Return to Video

How Can You Tell Satire from Misinformation?

  • 0:04 - 0:07
    Yakupendeza, Yakupendeza,
    Sawa, kuhusiana na kutoka nje,
  • 0:07 - 0:10
    nadhani kuna mtafaruku mwingi
    kuhusiana na jambo la kutoka nje.
  • 0:10 - 0:12
    Ni vitu vigani tunafaa kuwa
    tunachunguza kule nje?
  • 0:12 - 0:15
    Inachekesha, sijawahi kuwa mbishi katika
    muda wangu wote wa uandishi wa habari
  • 0:15 - 0:18
    hivyo kuna vile ina chekesha, sivyo?
  • 0:18 - 0:20
    Ilikuwa inachekesha
    kwenye onyesho lingine nilifanya kazi
  • 0:20 - 0:22
    inayoitwa Amanpour & Company.
  • 0:22 - 0:25
    Kwa kuwa tayari tulikuwa tunafanya utafiti wa kejeli na habari potovu,
  • 0:25 - 0:28
    Niliamua kuwaendea watu hawa wawili ili tuongee,
  • 0:28 - 0:30
    na niwaulize wanifafanulie utani wao.
  • 0:30 - 0:32
    Jeremy Levick na Rajat Suresh
  • 0:32 - 0:35
    ni wacheshi na wadhihaki
    wanaoishi Brooklyn.
  • 0:35 - 0:40
    Ikiwa wewe ni mcheshi
    au mdhihaki, ambayo ni kama,
  • 0:40 - 0:43
    Nadhani, ni neno kiasi la kujidai,
    ambalo sitatumia.
  • 0:43 - 0:45
    RS: Lakini sisi ni wa kujidai.
    JL: Apana. Sisi hujidai.
  • 0:45 - 0:46
    RS: Ndio. Ndio.
  • 0:46 - 0:49
    Hivi majuzi mliwadanganya
    Amanpour & Company.
  • 0:49 - 0:51
    Ni nini iliwapa wazo hilo?
  • 0:51 - 0:55
    Tulikuwa tukitazama video mingi sana
    ya aina hiyo na ...
  • 0:55 - 0:58
    Je, ilikuwa kimsingi kama,
    "Haiya, kuna mtu wa kahawia pale.
  • 0:58 - 0:59
    Najua mtu wa kahawia."
  • 0:59 - 1:03
    (Kucheka) Hapana,
    ilikuwa mbinu nadhifu zaidi kuliko hivyo tu.
  • 1:03 - 1:06
    Ilikuwa tu,
    Ni ya kushangaza kwetu tu
  • 1:06 - 1:10
    kusema utani wa Jeff Foxworthy,
    na kuwa wa kumaanisha sana kuihusu.
  • 1:10 - 1:14
    "Nilimwona mtu akiendesha gari kwenye
    barabara kuu, akampiga kulungu,
  • 1:14 - 1:16
    na akamuita 'chakula cha haraka'.
    RS: Ndio.
  • 1:16 - 1:19
    Hivyo, tunaona jinsi kejeli inatumiwa
  • 1:19 - 1:21
    kupitisha habari potovu.
  • 1:21 - 1:23
    Je, uliwahi fikiria
    ingetumika namna hii?
  • 1:23 - 1:27
    Hiyo kwa kawaida ni hatari kwa kejeli.
  • 1:27 - 1:29
    Inasaidia ikiwa una jina kubwa,
  • 1:29 - 1:33
    Inayoambatana na maudhui yako
    kama The Onion ama SNL.
  • 1:33 - 1:36
    Wakati unajifanyia mambo
    na kuyachapisha mwenyewe,
  • 1:36 - 1:38
    Kwenye mtandao haswa
  • 1:38 - 1:41
    kuna zile aina za lebo
    zinazoelekeza hadhara zinazokosekana,
  • 1:41 - 1:45
    hivyo kuna hatari ya kueneza
    habari potovu na ya uongo.
  • 1:46 - 1:49
    Kejeli kuonekana kama habari ya kweli-
  • 1:49 - 1:51
