{muziki} Neno moja kueleza unyenyekevu kwa utamaduni hakika, kwangu ni upendo ikiwa ningeweza kufafanua unyenyekevu kwa utamaduni dhana zake zote haipi ufafanuzi fika ila tu neno ninalofikiria ni la msingi Escuchar Kuwa Wewe Kufungua Kupokea huruma upendo kanuni za unyenyekevu kwa utamaduni hutoa muundo-mbinu moja ya ziada kuchangia kile ambacho kimekuwa lengo letu kuu. Naam, Lengo letu kuu ni kuwa na hisia sawazisha hisia ya usawa na aina ya heshima tunayoiendeleza [muziki] unyenyekevu kwa utamaduni ni dhana pana na kwa hakika Melanie Tervalon nami tumefikiria mielekeo tatu. ya kwanza ni kujifunza bila kukoma na tafakari ya kibinafsi ya kina Na kwa hiyo tafakari ya kibinasi ni uelewa wa jinsi kila mmoja wetu, ni mtu tata mwenye dhana kadhaa kila mmoja wetu huja na historia na hadithi zake urithi na mtazamo. Unaponiangalia sasa Nina ngozi ya kizungu Nilipokuwa mdogo nilikuwa na nywele ya njano mpakuo na macho ya hudhurungi Kila mtu alijaribu kuniita chochote ila Mwamerika mweusi. Nina historia Utambulisho wangu una mizizi hiyo. Wazazi wangu walinielimisha kuhusu utambulisho wa kijamii na uzoefu wangu umeiunda. nina haki ya kujitambulisha. msingi wa pili bada ya tafakari ya kibinafsi na elimu endelevu isiyo na mwisho ni dhana kuwa lazima tupunguze ukosefu wa usawa, na kutambua na kupunguza ukosefu huo ambao ina asili yake katika wagonjwa wetu wa kliniki. ama wateja wetu wa kliniki kwa mienendo wa jamii ya watoa huduma Na hatimaye kipengee amacho ningetoa na pamoja na Jann tunahisi kuwa watu hawasomi au hawapendi kusoma. na taasisi pia lazima itoe mfano ya kanuni hizi. [muziki] Mwamerika mweusi anayemuuguza mwanamke mlatino mwenye miaka makamo kwa masaa kadhaa baada ya mgonjwa kufanyiwa upasuaji. Tabibu Mlatino katika huduma ya kushauri alikaribia kitanda akabaini mgonjwa aliyekuwa akilia na kutoa maoni kwa muuguzi kuwa mgonjwa alionekana kuwa na maumivu mengi baada ya upasuaji. Muuguzi kwa muhtasari alipuuza mtazamo wake na kumuarifu kuwa alifanya kozi katika chuo cha uuguzi kuhusu utamaduni na matibabu na anajua kuwa wagonwa wenye asili ya hispania hutia chuku katika kueleza uchungu wao Tabibu mlatino alikuwa na wakati mgumu kushawishi mtazamo wa muuguzi huyu ambaye alikwama kwenye ujuzi wake wa kijamii ambaje alidai kujifunza Ilimshangaza huyu tabibu Mlatino ambaye kwanza ni Mlatino, sio wote kwa mfano wake sii kila Mwamerika mmeksiko anajua kila kitu ambacho kipo kuhusu wagonjwa waamerika wameksiko. haikuwa hivyo. Lakini angekuwa wa maana kwa huyo muuguzi Mwamfrika mweusi kwa wakati huo ambapo hakudhani kuwa angehitaji, tena, kwa sababu alileta dhana ya umahiri wake wa utamaduni. tofauti kati ya unyenyekevu kwa utamaduni na umahiri wa utamaduni ilikuwa ya kwamba bado tupo katika mchakato na mahusiano ambayo yana pande nyingi kwayo, na kuwa hatuko sawa hata na istilahi ya umahiri kwa njia ambayo watu wanaelewa vizuri. na inamaanisha kuwa wale ambao ni watoa huduma na wamefunzwa kielimu kuwa unafahamu yote na una nguvu zote. Tulihisi kuwa hiyo siyo iliyokuwa ikitufanyikia tulipokwa tukijifunza kutoka kwa jamii na kuelewa kwa vitendo jinsi familia walikuwa wakija hospitalini na kuhisi kuwa hawasikizwi kutokana na asili zao katika historia, na jinsi hiyo ili athiri walichokuja nacho hospitalini