-
Fikiria kuhusu rununu yako au kipakatalishi.
-
Wanajua kila kitu kuihusu.
-
Kila chembe ndani yake, mahali kilipozalishwa.
-
Halafu...
-
haujui chochote tena.
-
Taka za kielektroniki huwa kwa sababu vitu si muhimu kwetu tena,
-
kwa hivyo tunazitupa.
-
Tunazidisha hiyo shida kwa uhalisia kuwa
-
jinsi tumeziunda na kuzibuni
-
inakuwa vigumu kuzitenganisha,
-
Kudondoa vifaa muhimu,
-
na kuvitumua tena
-
tiubu zimeunganishwa na chasisi.
-
Chasisi imeunganishwa kwa kilicho kikuu...
-
Nasikia kuwa kuna takriban watu 4000 na wanaofanya kazi hapa.
-
Nimekuwa hapa kwa takriban miaka 15 sasa.
-
Tuligundua kuwa wengi wao
-
walikuwa na viwango vya juu vya vyembe vya chuma nzito damuni mwao.
-
Nadhani kuwa siyo tu Afrika
-
inapambana na suala hili la taka za kieletroniki
-
kwa sababu elektroniki na vifaa vyake ni sehemu ya maisha yetu ya kila siku.
-
Hatuwezi tu kuwapa hivi bidhaa
-
watu bilioni 7,8,9 watakao kuwa sayarini baadaye
-
tukiwa tunatupa idadi kubwa
-
baada ya kutumika kwa miaka miwili au mitatu.
-
Hakika, tunawaza kwa ujumla kuhusu taka za kieletroniki,
-
ni tofauti ukifikiria skrini za CRT,
-
au ukifikiria kuhusu rununu ya kizazi kipya.
-
Lakini hakika kuna thamani kubwa tunayoweza kurudisha kutoka kwa hizi taka.
-
Kunafaa kuwa na motisha ya kutengeneza upya
-
Mimi ni Professa katika MIT,
-
ninapoendesha mahali panapoitwa Senseable City Lab
-
na pia ofisi ya kubuni inayoitwa Carlo Rtii Associati.
-
Tulianza kushughuikia hii na mradi tuliyoiita Trash-Track.
-
Ilikuwa miaka michache iliyopita na tulishirikiana na jiji la Seattle
-
na kutupa elektoniki nyingi tulizozitambulisha
-
ili kufuata taka
-
tulifuata maganda ya ndizi,
-
skrini za CRT, tarakilishi, Katrigi na kadhalika
-
Taka nyingi zingeishia katika mipaka ya Marekani,
-
halafu, hatungeifuata tena.
-
Mara ya kwanza nilipofika hapa nilishtuka.
-
Unaona aina ya kazi watu wanaoifanya.
-
Wanajikata, wanajiweka wazi kwa vitu vingi.
-
Jina langu ni Bennett Nana Akuffo.
-
Mimi ni meneja wa Green Advocacy Ghana wa Miradi.
-
kwa hivyo, vijana hapa kawaida huzunguka na malori.
-
Wanaenda kwa kila nyumba.
-
Wakija kwangu,
-
hakika wanaweza kununua jokofu kutoka kwangu.
-
Halafu watalileta hadi hapa,
-
watalikata vipande.
-
Watapata aluminia kutokana na kasha.
-
watapata shaba kutokana na mota iliyoko jokofuni.
-
Kwa hivyo wanachokifanya ni kulikata kwa patasi na nyundo.
-
halafu nyaya zilizoko,
-
watazichoma kudondoa shaba.
-
Halafu kinachotendekea stairofomu,
-
ni kutumiwa kama mafuta.
-
Kwa hivyo wakitaka kusindika aina hizo zote za vyuma,
-
wataongezea Stairofomu halafu waliwashe.
-
Tunajua kuwa udongo umechafuka sana,
-
kwa viwango vya ledi, kadaminiamu na aseniki mchangani unaongezeka.
-
Tulifanya utafiti wa watu hapa.
-
Tulipata kuwa wengi wao
-
wameongeza viwango vya vyembe vya vyuma miilini mwao.
-
Vyembe vya vyuma vizito vinahusishwa na saratani
-
na magonjwa mengine.
-
Sehemu hii yote ni kama eneo la biashara.
-
Upo na watu wanaouza maji, vinywaji.
-
wengine wanafanya kazi,
-
wengine wanazurura wakiokota vitu mvunguni.
-
Kwa hivyo ni jumuiya yake yenyewe.
-
Nasikia kuwa kuna zaidi ya watu mia nne wanaofanya kazi hapa.
