-
[Maelezo ya uongo]
-
Maelezo yote yasiyo ya kweli ni uchafu.
-
Lakini ingawa baadhi yake ni kama uchafu,
-
baadhi yake ni kama uchafu wenye sumu.
-
Yanaweza kuchafua mazingira ya
mtandaoni na kuharibu jamii.
-
Maelezo ya uongo ni yasiyo ya kweli
au yanayopotosha
-
yanayosambazwa kimakusudi ili kusababisha
madhara.
-
Maelezo ya uongo yanaweza pia kutumiwa
kubuni mchanganyiko kuhusu
-
iwapo hata inawezekana kujua ukweli.
-
Wanaobuni na kusambaza maelezo ya uongo
-
wangependa kuathiri jinsi
wengine wanafikiri na kutenda.
-
Maelezo ya uongo yanaweza kubuniwa
na serikali za kigeni,
-
mashirika ya nchini,
-
au makundi ya watu.
-
Yanaweza kubuniwa ili:
-
kufedhehesha mtu au ujumbe wake;
-
kuzidisha migawanyiko ya jamii
kwa kuzidisha mzozo
-
kati ya walio na maoni tofauti;
-
kupunguza imani kwa taasisi za demokrasia
k.m vyombo vya habari na serikali,
-
kama njia ya kuwafanya raia
kuhisi beuzi au kutojali;
-
kuhimiza nadharia za uongo
zinazoshuku uhalisia wa matukio ya kweli;
-
au kuathiri matokeo ya uchaguzi.
-
Maelezo ya uongo yanaweza kuanza kwenye
ubao wa ujumbe
-
ambako watu "wachokozi" wanaeneza
uvumi usio wa kweli kuhusu watu,
-
matukio na masuala kwa kutumia
mtandao jamii,
-
au yanaweza kubuniwa katika
viwanda vya uchokozi,
-
ambako watu hulipwa kutunga makala
-
yanafanana na habari za kweli.
-
Kwa hivyo hili hufanya kazi vipi?
-
Wanaobuni maelezo ya uongo wanajua
-
jinsi ya kugeuza akili zetu na teknolojia
-
ili kusaidia kueneza maelezo ya uongo
na ya kupotosha.
-
Maelezo ya uongo yananuiwa
kulenga hisia zetu,
-
ili tuweze kuwa wepesi wa kuyakubali
-
na kuyashiriki kwa wengine.
-
Hadithi na madai yasiyo ya kweli yanaweza
pia kuwa na ukweli fulani
-
ili kufanya maelezo yote yaaminike zaidi.
-
Picha na meme zaweza kusaidia
kueneza maelezo ya uongo haraka,
-
kwa sababu watu
hawafikiri zaidi kuhusu picha
-
kuliko wanavyofikiri maneno.
-
Watu wanaweza kulengwa na maelezo ya uongo
-
kwa sababu ya sifa yetu au tunachoamini.
-
Mtandao unaruhusu ujumbe
kuenea mbali na haraka,
-
hasa wakati unajua
jinsi ya kufanya maudhui yasambae.
-
Kwenye mtandao jamii,
-
algoriti za kompyuta huamua watakachoona
watumiaji katika mipasho yao.
-
Algoriti hizi huonyesha
maudhui ambayo ni maarufu.
-
Watayarishaji wa maelezo ya uongo wanaweza
kuzidisha umaarufu wa wazo
-
kwa kutumia vijibu,
-
programu za kompyuta zinazochapisha,
kupenda na kushiriki kiotomatiki.
-
Akaunti za vijibu zinaweza kuifanya
ionekane kwamba watu wanazungumzia kitu
-
ilhali hawazungumzii.
-
Wazo ni kushawishi mazungumzo
-
kwa kutangaza mawazo fulani
au kukosoa mengine.
-
Baada ya watu kuona, kushiriki
na kuingiliana na machapisho haya bandia,
-
yatakuwa maarufu kihalisia.
-
Maelezo ya uongo
yanayotangazwa kwa njia hii
-
yanaweza kuvutia umakini
wa mashirika halali ya habari.
-
Wanahabari wanaweza kuripoti
kuyahusu, na kuyaeneza zaidi—
-
inayofanya wachokozi kufaulu.
-
Kuna watu wengi ambao
wangependa kushawishi jinsi unavyofikiri,
-
kuanzia wanasiasa hadi watangazaji,
hadi familia na marafiki.
-
Ni muhimu kujua kuwa pia kuna
makundi yaliyojipanga mtandaoni
-
ambayo yangependa kukupotosha,
kukuchanganya na kukushawishi
-
na huenda malengo yao yasijulikane mara
moja.
-
Hivyo, unaweza kuchukua hatua ipi?
-
Hatua nzuri ya kwanza ni
kutathmini hisia zako.
-
Je, hadithi au chapisho linakufanya
ukasirike, au ufurahi ili ulishiriki?
-
Huo ni wakati mzuri wa kusubiri
na kufanya utafiti kiasi.
-
Sifa ya chanzo ni ipi?
-
Je, maudhui ni ya kweli au yanapotosha?
-
Vyanzo vingine vina maoni yapi?
-
Subiri kisha ukague,
-
ili usidanganywe.
-
[Imeletwa kwako na CIVIX]
-
[Kwa usaidizi wa Kanada]
-
Manukuu ni ya Claudia Contreras
Ukaguzi ni wa Carol Wang