Mgogoro wa wakimbizi ni kipimo cha utu wetu
-
0:00 - 0:04Ninaenda kuongea nanyi kuhusu janga la kidunia la wakimbizi
-
0:04 - 0:08na lengo langu ni kuwaonyesha kwamba janga hili
-
0:08 - 0:11Linaweza kusimamiwa, halishindikani kutatuliwa,
-
0:12 - 0:17lakini pia kuwaonyesha kwamba hili jambo ni zaidi kuhusu sisi na vile tulivyo
-
0:17 - 0:21kama lilivyo ni jaribu kwa wakimbizi waliopo mstari wa mbele.
-
0:21 - 0:24Kwangu mimi, hili sio jukumu la kikazi tu,
-
0:24 - 0:29kwa vile ninaendesha taasisi isiyo ya kiserikali inayoshughululika na wakimbuzi duniani kote.
-
0:29 - 0:30nachukulia kama jukumu la kibinafsi.
-
0:31 - 0:33Naipenda picha hii.
-
0:34 - 0:36Yule kijana mtanashati sana upande wa kulia,
-
0:36 - 0:37yule sio mimi.
-
0:38 - 0:41Ni baba yangu, Ralph, akiwa London, mwaka 1940
-
0:41 - 0:43akiwa na baba yake Samwel.
-
0:44 - 0:46Walikuwa wakimbizi wa Kiyahudi tokea Ubelgiji.
-
0:46 - 0:50Walikimbia siku ambazo Nazi wa Ujerumani walivamia.
-
0:51 - 0:52Na naipenda picha hii, pia.
-
0:53 - 0:55Ni kundi la watoto wakimbizi
-
0:55 - 0:58walipowasili Uingereza mwaka 1946 kutokea Poland.
-
0:59 - 1:02Na katikati ni mama yangu, Marion.
-
1:03 - 1:06Alitumwa kwenda kuanza maisha mapya
-
1:06 - 1:07katika nchi mpya
-
1:07 - 1:08yeye mwenyewe
-
1:08 - 1:10akiwa na miaka 12.
-
1:11 - 1:13Najua hili;
-
1:13 - 1:16Kama Waingereza wasingeruhusu wakimbizi
-
1:16 - 1:17mwaka 1940,
-
1:18 - 1:21Nina uhakika nisingekuwa hapa leo.
-
1:22 - 1:26Bado katika miaka 70, gurudumu limezunguka kuwa kamili.
-
1:27 - 1:30Sauti za kuta ambazo zimejengwa,
-
1:30 - 1:32siasa za visasi,
-
1:32 - 1:36thamani ya ubinadamu na misingi katika moto
-
1:37 - 1:41katika nchi ambazo miaka 70 iliyopita zilisema hakuna tena kamwe
-
1:41 - 1:45wataokuwa bila mataifa na matumaini ambao ni wahanga wa vita.
-
1:47 - 1:49Mwaka uliopita, kila dakika,
-
1:50 - 1:54zaidi ya watu 24 walikuwa wakiondolewa kutoka majumbani mwao
-
1:54 - 1:56kwa mafarakano, machafuko na unyanyapaa wa kibaguzi:
-
1:57 - 2:00shambulio lingine la silaha za kemikali nchini Syria,
-
2:00 - 2:03Watalibani na machafuko nchini Afghanistan,
-
2:03 - 2:09wasichana waliotekwa na Boko Haram wakiwa shule Kaskazini- Mashariki mwa Nigeria.
-
2:10 - 2:13Hawa sio watu ambao wanahamia nchi nyingine
-
2:13 - 2:15kupata maisha bora.
-
2:15 - 2:17Wanahama kwa kuokoa maisha yao.
-
2:19 - 2:20Ni jambo la kuhuzunisha mno
-
2:22 - 2:27kwamba mkimbizi maarufu duniani hawezi kuja kuongea hapa leo hii.
-
2:27 - 2:29Wengi wenu mtaitambua picha hii.
-
2:30 - 2:32Inaonyesha mwili usio na maisha
-
2:32 - 2:35mwa mvulana wa miaka mitano aitwaye Alan Kurdi,
-
2:35 - 2:39mkimbizi wa Syria aliyefariki Mediterenian mwaka 2015.
