{muziki}
Neno moja kueleza unyenyekevu kwa utamaduni
hakika, kwangu ni upendo
ikiwa ningeweza kufafanua unyenyekevu kwa utamaduni
dhana zake zote
haipi ufafanuzi fika ila tu neno
ninalofikiria ni la msingi
Escuchar
Kuwa
Wewe
Kufungua
Kupokea
huruma
upendo
kanuni za unyenyekevu kwa utamaduni hutoa
muundo-mbinu moja ya ziada kuchangia kile ambacho
kimekuwa lengo letu kuu. Naam,
Lengo letu kuu ni kuwa na hisia sawazisha
hisia ya usawa na aina ya heshima
tunayoiendeleza
[muziki]
unyenyekevu kwa utamaduni ni dhana pana
na kwa hakika Melanie Tervalon
nami tumefikiria mielekeo tatu.
ya kwanza ni kujifunza bila kukoma
na tafakari ya kibinafsi ya kina
Na kwa hiyo tafakari ya kibinasi ni
uelewa wa jinsi kila mmoja wetu,
ni mtu tata mwenye dhana kadhaa
kila mmoja wetu huja na historia na hadithi zake
urithi na mtazamo.
Unaponiangalia sasa
Nina ngozi ya kizungu
Nilipokuwa mdogo nilikuwa na nywele ya njano mpakuo
na macho ya hudhurungi
Kila mtu alijaribu kuniita chochote ila Mwamerika mweusi.
Nina historia
Utambulisho wangu una mizizi hiyo.
Wazazi wangu walinielimisha kuhusu utambulisho wa kijamii
na uzoefu wangu umeiunda.
nina haki ya kujitambulisha.
msingi wa pili bada ya tafakari ya kibinafsi
na elimu endelevu isiyo na mwisho ni dhana
kuwa lazima tupunguze ukosefu wa usawa, na kutambua
na kupunguza ukosefu huo
ambao ina asili yake katika wagonjwa wetu wa kliniki.
ama wateja wetu wa kliniki kwa mienendo wa jamii ya watoa huduma
Na hatimaye kipengee amacho ningetoa na pamoja na Jann
tunahisi kuwa watu hawasomi au hawapendi kusoma.
na taasisi pia lazima itoe mfano ya kanuni hizi.
[muziki]
Mwamerika mweusi anayemuuguza
mwanamke mlatino mwenye miaka makamo kwa masaa kadhaa
baada ya mgonjwa kufanyiwa upasuaji.
Tabibu Mlatino
katika huduma ya kushauri alikaribia kitanda
akabaini mgonjwa aliyekuwa akilia na kutoa maoni kwa muuguzi
kuwa mgonjwa alionekana kuwa
na maumivu mengi baada ya upasuaji.
Muuguzi kwa muhtasari alipuuza mtazamo wake na kumuarifu
kuwa alifanya kozi katika chuo cha uuguzi kuhusu
utamaduni na matibabu na anajua kuwa wagonwa wenye asili ya hispania
hutia chuku katika kueleza uchungu wao
Tabibu mlatino alikuwa na wakati mgumu kushawishi
mtazamo wa muuguzi huyu ambaye alikwama
kwenye ujuzi wake wa kijamii ambaje alidai kujifunza
Ilimshangaza huyu tabibu Mlatino
ambaye kwanza ni Mlatino, sio wote
kwa mfano wake sii kila Mwamerika mmeksiko
anajua kila kitu ambacho kipo kuhusu wagonjwa waamerika wameksiko.
haikuwa hivyo.
Lakini angekuwa wa maana
kwa huyo muuguzi Mwamfrika mweusi kwa wakati huo
ambapo hakudhani kuwa angehitaji, tena,
kwa sababu alileta dhana ya umahiri wake
wa utamaduni.
tofauti kati ya unyenyekevu kwa utamaduni
na umahiri wa utamaduni ilikuwa ya kwamba bado tupo katika mchakato
na mahusiano ambayo yana pande nyingi kwayo,
na kuwa hatuko sawa hata na istilahi
ya umahiri kwa njia ambayo watu wanaelewa vizuri.
na inamaanisha kuwa wale ambao ni watoa huduma
na wamefunzwa kielimu
kuwa unafahamu yote na una nguvu zote.