ambacho hatukijui, na hatuna dokezo lolote kulihusu. kwetu, hii ndiyo sehemu ya kipengee cha unyenyekevu kupata kuelewa hayo. Si kujaribu kukudhalilisha, si kujaribu kukufanya uhisi vibaya, kukusaidia kuelewa kuwa maisha ni hivi. Na kuwa kwa dhana fulani umefurahi sana kwa kutojua. Aprili 1992 kwenye chanzo cha ghasia za Los Angeles kufuatia uamuzi wa kutopatwa na hatia kwa afisa wa polisi walioshtakiwa kumpiga Bwana King, jamii ya hospitali ya watoto ililazimishwa kukutana kwa misururo ya mikutano kufichua na kukosoa mifumo yetu ya ubaguzi wa kitaasisi udhalimu na ukosefu wa usawa. Jina langu ni Dkt. Melanie Tervalon, nami ni Mkurugenzi wa mambo ya tamaduni mseto katika hospitali ya watoto ya Oakland Nataka kushukuru kila aliyekuja kwa kile ambacho ni sherehe kwangu mwaka huu Mimi na Jann tulifanikiwa kuwa pamoja wakati haya yalikuwa yakichipuka ingawa mimi na Jann tumepishana kiumri sote ni wanawake waamerika weusi. na sote tulilelewa na wanawake ambao ni walimu. Na hapo tunachipuka na baba ambao ni wafanyikazi wanaotoka katika utamaduni wa kusini na waliojihusisha kikamilifu na harakati za haki za raia kwa kiwango cha kujitolea mhanga. na watoto wao pia walijinyima, na walitufunza kuhusu kujitolea mhanga na wakatulea kwa njia za kuelewa ya kuwa tunafaa hudumia. [muziki] Patty Vipi? Habari? Waambaje? Ni vyema kukuona Ni vyema kukuona Imekuwa muda mrefu Najua. Ndio Umekuwaje? Vyema Vyema. Asante kwa kunialika. Nimewekeza kwa watoto kwa umma hiyo Kwa sababu nimekuwa huko kwa muda mrefu Kwa sababu tulikuwa wakaazi. Na sasa naona kizazi cha pili cha familia yangu. mtaala wa utamaduni mseto ulianza mnamo 91-92 kama jaribio. Lini Rodney King... nadhani hito ilikuwa 90... Ilichochewa 92 ndio 92. tukio la Rodney King ambayo watu walishuhudia duniani kote dhidi ya watoto ilisababisha tuanze kuongea tena kuhusu tulichokiita akina Rodney King zetu za siri. mazingira ambayo familia zilihisi kuwa hawajashughulikiwa kwa heshima. Hiyo ilikuwa sehemu kubwa ya kazi yetu, kuhakikisha tunaishi kulingana na kanuni ambazo zilikuwa zimeundwa kutokana na mijadala hospitalini. kuwa kulingana na muundo wa kitivo katika hospitali ya watoto na muundo wa wagonjwa tuliokuwa tukiwahudumia hicho kitivo hakingeweza kufunza kuhusu mambo ya utamaduni na tofauti ya rangi na kadhalika Kwa hivyo tulitumia muda mwingi kufanya kazi na makundi ya kijamii na familia kuja kufunza Na nikifikiria istilahi mbili, umahiri wa kitamaduni na unyenyekevu kwa utamaduni kwangu umahiri wa kitamaduni inaelezea somo, mada na wajua... Na watu wanahisi kuwa nafaa kujua hili au la na kama sijui hili, siko mwerevu Ilhali kwangu unyenyekevu wa kitamaduni ni filosofia ni mtazamo, ni chombo Siyo kitu kilicho. Sitakuwa gwiji kwayo. Ni mtazamo wangu, ni jinsi nitashughulika hali. Mwaka uliopita nilikuwa mratibu wa timu ya msaada kwa wanafunzi amabayo ni mikutano ambayo familia huwa na walimu wakati ambapo watoto huwa mashakani. Na ilisisimua kujaribu kung'amua kuwa mikutano hiyo ilifaulu kwa njia moja au nyigine na kanuni za unyenyekevu kwa utamaduni. Kujaribu kusema kwa wenzangu kazini kusikia alichokuwa akipitia mzazi huyu na kile ambacho huyu mzazi anasikia kuhusu mtoto wake. Acha tujaribu kulizungumzia hili kama chanzo kuliko wajua...XYZ. Mojawapo ya vitu