    Unaona jambo hili kila mahali mtandaoni.
  • 1:51 - 1:52
    Chukua mfano kama huu,
  • 1:52 - 1:56
    Mada ya kuvutia iliekwa kwenye Twitter
    la gazeti la The New Yoker,
  • 1:56 - 2:00
    "Trump ana matumaini ya kushinda
    Nobel Prize katika uwanja wa matibabu."
  • 2:00 - 2:03
    Watoa maoni kadhaa walijibu,
    wakitokea kuamini
  • 2:03 - 2:05
    kuwa habari hizo ni za kweli.
  • 2:05 - 2:08
    Wengine walitumaini ilikuwa kutoka kwa
    The Onion
  • 2:08 - 2:09
    Haikuwa hivyo.
  • 2:09 - 2:12
    Lakini ilikuwa kejeli,
    tunawezaje kujua?
  • 2:12 - 2:14
    Haya, bonyeza kwenye kifungu,
  • 2:14 - 2:18
    na utaona kwamba The New Yorker
    wamekwenda kwa urefu mkubwa
  • 2:18 - 2:20
    kuilebo kama kejeli.
  • 2:21 - 2:24
    Wanafanya hivi na kila kitu
    kutoka kwa Ripoti ya Borowitz,
  • 2:24 - 2:25
    ambayo ni safu ya kejeli.
  • 2:25 - 2:30
    Hata kijipicha kwenye Twitter
    ina kidokezo katika kaulimbiu ya safu hiyo -
  • 2:30 - 2:32
    nukuu "Sio habari."
  • 2:32 - 2:36
    Huu ni mfano wa makala yenye lebo kamilifu
    kutoka kwa tovuti inayojulikana ya kejeli,
  • 2:36 - 2:38
    na bado, watu walidanganywa.
  • 2:38 - 2:42
    Kwa hiyo, ni nini kinatokea
    wakati sehemu ya kejeli haina muktadha?
  • 2:42 - 2:47
    Mbaya zaidi, ni nini kinatokea wakati huo
    muktadha umeondolewa kimakusudi?
  • 2:47 - 2:50
    Hivyo ndivyo mwandishi mmoja alipata
    katika mitandao kadhaa ya tovuti
  • 2:50 - 2:54
    inayochukua vipande vya kejeli
    kutoka kwa muktadha yao asili,
  • 2:54 - 2:57
    na kuondoa lebo yoyote au kanusho zozote,
  • 2:57 - 3:02
    kisha kuzichapisha tena kama makala
    ya 'habari' zinazoonekana kama za kweli.
  • 3:03 - 3:07
    Tumeona mamia ya tovuti hizi
    zikiongezeka tangu Desemba,
  • 3:07 - 3:09
    na zinapata kuenezwa kwa wingi
    kwenye Facebook.
  • 3:09 - 3:11
    Tovuti moja ambayo tulikuwa tukiifuatilia
    mara kwa mara
  • 3:11 - 3:12
    ilikuwa moja ya mwanzo wa
    habari za uwongo
  • 3:12 - 3:15
    maarufu zaidi kwenye Facebook.
  • 3:15 - 3:18
    Ilikuwa ikipata mamia
    ya maelfu ya ushirikiano
  • 3:18 - 3:19
    kwenye kila makala iliyochapishwa.
  • 3:19 - 3:22
    Wakati kuiga kejeli
    inaonekana kwenye uso wake,
  • 3:22 - 3:27
    njia haswa ya kimsingi ya kueneza
    habari potovu au uongo,
  • 3:27 - 3:30
    tovuti hizi zinaendeshwa na watu
    ambao wanajua wanachofanya.
  • 3:30 - 3:32
    Kwa nini wanafanya hivyo?
  • 3:32 - 3:34
    PolitiFact imechunguza
    mamia ya tovuti hizi,
  • 3:34 - 3:38
    na kwa karibu zote,
    kuna vifuatiliaji vya Google Adsense.
  • 3:38 - 3:41