Tulihisi kuwa hiyo siyo iliyokuwa ikitufanyikia
tulipokwa tukijifunza kutoka kwa jamii na kuelewa
kwa vitendo jinsi familia walikuwa wakija
hospitalini na kuhisi
kuwa hawasikizwi kutokana na asili zao
katika historia, na jinsi hiyo ili athiri walichokuja
nacho hospitalini ambacho hatukijui,
na hatuna dokezo lolote kulihusu.
kwetu, hii ndiyo sehemu ya kipengee cha unyenyekevu
kupata kuelewa hayo.
Si kujaribu kukudhalilisha, si kujaribu kukufanya uhisi vibaya,
kukusaidia kuelewa kuwa maisha ni hivi.
Na kuwa kwa dhana fulani umefurahi sana
kwa kutojua.
Aprili 1992 kwenye chanzo
cha ghasia za Los Angeles kufuatia uamuzi wa kutopatwa na hatia
kwa afisa wa polisi walioshtakiwa kumpiga Bwana King,
jamii ya hospitali ya watoto ililazimishwa kukutana
kwa misururo ya mikutano kufichua
na kukosoa mifumo yetu ya ubaguzi wa kitaasisi
udhalimu na ukosefu wa usawa.
Jina langu ni Dkt. Melanie Tervalon, nami ni Mkurugenzi
wa mambo ya tamaduni mseto katika hospitali ya watoto ya Oakland
Nataka kushukuru kila aliyekuja
kwa kile ambacho ni sherehe kwangu mwaka huu
Mimi na Jann tulifanikiwa kuwa pamoja
wakati haya yalikuwa yakichipuka
ingawa mimi na Jann tumepishana kiumri
sote ni wanawake waamerika weusi.
na sote tulilelewa na wanawake ambao ni walimu.
Na hapo tunachipuka na baba ambao ni wafanyikazi
wanaotoka katika utamaduni wa kusini
na waliojihusisha kikamilifu na harakati za haki za raia
kwa kiwango cha kujitolea mhanga.
na watoto wao pia walijinyima, na walitufunza
kuhusu kujitolea mhanga na wakatulea kwa njia
za kuelewa ya kuwa tunafaa hudumia.
[muziki]
Patty
Vipi?
Habari?
Waambaje?
Ni vyema kukuona
Ni vyema kukuona
Imekuwa muda mrefu
Najua. Ndio
Umekuwaje?
Vyema
Vyema. Asante kwa kunialika.
Nimewekeza kwa watoto kwa umma hiyo
Kwa sababu nimekuwa huko kwa muda mrefu
Kwa sababu tulikuwa wakaazi.
Na sasa naona kizazi cha pili cha familia yangu.
mtaala wa utamaduni mseto ulianza
mnamo 91-92 kama jaribio.
Lini Rodney King... nadhani hito ilikuwa 90...
Ilichochewa 92
ndio 92.
tukio la Rodney King ambayo watu walishuhudia
duniani kote dhidi ya watoto ilisababisha tuanze
kuongea tena kuhusu tulichokiita
akina Rodney King zetu za siri.
mazingira ambayo familia zilihisi
kuwa hawajashughulikiwa kwa heshima.
Hiyo ilikuwa sehemu kubwa ya kazi yetu, kuhakikisha
tunaishi kulingana na kanuni
ambazo zilikuwa zimeundwa
kutokana na mijadala hospitalini.
kuwa kulingana na muundo wa kitivo katika hospitali ya watoto
na muundo wa wagonjwa tuliokuwa tukiwahudumia
hicho kitivo hakingeweza kufunza kuhusu mambo
ya utamaduni na tofauti ya rangi na kadhalika
Kwa hivyo tulitumia muda mwingi kufanya kazi na makundi ya kijamii
na familia kuja kufunza
Na nikifikiria istilahi mbili, umahiri wa kitamaduni na
unyenyekevu kwa utamaduni kwangu umahiri wa kitamaduni inaelezea
somo, mada na wajua...