-
Na wengi wao hushinda hapa siku kutwa.
-
Wengi wao yamkini wapo hatarini.
-
Watu wengi hupaona Agbogbloshie kama biwi la taka.
-
Lakini ni huduma wanaopatia Waghana wa Kawaida.
-
Ndio, ni mbaya,
-
lakini ni huduma tunayohitaji.
-
Ikiwa Agbogbloshie haingekuwa,
-
ni nini ingefanyikia magari yetu kukuu,
-
majokofu yetu zee, maruninga na hayo yote?
-
Kila mara tumekuwa na azma hapa IDEO ya
-
kujaribu kuunganisha watu na teknolojia
-
kupitia ubunifu.
-
Mimi ni Tim Brown.
-
Na mimi ni mkurugenzi wa kampuni ya Ubunifu ya IDEO.
-
Siku za nyuma tulipoanza,
-
tulifanya vitu kama kiteuzi cha kwanza cha tarakilishi ya Macintosh ya asili,
-
na kipakatalishi cha kwanza, na kiboreshaji cha kwanza cha mashine iliyo otomatiki.
-
Utata wa mifumo
-
inayotegemeza bidhaa hizi na huduma
-
tunaelewa hayo bora sana sasa.
-
Ndiyo maana tulinuia vitu kama uchumi mzunguko.
-
Na umuhimu wa kufikiria kuhusu bidhaa
-
siyo tu kupitia zamu yao ya kutumiwa,
-
lakini pia kinachovitendekea baadaye.
-
Mimi ni Vincent Biruta,
-
mimi ni waziri wa mazingira wa jamhuri ya Rwanda.
-
Tunashughulika na tani 10,000 ya taka za kielektroniki kila mwaka.
-
Na tuliamua kuanzisha
-
kiwanda cha kuchanguka na kutengeneza upya taka za kielektroniki,
-
ambacho kina uwezo wa kushughulikia
-
haya matani 10,000 kila mwaka.
-
Leo kiwanda cha pili Rwanda
-
hufanya baadhi ya tarakilishi kuonekana mpya,
-
tarakilishi 400 zilizosafishwa
-
ambazo zinasambazwa kwa mashule.
-
Lakini tunapeleka sehemu za plastiki kwa kampuni za kutengeneza upya plastiki.
-
Tunapeleka vijenzi vya chuma kwa viwanda vya chuma.
-
Lakini tunapanga kuwa na awamu ya pili
-
kurudisha vyuma vya thamani
-
ambazo ni vijenzi vya hivi vifaa vya kielektroniki.
-
Kwa hisani ya Pure Health, Shirika lisilo la kiserikali kutoka Marekani,
-
tuliamua kutafuta njia ya kuondoa kuchoma
-
kama njia ya usindikaji wa shaba.
-
Tulianzisha eneo la jaribio hapa pamoja na vivua nyaya
-
Na waona hizi shimo unaposhinikizia nyaya
-
hizi ni vimo vya nyaya tunavyoweza kutengenezwa upya.
-
Na inafanya hivyo kwa sekunde, halafu imemaliza.
-
Plastiki inaenda upande mmoja,
-
na chuma inatokezea upande mwingine.
-
Unapoleta waya yako hapa,
-
Ni shaba au aluminia safi ambayo ina uzani zaidi.
-
Kwa hivyo vijana hupata pesa nyingi.
-
Imesababishwa kwa kubuni na kwa hivyo suluhisho ni shida ya kubuni.
-
Ikiwa tumechukulia uchumi mzunguko kwa uzito,
-
tungetaka kukamilisha
-
kuunda dhana mpya za usambazaji
-
Hatufai kutumia vifaa vingi sana.
-
Kuwa na vijenzi vilivyo na maisha mseto.
-
Halafu tunapofaa kuzitupa
-
tunahakikisha tu kuwa tumezitupa pale ambapo kuna mitambo
-
Bado tunapenda kidogo wazo
-
la bidhaa nzuri tunavyotaka kumiliki.
-
Lakini pengine huo sio mfano mzuri wa siku za usoni.
-
Inawezekana kuwa hatufai kununua bidhaa hizi kabisa,
-
lakini tunafaa kuzipeleka zihudumiwe
-
ili watengenezaji wawe na sababu ya kuzirudisha.
-
Itabidi tuwe wabunifu sana kwa miaka michache zijazo
-
ili kusuluhisha shida hizi.
-
Manukuu umefanywa na Adrian Castillo Uhakiki umefanywa na Jenny Lam Chowdhury.