-
2:39 - 2:43Alifariki na wengine 3700 wakati wakijaribu kuingia Ulaya.
-
2:44 - 2:46Mwaka uliofata, 2016,
-
2:47 - 2:49Watu 5000 walifariki.
-
2:51 - 2:52Walikuwa wamechelewa mno,
-
2:53 - 2:56lakini ni mapema kwa wengine mamilioni.
-
2:56 - 2:58Bado ni mapema kwa watu kama Frederick.
-
2:59 - 3:02Nilikutana nae katika kambi ya wakimbizi inayofahamika kama Nyarugusu nchini Tanzania.
-
3:02 - 3:03Anatokea Burundi.
-
3:04 - 3:06Alitaka kujua ni wapi angeweza kumaliza masomo yake.
-
3:06 - 3:09Amesoma madarasa 11, na alitaka malizia mwaka wa 12.
-
3:09 - 3:14Aliniambia, "Ninaomba kwa Mungu siku zangu zisiiishie hapa
-
3:14 - 3:15katika kambi hii ya wakimbizi."
-
3:16 - 3:18Na bado ni mapema kwa Halud.
-
3:19 - 3:22Wazazi wake walikuwa ni wakimbizi wa Kipalestina
-
3:22 - 3:25wanaoishi katika kambi ya Yarmouk nje ya mji mkuu wa Damascus.
-
3:25 - 3:27Alizaliwa wazazi wakimbizi,
-
3:27 - 3:30na sasa ni mkimbizi akiwa peke yake nchini Lebanon.
-
3:31 - 3:34Anafanya kazi katika kamati ya kimataifa ya kusaidia wakimbizi wengine,
-
3:35 - 3:38lakini hana uhakika wowote
-
3:38 - 3:40kuhusu maisha yake ya baadaye,
-
3:40 - 3:42yapo wapi na yana ahadi gani.
-
3:42 - 3:46Hotuba hii ni kuhusu Frederick, na kuhusu Halud
-
3:46 - 3:48na kuhusu mamilioni ya wengine;
-
3:48 - 3:50na walikuwa wameondolewa,
-
3:50 - 3:55wanaishi vipi, msaada gani wanahitaji na majukumu yetu ni yapi.
-
3:56 - 3:57Ninaamini katika hili,
-
3:58 - 4:01kwamba swali kubwa katika karne ya 21
-
4:02 - 4:05linahusu majukumu yetu kwa watu tusiowafahamu.
-
4:05 - 4:09Kesho yako inahusu majukumu yako
-
4:09 - 4:10kwa usiowafahamu.
-
4:10 - 4:12Unajua vyema kuliko mwingine yoyote,
-
4:12 - 4:16dunia imeunganishwa kirahisi sana kuliko miaka ya nyuma,
-
4:17 - 4:18lakini hatari kubwa
-
4:18 - 4:21ni kwamba tunatumia muda mwingi katika utengano wetu.
-
4:22 - 4:24Na hakuna jaribio bora kwa hilo
-
4:24 - 4:26kuliko jinsi tunavyowajali wakimbizi.
-
4:27 - 4:30Huu ni ukweli: watu milioni 65
-
4:30 - 4:33waliondolewa kutoka majumbani mwao kwa machafuko mwaka uliopita.
-
4:33 - 4:35Kama ingekuwa ni nchi,
-
4:35 - 4:38ingekuwa ni nchi kubwa kuliko zote duniani katika karne ya 21.
-
4:39 - 4:44Wengi ya hawa watu, takribani milioni 40, wanaishi katika nchi zao,
-
4:44 - 4:45lakini milioni 25 ni wakimbizi.
-
4:45 - 4:48Hii inamaanisha wanavuka mpaka kwenda nchi jirani.
-
4:49 - 4:53Wengi wao wanaishi katika nchi masikini,
-
4:53 - 4:56nchi za umasikini wa ulinganifu au zilizo na kipato cha chini cha kati, kama Lebanon,
-
4:56 - 4:57ambapo Halud anaishi.
-
4:59 - 5:03Nchini Lebanon, mtu mmoja kati ya wanne ni mkimbizi,
-
5:04 - 5:07robo ya watu wote.
