Return to Video

Namna gani gari za umeme zinatakiwa kutoa sauti?

  • 0:01 - 0:03
    Tuanze na ukimya.
  • 0:11 - 0:16
    Ukimya ni hali yenye thamani kwa wanadamu,
  • 0:16 - 0:19
    kwa sababu inatufanya kuhisi
    kina cha uwepo wetu.
  • 0:20 - 0:23
    Hii ni moja ya sababu kwanini
    ujio wa gari za umeme
  • 0:23 - 0:26
    umetengeneza hamasa kubwa kwa watu.
  • 0:27 - 0:31
    Kwa mara ya kwanza, tuliweza
    husisha muundo wa gari
  • 0:31 - 0:33
    na mazoea ya ukimya.
  • 0:34 - 0:36
    Magari hatimaye yanaweza kuwa kimya:
  • 0:37 - 0:38
    amani katika mitaa,
  • 0:38 - 0:41
    mapinduzi ya ukimya katika majiji.
  • 0:45 - 0:51
    (Hum)
  • 0:54 - 0:56
    Lakini unaweza pia kuwa tatizo.
  • 0:57 - 1:01
    Ukosefu wa sauti, kwa hakika,
    unapokuja katika gari,
  • 1:01 - 1:02
    inaweza kuwa hatari sana.
  • 1:03 - 1:05
    Fikiria watu wasiiona,
  • 1:05 - 1:07
    wasioweza kuona gari linalowasogelea.
  • 1:09 - 1:11
    Na sasa, kama ni la umeme,
    hawawezi kabisa kulisikia.
  • 1:12 - 1:15
    Au fikiria kuhusu kila mmoja
    wetu tunapotembea katika jiji,
  • 1:15 - 1:19
    tumezama katika mawazo yetu,
    na tumeachana na mazingira.
  • 1:21 - 1:25
    Katika hali hii, sauti inaweza kuwa
    mshiriki mwenye thamani.
  • 1:27 - 1:31
    Sauti ni moja ya zawadi murua
    katika ulimwengu.
  • 1:31 - 1:32
    Sauti ni hisia
  • 1:33 - 1:35
    na sauti ni utukufu,
  • 1:36 - 1:40
    na inapokuja kwenye gari,
    sauti pia ni taarifa.
  • 1:42 - 1:44
    Ili kuweza kuwalinda watembea kwa miguu
  • 1:44 - 1:47
    na kutoa mrejesho wa sauti kwa madereva,
  • 1:47 - 1:51
    serikali dunia kote wameunda
    namna baadhi za udhibiti
  • 1:51 - 1:55
    ambazo zinawajibisha uwepo wa sauti
    katika magari ya umeme.
  • 1:55 - 1:59
    Katika uhalisia, zinahitaji
    sauti kiasi kidogo
  • 1:59 - 2:01
    katika mrudio wa mawimbu mahususi
  • 2:01 - 2:04
    hadi kilomita 30 kwa saa.
  • 2:06 - 2:07
    Ukiachana na kasi,
  • 2:07 - 2:11
    sauti halisi ya gari huchukiliwa
    kama ya kutosha.
  • 2:13 - 2:17
    Sheria hizi zimetengeneza maoni tofauti
  • 2:17 - 2:21
    kati ya wale ambao wanahitaji sauti
    na wale walio na hofu ya uwepo
  • 2:21 - 2:22
    wa kelele nyingi katika jiji.
  • 2:24 - 2:28
    Hata hivyo, Sioni kwamba
    ni kelele ya gari.
  • 2:30 - 2:33
    Naona kwamba ni sauti ya gari.
  • 2:34 - 2:38
    Na hii ndiyo changamoto yangu kubwa,
    na kipaumbele, kwa wakati mmoja.
  • 2:39 - 2:41
    Ninarasimu sauti ya gari za umeme.
  • 2:44 - 2:47
    Tunaelewa namna gani injini
    za moto zinavyotoa mlio,
  • 2:47 - 2:51
    na pia tunaelewa namna gani gari
    za umeme zinavyotoa mlio.
  • 2:51 - 2:53
    Fikiria kuhusu mkokoteni wa umeme.