vilivyo nisaidia sana kuweza kuwa na amani na kutokujua ni kuwa, kwa muda mrefu nilichanganya kutojua na ukosefu wa akili. Na rafiki yangu mpendwa akanielezea mara moja nilipokuwa nazungumza kuhusu mada hii, alisema siyo kwamba siyo kuwa huna akili, ni kwamba chemchemi yako ya maarifa hususan katika eneo hili haipo. Kwa hivyo haikupunguzi akili kwa kiwango chochote cha mawazo. Haujui kwa sababu hakuna mtu amekuambia au haujawahi uliza swali hilo Na ilinifanya kuuliza maswali milioni kwa sababu sasa sikuhisi kuwa nilikuwa naambia dunia au mtu au mgonjwa au jamii kuwa mimi ni mjinga. Nilifurahi kusema tu kuwa sijui. Sawa na chemchemi ya maarifa na udaktari, hamna njia kujua kitu ila kwa kujifunza kulihusu. Lakini haipunguzi kwa njia yoyote akili zako. Mara ningeweza kutofautisha, nilikuwa sawa na kutojua tena. Makala huandikwa lakini haichapishwi mara moja kuhusu tuliojifunza kutokana na yote ya hii kazi ya kufanya kazi na majamii. Na hiki ndicho kifungo cha unyenyekevu kwa utamaduni ambacho watu sasa wamekitumia katika maeneo mengi, siyo tu katika udaktari lakini pia kwa elimu. Mashirika mengi yasiyo ya faida hutumia kanuni za unyenyekevu kwa utamaduni katika kazi zao Kanuni siyo tu kuhusu shughuli binafsi na tabia. Taasisi zimebidi kuwa na tafakari ya kibinafsi. wasomi wa kutokoma lazima waamini fika kuwa jamii zinazohudumiwa zinajua wanachotaka na wanachohitaji na kuwa wako katika sehemu nzuri kutueleza hicho wanachokitaka au kuhitaji [muziki] Wanaoishi katika umaskini wako na fursa ndogo na uwezo wa kubadili mfumo wa sera za umaskini na mara nyingi hunyimwa suluhisho fanisi kupambana na ukiukaji wa haki zao za kibinadamu. na nalijali sana hili swala kwa sababu kakangu ni mtu bila hatia mwenye ulemavu ambaye ameshikiliwa kwa ninachokiita utumwa mamboleo kwa miaka miwili sasa kwa yale ambayo hakuyafanya. Na ninakuja kwako kwa sababu mfumo wa haki unaokisia haijaundwa kunufaisha jamii yangu. Na ninaweza sauti ya mnyanyasaji ukisisitiza, la! Haufai kuwa na haki. Sisi tu. Hauna historia. sisi tu. Hauna uwezo wa kudhibiti nafsi, sisi tu. Haukumbuki kinachopiganiwa. Sisi tu. Kuna hizi nyakati ambazo hugusa umakini wa kila mtu na tunaweza tumia kama fursa ya kunufaika. Na nafikiria Rodney King, majibu mengi kwa Rodney King ndiyo iliibua mijadala nyingi na upelelezi mwingi wa moyo na watu kutafuta sana njia tunazoweza kuwa na mijadala hii na matokeo bora. halafu inafifia. [muziki] Afisa watatu wa polisi wanaokabiliwa na mashtaka ya uhalifu walikuwa miongoni mwa kundi la 15 waliomsimamisha mwanaumme mweusi mwenye miaka 25 jumamosi usiku halafu wakampiga, wakampiga mateke na kwa rungu Kile ambacho mtangazaji wa redioni Mary Mason alirekodi simu nyingi kutoka kwa wanachama wa jamii ya walioweusi waliokasirika na uamuzi, walioshtushwa na vurugu iliyofuatia. Tunahitaji upendo na heshima kwa kila mmoja Tunahitaji (haisikiki). Mwaka wa 2010 Arizona walipitisha sheria inaowapa mamlaka polisi wa mtaa kukagua hadhi ya uraia ya yeyote wanaomshuku kuwa ni mhamiaji haramu ndani ya Marekani. Ni nani aliye na haki ya kumuita binadamu mwenzake haramu? Wengi wa hawa wasio halali ndio wanaofanya kazi mashambani, kushafisha nyumba, kusawazisha ardhi- kazi ambazo zina haki ya kulipa chini ya msharaha wa chini. Kuna vitu