-
5:07 - 5:09Na wakimbizi hukaa kwa muda mrefu.
-
5:09 - 5:11Muda wa wastani wa kukimbia
-
5:11 - 5:12ni miaka kumi.
-
5:13 - 5:18Nilikwenda katika kambi kubwa ya wakimbizi duniani, mashariki ya Kenya.
-
5:18 - 5:19Inafahamika kama Dadaab.
-
5:19 - 5:21Ilijengwa kati mwaka 1991 hadi 92
-
5:21 - 5:25kama kambi ya muda kwa Wasomali waliokimbia kutokana na vita ya kisiasa.
-
5:26 - 5:27Nilikutana na Silo.
-
5:28 - 5:31Na nikajisemea kwa Silo,
-
5:31 - 5:33"Unadhani utaweza kurudi nyumbani Somalia?"
-
5:34 - 5:36Na alisema, "Unamaanisha nini, kurudi nyumbani?
-
5:36 - 5:38Nimezaliwa hapa."
-
5:39 - 5:41Na kisha nilipouliza utawala wa kambi ile
-
5:41 - 5:45ni wangapi kati ya watu 330,000 walizaliwa palepale kambini,
-
5:45 - 5:46Walinipa jibu;
-
5:47 - 5:49100,000
-
5:50 - 5:52Hii ndiyo maana ya ukimbizi wa muda mrefu.
-
5:53 - 5:56Sasa, chanzo cha haya matatizo kina kina kirefu;
-
5:56 - 5:58mataifa dhaifu ambayo hayawezi kujali watu wao,
-
5:59 - 6:01mfumo wa kimataifa wa siasa
-
6:01 - 6:04dhaifu kuliko muda wowote kuanzia 1945
-
6:04 - 6:08na tofauti za imani za kidini, utawala, mahusiano na dunia ya nje
-
6:08 - 6:11katika sehemu muhimu ya dunia ya Kiislamu
-
6:13 - 6:16Sasa, hizi ni changamoto za vizazi ambazo ni za muda mrefu.
-
6:16 - 6:19Ndiyo maana ninasema hili janga la wakimbizi ni jambo ambalo ni muendelezo na sio la kushtukiza.
-
6:20 - 6:25Ni tata, na pale unapokuwa na matatizo ambayo ni makubwa, ya muda mrefu,
-
6:25 - 6:27watu hufikiri hamna jambo linaloweza fanyika.
-
6:28 - 6:30Wakati Papa Francis alipokwenda Lampedusa,
-
6:31 - 6:33katika pwani za Italia, mwaka 2014,
-
6:33 - 6:36alitushutumu sisi sote na dunia nzima
-
6:36 - 6:40ambapo aliita ni dunia ya "utandawazi wa wasiojali."
-
6:41 - 6:42Ni msemo ambao upo nasi mara zote.
-
6:42 - 6:45Ina maana kwamba mioyo yetu imegeuka kuwa ya mawe.
-
6:47 - 6:48Sasa, sifahamu, uniambie.
-
6:48 - 6:52Unatakiwa kulumbana na Papa, hata katika mkutano wa TED?
-
6:53 - 6:54Lakini nafikiri si sahihi.
-
6:54 - 6:56Nadhani watu wanataka kufanya mabadiliko,
-
6:56 - 7:00lakini hawajui kama kuna utatuzi wowote wa hili janga.
-
7:00 - 7:02Na ninachotaka kuwaambia leo
-
7:02 - 7:05Ni kwamba ingawa matatizo ni makubwa, na ufumbuzi wake ni mkubwa pia
-
7:06 - 7:07Ufumbuzi wa kwanza:
-
7:07 - 7:11wakimbizi hawa wanatakiwa wajishughulishe katika nchi wanazoishi.
-
7:11 - 7:14na nchi ambazo wanaishi zinatakiwa kupewa msaada mkubwa wa kiuchumi.
-
7:14 - 7:16Mwaka 2014 nchini Uganda, walifanya utafiti:
-
7:17 - 7:20Asilimia 80 ya wakimbizi katika mji mkuu wa Kampala
-
7:20 - 7:22hawakuhitaji msaada wa kibinadamu kwa sababu walikuwa wakifanya kazi.