Na watu wanahisi kuwa nafaa kujua hili au la
na kama sijui hili, siko mwerevu
Ilhali kwangu unyenyekevu wa kitamaduni ni filosofia
ni mtazamo, ni chombo
Siyo kitu kilicho. Sitakuwa gwiji kwayo.
Ni mtazamo wangu, ni jinsi nitashughulika hali.
Mwaka uliopita nilikuwa mratibu
wa timu ya msaada kwa wanafunzi amabayo ni mikutano
ambayo familia huwa na walimu
wakati ambapo watoto huwa mashakani.
Na ilisisimua kujaribu kung'amua kuwa
mikutano hiyo ilifaulu kwa njia moja au nyigine
na kanuni za unyenyekevu kwa utamaduni.
Kujaribu kusema kwa
wenzangu kazini kusikia alichokuwa akipitia mzazi huyu
na kile ambacho huyu mzazi anasikia kuhusu mtoto wake.
Acha tujaribu kulizungumzia hili kama chanzo kuliko
wajua...XYZ.
Mojawapo ya vitu vilivyo nisaidia sana kuweza
kuwa na amani na kutokujua ni
kuwa, kwa muda mrefu nilichanganya kutojua
na ukosefu wa akili.
Na rafiki yangu mpendwa akanielezea mara moja
nilipokuwa nazungumza kuhusu mada hii, alisema siyo
kwamba siyo kuwa huna akili, ni kwamba chemchemi yako
ya maarifa hususan katika eneo hili haipo.
Kwa hivyo haikupunguzi akili
kwa kiwango chochote cha mawazo.
Haujui kwa sababu hakuna mtu amekuambia
au haujawahi uliza swali hilo
Na ilinifanya kuuliza maswali milioni
kwa sababu sasa sikuhisi kuwa nilikuwa naambia dunia
au mtu au mgonjwa
au jamii kuwa mimi ni mjinga.
Nilifurahi kusema tu kuwa sijui.
Sawa na chemchemi ya maarifa
na udaktari, hamna njia
kujua kitu ila kwa kujifunza kulihusu.
Lakini haipunguzi kwa njia yoyote
akili zako.
Mara ningeweza kutofautisha, nilikuwa sawa
na kutojua tena.
Makala huandikwa lakini haichapishwi mara moja
kuhusu tuliojifunza kutokana na yote
ya hii kazi ya kufanya kazi na majamii.
Na hiki ndicho kifungo cha unyenyekevu kwa utamaduni
ambacho watu sasa wamekitumia katika maeneo mengi,
siyo tu katika udaktari lakini pia kwa elimu.
Mashirika mengi yasiyo ya faida hutumia kanuni za unyenyekevu kwa utamaduni
katika kazi zao
Kanuni siyo tu
kuhusu shughuli binafsi na tabia.
Taasisi zimebidi kuwa na tafakari ya kibinafsi.
wasomi wa kutokoma lazima waamini fika kuwa jamii
zinazohudumiwa zinajua wanachotaka
na wanachohitaji na kuwa wako katika sehemu nzuri
kutueleza hicho wanachokitaka au kuhitaji
[muziki]
Wanaoishi katika umaskini wako na fursa ndogo na uwezo
wa kubadili mfumo wa sera za umaskini
na mara nyingi hunyimwa suluhisho fanisi
kupambana na ukiukaji wa haki zao za kibinadamu.
na nalijali sana hili swala
kwa sababu kakangu ni mtu bila hatia mwenye ulemavu
ambaye ameshikiliwa kwa ninachokiita utumwa mamboleo
kwa miaka miwili sasa kwa yale ambayo hakuyafanya.
