Dini na watoto
-
0:00 - 0:04Nitaenda kuongelea kuhusu dini.
-
0:05 - 0:09Lakini ni mada pana na nyeti sana,
-
0:09 - 0:11hivyo itabidi nijiwekee mpaka.
-
0:12 - 0:14Na kwahiyo nitajiwekea mpaka
-
0:14 - 0:18kuongelea tu kuhusu uhusiano kati ya dini
na kujamiiana. -
0:18 - 0:20(Kicheko)
-
0:20 - 0:22Haya ni majadiliano yenye uzito sana.
-
0:23 - 0:26Hivyo, nitaongelea juu ya ninachokumbuka
kua cha ajabu sana. -
0:26 - 0:29Ni pale wanandoa vijana walinong'oneza,
-
0:29 - 0:32"Usiku tutaenda kutengeneza mtoto."
-
0:32 - 0:37Maongezi yangu yatahusu athari ya dini
-
0:37 - 0:41kwa idadi ya watoto kwa mwanamke.
-
0:41 - 0:43Hii ni muhimu kweli,
-
0:43 - 0:44kwa sababu kila mtu anaelewa
-
0:44 - 0:47kua kuna aina fulani ya mpaka
-
0:47 - 0:50kwa jinsi watu wengi wanaweza kua kwenye
hii sayari. -
0:50 - 0:52Na kuna baadhi ya watu
-
0:52 - 0:55wanaosema kua idadi ya watu duniani imekua
kama hivi -- -
0:55 - 0:57bilioni tatu mwaka 1960,
-
0:57 - 1:00bilioni saba mwaka jana tu --
-
1:00 - 1:01na itaendelea kukua
-
1:01 - 1:05kwa sababu kuna dini zinazozuia wanawake
kuwa na watoto wachache, -
1:05 - 1:08na inaweza kuendelea hivi.
-
1:08 - 1:11Ni kwa kiasi gani hawa watu wako sahihi?
-
1:11 - 1:16Nilivyozaliwa kulikua na watoto chini ya
bilioni moja duniani, -
1:16 - 1:20na leo, 2000, kuna karibia bilioni mbili.
-
1:20 - 1:22Nini kimetokea tangu hapo,
-
1:22 - 1:25na nini wataalam wanatabiri kitatokea
-
1:25 - 1:27na idadi ya watoto karne hii?
-
1:27 - 1:30Hili ni jaribio. Unafikiri nini?
-
1:30 - 1:34Unafikiri itapungua mpaka bilioni moja?
-
1:34 - 1:38Itabaki sawa na kua bilioni mbili ifikapo
mwisho wa karne? -
1:38 - 1:41Idadi ya watoto itaongezeka kila mwaka
hadi miaka 15, -
1:41 - 1:44au itaendelea na kiwango cha haraka
kile kile -
1:44 - 1:46na kua watoto bilioni nne huko juu?
-
1:46 - 1:50Nitawaambia ifikapo mwisho wa hotuba
yangu. -
1:50 - 1:55Lakini sasa, dini inahusika vipi?
-
1:55 - 1:57Unapotaka kuainisha dini,
-
1:57 - 1:59ni ngumu kuliko unavyofikiri.
-
1:59 - 2:02Unaenda Wikipedia na ramani ya kwanza
unayopata ni hii. -
2:02 - 2:07Inagawanyisha dunia kwenye dini za
Ibrahimu na dini za Mashariki, -
2:07 - 2:09lakini hio haina undani wa kutosha.
-
2:09 - 2:13Hivyo tukaenda zaidi na kuangalia kwenye
Wikipedia, tukapata hii ramani. -
2:13 - 2:18Lakni hio inaianisha Ukristo, Uislamu na
Ubuddha -
2:18 - 2:19kwenye makundi mengi madogo,
-
2:19 - 2:21ambayo yalikua ya kina sana.
-
2:21 - 2:24Kwa hiyo pale Gapminder tulitengeneza
ramani yetu, -
2:24 - 2:27Na inaonekana hivi.
-
2:27 - 2:30Kila nchi ni puto.
-
2:30 - 2:33Ukubwa ni idadi ya watu -- China kubwa,
India kubwa hapa. -
2:33 - 2:38Na rangi sasa ni dini yenye wengi.
-
2:38 - 2:41Ni dini ambayo watu zaidi ya asilimia 50
-
2:41 - 2:42wanasema wanahusika.
