25
    au habari kutoka kwenye mazingira,
  • 3:25 - 3:28
    ubongo wetu, ambao ni maabara ya maarifa ya hisia
  • 3:28 - 3:30
    huchakata taarifa hizi zote,
  • 3:30 - 3:35
    hutambua ishara hizo kupitia hifadhidata ya kumbukumbu zetu
  • 3:35 - 3:38
    na hutoa majibu sahihi.
  • 3:38 - 3:42
    Haya yote hutokea katika wakati halisi.
  • 3:42 - 3:44
    Basi hebu tuiangalie milango hiyo mitano ya fahamu.
  • 3:44 - 3:49
    Kwa mlango wa fahamu wa kuona, tunaweza kuona na kutambua vitu
  • 3:49 - 3:52
    ambavyo Mungu aliviumba, vitu na watu wanaotuzunguka.
  • 3:52 - 3:54
    Kuona ndio hisia kuu katika
  • 3:54 - 3:56
    kusafiri kwa usalama katika mazingira yetu,
  • 3:56 - 3:59
    kuendesha gari, kutembea, kusoma.
  • 3:59 - 4:00
    Kwa mlango wa fahamu wa kusikia,
  • 4:00 - 4:03
    hata bila mawasiliano ya kuona, tunaweza kuwa na maarifa wazi
  • 4:03 - 4:05
    ya mazingira yetu ya sasa
  • 4:05 - 4:09
    kwa kutofautisha sauti maalum ambazo hutoa.
  • 4:09 - 4:14
    Kwa mfano, sauti ya ndege au kutambua sauti ya rafiki.
  • 4:14 - 4:15
    Kwa hisia ya harufu
  • 4:15 - 4:18
    tunaweza kujua harufu, manukato,
  • 4:18 - 4:22
    na kuangalia ikiwa kitu ni kizuri au labda chakula kimeharibika.
  • 4:22 - 4:24
    Kwa hisia ya ladha,
  • 4:24 - 4:27
    tunaweza kutathmini utamu au uchungu wa chakula
  • 4:27 - 4:29
    kabla ya kukitumia.
  • 4:29 - 4:32
    Kwa hisia ya kuhisi au kugusa,
  • 4:32 - 4:35
    tunaweza kuhisi halijoto iliyoko
  • 4:35 - 4:39
    kujua mavazi sahihi ya kuvaa ili kulinda miili yetu ipasavyo.
  • 4:39 - 4:43
    Pia,tunaweza kuhisi uzito au ugumu wa kitu.
  • 4:43 - 4:46
    Kwa mfano, chakula hiki kina harufu nzuri.
  • 4:46 - 4:48
    Je, ni chakula gani unachopenda zaidi, Racine?
  • 4:48 - 4:50
    Mchele wa Jollof.
  • 4:50 - 4:54
    Chakula hiki kina harufu nzuri - ndio, nataka kukionja.
  • 4:54 - 4:56
    Au, nguo hizi ni nzuri -
  • 4:56 - 4:57
    nataka kuzinunua.
  • 4:57 - 5:00
    Au, ni baridi sana na kuna upepo leo -
  • 5:00 - 5:03
    sitaki kwenda ufukweni tena.
  • 5:03 - 5:06
    Unaweza kuona jinsi hisia zetu zinavyoweza
  • 5:06 - 5:11
    kuwa na ushawishi kwenye chaguzi na matendo yetu.
  • 5:11 - 5:12
    Zingatia matumizi ya hisi zetu.
  • 5:12 - 5:15
    Kwa mfano, unaendesha gari.
  • 5:15 - 5:18
    ghafla, mtembea kwa miguu anavuka barabara.
  • 5:18 - 5:21
    Kama dereva, unajikuta mara moja
  • 5:21 - 5:24
    na uamuzi, jibu la kuchukua, unaweza kuvuta breki,
  • 5:24 - 5:27
    au kama kasi yako ni kubwa sana,
  • 5:27 - 5:30
    inabidi uende mbali na mtu huyo.
  • 5:30 - 5:33
    Unaweza kuona hisia zote zikifanya kazi pamoja;
  • 5:33 - 5:37
    ninaona, ninavuta breki; ninageuza gurudumu.
  • 5:37 - 5:41
    Kwa hivyo vitendo hivi vyote hufanyika wakati huo huo kwa wakati halisi.
  • 5:41 - 5:43
    Vyote vimeunganishwa.
  • 5:43 - 5:46
    Vinafanya kazi pamoja.
  • 5:46 - 5:49
    Unaweza kuona ni ushawishi kiasi gani
  • 5:49 - 5:54
    hisia zetu zinaweza kuwa kwenye chaguzi na matendo yetu.
  • 5:54 - 6:02
    Tunachoona, kusikia, kunusa, kuonja, kuhisi kinaweza kuathiri mawazo yetu.
  • 6:02 - 6:04
    Ninamaanisha nini kwa kushawishi mawazo yetu?
  • 6:04 - 6:10
    Ninamaanisha, vina ushawishi juu ya tamaa na mapenzi yetu.
  • 6:10 - 6:14
    Mawazo yetu yanaweza kuathiri matendo yetu au kutotenda.
  • 6:14 - 6:15
    Kwa nini?
  • 6:15 - 6:19
    Kwa sababu mwanadamu hufanya mapenzi yake kupitia akili yake.
  • 6:19 - 6:23
    Hiyo ndiyo maana ya busara au kufikiri.
  • 6:23 - 6:26
    Binadamu ni tofauti na wanyama.
  • 6:26 - 6:28
    Binadamu sio roboti.
  • 6:28 - 6:32
    Yeye ni wakala huru wa maamuzi.
  • 6:32 - 6:36
    Kwa sababu ya ushawishi kutokana na mwingiliano na mazingira
  • 6:36 - 6:40
    ambayo yanahitaji majibu au mtazamo sahihi,
  • 6:40 - 6:45
    Mungu anamtaka mtu kuwa na akili huru -
  • 6:45 - 6:49
    akili inayofikiri yenyewe.
  • 6:49 - 6:51
    Mungu amempa mwanadamu
  • 6:51 - 6:55
    uwezo wa kufikiria na kuchagua kati ya kile kinachofaa au la -
  • 6:55 - 6:57
    hiyo ni akili ya kawaida,
  • 6:57 - 7:00
    kuchagua kati ya mema au mabaya,
  • 7:00 - 7:02
    hiyo ni hisia ya hukumu,
  • 7:02 - 7:06
    kuchagua kati ya mema na mabaya - hiyo ni hisia ya maadili.
  • 7:06 - 7:10
    Hayo ni matokeo ya hisia za kufikiri na uwajibikaji -
  • 7:10 - 7:15
    ambazo ni muhimu kwa maisha katika jamii au kikundi.
  • 7:15 - 7:20
    Mwanadamu kulingana na urefu wa maisha yake, hukua kimwili
  • 7:20 - 7:24
    kutoka katika kiinitete hadi kuwa mtoto mchanga,
  • 7:24 - 7:30
    kupitia utoto, ujana, utu uzima na uzee.
  • 7:30 - 7:35
    Tunaweza kuona kwamba kukua kimwili ni kazi ya wakati.
  • 7:35 - 7:37
    Tunapokua katika umri,
  • 7:37 - 7:42
    tunapitia hatua za maisha ya mwanadamu.
  • 7:42 - 7:45
    Mwanadamu si mtu wa kimwili tu
  • 7:45 - 7:49
    bali mtu mwenye akili na maadili.
  • 7:49 - 7:52
    Hasa! Na ni muhimu kukumbuka kwamba
  • 7:52 - 7:56
    kwa sababu maisha na majukumu yake yako katika hatua,
  • 7:56 - 8:00
    mwanadamu pia lazima akue katika ukomavu wa kiakili.