Na ninakuja kwako kwa sababu
mfumo wa haki unaokisia haijaundwa
kunufaisha jamii yangu.
Na ninaweza sauti ya mnyanyasaji ukisisitiza, la!
Haufai kuwa na haki.
Sisi tu. Hauna historia. sisi tu.
Hauna uwezo wa kudhibiti nafsi, sisi tu.
Haukumbuki kinachopiganiwa.
Sisi tu.
Kuna hizi nyakati ambazo hugusa umakini wa kila mtu
na tunaweza tumia kama fursa ya kunufaika.
Na nafikiria Rodney King, majibu mengi
kwa Rodney King ndiyo iliibua mijadala nyingi na
upelelezi mwingi wa moyo na watu kutafuta sana njia
tunazoweza kuwa na mijadala hii
na matokeo bora.
halafu inafifia.
[muziki]
Afisa watatu wa polisi wanaokabiliwa na mashtaka ya uhalifu
walikuwa miongoni mwa kundi la 15
waliomsimamisha mwanaumme mweusi mwenye miaka 25 jumamosi usiku
halafu wakampiga, wakampiga mateke na kwa rungu
Kile ambacho mtangazaji wa redioni Mary Mason alirekodi simu nyingi
kutoka kwa wanachama wa jamii ya walioweusi waliokasirika
na uamuzi, walioshtushwa na vurugu iliyofuatia.
Tunahitaji upendo na heshima kwa kila mmoja
Tunahitaji (haisikiki).
Mwaka wa 2010 Arizona walipitisha sheria inaowapa mamlaka polisi wa mtaa
kukagua hadhi ya uraia ya yeyote wanaomshuku
kuwa ni mhamiaji haramu ndani ya Marekani.
Ni nani aliye na haki ya kumuita binadamu mwenzake haramu?
Wengi wa hawa wasio halali ndio wanaofanya kazi mashambani,
kushafisha nyumba, kusawazisha ardhi- kazi ambazo zina haki
ya kulipa chini ya msharaha wa chini.
Kuna vitu ambavyo ni vigumu kusikia,
na kuna vitu ambavyo ni vigumu kuona.
Sasa ni vipi samaki haoni maji.
Ni vigumu kama unanufaika
kutokana na upendeleo kuiona hivyo.
Na naweza sema inahitaji kumbukumbu ya kila mara
Na hakika siioni kila mara.
Na kila mara ninakumbushwa kuihusu. Nakumbushwa
kuwa nakumbushwa kuihusu.
Kuwa kwa nini lazima ni kumbushwe kuihusu, lakini nakumbushwa.
Nilisikia mwanamke mzungu nyuma yetu akisema nyinyi wageni
hamna adabu.
Mwanzoni nilijibu kwa hasira na kuchanganyikiwa.
Hasira kwa sababu nilihisi kubaguliwa
na kuhukumiwa
Kuchanganyikiwa kwa sababu alikuwa mwanamke mzee kutuliko, mbona hajaishi
kwa miaka ya kutosha kujua kuwa yeye pia si asili
wa nchi hii?
Kila mara tunakumbwa na ujumbe za kina
kuwa ngozi nyeupe ni bora zaidi.
Sera za uhamiaji huendelea kujadiliwa
katika ikulu ya White House, huku wenye rangi hudhurungi wakitarajia
kupata kazi ya ziada nje ya bohari ya nyumbani.
Ni vipi unyenyekevu wa kitamaduni unavyochipuka
katika Kikundi cha masomo ya uanahabari cha Berkeley?
lazima nitambue Tony Borbone [fonetiki].
Tony Borbone, na apumzike kwa amani,
alikuwa mtetezi stadi wa uzuiaji wa vurugu
niliyekutana naye katika miaka yetu ya awali ya kushughulikia uzuiaji wa vurugu
tulipoanzisha Kikundi cha masomo ya uanahabari cha Berkeley.