-
2:42 - 2:47Ni dini ya Mashariki huko India na
China na nchi jirani za Asia. -
2:47 - 2:49Uislamu ni dini ya wingi
-
2:49 - 2:52njia yote kutoka Bahari ya Atlantiki
kupitia Mashariki ya Kati, -
2:52 - 2:55Ulaya ya Kusini na kupitia Asia
-
2:55 - 2:57njia yote mpaka Indonesia.
-
2:57 - 3:00Hapo ndipo tunapata Waislamu wengi.
-
3:00 - 3:05Na dini nyingi za Kikristo, tunaona kwenye
hizi nchi. Ni za bluu. -
3:05 - 3:09Na hizo ni nchi nyingi za Marekani na
Ulaya, -
3:09 - 3:12nchi nyingi za Afrika na chache za Asia.
-
3:12 - 3:15Nyeupe hapa ni nchi ambazo haziwezi kuwa
kuainishwa, -
3:15 - 3:18kwa sababu dini moja haifiki asilimia 50
-
3:18 - 3:21au kuna shaka kuhusu takwimu au sababu
yoyote nyingine. -
3:21 - 3:23Hivyo tulikua makini na hilo.
-
3:23 - 3:27Hivyo vumilia urahisi wetu sasa
nikiwapeleka kwenye hii picha. -
3:27 - 3:29Hii ni 1960.
-
3:29 - 3:32Na sasa naonyesha idadi ya watoto kwa
mwanamke hapa: -
3:32 - 3:35mbili, nne au sita --
-
3:35 - 3:38watoto wengi, watoto wachache.
-
3:38 - 3:41Na hapa mapato kwa mtu ikilinganishwa
dola. -
3:41 - 3:44Sababu ya hio ni kua watu wengi wanasema
unapaswa kua tajiri kwanza -
3:44 - 3:46kabla hujapata watoto wachache.
-
3:46 - 3:50Hivyo mapato ya chini hapa, mapato ya juu
pale. -
3:50 - 3:51Na kweli mwaka 1960,
-
3:51 - 3:54ulitakiwa uwe Mkristo tajiri kuwa na
watoto wachache. -
3:54 - 3:56Ilikua isipokua Japan.
-
3:56 - 3:59Japan hapa ilionekana ya kipekee.
-
3:59 - 4:02Vinginevyo ni nchi za Kikristo tu.
-
4:02 - 4:04Lakini pia kulikua na nchi nyingi za
Kikristo -
4:04 - 4:06zilizokua na watoto sita mpaka saba kwa
mwanamke. -
4:06 - 4:12Lakini zilikua Amerika ya Kusini au
zilikua Afrika. -
4:12 - 4:16Na nchi zenye Kiislamu kama dini kuu,
-
4:16 - 4:21zote zilikua na karibia watoto sita mpaka
saba kwa mwanamke, -
4:21 - 4:23bila kujali kiwango cha mapato.
-
4:23 - 4:27Na dini zote za mashariki isipokua Japan
zilikua na kiwango sawa. -
4:27 - 4:29Sasa tuone kilichotokea kwenye dunia.
-
4:29 - 4:31Ninaanzisha dunia, na tunaenda hivi.
-
4:31 - 4:34Sasa 1962 -- unaweza kuona wanakua
tajiri zaidi, -
4:34 - 4:37lakini idadi ya watoto kwa mwanamke
inashuka? -
4:37 - 4:39Angalia China. Wanashuka kwa haraka sana.
-
4:39 - 4:44Na nchi zote zenye Wasilamu wengi katika
mapato zinakuja chini, -
4:44 - 4:49kama nchi zenye Wakristo wengi kwenye eneo
lenye mapato ya kati. -
4:49 - 4:51Na tunapoingia kwenye karne hii,
-
4:51 - 4:55utakuta zaidi ya nusu ya watu huku chini.
-
4:55 - 5:00Na ifikapo 2010, tuko kwa kweli asilimia
80 ya watu -
5:00 - 5:04wanaoishi kwenye nchi zenye kama watoto
wawili kwa mwanamke. -
5:04 - 5:08(Makofi)
-
5:08 - 5:11Ni maendeleo ya kushangaza kabisa ambayo
yametokea. -
5:11 - 5:13(Makofi)
-
5:13 - 5:16Na hizi ni nchi za Marekani hapa,
-
5:16 - 5:18zenye $40,000 kwa kila mtu,
-
5:18 - 5:21Ufaransa, Urusi, Uajemi,
-
5:21 - 5:25Mexico, Uturuki, Algeria,
-
5:25 - 5:27Indonesia, India
-
5:27 - 5:30na moja kwa moja mpaka Bangladesh na
Vietnam, -
5:30 - 5:34ambazo zinazo chini ya asilimia tano ya
mapato kwa mtu wa Marekani -
5:34 - 5:37na kiasi sawa cha watoto kwa mwanamke.