    Hiyo ina maana kwamba,
    yoyote atakaye bonyezea tovuti hiyo
  • 3:41 - 3:45
    ataenda kwenye maonyesho ya matangazo
    ya Google kwenye tovuti hiyo.
  • 3:45 - 3:47
    Hivyo kimsingi,
    zaidi watu wanaona nakala hiyo,
  • 3:47 - 3:49
    zaidi mwenye tovuti hiyo hulipwa.
  • 3:49 - 3:53
    Unajuaje wakati kitu ni mzaha
  • 3:53 - 3:56
    dhidi ya wakati kitu ni habari ya kweli?
  • 3:56 - 3:59
    kila wakati, utataka kufanya utafiti
    mwingi kabisa kwenye tovuti
  • 3:59 - 4:01
    iwezekanavyo
    kabla ya kusambaza kitu.
  • 4:01 - 4:03
    Hivyo, kila wakati
    nenda kwenye tovuti hiyo,
  • 4:03 - 4:05
    na utafute ukurasa wao wa Kuhusu.
  • 4:05 - 4:07
    Ikiwa hakuna habari nyingi hapo kuwahusu,
  • 4:07 - 4:10
    au kuna makosa ya tahajia,
    au inaonekana kama ya kienyeji,
  • 4:10 - 4:13
    hiyo inaweza kuwa ishara kwako
    kwamba tovuti hiyo si ya kuaminika.
  • 4:13 - 4:17
    Na ukiwa na shaka, kama huwezi
    kupata chochote kuhusu tovuti hiyo,
  • 4:17 - 4:18
    Usiieneze basi.
  • 4:18 - 4:21
    Ni sawa kabisa kutoshiriki
    kitu kwenye mitandao ya kijamii.
  • 4:21 - 4:23
    Ni bora kuwa salama kuliko pole.
  • 4:23 - 4:27
    Kejeli inakusudiwa kuchochea,
    kupata majibu ya kihisia,
  • 4:27 - 4:29
    kuvutia umakini wako,
    labda upate kucheka
  • 4:29 - 4:30
    au ubadilishe mawazo yako,
  • 4:30 - 4:34
    lakini kejeli haijakusudiwa
    kueneza habari potovu.
  • 4:34 - 4:36
    Kwa hivyo usidanganywe mtandaoni.
  • 4:36 - 4:38
    Soma zaidi ya vichwa vya habari.
  • 4:38 - 4:40
    Ikiwa kitu kinaonekana kuwa cha kijinga
  • 4:40 - 4:42
    na inaweza kuwa imeandikwa
    na watu kama marafiki wetu
  • 4:42 - 4:45
    Rajat na Jeremy - labda ni wao.
  • 4:45 - 4:47
    Mpaka wakati ujao.
    Usieneze habari za uwongo.
  • 4:47 - 4:48
    Iweke kweli.
  • 4:48 - 4:50
    Mimi ni Hari Sreenivasan.
    Hii ilikuwa Take on Fake.
  • 4:54 - 5:00
    Mama yangu alitaka sana
    kuelezea kila mtoa maoni
  • 5:00 - 5:01
    ambaye hakuelewa.
    (kucheka)
  • 5:01 - 5:04
    Kwa hivyo jibu la swali lako
    ni kumpata mama ambaye ata...
  • 5:04 - 5:05
    Nitasema ndio.
  • 5:05 - 5:08
    Nitasema "Wow, ilimbidi mama yake
    aeleze tani zake.'
  • 5:08 - 5:12
    Kweli, nadhani nahitaji kumpa mama yangu
    akaunti ya bandia au kitu kama hicho,
  • 5:12 - 5:17
    ili isiweze kufuatiliwa kwangu.
    (Kucheka)
Title:
How Can You Tell Satire from Misinformation?
Description:

more » « less
Video Language:
English
Team:
Amplifying Voices
Project:
Misinformation and Disinformation
Duration:
05:15

Swahili subtitles

Incomplete

Revisions Compare revisions