  • 2:53 - 2:55
    Pale unapotembea,
  • 2:55 - 2:58
    hutengeneza sauti inayopanda
    ambayo ni kali,
  • 2:59 - 3:00
    ambayo tunaita sauti ya "filimbi".
  • 3:02 - 3:05
    Hata hivyo, kama tutaweza
    kuongeza sauti hii,
  • 3:05 - 3:09
    hatutaweza kufikia kanuni zilizowekwa.
  • 3:09 - 3:12
    Ndiyo maana tunahitaji
    kutengeneza sauti mpya.
  • 3:13 - 3:16
    Sasa tunafanyaje?
  • 3:17 - 3:21
    Katika majiji mengi, msongamano
    wa magari una vurugu sana,
  • 3:21 - 3:22
    na hatuhitaji vurugu nyingine.
  • 3:23 - 3:28
    Lakini mitaa ya karne ya 21
    hutupa somo zuri sana
  • 3:28 - 3:32
    zikitiririka kutangatanga, na mvurugiko.
  • 3:33 - 3:37
    Na uwanda huu unatoa nafasi nzuri
  • 3:37 - 3:41
    ya kutengeneza fumbuzi mpya za
    namna ya kuondoa hizi vurugu.
  • 3:43 - 3:47
    Nimeunda namna mpya ya kujaribu
    kupunguza huu mvurugano
  • 3:47 - 3:49
    kwa kuleta mlingano.
  • 3:51 - 3:55
    Vile kwamba watu wengi hawafahamu namna
    ambavyo gari la umeme linatoa sauti,
  • 3:55 - 3:59
    Natakiwa kufafanua, kwanza ya yote,
    dunia mpya ya sauti,
  • 3:59 - 4:03
    jambo ambalo halipo katika mazoea ya nyuma
  • 4:03 - 4:06
    lakini linatengeneza kumbukumbu ya kesho.
  • 4:07 - 4:11
    Pamoja na timu ndogo, tunatengeneza
    sauti za kusikika na wanadamu
  • 4:11 - 4:15
    ambazo zinaweza safirisha hisia.
  • 4:16 - 4:18
    Kama vile mchoraji na rangi,
  • 4:18 - 4:23
    tunaweza kuunganisha hisia
    na mrudio wa mawimbi
  • 4:23 - 4:25
    ili kwamba pale mtu anaposogelea gari,
  • 4:25 - 4:27
    tunaweza kujisikia hisia
  • 4:27 - 4:31
    ambazo, ukiachalia kwamba zinafuata
    matakwa ya serikali,
  • 4:31 - 4:35
    pia huongea kuhusu tabia na
    utambulisho wa gari.
  • 4:38 - 4:41
    Naita namna hii "jenetikia ya sauti."
  • 4:42 - 4:48
    Na jenetikia ya sauti, naelezea, kwanza
    kuliko yote, nafasi ya sauti,
  • 4:48 - 4:52
    na wakati huo huo, natafuta njia
    mpya za ufumbuzi
  • 4:52 - 4:55
    za kutengeneza mazingira ya sauti
    ambayo hatufahamu,
  • 4:57 - 5:01
    mazingira ya sauti yanayoturuhusu
    kuwaza dunia ya kufikirika,
  • 5:02 - 5:04
    kuipa uhalisia na yenye kusikika.
  • 5:06 - 5:09
    Jenetikia ya sauti inahusiana
    na hatua tatu.
  • 5:10 - 5:14
    Ya kwanza ni kuelezea kiumbe anayesikia,
  • 5:15 - 5:19
    cha pili ni kudadafua mabadiliko ya sauti,
  • 5:20 - 5:24
    na ya tatu ni utengenezaji
    wa jeni za sauti.
  • 5:27 - 5:32
    Maelezo ya kiumbe anayesikia yanatokana
    na muunganiko wa tabia
  • 5:32 - 5:36
    za kila sauti ninayotengeneza
    inakua nayo.
  • 5:39 - 5:40
    [Sauti inasafiri]
  • 5:40 - 5:46
    Nasafirisha katika sauti ndogo,
    kama vile sauti ya gari,
  • 5:46 - 5:49
    nguvu ya mrindimo wa muziki,
  • 5:49 - 5:51
    ili sauti inaweza safiri.