  • 8:00 - 8:02
    Kivipi?
  • 8:02 - 8:05
    Ukuaji wa kiakili ni kazi ya kujifunza -
  • 8:05 - 8:07
    kujifunza kutokana na kile tunachofanya.
  • 8:07 - 8:10
    Kujifunza kutoka kwa kile tunachojifunza, kile kinachotokea karibu nasi
  • 8:10 - 8:14
    na kujifunza kile kinachotokea kwetu.
  • 8:14 - 8:17
    Umewahi kujiuliza kila mtu anapokutana na mtu mpya
  • 8:17 - 8:19
    katika uhusiano mpya?
  • 8:19 - 8:22
    Maswali ya kwanza watakayojiuliza wenyewe
  • 8:22 - 8:28
    yatahusu historia yao, elimu, kazi katika maisha.
  • 8:28 - 8:32
    Wachache sana watashughulikia maisha yao ya kiroho.
  • 8:32 - 8:36
    Na hilo ndilo linaloleta tofauti kati ya mtazamo wa mwanadamu
  • 8:36 - 8:40
    na mtazamo wa Mungu.
  • 8:40 - 8:44
    Ndiyo, katika Wagalatia 5,
  • 8:44 - 8:49
    Mungu asingetuamuru tuenende katika Roho
  • 8:49 - 8:54
    kama hakututengeneza sisi kufanya kazi katika Roho.
  • 8:54 - 8:57
    Biblia inasema kwamba Mungu alimuumba mwanadamu,
  • 8:57 - 9:02
    wanadamu, kwa sura na mfano wake.
  • 9:02 - 9:04
    Kitabu cha Ayubu 33:4 kinasema
  • 9:04 - 9:08
    mwanadamu ni zao kuu la Roho Mtakatifu;
  • 9:08 - 9:12
    mwanadamu ni kazi ya kiungu ya sanaa.
  • 9:12 - 9:13
    Kwa nini?
  • 9:13 - 9:17
    Kwa sababu wanadamu wamekusudiwa kufikiri, kuzungumza,
  • 9:17 - 9:22
    kutenda na kupanga na Mungu.
  • 9:22 - 9:26
    Kwa hiyo mwanadamu amekusudiwa kuishi katika kupatana na Mungu.
  • 9:26 - 9:28
    Je, tunaishi sambamba na Mungu?
  • 9:28 - 9:32
    Siku zote kumbuka Mungu ni Roho.
  • 9:32 - 9:36
    Kwa hiyo swali ambalo tunapaswa kujiuliza ni:
  • 9:36 - 9:39
    mwanadamu ni nani?
  • 9:39 - 9:41
    Hilo ndilo swali.
  • 9:41 - 9:48
    Biblia ni hifadhidata ya mwamini kwa maoni yake binafsi.
  • 9:48 - 9:54
    Je, Biblia inasema nini kuhusu mwanadamu, kuhusu wewe na mimi?
  • 9:55 - 10:00
    Biblia inasema katika kitabu cha 1Wathesalonike 5:23
  • 10:00 - 10:04
    kwamba, mtu ni kiumbe wa kiroho
  • 10:04 - 10:08
    ambaye ana roho na mwili.
  • 10:08 - 10:15
    Kwa maneno mengine, mwanadamu ana asili ya kimwili na ya kiroho.
  • 10:15 - 10:19
    Mwanadamu sio tu mtu wa kimwili, kiakili;
  • 10:19 - 10:25
    yeye pia ni mtu wa maadili na mtu wa kiroho,
  • 10:25 - 10:28
    kwa sababu tumeumbwa kuwa kama Mungu
  • 10:28 - 10:33
    ndani ya mioyo yetu na Mungu ni Roho.
  • 10:33 - 10:34
    Kwa hivyo zingatia.
  • 10:34 - 10:38
    Kila mara Biblia inaporejelea moyo wa mwanadamu,
  • 10:38 - 10:43
    inazungumzia roho ya mtu - roho ya mwanadamu.
  • 10:43 - 10:50
    Ndio maana katika Kitabu cha 1 Samweli 16:7, na Mathayo 15:8,
  • 10:50 - 10:53
    Biblia inakazia kwamba
  • 10:53 - 10:57
    inapokuja kwa hukumu ya haki, mtazamo wa Mungu,
  • 10:57 - 11:02
    kuhusu mwanadamu daima huelekea kwenye moyo wa mwanadamu, roho ya mwanadamu.
  • 11:02 - 11:06
    Hii ina maana kwamba Mungu humwona mwanadamu kama kiumbe cha roho,
  • 11:06 - 11:10
    anayeishi katika mwili wa kawaida.
  • 11:10 - 11:15
    Roho ya mwanadamu ni sehemu ya mwanadamu ambayo ina ufahamu wa kiroho.
  • 11:15 - 11:18
    Ninamaanisha, uelewa wa kiroho.
  • 11:18 - 11:21
    Roho ya mwanadamu ni sehemu ya mwanadamu
  • 11:21 - 11:24
    ambayo imeunganishwa na ulimwengu wa kiroho
  • 11:24 - 11:30
    na hupokea miongozo na ufunuo kutoka kwa Mungu, ambaye ni Roho.
  • 11:30 - 11:33
    Hebu tumfikirie sasa mtu kutoka kwenye kibiblia
  • 11:33 - 11:37
    ambaye alikuwa hasa katika maelewano na Mungu katika Roho.
  • 11:37 - 11:38
    Tunapaswa kumkumbuka Musa.
  • 11:38 - 11:40
    Fikiria mtazamo wa Musa
  • 11:40 - 11:43
    pale yeye na watu wake walipokuwa wamenaswa
  • 11:43 - 11:48
    katikati ya Bahari Nyekundu na majeshi ya Misri yanayowafuata.
  • 11:48 - 11:52
    Hakika watu wa Israeli walikuwa na kila sababu ya
  • 11:52 - 11:56
    kufikiri kwamba mwisho ulikuwa umefika
  • 11:56 - 12:00
    ukizingatia ukubwa na nguvu za kijeshi za majeshi ya Misri.
  • 12:00 - 12:03
    Tunaweza kusoma kuhusu hili katika Kitabu cha Kutoka 14:10.
  • 12:03 - 12:07
    "Basi Waisraeli wakalia si kwa hofu tu,
  • 12:07 - 12:12
    bali pia katika uasi na hasira iliyoelekezwa dhidi ya Musa na Mungu wake."
  • 12:12 - 12:17
    Waliruhusu hisia zao kuamuru mwelekeo wa imani yao
  • 12:17 - 12:20
    na kuingiwa na hofu
  • 12:20 - 12:25
    na kusahau kabisa miujiza yote ambayo Mungu alikuwa amewafanyia
  • 12:25 - 12:28
    na kufanya kwa niaba yao.
  • 12:28 - 12:33
    Badala ya kukasirishwa na mwitikio wa watu wake - ukosefu wa imani,
  • 12:33 - 12:37
    Musa alikuwa mtulivu, makini na dhabiti.
  • 12:37 - 12:41
    Hata katikati ya uchochezi mkali,
  • 12:41 - 12:45
    Biblia inasema alikuwa mtulivu sana, mwenye kujiamini na mwenye amani.
  • 12:45 - 12:46
    Kwa nini?
  • 12:46 - 12:49
    Kwa sababu mtazamo wa roho yake ulikuwa kwa Mungu.
  • 12:49 - 12:53
    Ninamaanisha, roho yake ilikuwa imeunganishwa na Mungu.
  • 12:53 - 12:57
    Na ndio maana aliweza kushinda kile ambacho akili zake zilikuwa zikimwambia.