ambavyo ni vigumu kusikia, na kuna vitu ambavyo ni vigumu kuona. Sasa ni vipi samaki haoni maji. Ni vigumu kama unanufaika kutokana na upendeleo kuiona hivyo. Na naweza sema inahitaji kumbukumbu ya kila mara Na hakika siioni kila mara. Na kila mara ninakumbushwa kuihusu. Nakumbushwa kuwa nakumbushwa kuihusu. Kuwa kwa nini lazima ni kumbushwe kuihusu, lakini nakumbushwa. Nilisikia mwanamke mzungu nyuma yetu akisema nyinyi wageni hamna adabu. Mwanzoni nilijibu kwa hasira na kuchanganyikiwa. Hasira kwa sababu nilihisi kubaguliwa na kuhukumiwa Kuchanganyikiwa kwa sababu alikuwa mwanamke mzee kutuliko, mbona hajaishi kwa miaka ya kutosha kujua kuwa yeye pia si asili wa nchi hii? Kila mara tunakumbwa na ujumbe za kina kuwa ngozi nyeupe ni bora zaidi. Sera za uhamiaji huendelea kujadiliwa katika ikulu ya White House, huku wenye rangi hudhurungi wakitarajia kupata kazi ya ziada nje ya bohari ya nyumbani. Ni vipi unyenyekevu wa kitamaduni unavyochipuka katika Kikundi cha masomo ya uanahabari cha Berkeley? lazima nitambue Tony Borbone [fonetiki]. Tony Borbone, na apumzike kwa amani, alikuwa mtetezi stadi wa uzuiaji wa vurugu niliyekutana naye katika miaka yetu ya awali ya kushughulikia uzuiaji wa vurugu tulipoanzisha Kikundi cha masomo ya uanahabari cha Berkeley. Tony alinikabili akaniuliza, unaishi Carlifonia, ni wafanyikazi wako wangapi wanaongea kihispania? Na sikuwa na yeyote. Na Tony, nilitaka kuseama ni mapenzi, haikuwa ni mapenzi ilikuwa njia ya kukabili. namaanisha hatimaye tulipenda kazi za kila mmoja wetu na tulikuwa na heshima kwa kila mmoja nadhani uhusiano wetu ulipo nawiri. Lakini hakuogopa kusema kilekilicho cha muhimu. [muziki] Ni muhimu sana kujitokeza. Kutenga muda katika maisha yako na kuonyesha unajali kuhusu jamii na kuwa hapo. Kwa hivyo wafanyikazi walikuwa wakishiriki katika vitendo vya kushurutisha mmiliki wa soko ya kuku aliyekuwa na deni ya mshahara ya wafanyikazi Wafanyikazi walikuwa wakitoka na mabango ya maandamano, na nilienda nao. hivyo nilihisi kuogopa. Unahisi ni kama umefichuliwa. Upo katika mazingira ambayo ni tofauti na baadhi ya vitu ambavyo nilikuwa nimefanya. [muziki] Tulipokuwa na mikutano hii kila mtu katika mradi alikuwa na uzoefu katika utafiti wa jamii lakini kuna msukumo. Unapokuwa katika mfumo wa utaalamu unazoea kushiriki katika mikutano na kujaribu kuchangia Halafu kuongezea tunaendeleza haya yote kwa kiingereza. kwa hivyo wafanyikazi wawili wengine kutoka kwa chama endelevu cha Uchina walikuwa wakiwatafsiria wafanyikazi wambao hawaelewi Kiingereza na kwa hivyo hawawezi kushiriki kikamilifu. halafu kila kitu kinafanyika haraka, watu wanajadiliana, na kwa mfanyikazi asioelewa Kiingereza ilikuwa ngumu kwake angalau kupata neno katika mdahalo. tulitafakari na watu wakatambua. halafu tukaanza kuendesha mikutano kwa kichina. halafu wanaozungumza Kiingereza wakavaa kipokea sauti masikioni huku wakitafsiriwa moja kwa moja. Wazungumzaji asili wa Kiingereza wallikuwa kimya, Na hiyo ilibadilisha sana hali ya mkutano. Lakini wafanyikazi bado walikuwa wamenyamaza. Kwa kuzingatia unyenyekevu wa kitamaduni tulipewa changamoto kufikiria kwa kina sana. kuhusu maana ya mila na jinsi haimaanishi kufikiria orodha ya hulka ambazo watu huzingatia. lakini kuwa inakuhusisha na dhana