Kwanini naongelea kuhusu kuishi na kifafa
-
0:00 - 0:03Nina jambo la kushuhudia.
-
0:05 - 0:07Nimekuwa katika mahusiano
-
0:08 - 0:10tangu nikiwa na miaka 17.
-
0:11 - 0:15Natamani ningeongelea kuhusu vipepeo ndani ya tumbo langu
-
0:15 - 0:18au ramani nilizochora ardhini
-
0:18 - 0:20kila ninapowaza kuhusu uhusiano huu,
-
0:20 - 0:21lakini siwezi.
-
0:22 - 0:25Natamani ningeongelea kuhusu maneno matamu yaliyotamkwa
-
0:25 - 0:27au zawadi nilizowahi kupokea
-
0:27 - 0:29kutokana na uhusiano huu,
-
0:29 - 0:31lakini siwezi.
-
0:32 - 0:35Yote ninayoweza kukwambia ni matokeo,
-
0:36 - 0:40ya kuhusu siku nilizotumia nikijiuliza mfululizo;
-
0:40 - 0:43Kwanini, kwanini, kwanini mimi?
-
0:45 - 0:48Nakumbuka yote haya yalipoanzia.
-
0:48 - 0:51Nilikuwa katika mwaka wangu wa mwisho wa shule ya sekondari,
-
0:51 - 0:54na darasa langu lilikuwa limeshinda katika michezo,
-
0:54 - 0:59hivyo tulikuwa tukiimba na kucheza na kukumbatiana.
-
0:59 - 1:01Nilikwenda kuoga.
-
1:01 - 1:02Kisha nikaenda kupata chakula cha jioni.
-
1:03 - 1:05Na nilipokaa ili nipate chakula,
-
1:06 - 1:08meno yangu yakaanza kugongana,
-
1:08 - 1:11na nikashindwa kuweka kijiko katika mdomo wangu.
-
1:11 - 1:13Nilikimbia katika ofisi ya nesi,
-
1:13 - 1:16na kwa sababu nilikuwa siwezi kuongea, nilinyooshea kidole mdomoni mwangu.
-
1:17 - 1:19Hakuelewa ni jambo gani lililokuwa likitokea,
-
1:19 - 1:21aliniambia nilale
-
1:21 - 1:22ilinisaidia --
-
1:22 - 1:25baada ya dakika chache, kugongana kwa meno kuliacha.
-
1:25 - 1:29Nilitaka kuondoka haraka, kisha akaniambia --
-
1:29 - 1:33Hapana, akisisitiza -- kwamba niende bwenini kulala.
-
1:34 - 1:37Wakati huu nilikuwa mwaka wa mwisho wa elimu yangu ya sekondari,
-
1:37 - 1:42miezi michache tu kabla sijaanza mitihani yangu ya mwisho
-
1:42 - 1:47na siku chache kabla ya kufanya mitihani ambayo kwa hapa Kenya tunaiita "mocks"
-
1:47 - 1:53ambayo dhumuni lake ni kumpima mwanafunzi ni kwa namna gani amejiandaa na mtihani wa mwisho.
-
1:53 - 1:55Hakuna namna ningeweza kulala
-
1:55 - 1:57na kuacha mitihani hii inifanyie mzaha.
-
1:57 - 2:00Nilienda darasani, nikaketi,
-
2:00 - 2:03nikachukua notisi zangu za historia ya Kenya,
-
2:03 - 2:07Nikaanza kusoma, kuhusu miji ya pwani za Kenya,
-
2:07 - 2:09kuhusu mfalme Mekatili wa Menza,
-
2:09 - 2:14mwanamke wa Giriama aliyeongoza watu wake kupinga ukoloni wa Waingereza.
-
2:15 - 2:18Baada ya hapo, bila kutambua chochote,
-
2:18 - 2:21mkono wangu wa kushoto ukaanza kutetemeka,
-
2:23 - 2:25na ikawa kama naweka alama katika karatasi la kufikirika.
-
2:26 - 2:28Ndani na nje,
-
2:29 - 2:32na kila mjongeo, mmoja baada ya mwingine,
-
2:32 - 2:36wanadarasa wenzangu wakaacha kujisomea
-
2:36 - 2:38na wakaanza kunishangaa mimi.
-
2:39 - 2:41Na kujaribu kwa bidii zote kuzuia hali hiyo,
-
2:41 - 2:43lakini sikuweza,
-
2:43 - 2:45kwa sababu ulikuwa na aina yake ya maisha.