  • 12:57 - 13:01
    Kweli - mtu wa kiroho na mtu wa imani - Musa.
  • 13:01 - 13:04
    Mafunzo ni mengi ya kujifunza kutoka kwake.
  • 13:04 - 13:10
    Swali ni kwa nini mwanadamu hawezi kutumia hisia zake kumtafuta Mungu?
  • 13:10 - 13:12
    Hilo ndilo swali.
  • 13:12 - 13:15
    Jibu la swali hili ni la moja kwa moja.
  • 13:15 - 13:18
    Mungu ni Roho.
  • 13:18 - 13:22
    Kwa hiyo, hatuwezi kumjua Mungu kwa hisia na
  • 13:22 - 13:25
    ufahamu au uwezo wa nje wa binadamu
  • 13:25 - 13:31
    kwa sababu Mungu haonekani, ni wa kiroho, si wa kimwili.
  • 13:31 - 13:35
    Yeye ni kiumbe mkuu anayeishi katika ulimwengu juu ya hisia.
  • 13:35 - 13:38
    Anaishi katika Roho.
  • 13:38 - 13:45
    Kwa hiyo, ili kumtafuta Mungu, ni lazima uwe katika roho.
  • 13:45 - 13:48
    Na unaweza tu kumuona na kuhusiana Naye
  • 13:48 - 13:52
    katika ulimwengu wa roho kupitia ufunuo.
  • 13:52 - 13:54
    Je, tunamaanisha nini kwa ufunuo?
  • 13:54 - 13:58
    Ufunuo huleta katika hisia zetu za kiroho
  • 13:58 - 14:03
    ukweli wa mambo ya kiroho ambayo hayawezi kutambulika
  • 14:03 - 14:08
    kwa hisiai zetu za asili za kibinadamu.
  • 14:08 - 14:14
    Kama vile tulivyo na viungo vya asili vilivyowekwa katika miili yetu ya kimwili
  • 14:14 - 14:18
    ambazo hulisha hisia zetu za kibinadamu kwa habari
  • 14:18 - 14:20
    kutoka kwenye mazingira
  • 14:20 - 14:26
    kama macho yetu, masikio yetu, mikono yetu, nk
  • 14:26 - 14:31
    Mungu pia ametujalia hisia za kiroho
  • 14:31 - 14:36
    vile vile, zilizounganishwa katika roho zetu.
  • 14:36 - 14:40
    Hisia kuu ya kiroho ambayo Mungu ameiweka ndani ya roho zetu
  • 14:40 - 14:43
    ni dhamiri zetu.
  • 14:43 - 14:50
    Dhamiri ni kiungo cha roho cha kutambua mambo ya kiroho.
  • 14:50 - 14:55
    Hiyo ndiyo maana Nabii TB Joshua anaiita hali ya haki.
  • 14:55 - 15:11
    Hebu tumsikilize Mtume Paulo alivyosema katika kitabu cha Warumi 8:16.
  • 15:12 - 15:14
    Paulo alisema,
  • 15:17 - 15:25
    16 "Ni Roho mwenyewe anayeshuhudia pamoja na roho zetu kwamba sisi ni wana wa Mungu."
  • 15:25 - 15:28
    Hii ina maana gani?
  • 15:28 - 15:31
    Hii ina maana kwamba hisia ya haki
  • 15:31 - 15:34
    huleta mwamko wa kujijua.
  • 15:34 - 15:40
    Ninaamaanisha, ufahamu wa wewe ni nani katika Kristo Yesu.
  • 15:40 - 15:44
    Swali ni: Je, ufahamu huu unakujaje?
  • 15:44 - 15:47
    Ufahamu huo unakuja kwa njia ya ufunuo
  • 15:47 - 15:52
    wakati Roho Mtakatifu anaposhuhudia rohoni mwetu.
  • 15:52 - 15:56
    Roho Mtakatifu anashuhudiaje rohoni mwetu?
  • 15:56 - 15:59
    Kupitia dhamiri zetu.
  • 15:59 - 16:05
    Paulo alielezea zaidi katika Warumi 9:1.
  • 16:05 - 16:07
    Anasema,
  • 16:07 - 16:24
    9 "Ninasema kweli katika Kristo na dhamiri yangu inanishuhudia kwa njia ya Roho Mtakatifu kuwa sisemi uongo."
  • 16:26 - 16:34
    Kwa hiyo, 1 Wakorintho 2:9-15 inatufundisha kwamba hisia zetu za asili
  • 16:34 - 16:39
    haziwezi kufahamu wala kujua mambo ya Mungu au mambo ya Roho
  • 16:39 - 16:43
    kwa sababu yanaweza tu kutambulika kiroho.
  • 16:43 - 16:46
    Na ikiwa haya yote yanaonekana kuwa mengi kwako, usijali.
  • 16:46 - 16:50
    Katika safu ya msingi tunapoendelea, haya yote yatanyambulishwa.
  • 16:50 - 16:52
    ili kwamba uweze kuelewa kweli
  • 16:52 - 16:56
    jinsi tunavyoweza kuhusiana na Mungu kupitia roho zetu
  • 16:56 - 17:00
    na mtu ni nini hasa - roho yake, mwili wake, nafsi yake.
  • 17:00 - 17:04
    Kwa hivyo subiri unapopata zaidi juu ya haya kwenye safu ya msingi
  • 17:04 - 17:05
    inayokuja hivi karibuni.
  • 17:05 - 17:07
    Kwa hivyo inapokuja kwenye maarifa ya mwanadamu,
  • 17:07 - 17:10
    hisia zetu haziwezi kuona moyo au roho ya mwanadamu.
  • 17:10 - 17:13
    Vinaweza tu kuona mwili wa mwanadamu kwa sababu ndiyo
  • 17:13 - 17:18
    sehemu ya mwanadamu ambayo imeunganishwa na ulimwengu huu unaoonekana.
  • 17:18 - 17:20
    Eneo la hisia.
  • 17:20 - 17:25
    Mwili na hisi za mwanadamu haziwezi kuunganishwa na ulimwengu wa kiroho.
  • 17:25 - 17:30
    Ni roho ya mwanadamu pekee ambayo ni sehemu ya kiroho ya mwanadamu
  • 17:30 - 17:35
    ambayo inaweza kuunganishwa na makao ya roho, ambayo ni mahala pa Mungu.
  • 17:35 - 17:37
    Kweli, ndivyo hivyo.
  • 17:37 - 17:41
    Swali ni: Je, tunaangaliaje katika mwelekeo huo?
  • 17:41 - 17:45
    Ili kuingia kwenye ulimwengu huo wa roho,
  • 17:45 - 17:50
    mwanadamu lazima awe katika roho akiongozwa na Roho Mtakatifu.
  • 17:50 - 17:53
    Roho zetu, mioyo yetu ndio sehemu ya mawasiliano,
  • 17:53 - 17:56
    mahali pa kuwasiliana na Roho Mtakatifu.
  • 17:56 - 17:58
    Roho Mtakatifu anatumia mioyo yetu
  • 17:58 - 18:01
    kuwasiliana nasi.
  • 18:01 - 18:08
    Na Mungu anazungumza na mioyo yetu, na roho zetu, sio masikio yetu.
  • 18:08 - 18:13
    Ninakushauri usome Kitabu cha Matendo 17 -
  • 18:13 - 18:17
    wakati watu wa Athene walipokuwa wakimtafuta Mungu
  • 18:17 - 18:20
    kwa akili zao na maarifa ya hisia
  • 18:20 - 18:25
    ili kumtafuta na kumwabudu Mungu.
