-
Nchini India, wasichana milioni tatu
hawaendi shule.
-
Hiyo ni msichana mmoja kati ya watatu
wenye umri wa miaka 10 hadi 14.
-
Lakini 'Educate Girls' inabadilisha
hali hiyo.
-
Mtazamo uliokithiri ni
-
kwamba mbuzi yangu ni mali
na msichana wangu ni dhima.
-
Na inahusu tu kubadilisha mtazamo.
-
Jina langu ni Bhagwanti.
-
Kabla niende shule, lazima
nifanye kazi ya nyumbani:
-
kupika vyakula, kuosha,
kupeleka mbuzi malishoni.
-
Wakati mwingine nasafisha nyumba pia.
-
Kwanza, katika kila kijiji tunakoingia
-
tunapata mtu aliyejitolea wa jamii.
-
Watu wetu waliojitolea ni wachanga,
wamesoma na wana shauku.
-
Wenyewe wangependa kuona mabadiliko.
-
Wanakweda lango hadi lango, na wanapata
kila msichana ambaye haendi shuleni.
-
Kisha, wanaketi na jamii
-
na wanabuni mipango ya usajili
kulingana na jamii
-
ya kurudisha wasichana hawa shuleni.
-
Wanaojitolea au 'Balikas'
hufanya kazi na shule za vijiji...
-
ili kuhakikisha ziko salama
na zina vyoo vya wasichana.
-
Pia wanasaidia kuwafunza wasichana.
-
Kwa hivyo, kisha wanaojitolea
"Team Balika' huingia
-
katika darasa la shule ya serikali
-
na wanatoa mafunzo ya Hindi,
Kiigereza na Hesabu
-
ili kuhakikisha kuwa watoto wote -
wavulana na wasichana,
-
wanapata matokeo yanayohitajika ya elimu.
-
Inahusu kila msichana kuja shuleni.
-
Inahusu kila msichana
kuchangia katika dunia inayobadilika.
-
Inahusu kila msichana
kuchangia mabadiliko katika famili,
-
na inahusu kila msichana
kuchangia katika mabadiliko
-
katika jamii pana.
-
Tunazungumzia afya bora, mapato bora.
-
Tunazungumzia elimu bora,
kwa hivyo ni kwa kila mtoto.
-
Kuna takribani asilimia 50, 60 ya
wasichana huko Rajasthan ambao wameolewa
-
chini ya umri wa miaka 18.
-
Kote nchini, asilimia hiyo ya watoto
kuolewa iko juu sana.
-
Watoto wengi pia,
takribani asilimia 10 hadi 15
-
wameolewa chini ya umri wa miaka 10.
-
Niliozwa na wazazi wangu nikiwa
na miaka 14.
-
Nilikuwa mwanafunzi katika darasa la 8.
Wazazi wa mvulana walikuwa wamekubali
-
kuendeleza masomo yangu
lakini baada tu ya matokeo yangu kutoka
-
hawakutimiza ahadi yao.
-
Neelam ni mojawapo ya Balikas 10,000
katika Educated Girls.
-
Wamewasaidia watoto milioni mbili.
-
Ningependa kuwa mwalimu baada ya masomo
na niwafundishe wasichana wengine
-
kwa sababu ukipata elimu una ujasiri,
-
unaweza kujitegemea, kupata kazi
-
na kusaidia familia yako kifedha.
-
Kila mwaka wa ziada wa shule unaweza
kuzidisha mapato ya mwanamke kwa hadi 20%.
-
Katika miaka 10 iliyopita,
najivunia kusema tumewapata
-
na kuwarudisha shuleni wasichana 150,000
walioondoka shule
-
ambao sasa wameunganishwa na
wanahudhuria shule na kupata mafunzo.