Tony alinikabili akaniuliza, unaishi Carlifonia,
ni wafanyikazi wako wangapi wanaongea kihispania?
Na sikuwa na yeyote.
Na Tony, nilitaka kuseama ni mapenzi,
haikuwa ni mapenzi ilikuwa njia ya kukabili.
namaanisha hatimaye tulipenda kazi za kila mmoja wetu
na tulikuwa na heshima kwa kila mmoja nadhani
uhusiano wetu ulipo nawiri.
Lakini hakuogopa kusema kilekilicho cha muhimu.
[muziki]
Ni muhimu sana kujitokeza.
Kutenga muda katika maisha yako na kuonyesha unajali
kuhusu jamii na kuwa hapo.
Kwa hivyo wafanyikazi walikuwa wakishiriki katika vitendo
vya kushurutisha mmiliki wa soko ya kuku
aliyekuwa na deni ya mshahara ya wafanyikazi
Wafanyikazi walikuwa wakitoka na mabango ya maandamano,
na nilienda nao.
hivyo nilihisi kuogopa.
Unahisi ni kama umefichuliwa.
Upo katika mazingira ambayo ni tofauti na baadhi
ya vitu ambavyo nilikuwa nimefanya.
[muziki]
Tulipokuwa na mikutano hii kila mtu
katika mradi alikuwa na uzoefu
katika utafiti wa jamii
lakini kuna msukumo.
Unapokuwa katika mfumo wa utaalamu unazoea
kushiriki katika mikutano na kujaribu kuchangia
Halafu kuongezea
tunaendeleza haya yote kwa kiingereza.
kwa hivyo wafanyikazi wawili wengine
kutoka kwa chama endelevu cha Uchina walikuwa wakiwatafsiria
wafanyikazi wambao hawaelewi Kiingereza
na kwa hivyo hawawezi kushiriki kikamilifu.
halafu kila kitu kinafanyika haraka, watu
wanajadiliana, na kwa mfanyikazi
asioelewa Kiingereza ilikuwa ngumu kwake angalau
kupata neno katika mdahalo.
tulitafakari na watu wakatambua.
halafu tukaanza kuendesha mikutano kwa kichina.
halafu wanaozungumza Kiingereza wakavaa kipokea sauti masikioni
huku wakitafsiriwa moja kwa moja.
Wazungumzaji asili wa Kiingereza wallikuwa kimya,
Na hiyo ilibadilisha sana hali ya mkutano.
Lakini wafanyikazi bado walikuwa wamenyamaza.
Kwa kuzingatia unyenyekevu wa kitamaduni tulipewa changamoto
kufikiria kwa kina sana.
kuhusu maana ya mila na jinsi haimaanishi kufikiria
orodha ya hulka ambazo watu huzingatia.
lakini kuwa inakuhusisha
na dhana zako na jinsi unavyoonyesha dhana zako
kwa mtu mwingine kinyume na uzoefu
ya walivyo
[muziki]
Nilisikia kuhusu unyenyekevu wa kitamaduni
nilipokuwa mwanafunzi wa uzamili hapa
katika jimbo la San Francisco.
Lakini nahisi nilielewa kwanza unyenyekevu wa utamaduni
kama dhana sana hapo awali maishani mwangu.
Ilichipukia mahali pa kutoona, mahali pa kama
kukandamiza nafsi yangu kama mwanamke mweusi
na sasa imedilishwa kikamilifu, kama mkufunzi,
kutambua nilivyo, ninaposimama
darasani, ni nini hadhi yangu.
Na pia sauti yangu yamaanisha nini duniani
na inamaanisha nini kama mkufunzi.
Ilitokezea kwa kujaribu kutoshea, kufanya ninachoweza
kuwa mhindi nyumbani na siyo nje ulimwenguni.
Na bila kueleza, imekuwa kielelezo cha utambulisho
niliyojua ipo
ambayo singeweza kueleza nilipokuwa.
na sasa inasema huyo mtu ni nani
na kutambua nguvu na hadhi yangu
kujiangalia kwa njia fulani.
pia nasema kuwa mimi ni mwanamke wa rangi,
Niko na cha muhimu cha kusema na niko hapa.