  • 18:25 - 18:26
    Acha nisome
  • 18:33 - 18:39
    Matendo ya Mitume 17:23
  • 18:39 - 18:58
    23 "Kwa kuwa nilipokuwa nikitembea mjini niliona sehemu nyingi za kuabudia. Niliona pia madhabahu moja iliyoandikwa, ‘Kwa Mungu asiyejulikana.’ Huyo Mungu mnayemwabudu bila kumfahamu, ndiye ninayemtangaza kwenu."
  • 18:58 - 19:09
    24 Mungu aliyeumba dunia na vitu vyote vilivyomo, ambaye pia ni Bwana wa mbingu na nchi, haishi katika mahekalu yaliyojengwa na wanadamu.
  • 19:09 - 19:20
    25 Wala hahudumiwi kwa mikono ya wanadamu kana kwamba anahitaji cho chote; kwa sababu yeye ndiye anayewapa watu wote uhai na pumzi na kila kitu.
  • 19:21 - 19:35
    26 Yeye aliumba mataifa yote ya wanadamu waishi juu ya nchi kutokana na mtu mmoja. Pia amepanga muda wa maisha ya watu wote, akaweka na mipaka ya mahali watakapoishi
  • 19:35 - 19:47
    27 ili wamtafute Mungu na wamfahamu. Lakini Yeye hayuko mbali nasi kwa maana
  • 19:47 - 20:00
    28 ‘Tunaishi na kuenenda na kuwa na uhai ndani yake,’ na kama mtunga mashairi wenu alivyosema, ‘Sisi ni uzao wa Mungu.’
  • 20:00 - 20:21
    29 Kwa kuwa sisi ni wa uzao wa Mungu hatupaswi kudhani kuwa yeye ni kama sanamu ya dhahabu au fedha au jiwe iliyotengenezwa kwa akili na ufundi wa mwanadamu.
  • 20:23 - 20:27
    Kwa kuwa watu wote wana roho, tunapaswa kujiuliza swali
  • 20:27 - 20:36
    Kwa nini inaonekana kwamba wanadamu wengi hawana uhusiano wowote na Mungu?
  • 20:36 - 20:40
    Ukweli ni kwamba Mungu amewaumba wanadamu
  • 20:40 - 20:45
    kufanya kazi katika ulimwengu wa asili na wa kiroho.
  • 20:45 - 20:51
    Lakini wengi wetu tunaishi katika hisia, ninamaanisha katika asili.
  • 20:51 - 20:56
    Na sisi tuko butu inapokuja kwa mambo ya Roho.
  • 20:56 - 21:00
    Kwa sababu kama Maandiko yanavyosema katika Kitabu cha 1 Wakorintho 2:9
  • 21:00 - 21:03
    mambo ya Rohoni si dhahiri.
  • 21:03 - 21:05
    Hatuwezi kuyaona.
  • 21:05 - 21:12
    Na Biblia inasema zaidi katika 1 Wakorintho 15:46-47,
  • 21:12 - 21:15
    Ngoja nisome.
  • 21:16 - 21:38
    1 Wakorintho 15:46.
  • 21:38 - 21:46
    46 Lakini si yule wa kiroho aliyekuja kwanza; bali ni yule wa mwili, na kisha yule wa kiroho.
  • 21:47 - 22:01
    47 Mtu wa kwanza alitoka katika nchi, alifanywa kwa mavumbi; mtu wa pili ni Bwana kutoka mbinguni.
  • 22:01 - 22:14
    48 Na kama alivyokuwa yule wa ardhini, ndivyo walivyo wale walio wa ardhini; na alivyo mtu wa mbinguni, ndivyo walivyo wale walio wa mbinguni.
  • 22:15 - 22:21
    Maandiko haya tuliyosoma hivi punde yanabainisha aina mbili za wanaume.
  • 22:21 - 22:25
    Mtu wa asili na mtu wa kiroho.
  • 22:25 - 22:31
    Mwanadamu wa asili ni kipofu wa kiroho na ni butu katika ufahamu
  • 22:31 - 22:34
    katika ulimwengu usioonekana.
  • 22:34 - 22:40
    Ulimwengu wa roho umefungwa kabisa nje ya maono yake ya kiroho.
  • 22:40 - 22:44
    Ni wakati tu Roho Mtakatifu anaangaza macho yake ya kiroho
  • 22:44 - 22:50
    ili aweze kuona na kuelewa mambo ya Rohoni.
  • 22:50 - 22:55
    Waefeso 1:7-18 inasema kwamba Bwana Mungu wetu Yesu Kristo,
  • 22:55 - 22:58
    Baba wa Utukufu, anaweza kutupa Roho wa Ufunuo
  • 22:58 - 23:02
    na hekima katika kumjua Yeye
  • 23:02 - 23:06
    ili macho ya ufahamu wetu yafumbuliwe
  • 23:06 - 23:10
    Ili tuweze kujua tumaini la mwito wake ni nini
  • 23:10 - 23:13
    na utajiri wa utukufu wake ukoje
  • 23:13 - 23:17
    katika urithi wake wa watakatifu.
  • 23:17 - 23:32
    Ninatumaini mna Biblia zenu hapo, twende sasa kwenye 1 Wakorintho 2:9 na tusome pamoja kuanzia mstari wa 9 mpaka ule wa 12.
  • 23:32 - 23:43
    9 Lakini, kama Maandiko yasemavyo, Hakuna aliyeona, hakuna aliyesikia, hakuna aliyewaza, kile ambacho Mungu amekiandaa kwa ajili ya watu wampendao.
  • 23:43 - 23:53
    10 Lakini Mungu amejidhihirisha kwetu kwa njia ya Roho wake. Roho huchunguza kila kitu, hata mambo ya ndani ya Mungu.
  • 23:53 - 24:06
    11 Kwa maana ni nani anajua mawazo ya mtu isipo kuwa roho aliye ndani ya huyo mtu? Vivyo hivyo hakuna mtu anayeelewa mawazo ya Mungu isipokuwa Roho wa Mungu.
  • 24:06 - 24:15
    12 Sisi hatukupokea roho ya dunia hii bali Roho aliyetoka kwa Mungu ili tuweze kuelewa yale ambayo Mungu ametupatia bure
  • 24:15 - 24:20
    Kwa hiyo swali ni: Je, tunaunganishwaje na Roho?
  • 24:20 - 24:22
    Je, unaunganaje na Roho?
  • 24:22 - 24:25
    Kwa imani.
  • 24:25 - 24:31
    Kumwamini Kristo Yesu - huo ndio muunganiko wetu pekee.
  • 24:31 - 24:34
    Kwa hiyo tunaishije kwa imani?
  • 24:34 - 24:37
    Kumbuka, tunaishi kwa imani
  • 24:37 - 24:45
    tunapotambua muungano wetu na Yesu Kristo katika roho.
  • 24:45 - 24:46
    Kuishi kwa imani,
  • 24:46 - 24:51
    roho zetu lazima zitawale hisia zetu,
  • 24:51 - 24:53
    na ili roho zetu zitawale hisia zetu,
  • 24:53 - 24:57
    mawazo yetu lazima yafanywe upya kwa kulijua Neno
  • 24:57 - 25:00
    na kulifanyia kazi.
  • 25:00 - 25:05
    Kwa hiyo tunajuaje kwamba akili zetu zimefanywa upya?
  • 25:05 - 25:07
    Swali zuri.
  • 25:07 - 25:10
    Akili zetu zinafanywa upya
  • 25:10 - 25:14
    tunapoanza kufikiria sio juu ya udhaifu wetu
  • 25:14 - 25:21
    na mapungufu, bali haki yetu katika Kristo Yesu.
  • 25:21 - 25:26
    2 Wakorintho 12:7-10
  • 25:26 - 25:32
    Yote ni kuhusu uzoefu wa Mtume Paulo na mwiba.