zako na jinsi unavyoonyesha dhana zako kwa mtu mwingine kinyume na uzoefu ya walivyo [muziki] Nilisikia kuhusu unyenyekevu wa kitamaduni nilipokuwa mwanafunzi wa uzamili hapa katika jimbo la San Francisco. Lakini nahisi nilielewa kwanza unyenyekevu wa utamaduni kama dhana sana hapo awali maishani mwangu. Ilichipukia mahali pa kutoona, mahali pa kama kukandamiza nafsi yangu kama mwanamke mweusi na sasa imedilishwa kikamilifu, kama mkufunzi, kutambua nilivyo, ninaposimama darasani, ni nini hadhi yangu. Na pia sauti yangu yamaanisha nini duniani na inamaanisha nini kama mkufunzi. Ilitokezea kwa kujaribu kutoshea, kufanya ninachoweza kuwa mhindi nyumbani na siyo nje ulimwenguni. Na bila kueleza, imekuwa kielelezo cha utambulisho niliyojua ipo ambayo singeweza kueleza nilipokuwa. na sasa inasema huyo mtu ni nani na kutambua nguvu na hadhi yangu kujiangalia kwa njia fulani. pia nasema kuwa mimi ni mwanamke wa rangi, Niko na cha muhimu cha kusema na niko hapa. Nadhani kuwa il mradi tupo na nguvu na hadhi katika jamii tutapambana na kuwa wanyenyekevu sana kama wanawake wa rangi, kama wanawake wanatoka katika tabaka ya wafanyikazi, kama wanawake wanatoka katika asili ya kulipwa mshahara mdogo ama asili za mali finyu, sawa? Il mradi kuna nguvu na hadhi katika jamii, najua kuwa nitakuwa nikipambana nazo na kupambana nazo kila siku. [Muziki] Nilichunguza {haisikiki] hapa kuona jinsi sera zetu za sasa zinaunganisha na kuratibisha zinalenga wanafunzi wenye jinsia isiyo asili. Na nilikuwa nikitafakari kuhusu jinsi inavyohusika na mada ya jioni ya leo ya unyenyekevu kwa utamaduni kwa sababu tunaongea kuhusu huntha. au hulka za rika katika [haisikiki] na jinsi inavyoheshimiwa au la >>Sawa. na jinsi taasisi hii inaweza kuwa kufaa kitamaduni au kunyenyekea ama kuheshimu wanaopitia huntha wanapokuja hapa. Wakufunzi wakiafya ninaofanya kazi nao wote ni wanawake huntha. Na haswa siku yangu ya pili kazini, niliingia kwenye mkutano, na ilikuwa kamati ya bodi ya ushauri ya wanawake wote huntha. Ilikuwa ya kutatiza sana lakini kwa wakati huo huo walinifanya nitulie. Walianza kuniuliza maswali ni kama waliona , na kusema kwa hivyo unatoka wapi? Nikawajibu mimi ni mhajemi. oh twajua huu msichana huntha kutoka mashariki ya kati, unamjua? Nikajibu, simjui Kwa hivyo ufafanuzi wangu wa unyenyekevu wa utamaduni ni kuwa tayari kujifunza kila wakati Ninachowataka mfanye ni zunguka na kujitambulisha na kutuambia unyenyekevu kwa utamaduni unamaanisha nini kwako. Wakati wangu wa kwanza kuwa na shauku kuhusu unyenyekevu wa kitamaduni ilikuwa nilipokuwa mwanafunzi wa shahada ya kwanza katika chuo kikuu. nilikuwa kurutu katika shirika fulani. Na walikuwa wakifanya mafunzo ya umahiri wa utamaduni kwa jamii wakazi wa kisiwa cha Pasifiki na kufanya kazi na jamii za wakazi wa visiwa vya Pasifiki Na kama mwanamke wa ukoo mbili za kisiwa cha Pasiki. Nilifurahi sana na pia na wasiwasi kuhudhuria mafunzo yale na kujifunza kuhusu nyenzo ambayo ingeainishwa na kujadiliwa. na jinsi mimi na wengine tungejifunza, kuhusu mila za kisiwa cha pasifiki na kufanya kazi na wakazi wa huko kuhusu mambo ya afya ambayo yalikuwa muhimu kwa jamii. Nadhani baada ya kuhudhuria mafunzo niligundua kuwa kulikuwa na hisia ya mafanikio na ukamilishaji kwa wale ambao