-
7:22 - 7:24Walikuwa wakisaidiwa katika kazi.
-
7:24 - 7:26Ufumbuzi namba mbili:
-
7:26 - 7:30elimu kwa watoto ni msingi wa maisha, sio starehe,
-
7:30 - 7:32Unapokuwa umekimbia kwa muda mrefu.
-
7:33 - 7:38Watoto wanaweza shindwa pale wanapopewa msaada sahihi wa kijamii na kihisia
-
7:38 - 7:39pamoja na maarifa
-
7:39 - 7:41Nimejionea mwenyewe.
-
7:43 - 7:46Lakini nusu wa wakimbizi watoto duniani walio katika umri wa elimu ya msingi
-
7:46 - 7:48hawapati elimu kabisa,
-
7:48 - 7:51na robo tatu ya umri wa shule ya sekondari hawapati elimu kabisa.
-
7:51 - 7:53Inachanganya akili sana!
-
7:54 - 7:56Ufumbuzi namba tatu:
-
7:56 - 8:00wakimbizi wengi wapo katika maeneo ya mijini, katika majiji, na sio katika makambi.
-
8:00 - 8:02Ni kipi utachotaka au nitachotaka kama tungekuwa wakimbizi katika jiji?
-
8:02 - 8:05Tungehitaji fedha kwa ajili ya kulipa kodi na kununua nguo.
-
8:07 - 8:09Hiyo ni kesho ya mfumo wa kibinadamu,
-
8:09 - 8:10au nyanja muhimu:
-
8:10 - 8:13wape watu fedha ili uongeze nguvu ya wakimbizi
-
8:13 - 8:15na utasaidia uchumi wa eneo husika.
-
8:15 - 8:17Na kuna ufumbuzi wa nne, pia,
-
8:17 - 8:20unatatiza lakini unatakiwa kuongelewa.
-
8:20 - 8:23Wale wakimbizi ambao wapo katika mazingira hatarishi wanatakiwa kupewa mwanzo mpya
-
8:23 - 8:25na maisha mapya katika nchi mpya,
-
8:26 - 8:27ukijumuisha na nchi za Magharibi.
-
8:28 - 8:32Takwimu ni ndogo sana ukilinganisha, mamia ya maelfu, na sio mamilioni,
-
8:32 - 8:35lakini ubaguzi ni mkubwa.
-
8:36 - 8:39Sasa sio muda wa kukataa wakimbizi,
-
8:39 - 8:40kama vile utawala wa Trump unavyohimiza.
-
8:40 - 8:44Ni muda wa kuwapa msaada wale ambao ni wahanga wa machafuko.
-
8:44 - 8:45Na kumbuka --
-
8:45 - 8:48(Makofi)
-
8:52 - 8:56Kumbuka, kila anayekuuliza, "Wamechunguzwa vyema?"
-
8:56 - 8:59hilo ni swali muhimu mno kuuliza.
-
9:00 - 9:04Ukweli ni kwamba, wakimbizi wanaowasili kutokana na machafuko
-
9:04 - 9:08huchunguzwa kuliko wakimbizi wengine wote wanaoingia katika nchi.
-
9:08 - 9:10Kwa hiyo pale ambapo ina maana kuuliza swali,
-
9:10 - 9:14si sahihi kusema kwamba mkimbizi ni neno lingine linalomaanisha gaidi.
-
9:15 - 9:16Sasa, kipi kinatokea --
-
9:16 - 9:20(Makofi)
-
9:20 - 9:23Kipi kinatokea kama wakimbizi hawawezi kupata kazi,
-
9:23 - 9:25hawawezi peleka watoto wao shuleni,
-
9:25 - 9:28hawawezi kupata fedha, hawawezi kupata njia halali ya matumaini?
-
9:28 - 9:30Kinachotokea ni kwamba wanaamua kufanya njia hatarishi.
-
9:30 - 9:35Nilikwenda Lesbos, kisiwa kizuri kilichopo Ugiriki, miaka miwili iliyopita.
-
9:35 - 9:37Kina wakazi 90,000.
-
9:37 - 9:41Katika mwaka mmoja, wakimbizi 500,000 walikwenda katika kisiwa hiki.