  • 25:35 - 25:54
    7 Na ili nisijione bora kuliko nilivyo, kutokana na mafunuo haya makuu, nilipewa mwiba katika mwili wangu, mtumishi wa shetani, ili anitese.
  • 25:54 - 26:00
    8 Nilimsihi Bwana mara tatu aniondolee mwiba huu.
  • 26:01 - 26:21
    9 Lakini aliniambia, “Neema yangu inakutosha, kwa kuwa uwezo wangu unakamilika katika udhaifu.” Kwa hiyo nitajisifu kwa furaha zaidi kuhusu udhaifu wangu ili uwezo wa Kristo ukae juu yangu.
  • 26:22 - 26:27
    Unaona, wakati Paulo alipoteswa na mwiba katika mwili wake.
  • 26:27 - 26:31
    alimwomba Mungu mara nyingi ili Mungu aondoe mwiba huo.
  • 26:31 - 26:35
    Lakini Mungu akamwambia: “Neema yangu yakutosha.”
  • 26:35 - 26:36
    Kwa nini?
  • 26:36 - 26:42
    Maana nguvu zangu hukamilishwa katika udhaifu.
  • 26:42 - 26:46
    Mara, ufunuo wa mapenzi ya Mungu ulippomjia,
  • 26:46 - 26:49
    Paulo hakulalamika tena.
  • 26:49 - 26:53
    Akasema badala yake, ninapokuwa dhaifu, nina nguvu.
  • 26:53 - 26:57
    Akili yake ilifanywa upya na akaacha kuwa na wasiwasi
  • 26:57 - 27:00
    kuhusu mwiba katika mwili wake.
  • 27:00 - 27:05
    Kwa hivyo, hebu tufanye muhtasari wa majibu ya maswali haya yote.
  • 27:05 - 27:11
    Mtu wa asili - mtu wa hisia anaufahamu kuhusu mwili wake tu.
  • 27:11 - 27:13
    na hana ufahamu wa ulimwengu wa roho.
  • 27:13 - 27:16
    Kwa nini iko hivyo?
  • 27:16 - 27:18
    Biblia inasema tangu kuanguka kwa mwanadamu,
  • 27:18 - 27:22
    mwanadamu amepoteza fahamu zake za roho
  • 27:22 - 27:26
    kwa sababu ya dhambi na hufanya kazi katika asili tu.
  • 27:26 - 27:29
    Tunaweza kusoma kuhusu hili katika Mwanzo 6:3.
  • 27:29 - 27:33
    Roho ya mwanadamu wa asili imekufa kwa Mungu kwa sababu ya dhambi
  • 27:33 - 27:35
    tangu Adamu,
  • 27:35 - 27:39
    mwili wa mwanadamu, ambao Biblia inauita utu wa nje,
  • 27:39 - 27:44
    mtu wa nje au mzee ni sehemu ya mwili ya mwanadamu
  • 27:44 - 27:48
    iliyoundwa na Mungu kuingiliana na ulimwengu unaoonekana au wa mwili.
  • 27:48 - 27:50
    Hiyo ni kweli.
  • 27:50 - 27:52
    Wakati roho ya mwanadamu
  • 27:52 - 27:56
    ni sehemu ya kiroho ya mwanadamu iliyoundwa na Mungu
  • 27:56 - 28:00
    kuingiliana au kuwasiliana na yasiyoonekana
  • 28:00 - 28:05
    au ulimwengu wa kiroho ambapo Mungu anakaa.
  • 28:05 - 28:07
    Kwa hiyo mtu wa kiroho ni,
  • 28:07 - 28:11
    yule ambaye roho yake imeumbwa upya au kufanywa upya
  • 28:11 - 28:16
    kwa nguvu za Mungu katika hatua ya kuzaliwa upya kiroho kwa imani
  • 28:16 - 28:18
    katika Kristo Yesu.
  • 28:18 - 28:21
    Hivyo ndivyo Yesu alimaanisha alipomwambia Nikodemo
  • 28:21 - 28:23
    katika kitabu cha Yohana 3:3.
  • 28:23 - 28:25
    Unahitaji kuzaliwa mara ya pili.
  • 28:25 - 28:28
    Yesu akajibu, akamwambia, Hakika,
  • 28:28 - 28:32
    Nawaambia, Mtu asipozaliwa mara ya pili,
  • 28:32 - 28:36
    hawezi kuuona ufalme wa Mungu” (Yohana 3:3).
  • 28:37 - 28:40
    Tuko hapa leo kuutafuta Ufalme wa Mungu
  • 28:57 - 29:05
    Unamaanisha nini unaposema kwa nje?
  • 29:07 - 29:12
    Kwa hivyo unamaanisha nini unaposema kwa "nje"?
  • 29:12 - 29:18
    Kwa "nje", tunamaanisha kile kinachoonekana, nyenzo, kimwili -
  • 29:18 - 29:22
    vitu unavyoweza kuona kwa macho yako ya asili,
  • 29:22 - 29:24
    kusikia kwa masikio yako,
  • 29:24 - 29:29
    mambo ambayo unaweza kuhisi au kuyajua kiakili.
  • 29:29 - 29:31
    Kinyume chake, 'ndani' inarejelea
  • 29:31 - 29:36
    mambo ambayo hatuwezi kuyaona, kama moyo wa mwanadamu, roho ya mwanadamu,
  • 29:36 - 29:41
    ambayo ni hali ya kiroho ya mwanadamu ambayo ni Mungu pekee anaweza kuona.
  • 29:41 - 29:44
    Ndiyo maana, kuhusu wanadamu,
  • 29:44 - 29:46
    mtu anahitaji kuongozwa na ufunuo wa kiungu
  • 29:46 - 29:51
    ili kupata kiini cha jambo linapokuja suala la hukumu.
  • 29:51 - 29:53
    Tunapolijua hili.
  • 29:53 - 29:56
    Tunajua kwamba hatupaswi kumhukumu mtu yeyote kwa sura
  • 29:56 - 29:59
    kwa sababu Mungu pekee ndiye anayejua hali halisi
  • 29:59 - 30:03
    ya moyo wa mwanadamu.
  • 30:03 - 30:08
    Inapokuja kwa mambo ya Mungu asiyeonekana,
  • 30:08 - 30:10
    tunahitaji kuwa katika roho
  • 30:10 - 30:13
    kwa sababu imani pekee ndiyo impendezayo Mungu.
  • 30:13 - 30:17
    Waebrania 11:6
  • 30:17 - 30:22
    Pasipo imani haiwezekani kumpendeza;
  • 30:22 - 30:27
    kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba Mungu yuko
  • 30:27 - 30:32
    na kwamba Yeye ndiye Mlipaji wa wale wanaomtafuta kwa bidii.
  • 30:32 - 30:37
    Tunamtafuta kwa bidii, kama tulivyosema leo, kwa imani.
  • 30:37 - 30:41
    Kumbuka, imani inamlenga Mungu asiyeonekana,
  • 30:41 - 30:45
    wakati maono ya asili yanalenga nje, kinachoonekana,
  • 30:45 - 30:49
    kile kinachoonekana, ambacho ni halisi.
  • 30:49 - 30:52
    Kwa hiyo mtu wa kiroho, ninamaanisha, mtu wa imani
  • 30:52 - 30:56
    haridhiki na ujuzi wa akili bali hutazama zaidi ya hayo,
  • 30:56 - 31:00
    kwa sababu Biblia inasema katika 2 Wakorintho 5:7,
  • 31:00 - 31:02
    tunaenenda kwa imani, si kwa kuona.
  • 31:02 - 31:05
    Ndiyo, imani ni kutoka katika roho ya mwanadamu.
  • 31:05 - 31:08
    Ninamaanisha ulimwengu usioonekana au ulimwengu wa kiroho.
