< Return to Video

Siri yangu ya Uraibu! | USHUHUDA WA UKOMBOZI

  • 0:00 - 0:05
    Ningependa kumhimiza kila mtu ambaye anapitia aina yoyote ya uraibu
  • 0:05 - 0:12
    kushikilia tumaini na kutomkatia tamaa Mungu.
  • 0:18 - 0:25
    Sema, 'Wewe ibilisi, ninakuamuru kwa mamlaka katika jina la Yesu Kristo
  • 0:25 - 0:27
    kuondoka sasa hivi!
  • 0:27 - 0:31
    Ondoka na utumwa wako!
    Ondoka na mzigo wako!
  • 0:31 - 0:35
    Ondoka na ndoto zako mbaya!
    Ondoka na ugonjwa wako!
  • 0:35 - 0:37
    Ondoka sasa hivi!'
  • 0:39 - 0:43
    Jina langu ni Bokamoso.
    Ninaishi Botswana.
  • 0:43 - 0:48
    Yote yalianza mnamo 2002.
  • 0:48 - 0:55
    Nilikuwa nikiishi na familia yangu kubwa - nyanya yangu, shangazi yangu na watoto wake wawili.
  • 0:55 - 0:57
    Tulikuwa tunaishi kijijini.
  • 0:57 - 1:05
    Kwa hivyo wakati huo, shangazi yangu
    ndiye alikuwa anakula udongo huu wa kichuguu
  • 1:05 - 1:10
    kwa sababu kulikuwa na kichuguu karibu na
    tulipokuwa tukikaa kijijini.
  • 1:10 - 1:12
    Hapo ndipo udongo wa kichuguu ulipokuwa.
  • 1:12 - 1:17
    Ilianza nilipokuwa
    nikienda na shangazi yangu.
  • 1:17 - 1:21
    Alikuwa akienda kukusanya udongo huu wa kichuguu.
  • 1:21 - 1:26
    Nilikuwa nikienda naye wakati
    anaenda kuuchukua.
  • 1:26 - 1:32
    Tungeenda na mfuko wa plastiki ambapo
    angeuweka - mara zote.
  • 1:32 - 1:36
    Ilitokea siku moja nilienda peke yangu, bila yeye kujua.
  • 1:36 - 1:41
    Na hapo ndipo nilianza
    kuuonja.
  • 1:41 - 1:47
    Kadiri muda ulivyosonga, nilianza kuwa na
    hamu ya kula udongo wa kichuguu.
  • 1:47 - 1:51
    Hakujua kuwa nilikuwa nikifanya hivi.
    Nilikuwa nikifanya kwa siri.
  • 1:51 - 1:58
    Hakuna mtu aliyejua kuwa nilikuwa nikifanya hivi kwa sababu alikuwa mkali dhidi ya sisi kuula udogo huo,
  • 1:58 - 2:00
    lakini nilikuwa nikifanya kwa siri.
  • 2:00 - 2:03
    Miaka mitano baadaye, nilihamia
    kwa wazazi wangu.
  • 2:03 - 2:08
    Nilihama kijijini kwenda
    kukaa na wazazi wangu.
  • 2:08 - 2:13
    Na hapo ndipo hamu
    ilipoanza kuongezeka.
  • 2:13 - 2:17
    Hamu ilianza kukua
    kadri muda ulivyozidi kwenda.
  • 2:17 - 2:23
    Nilikuwa na umri wa miaka 14 wakati huo, nikiishi na wazazi wangu.
  • 2:23 - 2:29
    Tuliishi shambani na
    kulikuwa na vichaka karibu nasi.
  • 2:29 - 2:33
    Hapo ndipo tulipoishi na ambapo
    ningeweza kupata udongo wa kichuguu.
  • 2:33 - 2:40
    Kwa hivyo nilikuwa nikitoroka ili
    niende kula au kuukusanya.
  • 2:40 - 2:46
    Kama nilivyosema, hakuna mtu aliyejua kuwa
    nilikuwa nikifanya hivi. Ilikuwa siri yangu.
  • 2:46 - 2:51
    Hii iliendelea kwa muda mrefu sana.
  • 2:51 - 2:55
    Ilinisababishia mashambulizi mengi sana ya kiroho.
  • 2:55 - 3:00
    Kwa sababu hata shuleni,
    sikuweza kuzingatia.
  • 3:00 - 3:03
    Na nilikabiliwa na kukataliwa sana.
  • 3:03 - 3:05
    Darasani, sikuweza kuzingatia vizuri.
  • 3:05 - 3:10
    Hata nikiwaambia walimu kuwa sikuelewa darasani, hakuna aliyenisikiliza.
  • 3:10 - 3:16
    Hata nilipowaambia hali yangu,
    hakuna aliyenisikiliza.
  • 3:16 - 3:21
    Sikuweza kuzingatia vizuri shuleni kwa sababu nilijikita katika kula udongo wa kichuguu.
  • 3:21 - 3:26
    Sikuweza kula vizuri kwa sababu nilihakikisha kwamba nakula kwanza kabla ya kula.
  • 3:26 - 3:28
    Hata wakati mwingine, sikuweza kula kabisa.
  • 3:28 - 3:34
    Ningeenda kwa siku mbili au tatu
    bila kula chakula.
  • 3:34 - 3:39
    Nilijaribu sana kuacha
    uraibu huu kwa muda mrefu sana.
  • 3:39 - 3:43
    Nilitembelea hata makanisa; Nilitembelea moja ya makanisa makubwa hapa Botswana.
  • 3:43 - 3:47
    Mchungaji aliniambia kuna nyoka
    alinitembelea usiku.
  • 3:47 - 3:52
    Niliamini kwa sababu nilikuwa
    naota juu ya nyoka.
  • 3:52 - 3:56