Nadhani kuwa il mradi tupo na nguvu na hadhi
katika jamii tutapambana na kuwa wanyenyekevu sana
kama wanawake wa rangi, kama wanawake wanatoka
katika tabaka ya wafanyikazi, kama wanawake wanatoka
katika asili ya kulipwa mshahara mdogo
ama asili za mali finyu, sawa?
Il mradi kuna nguvu na hadhi
katika jamii, najua kuwa nitakuwa nikipambana nazo
na kupambana nazo kila siku.
[Muziki]
Nilichunguza {haisikiki] hapa
kuona jinsi sera zetu za sasa zinaunganisha
na kuratibisha zinalenga wanafunzi wenye jinsia isiyo asili.
Na nilikuwa nikitafakari
kuhusu jinsi inavyohusika
na mada ya jioni ya leo ya unyenyekevu kwa utamaduni
kwa sababu tunaongea kuhusu huntha.
au hulka za rika katika [haisikiki] na jinsi inavyoheshimiwa au la
>>Sawa.
na jinsi taasisi hii inaweza kuwa kufaa kitamaduni
au kunyenyekea ama kuheshimu wanaopitia huntha
wanapokuja hapa.
Wakufunzi wakiafya ninaofanya kazi nao
wote ni wanawake huntha.
Na haswa siku yangu ya pili kazini, niliingia kwenye mkutano,
na ilikuwa kamati ya bodi ya ushauri
ya wanawake wote huntha.
Ilikuwa ya kutatiza sana
lakini kwa wakati huo huo walinifanya nitulie.
Walianza kuniuliza maswali ni kama waliona , na kusema
kwa hivyo unatoka wapi?
Nikawajibu mimi ni mhajemi.
oh twajua huu msichana huntha kutoka mashariki ya kati,
unamjua?
Nikajibu, simjui
Kwa hivyo ufafanuzi wangu wa unyenyekevu wa utamaduni ni
kuwa tayari kujifunza kila wakati
Ninachowataka mfanye ni zunguka na kujitambulisha
na kutuambia unyenyekevu kwa utamaduni unamaanisha nini kwako.
Wakati wangu wa kwanza kuwa na shauku kuhusu unyenyekevu wa kitamaduni
ilikuwa nilipokuwa mwanafunzi wa shahada ya kwanza katika chuo kikuu.
nilikuwa kurutu katika shirika fulani.
Na walikuwa wakifanya mafunzo ya umahiri wa utamaduni
kwa jamii wakazi wa kisiwa cha Pasifiki na kufanya kazi
na jamii za wakazi wa visiwa vya Pasifiki
Na kama mwanamke wa ukoo mbili za kisiwa cha Pasiki.
Nilifurahi sana na pia na wasiwasi kuhudhuria mafunzo yale na kujifunza
kuhusu nyenzo ambayo ingeainishwa na kujadiliwa.
na jinsi mimi na wengine tungejifunza,
kuhusu mila za kisiwa cha pasifiki na kufanya kazi na wakazi wa huko
kuhusu mambo ya afya ambayo yalikuwa muhimu kwa jamii.
Nadhani baada ya kuhudhuria mafunzo niligundua kuwa
kulikuwa na hisia ya mafanikio na ukamilishaji
kwa wale ambao walishiriki
halafu nilitangulizwa kwa unyenyekevu wa kitamaduni
kama mwanafunzi wa shahada ya kwanza darasani,
ilifanyika wakati huo huo.
Na nikawa na hisia ya mafanikio na ufanikishaji
na umahiri na kuelewa mipaka ya kujielimisha.
Siwezi kukuambia kihakika maana ya unyenyekevu wa kitamaduni kwangu.