  • 31:08 - 31:11
    Na kuona ni kutoka katika mwili wa mwanadamu,
  • 31:11 - 31:15
    ulimwengu unaoonekana au ulimwengu wa asili.
  • 31:16 - 31:22
    Na sasa, hebu tutazame tena katika kitabu cha 2 Wakorintho 4 kuanzia mstari wa 18.
  • 31:22 - 31:23
    Hebu tusome pamoja.
  • 31:23 - 31:27
    2 Wakorintho 4:18
  • 31:28 - 31:42
    18 Kwa maana hatuweki mawazo yetu kwenye vitu vinavyoonekana bali kwenye vitu visivyoonekana. Maana vile vinavyoonekana ni vya muda mfupi, lakini vile visivyoonekana vinadumu milele.
  • 31:42 - 31:50
    Na Biblia inasema zaidi katika 1 Samweli 16:6-13, unaweza kusoma zaidi kwa undani katika wakati wako.
  • 31:50 - 31:55
    yote ni kuhusu Samweli na Daudi, mfalme wa pili wa Israeli.
  • 31:55 - 32:00
    Samweli, nabii alitumwa kwenye nyumba ya Yese huko Bethlehemu
  • 32:00 - 32:05
    kumtia mafuta mfalme mpya aliyewekwa rasmi wa Israeli.
  • 32:05 - 32:10
    Alipofika, alimtazama mwana wa Yese mwenye sura nzuri zaidi
  • 32:10 - 32:15
    kama mfalme mteule lakini Mungu alimkataa
  • 32:15 - 32:17
    na akamchagua aliyepuuzwa.
  • 32:17 - 32:23
    mvulana wa kawaida mdogo na mchungaji, Daudi
  • 32:23 - 32:27
    Muulize Nabii Samweli katika Kitabu cha 1 Samweli 16:7
  • 32:27 - 32:30
    na angekufundisha kwamba
  • 32:30 - 32:33
    tunapaswa kujifunza kutozingatia nje.
  • 32:33 - 32:39
    Ninamaanisha, sio juu ya sifa za nje za mwanadamu zinazoonekana.
  • 32:39 - 32:42
    Lakini tunapaswa kuzingatia ndani kwa kuangalia ndani
  • 32:42 - 32:45
    moyoni kwa msaada wa Roho Mtakatifu.
  • 32:45 - 32:51
    Ikiwa tunataka kuona mambo jinsi Mungu anavyoyaona juu ya mwanadamu.
  • 32:51 - 32:53
    Kwa hiyo asante sana.
  • 32:53 - 32:57
    Ndio, huo ulikuwa mtazamo mfupi wa maana yake - 'nje' na 'ndani'.
  • 32:57 - 33:02
    Na ndio, sote tunahitaji kuukuza utu wetu wa ndani, mtu wetu wa kiroho.
  • 33:02 - 33:06
    Na kwa msaada wa Roho Mtakatifu kila siku, kila wakati tunaweza.
  • 33:11 - 33:18
    Mtu anawezaje kukuza imani kwa Mungu, kwa dhati?
  • 33:18 - 33:24
    Kwanza, kuna haja ya kujua imani ni nini.
  • 33:24 - 33:28
    Tatizo la imani linafanywa kuwa rahisi kueleweka pale tu
  • 33:28 - 33:31
    tunapojua kwamba imani ni kutenda tu
  • 33:31 - 33:34
    juu ya kile ambacho Mungu amesema.
  • 33:34 - 33:40
    Suala kuu la imani yetu ni ukweli wa imani hiyo.
  • 33:40 - 33:44
    Ili imani iwe ya kweli, lazima itegemee Neno la Mungu,
  • 33:44 - 33:52
    ambalo ni Roho na Uzima. ( Yohana 6:63 )
  • 33:52 - 33:55
    Mwanadamu huongea maneno ya kawaida
  • 33:55 - 34:02
    bali Mungu hunena Maneno ambayo ni Roho na Uzima.
  • 34:02 - 34:05
    Lakini ili neno la mwanadamu liwe Neno la Mungu,
  • 34:05 - 34:09
    lazima liathiriwe na Roho Mtakatifu kwa uzima.
  • 34:09 - 34:14
    Swali ni: Je, mwanadamu anaweza kusema Maneno ya Uzima?
  • 34:14 - 34:16
    Mwanadamu huongea maneno ya kawaida
  • 34:16 - 34:21
    lakini mwanadamu anaweza kunena Maneno ya Uzima ambayo ni Roho na Uzima
  • 34:21 - 34:25
    yanapoathiriwa na Roho Mtakatifu.
  • 34:25 - 34:31
    Maneno hayo lazima yaathiriwe na Roho Mtakatifu kwa uzima.
  • 34:31 - 34:34
    Ninamaanisha nini ninaposema kuna uzima katika Neno?
  • 34:34 - 34:36
    Neno la Mungu ni Roho na Uzima
  • 34:36 - 34:41
    kwa sababu lina uwezo wa kuzalisha nguvu ya kiroho
  • 34:41 - 34:47
    ambayo hukua na kustawi ndani ya mioyo yetu iitwayo imani.
  • 34:47 - 34:52
    Imani hiyo ndiyo inayosukuma maneno yetu kufanya maajabu.
  • 34:52 - 34:55
    Hiyo ni imani ya Biblia.
  • 34:55 - 35:14
    Imani ya Biblia inaitwa Imani ya Kiroho, katika kitabu cha 2 Wakorintho 4:13
  • 35:14 - 35:37
    13 Na kwa kuwa tuna roho ile ile ya imani; kama ilivyoandikwa, niliamini, na kwa sababu hiyo nilinena; sisi nasi twaamini, na kwa sababu hiyo twanena
  • 35:37 - 35:43
    Kwa hivyo imani hufanyika katika sehemu mbili:
  • 35:43 - 35:45
    Kwa mioyo yetu tunaamini;
  • 35:45 - 35:52
    Kwa vinywa vyetu tunakiri, na imani ni yote mawili.
  • 35:52 - 35:56
    Unajua, mfano wa wana saba wa Skeva unaonyesha hivyo
  • 35:56 - 35:59
    imani ya kweli si kuiga.
  • 35:59 - 36:03
    Imani lazima itokee katika moyo wa kila mtu
  • 36:03 - 36:07
    au katika usadikisho, ambao unaongoza kwenye harakati halisi
  • 36:07 - 36:10
    au maungamo halisi ya imani.
  • 36:10 - 36:15
    Ili imani iwe ya kweli, moyo na kinywa havipaswi kupingana kamwe.
  • 36:15 - 36:19
    Kwa maneno mengine, tunapaswa kumaanisha kile tunachosema.
  • 36:19 - 36:22
    Hii ina maana kwamba tunapaswa kuamini kile tunachokiri.
  • 36:22 - 36:24
    Je, unaamini unachokiri?
  • 36:24 - 36:26
    Unamaanisha unachosema?
  • 36:26 - 36:29
    Kwa sababu imani ya kimaandiko au imani ya kibiblia imeonyeshwa
  • 36:29 - 36:35
    kwa kuamini kwenye moyo na kukiri kwa kinywa.
  • 36:35 - 36:39
    Kinywa lazima kiwe na makubaliano kamili ya moyo
  • 36:39 - 36:42
    kabla ya kuwa na maungamo ya imani yanayokubalika au ya kweli.
  • 36:42 - 36:45
    Kweli kabisa.
  • 36:45 - 36:47
    Huo ndio ufunguo, makubaliano.
  • 36:47 - 36:52
    Swali ni: Imani inaweza kustawije?
  • 36:52 - 36:56
    Ukuaji wa Neno la Mungu moyoni mwako,
  • 36:56 - 37:01
    huzaa imani ndani ya moyo wako.