  • 5:52 - 5:54
    [Sauti inatenda.]
  • 5:54 - 5:56
    Na kama kwa mchezaji katika jukwaa,
  • 5:56 - 6:00
    sauti itatengeneza njia katika hewa.
  • 6:02 - 6:03
    [Sauti ni kumbukumbu.]
  • 6:03 - 6:06
    Na siyo tu kuhusu sauti ya gari.
  • 6:06 - 6:09
    Ni kumbukumbu ya baba yangu
    akirudi nyumbani.
  • 6:12 - 6:13
    [Sauti inavutia.]
  • 6:13 - 6:19
    Na sauti ina nguvu ya kutengeneza
    maajabu yasiyotegemewa,
  • 6:19 - 6:20
    ambayo huvutia.
  • 6:22 - 6:23
    Na kwa ujumla,
  • 6:23 - 6:25
    [sauti ni binadamu wa ajabu.]
  • 6:25 - 6:27
    sauti huenda zaidi ya hali ya kibinadamu,
  • 6:27 - 6:29
    kwa sababu inaturuhusu sisi kujongea.
  • 6:33 - 6:37
    Katika hatua ya pili, tunaeleza
    mabadiliko ya sauti.
  • 6:37 - 6:38
    [Prizmu ya utambuzi]
  • 6:38 - 6:43
    Kama vile wanadamu, ambapo miili
    hutengeneza sauti mbalimbali,
  • 6:43 - 6:48
    na pia maumbo mbalimbali ya gari yana
    tabia mbalimbali za sauti
  • 6:48 - 6:51
    ambazo hutegemea maombi na malighafi.
  • 6:52 - 6:58
    Hivyo tunapaswa kujua, kwanza kabisa,
    jinsi gari hili husafirisha sauti nje
  • 6:58 - 7:00
    namna ya vipimo vya sauti.
  • 7:02 - 7:07
    Na kama vile sauti moja inaweza kutoa
    mirindimo ya sauti mbalimbali,
  • 7:07 - 7:11
    na kwa wakati huohuo, tunatengeneza
    utofauti mbalimbali wa sauti
  • 7:11 - 7:15
    katika nafasi ya maneno
    nane ambayo naelezea.
  • 7:16 - 7:19
    Na baadhi yao, kwangu, ni muhimu sana,
  • 7:19 - 7:21
    kama vile suala la "maono,"
  • 7:21 - 7:25
    ya "utashi," ya "mabadiliko,"
    ya "kufumbata."
  • 7:28 - 7:31
    Na pale tutapoweza kuelezea
    hizi namna mbili,
  • 7:31 - 7:34
    tunakuwa tumepata ninaoita
    mche wa utambuzi,
  • 7:34 - 7:38
    ambao ni kama kadi ya
    utambuzi wa sauti ya gari.
  • 7:41 - 7:46
    Na katika hatua ya tatu, tunaingia katika
    dunia ya utengenezaji wa sauti,
  • 7:47 - 7:50
    ambapo jeni za sauti zinatengenezwa
  • 7:50 - 7:52
    na muundo mpya unatengenezwa.
  • 7:54 - 7:56
    Sasa ngoja nikuonyeshe mfano mwingine
  • 7:56 - 8:00
    wa namna ya kubadili sauti kuwa mlio
  • 8:02 - 8:04
    Fikiria kua mimi ni mpiga
    fidla jukwaani.
  • 8:05 - 8:06
    Kama nitaanza kupiga fidla,
  • 8:06 - 8:10
    Nitatengeneza sauti ambayo
    itatembea katika ukumbi huu,
  • 8:10 - 8:14
    na kwa wakati huo huo, sauti itagonga kuta
  • 8:14 - 8:18
    na itasambaa hapa kote.
  • 8:18 - 8:19
    Na ndivyo itavyoonekana.
  • 8:19 - 8:25
    Muda fulani uliopita, nilinasa namna
    baadhi ya sauti inavyogonga kuta.
  • 8:26 - 8:30
    Na mwaka jana, niliombwa na bendi
    ya Bavarian Radio Symphony
  • 8:30 - 8:34
    kutengeneza milio ambayo wangeipiga.