-
9:41 - 9:43Na ninataka kuwaonyesha nilichoshuhudia
-
9:43 - 9:46Nilipokuwa nikiendesha kuelekea kaskazini ya kisiwa:
-
9:46 - 9:50mrundikano wa makoti ya kuokoa maisha ya wale waliofankiwa kufika katika kile kisiwa.
-
9:51 - 9:52Na nilipoangalia kwa ukaribu,
-
9:52 - 9:55kulikuwa na makoti madogo ya kuokoa maisha ya watoto,
-
9:55 - 9:56ya rangi ya njano.
-
9:56 - 9:58Na nikachukua picha hii.
-
9:58 - 10:02Huwezi kuona maandishi, lakini nataka nikusomee.
-
10:02 - 10:05"Ilani: haitakukinga na dhidi za kuzama."
-
10:06 - 10:07Katika katika karne ya 21,
-
10:08 - 10:11watoto wanapewa makoti ya kuokoa maisha
-
10:11 - 10:13ili kufika salama Ulaya
-
10:13 - 10:16hata kama yale makoti hayawezi kuokoa maisha yao
-
10:16 - 10:19kama wataanguka kutoka katika mtumbwi ambao unawavusha.
-
10:21 - 10:24Hili sio janga, ni jaribio.
-
10:26 - 10:29Ni jaribio kwamba ustaarabu unaangalia chini.
-
10:30 - 10:31Ni jaribio la ubinadamu wetu.
-
10:32 - 10:34Ni jaribio la sisi tuliopo dunia ya Magharibi
-
10:34 - 10:37ya jinsi tulivyo na msimamo wetu.
-
10:39 - 10:42Ni jaribio la tabia zetu, sio sera zetu.
-
10:43 - 10:45Na wakimbizi ni kesi ngumu.
-
10:45 - 10:47Wanatokea mbali katika pande za dunia.
-
10:48 - 10:50Wamepitia magumu.
-
10:50 - 10:52Wengi wao ni wa dini tofauti.
-
10:52 - 10:55Hizi ni sababu sahihi ambazo zinatupasa kuwasaidia wakimbizi,
-
10:55 - 10:57na sio sababu za kutowasaidia.
-
10:57 - 11:01Na ni sababu ya kuwasaidia kwa sababu ya vile inavyosema kuhusu sisi.
-
11:02 - 11:04Inaonyesha thamani yetu.
-
11:05 - 11:10Uelewa na kujali ni misingi miwili ya ustaarabu.
-
11:11 - 11:14Badili uelewa na kujali katika vitendo
-
11:14 - 11:16na tutaishi katika mila ya kistaarabu.
-
11:17 - 11:19Na katika dunia ya sasa, hatuwezi toa sababu.
-
11:19 - 11:23Hatuwezi sema hatufahamu kinachotokea Juba, Sudani Kusini
-
11:23 - 11:25au Aleppo, Syria.
-
11:25 - 11:28Kipo hapa, katika simujanja zetu
-
11:28 - 11:29zilizopo mikononi mwetu.
-
11:29 - 11:32Ukosefu wa maarifa sio sababu kabisa.
-
11:32 - 11:36Kushindwa kusaidia, tutaonyesha hatuna dira ya ustaarabu kabisa.
-
11:37 - 11:40Na pia inaonyesha kuhusu pengine kama tunatambua historia yetu.
-
11:41 - 11:43Sababu ya kwamba wakimbizi wana haki duniani kote.
-
11:43 - 11:46ni kwa sababu ya uongozi usio wa kawaida ya Magharibi
-
11:46 - 11:49wa viongozi wake kwa waume baada ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia
-
11:49 - 11:51ikaja kuwa haki ya wote.
-
11:52 - 11:55Ukitupa jalalani ulinzi wa wakimbizi, unatupa historia yetu pia.
-
11:56 - 11:58Hii ni --
-
11:58 - 11:59(Makofi)
-
11:59 - 12:03Hii inadhihirisha nguvu ya demokrasia
-
12:03 - 12:06kama kimbilio kutokana na udikteta.