  • 37:01 - 37:02
    Warumi 10:17
  • 37:02 - 37:08
    Imani hukua tunaposikia na kutii Neno la Mungu.
  • 37:16 - 37:30
    Je, mtu anahamaje kutoka kwenye ujuzi wa hisia hadi ujuzi wa ufunuo?
  • 37:37 - 37:42
    Je, mtu anahamaje kutoka kwenye ujuzi wa hisia hadi ujuzi wa ufunuo?
  • 37:42 - 37:47
    Ndiyo, hilo ndilo jambo ambalo sisi sote waumini tunapaswa kujiuliza.
  • 37:47 - 37:51
    Hebu tukumbuke kilichompata mtumishi wa Elisha.
  • 37:51 - 37:53
    Kwa macho yake ya kimwili,
  • 37:53 - 37:58
    mtumishi wa Elisha aliona hatari ya papo hapo na hofu ikamshika.
  • 37:58 - 38:03
    Bwana wake alipomwomba Mungu amfungue macho ya rohoni.
  • 38:03 - 38:08
    Macho yake yakafunguliwa na katika roho,
  • 38:08 - 38:11
    aliona malaika wakimzunguka.
  • 38:11 - 38:12
    Na nini kilitokea?
  • 38:12 - 38:14
    Hofu yake ikatoweka.
  • 38:14 - 38:15
    Ndiyo.
  • 38:15 - 38:20
    Kwa hiyo kuhama kutoka maarifa ya hisia hadi maarifa ya ufunuo
  • 38:20 - 38:26
    ni suala la kuukabidhi moyo wako kwa Roho Mtakatifu.
  • 38:26 - 38:30
    Roho Mtakatifu ndiye anayefungua macho ya imani yetu
  • 38:30 - 38:34
    kuona ukweli uliofichwa katika Neno la Mungu.
  • 38:34 - 38:38
    Kutafakari katika Neno la Mungu huleta ufunuo.
  • 38:38 - 38:40
    Huo ndio ufunguo.
  • 38:40 - 38:47
    Tunatafakari hadi Mungu atupe nuru iliyo wazi, ufahamu wa wazi.
  • 38:47 - 38:49
    Kwa hiyo unapotafakari Neno la Mungu,
  • 38:49 - 38:55
    kumruhusu Roho Mtakatifu kuchukua uongozi, ufunuo utakuja
  • 38:55 - 38:58
    na ufunuo utakapokuja , utakubeba
  • 38:58 - 39:02
    juu ya ulimwengu wa hisia hadi katika uwepo wa Mungu
  • 39:02 - 39:06
    katika roho na huko utaona waziwazi;
  • 39:06 - 39:10
    hapo ndipo ufahamu wa kiroho unakuja.
  • 39:10 - 39:24
    Ngoja tusome katika kitabu cha 2 Wafalme 6 kuanzia mstari wa 15
  • 39:25 - 39:38
    15 Kesho yake asubuhi na mapema, mtumishi wa mtu wa Mungu alipoamka na kutoka nje, jeshi, pamoja na farasi na magari ya vita, likawa limeuzunguka mji. Mtumishi wake akasema, “Ole wetu, bwana wangu! Tutafanya nini?
  • 39:38 - 39:47
    16 Nabii akajibu, “Usiogope. Wale walio pamoja nasi ni wengi zaidi kuliko wale walio pamoja nao.”
  • 39:47 - 39:51
    Jiweke katika Maandiko na umsikie Mungu akikuambia,
  • 39:51 - 39:55
    Walio pamoja nawe ni wengi kuliko wale walio kinyume chako.
  • 39:55 - 40:10
    17 Kisha Elisha akaomba, “Ee Bwana, mfumbue macho huyu mtumishi ili apate kuona.” Ndipo Bwana akayafumbua macho ya yule mtumishi, naye akatazama na kuona vilima vimejaa farasi na magari ya moto, yamemzunguka Elisha pande zote.
  • 40:10 - 40:14
    Nakipenda sana hiki kipande cha maandiko.
  • 40:14 - 40:19
    Ni mfano mzuri wa swali lako kuhusu kuhama kutoka kwenye maarifa ya hisia kwenda kwenye maarifa ya ufunuo.
  • 40:19 - 40:23
    Hiki ndicho hasa kilichomtokea mtumishi wa Elisha.
  • 40:23 - 40:26
    Na hiki ndicho hasa kinachotokea kwa wengi wetu leo.
  • 40:26 - 40:29
    Wengi leo katika nyumba zao wameelemewa na hali zao
  • 40:29 - 40:31
    kwa sababu tunazitazama kwa asili
  • 40:31 - 40:35
    na unazidiwa na hofu inakuja na shaka inakuja.
  • 40:35 - 40:37
    Kwa hivyo kuna haja ya sisi kubadili mtazamo wetu
  • 40:37 - 40:41
    kutoka asili hadi kwenda rohoni.
  • 40:41 - 40:44
    Kwa hivyo kuhama kutoka maarifa ya hisia kwenda kwenye ufunuo
  • 40:44 - 40:47
    ni kwa neema.
  • 40:47 - 40:50
    Unachohitaji kufanya ni kujinyenyekeza
  • 40:50 - 40:57
    chini ya uongozi wa Roho Mtakatifu - Roho wa Ufunuo.
  • 40:57 - 41:01
    Mabadiliko hayo, hatua hiyo ni kidogo kidogo,
  • 41:01 - 41:04
    kila siku, kidogo kidogo, kila dakika, kidogo kidogo.
  • 41:04 - 41:09
    Ni safari na safari ya maili elfu moja huanza na hatua moja.
  • 41:09 - 41:11
    Kwa hivyo tuna furaha sana leo
  • 41:11 - 41:14
    kwamba ulijiunga nasi kuchukua hatua hiyo, hatua hiyo kuelekea rohoni
  • 41:14 - 41:16
    kwa kuungana nasi kwenye programu leo,
  • 41:16 - 41:20
    ambayo ni 'KATIKA NURU YA NENO LA MUNGU'
  • 41:20 - 41:24
    Kwa hivyo safari hiyo leo imeanza na hatua hii ambayo umechukua.
  • 41:24 - 41:28
    Na kumbuka MFULULIZO WA MSINGI - MIHADHARA YA KIMUNGU
  • 41:28 - 41:30
    ambayo umekuwa ukiona kwenye Chuo Kikuu cha Mungu -
  • 41:30 - 41:31
    huhitaji tu kutazama mara moja
  • 41:31 - 41:33
    unajua, Neno la Mungu halifungwi na wakati.
  • 41:33 - 41:35
    Kila Neno la Mungu ni Roho na Uzima.
  • 41:35 - 41:38
    Chukua muda kutazama tena na tena,
  • 41:38 - 41:43
    pitia vifungu vya Biblia, tafakari ukweli uliofichwa hapo
  • 41:43 - 41:46
    na ukitaka kutafuta mahali mafundisho hayo yalipo,
  • 41:46 - 41:48
    unaweza kuangalia katika maelezo hapa chini.
  • 41:48 - 41:52
    Kuna kiunganishi na ikiwa una maswali zaidi, kumbuka,
  • 41:52 - 41:56
    unapotafakari mafundisho haya, maswali yatatokea moyoni mwako
  • 41:56 - 41:59
    na unaweza kutuma maswali yako kwetu kwa kwenda
  • 41:59 - 42:03
    kwenye tovuti yetu - theuog.org - kwenda kwenye sehemu ya mawasiliano
  • 42:03 - 42:05
    na kututumia ujumbe.
  • 42:05 - 42:09
    Na tutapitia maswali yako yote na kwa neema ya Mungu,
  • 42:09 - 42:13
    yatajibiwa chini ya uongozi wa Roho Mtakatifu.