-
2:46 - 2:51Kisha, ulipokuwa umehakikisha kwamba kila mtu alikuwa akituangalia,
-
2:51 - 2:55Ukaonyesha rasmi,
-
2:55 - 2:58Kuwa na degedege kwa mara ya kwanza,
-
2:58 - 3:03ambapo ilikuwa ni mwanzo wa mahusiano ambayo yana miaka 15 mpaka sasa.
-
3:06 - 3:12Mpapatiko ni moja dalili ya aina nyingi za kifafa,
-
3:12 - 3:17na kila mpapatiko wowote wa mapema hutakiwa kuchunguzwa na daktari
-
3:17 - 3:19kugundua kama mtu ana kifafa
-
3:19 - 3:22au kama ni dalili ya ugonjwa mwingine.
-
3:22 - 3:26Katika tatizo langu, iligundulika kwamba nilikuwa na kifafa.
-
3:26 - 3:31Nilitumia muda mwingi sana hospitali na nyumbani,
-
3:31 - 3:34na shule nilirudi kufanya mtihani wangu wa mwisho tu.
-
3:35 - 3:39Nilikuwa nikipatwa na mpapatiko katika ya mitihani,
-
3:39 - 3:41lakini nilifanikiwa kupata alama nzuri za kutosha
-
3:41 - 3:45kupata nafasi ya kujiunga na shahada ya sayansi ya takwimu za bima
-
3:45 - 3:46katika chuo cha Nairobi.
-
3:46 - 3:50(Makofi)
-
3:53 - 3:57Kwa bahati mbaya, niliacha chuo nikiwa mwaka wa pili.
-
3:57 - 4:00Sikuwa na uwezo wa kutosha wa kuendana na wenzangu
-
4:00 - 4:02na jamii iliyokuwa inanizunguka.
-
4:02 - 4:04Nilibahatika kupata kazi,
-
4:05 - 4:10lakini nilifukuzwa baada ya kupatwa na mpapatiko nikiwa kazini.
-
4:11 - 4:15Nikajikuta katika mahala
-
4:15 - 4:18ambapo nilikuwa najiuliza kila wakati
-
4:18 - 4:21kwanini suala hili limenitokea mimi.
-
4:22 - 4:25Nimeishi katika kukataa ukweli kwa muda mrefu,
-
4:25 - 4:32na kujikataa huku pengine ni kwa sababu ya mambo ambayo yalitokea,
-
4:32 - 4:35kuacha chuo na kufukuzwa kazi.
-
4:36 - 4:40Au kwa sababu ya vitu nilivyosikia kuhusu kifafa
-
4:40 - 4:42na kuhusu watu wanaoishi na kifafa;
-
4:42 - 4:45kwamba hawawezi kuishi wenyewe
-
4:45 - 4:47na hawawezi kusafiri wakiwa peke yao
-
4:47 - 4:48au hata kupata kazi;
-
4:49 - 4:51Kwamba ni watu walio tofauti,
-
4:51 - 4:55walio na roho ambayo wanatakiwa kuokolewa kutoka hiyo roho.
-
4:57 - 5:00Hivyo, nilipokuwa nikizidi kuwaza kuhusu haya mambo,
-
5:00 - 5:04na ndiyo hali yangu ilikuwa ikinitokea,
-
5:04 - 5:07Niliishi miguu yangu ikiwa inafungwa kamba kwa siku kadhaa,
-
5:07 - 5:11sauti yangu ilikuwa ikififia
-
5:11 - 5:14na katika mwisho wa siku, hivi ndivyo ambavyo ningekuwa.
-
5:15 - 5:17Siku mbili au tatu baada ya mpapatiko,
-
5:17 - 5:20kichwa na mikono yangu vilikuwa bado vinatingishika.
-
5:22 - 5:24Nilijihisi kupotea,
-
5:25 - 5:27kama vile ningepoteza kila kitu,
-
5:28 - 5:29na wakati mwingine,
-
5:31 - 5:32hata shauri la kuishi.
-
5:42 - 5:43(Mguno)
-
5:49 - 5:51Nilikuwa na msongo mkubwa wa mawazo.
-
5:52 - 5:54Nikaanza kuandika,
-
5:54 - 5:56kwa sababu watu waliokuwa wananizunguka hawakuwa na majibu
-
5:56 - 5:58ya maswali niliyokuwa nayo.
-
5:59 - 6:02Kisha nikaandika hofu zangu zote
-
6:02 - 6:03na wasiwasi wangu.