-
12:06 - 12:08Ni wanasiasa wangapi umewahi kuwasikia wakisema,
-
12:09 - 12:13"Tunaamini katika nguvu ya mifano yetu, na sio mifano ya nguvu yetu."
-
12:14 - 12:17Wanachomaanisha ndicho tunachoamini ni muhimu sana kuliko mabomu tunayodondosha.
-
12:18 - 12:20Wakimbizi wanaotafuta utakatifu
-
12:21 - 12:25wameona Magharibi ndiyo chanzo cha matumaini na bandari salama.
-
12:27 - 12:29Warusi, Wairan,
-
12:29 - 12:32Wachina, Waeritrea, Wakyuba,
-
12:32 - 12:34wamekuja magharibi kwa ajili ya usalama.
-
12:35 - 12:37Hatujali ili kuepuka maafa.
-
12:38 - 12:40Na kuna kitu kimoja kingine kinachodhihirisha kuhusu sisi:
-
12:40 - 12:43kama tuna unyenyekevu wowote kutokana na makosa yetu.
-
12:43 - 12:45Mimi sio mmoja ya watu hawa
-
12:45 - 12:49ambae naamini kwamba matatizo yote ya dunia yanasababishwa na nchi za Magharibi.
-
12:49 - 12:50Hapana.
-
12:50 - 12:52Lakini tunapofanya makosa, lazima tuyatambue.
-
12:53 - 12:55Sio ajali kwamba nchi ambayo imechukua
-
12:55 - 12:58wakimbizi wengi zaidi kuliko nchi nyingine, Marekani,
-
12:58 - 13:01imechukua wakimbizi wengi zaidi kutoka Vietnam kuliko nchi yoyote ile.
-
13:02 - 13:03Inaongea katika historia.
-
13:04 - 13:07Lakini kuna historia ya hivi karibuni, nchini Iraq na Afghanistan.
-
13:08 - 13:11Huwezi rekebisha makosa ya siasa za nje
-
13:11 - 13:13kwa kutumia hatua za kibinadamu,
-
13:13 - 13:17lakini unapovunja kitu fulani, una jukumu la kusaidia katika kujaribu kukiunga tena,
-
13:17 - 13:19na ni jukumu letu sasa.
-
13:22 - 13:24Unakumbuka mwanzo wa hii hotuba yangu,
-
13:24 - 13:26Nilisema nataka kueleza kwamba janga la wakimbizi
-
13:26 - 13:28linaweza kusimamiwa, na sio lisiloshindikana?
-
13:29 - 13:32Ni ukweli, Nataka muwaze katika namna mpya,
-
13:32 - 13:34lakini pia nataka mfanye vitu.
-
13:36 - 13:38Kama wewe ni mwajiri,
-
13:38 - 13:39ajiri mkimbizi.
-
13:40 - 13:43Kama unapitishwa katika malumbano,
-
13:43 - 13:45waza mambo ya nyuma
-
13:45 - 13:47pale familia au marafiki au wafanyakazi wenzio wanaporudia.
-
13:48 - 13:51Kama una hela, toa kama msaada
-
13:51 - 13:53inaleta utofauti kwa wakimbizi wote duniani.
-
13:54 - 13:55Kama wewe ni mwananchi,
-
13:56 - 13:58mpigie kura mwanasiasa
-
13:58 - 14:02ambaye atafanyia kazi utatuzi wa haya niliyoongelea.
-
14:02 - 14:06(Makofi)
-
14:06 - 14:08Jukumu la asiyejulikana
-
14:08 - 14:10hujionyesha
-
14:10 - 14:13katika njia ndogo na kubwa,
-
14:13 - 14:15kawaida na kishujaa.
-
14:16 - 14:17Mwaka 1942,
-
14:19 - 14:21shangazi yangu na bibi yangu walikuwa wakiishi Brussels
-
14:21 - 14:22chini ya utawala wa Ujerumani.
-
14:24 - 14:26Walipokea wito
-
14:26 - 14:30kutoka katika mamlaka ya Nazi, kwenda katika stesheni ya reli ya Brussels.
-
14:32 - 14:35Bibi yangu mara moja alitambua kwamba kuna kitu hakipo.
-
14:37 - 14:39Aliwasihi ndugu zake
-
14:39 - 14:41wasiende stesheni ya reli ya Brussels.