  • 42:13 - 42:17
    Hakuna njia ya mkato ya ukomavu wa kiroho.
  • 42:17 - 42:24
    Ufahamu wetu wa kidunia lazima utoe nafasi kwa ufahamu wa kiroho au ufunuo, kufikia ukomavu. ” – Nabii TB Joshua
  • 42:24 - 42:27
    Mafundisho yote tunayokupa hayana mpaka wa muda.
  • 42:27 - 42:30
    Tafadhali pitia, tafakari juu yake,
  • 42:30 - 42:34
    na umwombe Roho Mtakatifu akusaidie kuwa na uelewa mzuri juu yake.
  • 42:34 - 42:38
    Hiyo ndiyo njia pekee imani inaweza kukua katika maisha yetu.
  • 42:38 - 42:42
    Kwamba tuna ufunuo haimaanishi tunaweza kukulazimisha kuamini;
  • 42:42 - 42:44
    lazima uwe na ufunuo na usadikisho wako mwenyewe.
  • 42:44 - 42:45
    Unakujaje?
  • 42:45 - 42:47
    Soma, tafakari.
  • 42:47 - 42:52
    Ruhusu Roho wa Mungu akuongezee ufahamu wako.
  • 42:52 - 42:54
    Tunahitaji kuwa wakristo wakomavu
  • 42:54 - 42:57
    kwa sababu tuko katika mazingira yenye changamoto nyingi
  • 42:57 - 42:58
    na Mungu anataka uishi kwa imani, uwe hodari katika imani.
  • 42:58 - 43:01
    Unaweza kufanya hivyo jinsi gani?
  • 43:01 - 43:04
    Unaweza kufikia hilo tu kwa kuendeleza uhusiano wako
  • 43:04 - 43:08
    pamoja na Mgeni wa ajabu asiyeonekana - Roho Mtakatifu.
  • 43:08 - 43:11
    Vipi? Vutia umakini wake.
  • 43:11 - 43:15
    Na unaweza kufanya hivyo tu unapotafakari Neno na kuomba
  • 43:15 - 43:19
    na atakuja na kuboresha mipaka yako ya kiroho.
  • 43:19 - 43:20
    katika jina la Yesu.
  • 43:20 - 43:23
    Kwa hiyo, ahsante kwa kujiunga nasi kwenye kipindi hiki cha leo,
  • 43:23 - 43:26
    'KATIKA NURU YA NENO LA MUNGU'
  • 43:26 - 43:30
    Kama vile Nikodemo alivyomwendea Yesu usiku ili kuuliza maswali,
  • 43:30 - 43:34
    kujua na kukuza imani katika Yesu,
  • 43:34 - 43:39
    wewe pia unaweza kutazama hili na kuuliza maswali moyoni mwako kwa Mungu
  • 43:39 - 43:40
    na Roho Mtakatifu,
  • 43:40 - 43:44
    Msaidizi, Mshauri atakuja na kujibu maswali yako
  • 43:44 - 43:46
    kupitia Neno la Mungu.
  • 43:46 - 43:50
    Ndiyo, ndiyo maana kila kitu kiko katika nuru ya Neno la Mungu.
  • 43:50 - 43:54
    Amina. Watakatifu, ndugu, dada, waumini duniani kote,
  • 43:54 - 43:58
    tunaenda kukuombea.
  • 43:58 - 44:00
    Tumeona barua pepe nyingi sana.
  • 44:00 - 44:02
    Tulipitia maswali na majibu yote.
  • 44:02 - 44:05
    Tumeona watu wengi wakipitia uchungu,
  • 44:05 - 44:07
    maumivu na matatizo.
  • 44:07 - 44:11
    Kwa hiyo tunaenda kuomba pamoja, mwamini Mungu
  • 44:11 - 44:15
    kwamba Mungu Mwenyezi atakutana nawe katika sehemu ya hitaji lako muhimu,
  • 44:15 - 44:17
    kwa maana Yesu hafanyi neno lolote pasipo Neno lake.
  • 44:17 - 44:21
    Usisahau, Neno la Mungu lina kipaumbele kuliko jina.
  • 44:21 - 44:23
    Ndio maana tunakupa mafundisho haya.
  • 44:23 - 44:27
    Lakini tunasimama mbele za Mungu tukiwaombea,
  • 44:27 - 44:31
    na Mungu atakuweka katika rehema zake, katika jina la Yesu.
  • 44:31 - 44:35
    Kwa hiyo, endelea kuungana nasi hapa kwenye Chuo Kikuu cha Mungu.
  • 44:35 - 44:38
    Ujuzi wa hisia hukoma pale ufunuo uwadiapo.
Title:
MAJIBU YA BIBLIA YALIYOFICHIKA | INGIA KATIKA ROHO - SEHEMU YA 2
Description:

Je, umepata ukweli uliofichika kutoka kweye Sehemu ya 1 ya Mfululizo wa Msingi, ‘Pga Hatua Katika Roho’? Jiunge na Racine na Ruth wanapochukua muda kujibu baadhi ya maswali yako.

Kama vile Nikodemo alivyomjia Yesu usiku kuuliza maswali yaliyokuwa yakisumbua imani yake, wengi wametuma maswali yao. Jibu la kila swali letu liko katika Neno la Mungu. Fungua moyo wako kwa Roho Mtakatifu, Mwalimu wa Kimungu na kuruhusu majibu ya maswali haya yaimarishe imani yako, katika programu hii maalum, ‘KATIKA NURU YA NENO LA MUNGU’.

Je! una swali kwa Racine & Ruth katika Chuo Kikuu cha Mungu?
Tutuma ujumbe kwenye https://theuog.org/contact/

SURA:
00:00 - Utangulizi
01:26 - Ni matumizi gani ya kweli ya hisia zetu?
28:53 - Unamaanisha nini usemapo kwa 'nje'?
37:19 - Je, mtu anahamaje kutoka kwenye ujuzi wa hisia kwenda kwenye ujuzi wa ufunuo?
41:19 - Safari yako imeanza
43:54 - Jitayarishe kwa maombi...

#Racine #Ruth #TheUOG #Teaching

-----------------------------------------
Mfululizo wa Msingi wa Chuo Kikuu cha Mungu: "PIGA HATUA KATIKA ROHO!" ni mfululizo wa mafundisho chini ya uongozi wa Roho Mtakatifu utakaopatikana kwa wote, akifunua hazina iliyofichwa katika Neno la Mungu ambayo huchochea roho zetu kupiga hatua katika roho…. maana hapo ndipo Mungu alipo. Ni dhana potofu kwamba kweli za kiroho zinaweza kutambulika kiakili. Tunahitaji kuwa wabichi; yaani tunahitaji kuwa katika Roho - ulimwengu wa maarifa ya ufunuo, tukiikabidhi mioyo yetu kwa uvuvio wa Roho Mtakatifu, Roho yule yule wa Ufunuo (Waefeso 1:17-18). Ufunuo huleta usadikisho na usadikisho huleta harakati za kweli katika safari yetu na Yesu, safari yetu ya Umilele.

------------------------------------------
Tufuate kwenye mitandao ya kijamii @theuogofficial:
https://facebook.com/theuogofficial
https://instagram.com/theuogofficial
https://twitter.com/theuogofficial
https://tiktok.com/theuogofficial

------------------------------------------
➡️ Tuma Ombi Lako la Maombi: https://theuog.org/contact/
➡️ Kuwa Mjitoleaji: https://theuog.org/contact/volonteer/
➡️ Toa: https://theuog.org/?form=give

more » « less
Video Language:
English
Team:
The University of God
Duration:
44:49

Swahili subtitles

Revisions Compare revisions