-
6:04 - 6:08Niliandika kuhusu siku zangu nzuri na siku zangu mbaya na zile zilizo mbaya zaidi,
-
6:08 - 6:10kisha nikashirikisha katika blogu.
-
6:11 - 6:12Na kabla ya muda kupita,
-
6:13 - 6:17Nilianza kuonekana na kusikika na watu waliokuwa na kifafa
-
6:17 - 6:19na familia zao,
-
6:19 - 6:21na hata wale ambao hawana ugonjwa huu.
-
6:22 - 6:26Na nikaondoka kutoka kwa yule msichana ambae alikuwa akijiuliza ni kwanini mimi kila wakati mimi
-
6:26 - 6:29na nikawa ambae sio tu najishauri mwenyewe
-
6:29 - 6:32lakini hata kwa wale ambao bado hawajatambua sauti zao.
-
6:35 - 6:40(Makofi)
-
6:43 - 6:47Mpapatiko wangu umepungua mno, kutoka mara mbili hadi tatu kwa siku,
-
6:47 - 6:50na wakati mwingine mara mbili hadi tatu ndani ya mwaka.
-
6:50 - 6:52Nikaendelea --
-
6:52 - 6:56(Makofi)
-
6:57 - 7:00Nikafanikiwa kuajiri watu watano,
-
7:00 - 7:02nilipoanzisha inayofahamika kama taasisi ya kwanza Kenya
-
7:02 - 7:05ya bure kuhusu ushauri wa afya ya akili na kifafa.
-
7:06 - 7:07Na nikasafiri --
-
7:07 - 7:10(Makofi)
-
7:10 - 7:14Nikasafiri kuongelea kuhusu uhusiano wangu,
-
7:14 - 7:16vitu hivi vyote ambavyo niliambiwa
-
7:16 - 7:21kwamba watu wenye kifafa kama mimi hawatoweza kamwe.
-
7:21 - 7:27Kila mwaka, watu takribani asilimia 80 sawa na watu waliopo jijini Nairobi
-
7:27 - 7:29hugundulika kuwa na kifafa
-
7:29 - 7:31dunia nzima.
-
7:31 - 7:33Na ni watu kama mimi.
-
7:33 - 7:37ambao wanapitia hisia za unyanyapaa na kutengwa.
-
7:39 - 7:42Nimeifanya kuwa safari ya maisha yangu
-
7:42 - 7:45kufanya maongezi yaendelee,
-
7:45 - 7:48na bado ninakubaliana na uhusiano wangu
-
7:48 - 7:51Ili watu ambao hawana kifafa
-
7:51 - 7:55wanaweza tambua na kukumbuka kila wakati
-
7:55 - 7:58kwamba hakuna tatizo kuwa pamoja na watu kama sisi.
-
7:58 - 8:04kwa kadiri wanavyodidimiza ukuta wala unyanyapaa na kutengwa,
-
8:04 - 8:06Ya kwamba sisi, kama wao,
-
8:06 - 8:10tunaweza kabiliana na chochote kinachotujia maishani.
-
8:10 - 8:11Asante.
-
8:11 - 8:16(Makofi)
- Title:
- Kwanini naongelea kuhusu kuishi na kifafa
- Speaker:
- Sitawa Wafula
- Description:
-
Aliyewahi kubaki nyumbani kutokana na ugonjwa wa kifafa. Sitawa Wafula, ambae ni mhamasishaji wa afya ya akili alipata nguvu kuandika kuhusu ugonjwa wake. Kwa sasa, anahamasisha kwa ajili ya wengine ambao bado hawajatambua sauti zao, akivunja unyanyapaa na kutengwa katika kuongelea ni namna gani inavyokuwa kwa mtu anayeishi na ugonjwa wa kifafa.
- Video Language:
- English
- Team:
- closed TED
- Project:
- TEDTalks
- Duration:
- 08:29
Joachim Mangilima approved Swahili subtitles for Why I speak up about living with epilepsy | ||
Joachim Mangilima accepted Swahili subtitles for Why I speak up about living with epilepsy | ||
Nelson Simfukwe edited Swahili subtitles for Why I speak up about living with epilepsy | ||
Nelson Simfukwe edited Swahili subtitles for Why I speak up about living with epilepsy | ||
Nelson Simfukwe edited Swahili subtitles for Why I speak up about living with epilepsy | ||
Nelson Simfukwe edited Swahili subtitles for Why I speak up about living with epilepsy | ||
Nelson Simfukwe edited Swahili subtitles for Why I speak up about living with epilepsy | ||
Nelson Simfukwe edited Swahili subtitles for Why I speak up about living with epilepsy |