Shikilia sana ujasiri wako katika Neno la Mungu
hata pale ambapo imani yako inapojaribiwa.
Awe ameniponya au la, Yeye ndiye Mponyaji wangu.
Ikiwa ataondoa hali hii au la,
Yeye ndiye Mwokozi wangu.
Iwe ameniokoa au la, Yeye ni Mwokozi wangu.
Atanirejesha au la, Yeye ndiye Mrejeshaji wangu.
Huu ni ujasiri wangu.
Sina mbadala mwingine.
Sina njia nyingine.
Nimemjaribu Mungu na kumwona kuwa ni wa kutumainika.
Nimemjaribu Mungu na kumuona anategemewa.
Nimemjaribu Mungu na kugundua kuwa ni kweli, anastahili.