  • 8:35 - 8:39
    Katika mmoja wao, niliwaza kuanza
    na mrindimo wa sauti.
  • 8:40 - 8:42
    Nilichukua kipande,
  • 8:42 - 8:44
    Nikakijumuisha katika mgawanyo
  • 8:44 - 8:47
    wa wanamuziki wakiwa jukwaani,
  • 8:47 - 8:50
    na kisha nikifata mrindimo wa sauti
  • 8:50 - 8:51
    kwa namna ya vipimo vitatu:
  • 8:52 - 8:54
    muda, kiasi na mrudio wa mawimbi.
  • 8:55 - 9:00
    Kisha nikaandika ulalo wa kila kifaa,
  • 9:00 - 9:01
    na unaweza kuona, kwa mfano,
  • 9:01 - 9:06
    vipande vitaanza na kipande cha
    uzi kikipiga kwa umororo,
  • 9:06 - 9:12
    na kisha kitaanza ongezeka pale shaba,
    mbao zitapoanza sikika,
  • 9:12 - 9:16
    na mlio utaishia na kinubi na kinanda
  • 9:16 - 9:18
    zikilia katika kiwango cha juu.
  • 9:22 - 9:25
    Tusikilize inalia vipi.
  • 9:27 - 9:34
    (Mziki wa mbinguni)
  • 9:44 - 9:45
    (Muziki unaisha)
  • 9:48 - 9:51
    Kwa hiyo huu ni mlio wa saa yangu
    inayoniamsha, kiukweli, asubuhi.
  • 9:51 - 9:52
    (Kicheko)
  • 9:54 - 9:56
    Na sasa turudi katika gari za umeme.
  • 9:57 - 10:03
    Na kisha tusikilize mfano wa kwanza
    ambao nimewaonyesha.
  • 10:08 - 10:15
    (Hum)
  • 10:17 - 10:22
    Na sasa nitawaonyesha namna
    gani mlio muhimu,
  • 10:22 - 10:26
    ambao unatokana na jini ya sauti kwa ajili
    ya gari za umeme, itasikika hivi.
  • 10:28 - 10:32
    (Muziki wa mbinguni)
  • 10:32 - 10:38
    (Kiwango kinapanda na kuongezeka mwendo)
  • 10:40 - 10:47
    Gari ni mifano inayohusiana
    na muda, umbali na safari,
  • 10:47 - 10:50
    ya kuondoka na kurudi,
  • 10:50 - 10:53
    ya shauku na safari,
  • 10:53 - 10:58
    lakini, kwa wakati huo huo,
    na utashi na utata,
  • 10:58 - 11:01
    ya uelewa wa binadamu na mafanikio.
  • 11:01 - 11:04
    Na sauti imetukuza hayo yote.
  • 11:06 - 11:10
    Naona magari yote kama viumbe vinavyoishi
  • 11:10 - 11:14
    na vifaa vilivyotengenezwa
    na sanaa tata sana.
  • 11:16 - 11:20
    Sauti ambazo tunaziunda
    kupitia sauti za jenetikia
  • 11:20 - 11:23
    sio tu zinaturuhusu kufurahia utata huu
  • 11:25 - 11:29
    bali pia kufanya dunia iwe sehemu
    maridadi na yenye usalama.
  • 11:30 - 11:31
    Asante.
  • 11:31 - 11:34
    (Makofi)
Title:
Namna gani gari za umeme zinatakiwa kutoa sauti?
Speaker:
Renzo Vitale
Description:

Magari ya umeme yapo kimya sana, huleta ukimya mzuri katika majiji yetu. Lakini pia huleta hatari mpya, kutokana na kwamba yanaweza kumgonga kirahisi mtembea kwa miguu. Sauti gani yanatakiwa kutoa ili kufanya watembeaji kuwa salama? Pata maelezo ya namna gani sauti ya kesho itavyokuwa pale mhandisi wa sauti na mwanamuziki Renzo Vitale akionyesha namna anavyotengeneza sauti kwa ajili ya gari za umeme.

more » « less
Video Language:
English
Team:
closed TED
Project:
TEDTalks
Duration:
11:51

Swahili subtitles

Revisions