-
5:37 - 5:40Naweza kukuambia kua takwimu ya idadi ya
watoto kwa mwanamke -
5:40 - 5:42ina uzuri wa kushangaza nchi zote.
-
5:42 - 5:44Tunapata hizo kutoka takwimu za sensa.
-
5:44 - 5:48Sio moja ya hizi takwimu zilizo na
mashaka sana. -
5:48 - 5:49Hivyo tunachohitimisha
-
5:49 - 5:52ni hauhitaji kua tajiri kuwa na watoto
wachache. -
5:52 - 5:54Imetokea katika dunia.
-
5:54 - 5:57Na kisha tunapoangalia dini.
-
5:57 - 5:59tunaona kua dini za mashariki,
-
5:59 - 6:02kwa kweli hakuna nchi hata moja yenye
wingi wa hio dini -
6:02 - 6:04ambayo ina zaidi ya watoto watatu.
-
6:04 - 6:08Ambapo na Uislamu kama dini ya wingi na
Ukristo, -
6:08 - 6:10unaona nchi njia yote.
-
6:10 - 6:12Lakini hakuna tofauti kubwa.
-
6:12 - 6:15Hakuna tofauti kubwa kati ya hizi dini.
-
6:15 - 6:18Kuna tofauti kwenye mapato.
-
6:18 - 6:22Nchi ambazo zina watoto wengi kwa mwanamke
hapa, -
6:22 - 6:24zina mapato ya chini kweli.
-
6:24 - 6:27Nyingi zao ziko Afrika kusini mwa Sahara.
-
6:27 - 6:30Lakini pia kuna nchi huku
-
6:30 - 6:34kama Guatemala, kama Papua New Guinea,
-
6:34 - 6:37kama Yemen na Afghanistan.
-
6:37 - 6:40Wengi hufikiri kua Afghanistan hapa
na Kongo, -
6:40 - 6:44ambazo zimeteseka na migogoro mikali,
-
6:44 - 6:47kua hazina ukuaji wa idadi ya watu wa
haraka. -
6:47 - 6:48Ni kinyume chake.
-
6:48 - 6:52Kwenye dunia leo, ni nchi zenye
kiwango cha juu cha vifo -
6:52 - 6:55ambazo zina ukuaji wa haraka wa idadi ya
watu. -
6:55 - 6:59Kwa sababu kifo cha mtoto kimefidiwa
na mtoto mmoja zaidi. -
6:59 - 7:01Hizi nchi zina watoto sita kwa mwanake.
-
7:01 - 7:06Zina kiwango cha vifo cha kusikitisha cha
mtoto mmoja mpaka wawili kwa mwanamke. -
7:06 - 7:09Lakini miaka 30 kutoka sasa, Afghanistan
inatoka milioni 30 mpaka milioni 60. -
7:09 - 7:13Kongo inaenda kutoka 60 mpaka 120.
-
7:13 - 7:16Hapo ndipo tunapata ukuaji wa idadi ya
watu. -
7:16 - 7:20Na wengi wanafikiri kua hizi nchi ziko
palepale, lakini hazipo. -
7:20 - 7:24Ngoja nilinganishe Senegal, nchi
iliotawaliwa na Waislamu, -
7:24 - 7:26na nchi iliotawaliwa na Wakristo, Ghana.
-
7:26 - 7:30Nazipeleka nyuma hapa kwenye uhuru wao,
-
7:30 - 7:33ambapo walikua huku juu mwanzoni mwa miaka
ya 1960. -
7:33 - 7:35Angalia tu walichokifanya.
-
7:35 - 7:37Ni maendeleo ya kushangaza,
-
7:37 - 7:39kutoka watoto saba kwa mwanake,
-
7:39 - 7:42wameenda moja kwa moja chini mpaka
wanne na watano. -
7:42 - 7:44Ni maendeleo makubwa.
-
7:44 - 7:45Hivyo inachukua nini?
-
7:45 - 7:49Basi tunajua vizuri kabisa
kinachohitajika kwenye hizi nchi. -
7:49 - 7:51Unahitaji kua na watoto kuishi.
-
7:51 - 7:54Unahitaji kutoka nje ya umasikini
uliokithiri -
7:54 - 7:58hivyo watoto sio wa muhimu kwa kazi kwenye
familia. -
7:58 - 8:00Unahitaji kua na upatikanaji wa baadhi ya
uzazi wa mpango. -
8:00 - 8:05Na unahitaji sababu ya nne, ambayo pengine
ni sababu muhimu kuliko zote. -
8:05 - 8:08Lakini ngoja nionyeshe hio sababu ya nne
-
8:08 - 8:10kwa kuangalia Qatar.