-
14:42 - 14:44Ndugu zake walimwambia,
-
14:45 - 14:48"Kama hatutakwenda, kama hatutafanya tulichoambiwa,
-
14:48 - 14:50tutakuwa katika hatari kubwa."
-
14:51 - 14:53Unaweza tabiri nini kilitokea
-
14:53 - 14:55kwa wale ndugu waliokwenda stesheni ya reli ya Brussels.
-
14:56 - 14:57Hawakuonekana tena.
-
14:58 - 15:00Lakini bibi yangu na shangazi yangu,
-
15:01 - 15:03walikwenda katika kijiji kidogo
-
15:03 - 15:05kusini mwa Brussels
-
15:06 - 15:09ambapo walishawahi kwenda likizo muongo mmoja uliopita,
-
15:09 - 15:13na walifikia katika nyumba ya mwanakijiji ambaye ni mkulima,
-
15:13 - 15:15wa Kikatoliki aliyeitwa Monsieur Maurice,
-
15:16 - 15:18na waliomba kuishi pale.
-
15:19 - 15:21na aliwakubalia,
-
15:21 - 15:22na baada ya vita kuisha,
-
15:23 - 15:27Wayahudi 17, niliambiwa, walikuwa wakiishi katika kijiji kile.
-
15:28 - 15:30Na nilipokuwa kijana, nilimuuliza shangazi yangu,
-
15:30 - 15:32"Unaweza nipeleka nikamuone Monsieur Maurice?"
-
15:33 - 15:37Na alisema, "Ndiyo, ninaweza. Bado yupo hai. Twende ukamuone."
-
15:37 - 15:38Hivyo, ilikuwa ni mwaka '83,'84
-
15:39 - 15:41tulikwenda kumuona.
-
15:41 - 15:44Na tuseme, kama kijana tu ningeweza,
-
15:44 - 15:45pale nilipoonana nae,
-
15:45 - 15:48alikuwa ni mwanaume mstaarabu aliye na mvi,
-
15:48 - 15:50Nikamwambia,
-
15:51 - 15:52"Kwanini ulifanya vile?
-
15:53 - 15:56Kwanini ulikubali kuingia katika hatari?"
-
15:57 - 15:59Aliniangalia
-
15:59 - 16:01na akasema, katika lugha ya Kifaransa,
-
16:01 - 16:03"On doit."
-
16:03 - 16:04ikimaanisha "Yatupasa."
-
16:04 - 16:07Ilikuwa ndani yake.
-
16:07 - 16:08Ni asili.
-
16:08 - 16:13Na hoja yangu kwenu inatakiwa halisi na asili ndani yetu, pia.
-
16:13 - 16:14Iambie nafsi yako,
-
16:15 - 16:18hili janga la wakimbizi linaweza simamiwa,
-
16:18 - 16:19lina ufumbuzi,
-
16:19 - 16:21na kila mmoja wetu
-
16:21 - 16:25ana jukumu binafsi la kuhakikisha jambo hili linafanikiwa.
-
16:25 - 16:29Kwa sababu hili jambo ni kuhusu wokozi wetu na thamani yetu
-
16:29 - 16:32vile vile na wokozi wa wakimbizi na maisha yao.
-
16:32 - 16:34Asante sana.
-
16:34 - 16:37(Makofi)
-
16:45 - 16:48Bruno Giussani: David, asante. David Miliband: Asante.
-
16:48 - 16:50BG: Haya ni mapendekezo yenye nguvu
-
16:50 - 16:53na wito wako kwa kila mmoja ni wenye nguvu pia,
-
16:53 - 16:55lakini ninatatizwa na wazo moja, ni hili hapa:
-
16:55 - 16:59umetaja, na haya ni maneno yako,"utawala usio wa kawaida wa Magharibi"
-
16:59 - 17:01ambao umeongoza kwa miaka 60 hivi iliyopita
-
17:01 - 17:03kuhusu majadiliano mazima kuhusu haki za binadamu,
-
17:03 - 17:06hadi kwenye makongamano kuhusu wakimbizi, kadhalika na kadhalika.