Nahisi kuwa naitenda na hivyo ndivyo naijua
Kitu moja ambayo naifikiria
au ninayoitenda ni unenyekevu wa kitamaduni ni
kihispania
kihispania
kihispania
kihispania
Kihispania
kuwa na asili ya kisayansi na kuja
katika afya ya kijamii bila kuwahi kusikia unyenyekevu wa kitamaduni
katika sayansi iliibua maswali
Kwa sababu utamaduni ni kitu kinacho sisitizwa,
siyo kitu kitu kinacho zungumzwa kwa njia inayofaa
Kumekuwa na vizuizi vinavyoonekana peupe
kwa jamii ya wachache katika sayansi.
Unaweza iona ukiwa katika madarasa ya sayansi.
Unaweza iona ukiwa katika makundi ya utafiti.
Unaweza iona ukimwangalia maprofesa wako.
nasiongelei tu jamii za wachache kwa kuzingatia ukoo au rangi
naongelea jamii za wachache ambao hawana uakilishi
katika sayansi, kwa mfano ukoo au rangi ni sababu
lakini jinsia na maumbil ya kijinsia siyo.
Nilijifunza kuhusu unyenyekevu wa kitamaduni sehemu mbili
kwa utamaduni wangu kuwa wa kikambodia na kusini mashariki mwa Asia
kutojua chochote kuihusu kulifanya nikejeliwe na jamaa zangu
kuhusu kutoongea vizuri.
halafu baada ya kuenda chuoni na kujifunza kuihusu
katika anthropolojia na kuhoji wazazi wangu
kuhusu uzoefu wao macho yangu yalifumbuka.
Mojawapo ya vitu ambayo nimejifunza katika
miaka kadhaa iliyopita nataka kusema ni kusikiza ninachokisema.
Na namaanisha kusikiliza kwa makini ninachokisema.
Na kitu ambacho nimejifunza kusikiliza ni
ninaposema mimi, Naamini hii, nafanya hii, na kusikiliza sasa
kuwa ni tofauti na sisi
Sisi nasikia sana katika habari, sisi Wamarekani, sawa?
kama sisi, ni nani 'sisi' anaongea kumhusu?
Ni kufikiria na kusikiliza tunapotumia mimi na sisi.
Nilipokuwa nakua nilipata hamu ya utamaduni
na dini nyinginezo na kujifunza tu kuhusu vitu
kutoka kwa asili nyinginezo.
Kwa hivyo nadhani hiyo ilinifanya kuwa mnenyekevu kitamaduni
kwa sababu nilikuwa na hamu
kwa hivyo baada ya kusoma kwa mwaka moja Afrika magharibi, nilirudi nikisema,
Eh Mungu wangu, sijui chochote, sijui chochote
kuhusu watu weusi, sijui chochote kuhusu Waafrika.
namaanisha ilibadilisha mtazamo wangu.
Amani. Nafikiria ninapoketi mahali pa unyenyekevu
kuwa kuwa utulivu na nafasi na kuwa sawa
na raha ambayo inakaribia amana ya kuwa
na mtu mwingine amabye naweza fikiria.
Kama lazima niifikirie
kama barabara basi ningeweza fikiria
kuhusu barabara inayopinda.
Na kama upinde hauwezi --kwangu kwa dhana ya kucheza
upinde unaoenda juu lazima uje chini pia
ina uendelevu
na katika uendelevu vitu vingi hufanyika
na nguvu za aina nyingi zinaweza badili umbo lake
au kina cha kinapoweza kufika.
Unyenyekevu wa utamaduni hakika ni safari kwangu
Unyenyekevu wa kitamaduni hakika ni safari kwangu,
Na ni safari ambayo najua kutakuwa na
changamoto na nipo ndani yazo.
Na ninajua kila changamoto nitakayo jifunza kwayo.
Na nadhani ni mchakato ambao lazima nipitie kila siku
na ambayo niko sawa kupitia.
Na hakika inanifanya kuwa na nguvu zaidi na uerevu zaidi
na natuhahi hekima zaidi kuliko nilivyokuwa jana.
[muziki]
muziki