walishiriki halafu nilitangulizwa kwa unyenyekevu wa kitamaduni kama mwanafunzi wa shahada ya kwanza darasani, ilifanyika wakati huo huo. Na nikawa na hisia ya mafanikio na ufanikishaji na umahiri na kuelewa mipaka ya kujielimisha. Siwezi kukuambia kihakika maana ya unyenyekevu wa kitamaduni kwangu. Nahisi kuwa naitenda na hivyo ndivyo naijua Kitu moja ambayo naifikiria au ninayoitenda ni unenyekevu wa kitamaduni ni kihispania kihispania kihispania kihispania Kihispania kuwa na asili ya kisayansi na kuja katika afya ya kijamii bila kuwahi kusikia unyenyekevu wa kitamaduni katika sayansi iliibua maswali Kwa sababu utamaduni ni kitu kinacho sisitizwa, siyo kitu kitu kinacho zungumzwa kwa njia inayofaa Kumekuwa na vizuizi vinavyoonekana peupe kwa jamii ya wachache katika sayansi. Unaweza iona ukiwa katika madarasa ya sayansi. Unaweza iona ukiwa katika makundi ya utafiti. Unaweza iona ukimwangalia maprofesa wako. nasiongelei tu jamii za wachache kwa kuzingatia ukoo au rangi naongelea jamii za wachache ambao hawana uakilishi katika sayansi, kwa mfano ukoo au rangi ni sababu lakini jinsia na maumbil ya kijinsia siyo. Nilijifunza kuhusu unyenyekevu wa kitamaduni sehemu mbili kwa utamaduni wangu kuwa wa kikambodia na kusini mashariki mwa Asia kutojua chochote kuihusu kulifanya nikejeliwe na jamaa zangu kuhusu kutoongea vizuri. halafu baada ya kuenda chuoni na kujifunza kuihusu katika anthropolojia na kuhoji wazazi wangu kuhusu uzoefu wao macho yangu yalifumbuka. Mojawapo ya vitu ambayo nimejifunza katika miaka kadhaa iliyopita nataka kusema ni kusikiza ninachokisema. Na namaanisha kusikiliza kwa makini ninachokisema. Na kitu ambacho nimejifunza kusikiliza ni ninaposema mimi, Naamini hii, nafanya hii, na kusikiliza sasa kuwa ni tofauti na sisi Sisi nasikia sana katika habari, sisi Wamarekani, sawa? kama sisi, ni nani 'sisi' anaongea kumhusu? Ni kufikiria na kusikiliza tunapotumia mimi na sisi. Nilipokuwa nakua nilipata hamu ya utamaduni na dini nyinginezo na kujifunza tu kuhusu vitu kutoka kwa asili nyinginezo. Kwa hivyo nadhani hiyo ilinifanya kuwa mnenyekevu kitamaduni kwa sababu nilikuwa na hamu kwa hivyo baada ya kusoma kwa mwaka moja Afrika magharibi, nilirudi nikisema, Eh Mungu wangu, sijui chochote, sijui chochote kuhusu watu weusi, sijui chochote kuhusu Waafrika. namaanisha ilibadilisha mtazamo wangu. Amani. Nafikiria ninapoketi mahali pa unyenyekevu kuwa kuwa utulivu na nafasi na kuwa sawa na raha ambayo inakaribia amana ya kuwa na mtu mwingine amabye naweza fikiria. Kama lazima niifikirie kama barabara basi ningeweza fikiria kuhusu barabara inayopinda. Na kama upinde hauwezi --kwangu kwa dhana ya kucheza upinde unaoenda juu lazima uje chini pia ina uendelevu na katika uendelevu vitu vingi hufanyika na nguvu za aina nyingi zinaweza badili umbo lake au kina cha kinapoweza kufika. Unyenyekevu wa utamaduni hakika ni safari kwangu Unyenyekevu wa kitamaduni hakika ni safari kwangu, Na ni safari ambayo najua kutakuwa na changamoto na nipo ndani yazo. Na ninajua kila changamoto nitakayo jifunza kwayo. Na nadhani ni mchakato ambao lazima nipitie kila siku na ambayo niko sawa kupitia. Na hakika inanifanya kuwa na nguvu zaidi na uerevu zaidi na natuhahi hekima zaidi kuliko nilivyokuwa jana. [muziki] muziki