-
17:07 - 17:10Uongozi huu ulitokea baada ya mkanganyiko mkubwa
-
17:10 - 17:14na ulitokea katika nafasi ya makubaliano ya kisiasa,
-
17:14 - 17:16na sasa tupo mgawanyiko wa kisiasa.
-
17:16 - 17:19Kiuhalisia, wakimbizi wamekuwa moja ya jambo la mgawanyiko.
-
17:19 - 17:21Kwa hiyo ni wapi uongozi utatokea leo hii?
-
17:21 - 17:24DM: Ninadhani upo sahihi kusema
-
17:24 - 17:26uongozi uliozua vita
-
17:27 - 17:29una hasira tofauti na mwendo tofauti
-
17:29 - 17:30na muonekano tofauti pia
-
17:30 - 17:33kuliko uongozi uliozua amani.
-
17:34 - 17:37Na kwa hiyo jibu langu litakuwa kwamba uongozi unatakiwa kutokea chini,
-
17:37 - 17:39na sio juu.
-
17:39 - 17:42Ninamaanisha, maudhui yanayojirudia ya mkutano wiki hii
-
17:42 - 17:46yamekuwa kuhusu kuleta demokrasia katika nguvu.
-
17:46 - 17:48Na tunatakiwa kulinda demokrasia yetu,
-
17:48 - 17:51lakini pia tunatakiwa amsha demokrasia yetu wenyewe.
-
17:51 - 17:53Na pale watu wanaponiambia,
-
17:53 - 17:54"Kuna upinzani katika suala la wakimbizi,"
-
17:54 - 17:56ninachowaambia ni hiki,
-
17:56 - 17:58"Hapana, kuna matabaka,
-
17:58 - 17:59na kwa wakati huu,
-
17:59 - 18:01wale ambao wanaogofya wanapiga kelele zaidi
-
18:01 - 18:03kuliko wale ambao wenye fahari."
-
18:03 - 18:07Kwa hiyo jibu langu kuhusu swali lako ni kwamba tutadhamini na kuhamasisha
-
18:07 - 18:08na kutoa ujasiri katika uongozi
-
18:08 - 18:10pale tunapoungana.
-
18:10 - 18:14Na ninadhani pale pale ambapo unakuwa katika nafasi ya kutafuta uongozi,
-
18:14 - 18:15unatakiwa kuangalia ndani
-
18:15 - 18:17na kuunganisha jamii yako
-
18:17 - 18:20kujaribu kutengeneza mazingira ya tofauti kwa makazi.
-
18:20 - 18:22BG: Asante, David. Asante kwa kuja TED.
-
18:22 - 18:26(Makofi)
- Title:
- Mgogoro wa wakimbizi ni kipimo cha utu wetu
- Speaker:
- David Miliband
- Description:
-
more » « less
Watu millioni sitini na tano walitolewa katika makazi yao na migogoro na majanga katika mwaka 2016. Huu sio tu ni mgogoro; lakini pia ni kipimo cha kuwa sisi ni nani na tunasimamia nini, anasema David Miliband - kila moja wetu ana jukumu binafsi kutatua hali hii. Katika mazungumzo haya yenye umuhimu wa kipekee kuyaangalia , Miliband anatupa njia za dhahiri za kuwasaidia wakimbizi na kugeuza huruma na kuwawazia wengine kuwa vitendo.
- Video Language:
- English
- Team:
closed TED
- Project:
- TEDTalks
- Duration:
- 18:38
| Joachim Mangilima edited Swahili subtitles for The refugee crisis is a test of our character | ||
| Joachim Mangilima approved Swahili subtitles for The refugee crisis is a test of our character | ||
| Joachim Mangilima edited Swahili subtitles for The refugee crisis is a test of our character | ||
| Joachim Mangilima accepted Swahili subtitles for The refugee crisis is a test of our character | ||
| Joachim Mangilima edited Swahili subtitles for The refugee crisis is a test of our character | ||
|
Nelson Simfukwe edited Swahili subtitles for The refugee crisis is a test of our character | |
|
Nelson Simfukwe edited Swahili subtitles for The refugee crisis is a test of our character | |
|
Nelson Simfukwe edited Swahili subtitles for The refugee crisis is a test of our character |