-
8:10 - 8:14Hapa tuna Qatar leo, na pale tuna
Bangladesh leo. -
8:14 - 8:17Kama nikizipeleka hizi nchi nyuma kwenye
miaka ya uhuru wao, -
8:17 - 8:20ambazo ni karibia mwaka mmoja
-- '71, '72 -- -
8:20 - 8:24ni maendeleo ya kushangaza kabisa ambayo
yalitokea. -
8:24 - 8:26Angalia Bangladesh na Qatar.
-
8:26 - 8:29Zenye mapato yanayotofautiana kabisa, ni
karibia muanguko sawa -
8:29 - 8:31kwenye idadi ya watoto kwa mwanamke.
-
8:31 - 8:33Na nini sababu ya Qatar?
-
8:33 - 8:35Basi kama kawaida yangu.
-
8:35 - 8:39Nilienda kwenye mamlaka ya takwimu ya
Qatar, kwenye tovuti yao -- -
8:39 - 8:41Ni tovuti nzuri sana. Ninaipendekeza --
-
8:41 - 8:47na nikaangalia juu -- ndio, ni burudani
nyingi hapa -- -
8:47 - 8:51na zinatolewa bure, nilikuta mwenendo
wa kijamii wa Qatar. -
8:51 - 8:54Ya kuvutia sana. Vingi vya kusoma.
-
8:54 - 8:58Nilikuta nguvu ya uzazi, na nikaangalia
jumla ya kiwango cha uzazi kwa mwanamke. -
8:58 - 9:02Hawa ni wasomi na wataalamu kwenye wakala
wa serikali wa Qatar, -
9:02 - 9:05na wakasema sababu za muhimu zaidi ni:
-
9:05 - 9:06"Ongezeko la umri kwenye ndoa ya kwanza,
-
9:06 - 9:10ongezeko la kiwango cha elimu cha mwanamke
wa Qatar -
9:10 - 9:13na wanawake zaidi kujumuika kwenye
nguvukazi." -
9:13 - 9:17Nisingekubali zaidi. Sayansi isingekubali
zaidi. -
9:17 - 9:19Hii ni nchi ambayo kweli imepitia
-
9:19 - 9:23utamaduni wa kushangaza sana sana.
-
9:23 - 9:25Hivyo kilichopo, ni hizi nne:
-
9:25 - 9:28Watoto wanatakiwa waishi, watoto
hawatakiwi kuhitajika kwa kazi, -
9:28 - 9:31wanawake wanatakiwa kupata elimu na
kujiunga na nguvukazi -
9:31 - 9:33na uzazi wa mpango unatakiwa kupatikana.
-
9:33 - 9:37Sasa angalia tena hii.
-
9:37 - 9:39Wastani ya idadi ya watoto duniani
-
9:39 - 9:43ni kama ya Colombia -- ni 2.4 leo.
-
9:43 - 9:46Kuna nchi huku juu amabazo ni maskini
sana. -
9:46 - 9:50Na ndipo uzazi wa mpango, maisha bora ya
watoto zinahitajika. -
9:50 - 9:53Nina pendekeza kwa nguvu mazungumzo ya
TED ya mwisho ya Melinda Gates. -
9:53 - 9:59Na hapa, chini, kuna nchi nyingi ambazo
zina chini ya watoto wawili kwa mwanamke. -
9:59 - 10:02Hivyo nikirudi sasa kuwapa jibu la
jaribio, -
10:02 - 10:04ni mbili.
-
10:04 - 10:07Tumefikia kilele mtoto.
-
10:07 - 10:09Idadi ya watoto haikui tena zaidi duniani.
-
10:09 - 10:11Bado tunajadili kilele mafuta,
-
10:11 - 10:14lakini ni dhahiri tumefika kilele mtoto.
-
10:14 - 10:17Idadi ya watu duniani itaacha kukua.
-
10:17 - 10:19Umoja wa Mataifa kitengo cha Wakazi
kilisema -
10:19 - 10:22kitaacha kukua kwenye bilioni 10.
-
10:22 - 10:26Lakini kwanini tunaongezeka kama idadi ya
watoto haiongezeki? -
10:26 - 10:28Basi nitawaonyesha hapa.
-
10:28 - 10:32Nitatumia hizi sanduku za kadi ambazo
madaftari yenu yalikuja. -
10:32 - 10:36Ni muhimu sana kwa madhumuni ya elimu.
-
10:36 - 10:39Kila kisanduku ni watu bilioni moja.