    Nilijaribu kuacha hiki kitu kwa
    muda mrefu lakini sikuweza.
  • 3:56 - 4:00
    Labda ningeenda wiki bila kula
  • 4:00 - 4:05
    lakini hapo ndipo ningeanza kuwa na mashambulizi ya kiroho - kula ndotoni.
  • 4:05 - 4:11
    Ningekuwa na ndoto nikila na hamu ingeongezeka zaidi.
  • 4:11 - 4:14
    Ilikuwa ngumu kusamehe watu.
  • 4:14 - 4:18
    Sikuwa na amani moyoni mwangu.
  • 4:18 - 4:20
    Nilikuwa na hasira kali.
  • 4:20 - 4:26
    Hata watu walipokuwa wakijaribu kunishauri, niliichukulia kwa njia hasi.
  • 4:26 - 4:32
    Nilikuwa na migogoro nyumbani.
    Sikumsikiliza mtu yeyote.
  • 4:32 - 4:36
    Nilikuwa na migogoro na ndugu zangu.
    Sikuweza kumsikiliza mtu yeyote.
  • 4:36 - 4:40
    Nilikuwa na kuvimbiwa kwa sababu
    nilikuwa nakula sana.
  • 4:40 - 4:47
    Kwa hiyo ningetumia labda wiki tatu au mwezi bila kwenda chooni.
  • 4:47 - 4:52
    Hilo liliniathiri kwa njia nyingi sana.
    Sikuwa na imani.
  • 4:52 - 4:58
    Nilijiunga na
    Maombi ya Pamoja mnamo Agosti 2023.
  • 4:58 - 5:08
    Nilihakikisha nimejiunga na kila Maombi ya Pamoja na nilianza kuona mabadiliko mengi sana.
  • 5:08 - 5:11
    Kwa kila Sala ya Pamoja
    niliyokuwa najiunga nayo kila mwezi,
  • 5:11 - 5:15
    Niligundua sasa nina amani moyoni mwangu.
  • 5:15 - 5:19
    Nilianza kuona mambo kwa njia tofauti.
  • 5:19 - 5:25
    Nilianza kuwa na upeendo. Nilianza
    kuwa na roho hiyo ya utii.
  • 5:25 - 5:33
    Nilianza pia kusikiliza kila ushauri kutoka kwa watu ambao walikuwa wanajaribu kunishauri.
  • 5:33 - 5:38
    Mwanzoni, sikuwa na matazamo wowote chanya.
    Kama nilivyosema, nilikuwa na hasira kali.
  • 5:38 - 5:41
    Lakini tangu wakati huo na kuendelea,
    nilianza kuwa na utulivu huo.
  • 5:41 - 5:46
    Nilikuwa na kiburi sana lakini sasa
    naweza kuwashauri watu
  • 5:46 - 5:50
    kwa njia bora, kwa njia nzuri,
    kwa namna nzuri.
  • 5:50 - 5:54
    Sasa nina ujasiri wa kusimama
    mbele ya watu na kuzungumza nao.
  • 5:54 - 5:59
    Mwanzoni, nilikuwa na kujistahi. Kama nilivyosema , nilikabili kukataliwa sana.
  • 5:59 - 6:03
    Lakini sasa, watu wameanza
    kunikaribia.
  • 6:03 - 6:10
    Watu sasa wananitambua,
    na ninamshukuru Mungu wangu kwa hilo.
  • 6:10 - 6:19
    Sasa tuambie mabadiliko uliyoyaona
    katika hamu ya kula udongo wa kichuguu na
  • 6:19 - 6:22
    juu ya mtazamo wa roho ya kutosamehe,
  • 6:22 - 6:26
    ni mabadiliko gani uliyopata
    katika maeneo hayo?
  • 6:26 - 6:34
    Ilikoma kabisa. Sina tena hamu hiyo. Sipendi tena kula.
  • 6:34 - 6:39
    Sina tena
    mashambulizi ya kiroho ya kula.
  • 6:39 - 6:41
    Kila nilipojaribu kuacha hapo awali,
  • 6:41 - 6:45
    Ningekuwa na mashambulizi ya kiroho
    ambapo ningekula katika ndoto.
  • 6:45 - 6:48
    Kwa hivyo sina hiyo tena.
  • 6:48 - 6:52
    Nimepona kabisa kwa neema ya Mungu.
  • 6:52 - 6:56
    Ninaweza kwenda chooni kila siku.
  • 6:56 - 6:59
    Sina tena maumivu hayo kwenye tumbo langu.
  • 6:59 - 7:04
    Nilivyokuwa nikisema nilikuwa naumwa tumboni kwa sababu sikuenda chooni.
  • 7:04 - 7:08
    Hapo awali, nilikuwa mkorofi; ilikuwa ngumu
    kwangu kusamehe watu.
  • 7:08 - 7:15
    Baada ya maombi, nilianza kuwa na msamaha huo na utulivu ndani yangu.
  • 7:15 - 7:19
    Ningependa kumhimiza kila mtu ambaye anapitia aina yoyote ya uraibu
  • 7:19 - 7:25
    kushikilia tumaini na
    kutomkatia tamaa Mungu.
  • 7:25 - 7:28
    Wanapaswa kumwamini na kumtumainia Mungu.
  • 7:28 - 7:30
    Neno la Mungu linasema kuwa
    wakati wa Mungu ni bora zaidi.
  • 7:30 - 7:35
    Kwa hivyo usikate tamaa kwa Mungu,
    haijalishi hali ikoje.
  • 7:35 - 7:39
    Endelea kushikilia na kumwamini Mungu.
  • 7:39 - 7:43
    Chochote unachopitia,
    kitaisha, ni suala la muda tu.
Title:
Siri yangu ya Uraibu! | USHUHUDA WA UKOMBOZI
Description:

Bokamoso kutoka Botswana alipambana na uraibu wa ajabu tangu utotoni ambao aliuficha. Baada ya kupokea maombi katika jina la Yesu Kristo wakati wa Huduma ya Maombi ya Pamoja, sio tu kwamba aliwekwa huru kutokana na uraibu huo bali pia mashambulizi ya kiroho yanayohusiana nayo. Utukufu ni kwa Mungu!

Ili kupokea maombi bila malipo kutoka kwa Ndugu Chris kupitia Zoom, wasilisha ombi lako la maombi hapa - https://www.godsheart.tv/zoom

➡️ Pata Kutiwa Moyo Kila Siku kwenye WhatsApp - https://godsheart.tv/whatsapp/
➡️ Kuwa Mshirika wa TV wa Moyo wa Mungu - https://godsheart.tv/partnership
➡️ Habari kuhusu Maombi ya Mwingiliano - https://godsheart.tv/interactive-prayer/
➡️ Jitolee kama Mtafsiri wa TV ya Moyo wa Mungu - https://godsheart.tv/translate/
➡️ Shirikisha ushuhuda wako - https://godsheart.tv/testimony
➡️ Jiunge na Ibada yetu ya Maombi ya Moja kwa Moja Jumamosi ya kwanza ya kila mwezi - https://www.youtube.com/godshearttv/live

more » « less
Video Language:
English
Team:
God's Heart TV
Duration:
08:13

Swahili subtitles

Revisions Compare revisions