-
10:39 - 10:41Na kuna watoto bilioni mbili duniani.
-
10:41 - 10:48Kuna vijana bilioni mbili kati ya 15
na 30. -
10:48 - 10:50Hizi ni namba zilizokadiriwa.
-
10:50 - 10:55Halafu kuna bilioni moja kati ya 30 na 45,
-
10:55 - 10:58karibia moja kati ya 45 na 60.
-
10:58 - 11:00na tena kuna sanduku langu.
-
11:00 - 11:02Huyu ni mimi: 60-na zaidi.
-
11:02 - 11:04Tupo hapa juu.
-
11:04 - 11:10Hivyo kitakachotokea sasa hivi ni
tunachoita "ujazo mkubwa." -
11:10 - 11:13Utaona kua kuna kama bilioni tatu
inayokosekana hapa. -
11:13 - 11:17Haionekani kwa sababu wamekufa; hawakuwahi
kuzaliwa. -
11:17 - 11:21Kwa sababu kabla ya 1980, kulikua na watu
wachache zaidi waliozaliwa -
11:21 - 11:24kuliko waliopo wakati wa miaka 30
iliopita. -
11:24 - 11:27Hivyo kitakachotokea sasa ni wazi sana.
-
11:27 - 11:30Wazee, kwa sikitiko, tutakufa.
-
11:30 - 11:34Nyie wengine, mtakua wakubwa na mtapata
watoto bilioni mbili. -
11:34 - 11:37Kisha wazee watakufa.
-
11:37 - 11:41Wengine watakua wakubwa na kupata watoto
bilioni mbili. -
11:41 - 11:47Na tena wazee watakufa na mtapata watoto
bilioni mbili. -
11:47 - 11:49(Makofi)
-
11:49 - 11:53Hii ni ujazo mkubwa.
-
11:53 - 11:55Haiepukiki.
-
11:55 - 11:58Na unaona kua hili ongezeko lilitokea
-
11:58 - 12:03bila maisha kua marefu na bila kuongeza
watoto? -
12:03 - 12:08Dini inahusika kidogo sana kwenye idadi ya
watoto kwa mwanamke. -
12:08 - 12:11Dini zote duniani zina uwezo wa kikamilifu
-
12:11 - 12:16kudumisha thamani zao na kukabiliana
na hii dunia mpya. -
12:16 - 12:21Na tutakua tu bilioni 10 kwenye dunia hii,
-
12:21 - 12:25kama watu maskini watatoka kwenye
umaskini, -
12:25 - 12:28watoto wao wataishi, watakua na
upatikanaji wa uzazi wa mpango. -
12:28 - 12:30Hio inahitajika.
-
12:30 - 12:36Lakini haiepukiki kua tutakua bilioni
mbili mpaka tatu zaidi. -
12:36 - 12:39Hivyo unavyojadili na unavyopanga
-
12:39 - 12:42kwa rasilimali na nishati zinazohitajika
baadae, -
12:42 - 12:45kwa wanadamu kwenye hii sayari,
-
12:45 - 12:47unatakiwa upange kwa bilioni 10
-
12:47 - 12:49Asante sana.
-
12:49 - 12:55(Makofi)
- Title:
- Dini na watoto
- Speaker:
- Hans Rosling
- Description:
-
Hans Rosling alikua na swali: Kuna baadhi ya dini zenye kiwango cha juu cha uzazu zaidi ya nyingine -- na jinsi gani hii ina athiri ongezeko la idadi ya watu duniani? Akiongea kwenye TEDxSummit huko Doha, Qatar, alionyesha jedwali la takwimu kwa mda na katika dini. Akiwa na ishara yake ya ucheshi na ufahamu wa makini, Hans alifikia hatima ya kushangaza juu ya viwango vya uzazi duniani.
- Video Language:
- English
- Team:
closed TED
- Project:
- TEDTalks
- Duration:
- 13:20
![]() |
Nelson Simfukwe approved Swahili subtitles for Religions and babies | |
![]() |
Nelson Simfukwe accepted Swahili subtitles for Religions and babies | |
![]() |
Nelson Simfukwe edited Swahili subtitles for Religions and babies | |
![]() |
Doris Mangalu edited Swahili subtitles for Religions and babies | |
![]() |
Doris Mangalu edited Swahili subtitles for Religions and babies | |
![]() |
Doris Mangalu edited Swahili subtitles for Religions and babies | |
![]() |
Doris Mangalu edited Swahili subtitles for Religions and babies | |
![]() |
Doris Mangalu edited Swahili subtitles for Religions and babies |