Mwili wangu ulikuwa ukitetemeka. Sikuweza kujizuia. Sikujua nini kilikuwa kinatokea. Nilijikuta tu sakafuni. Katika jina kuu la Yesu Kristo. Zungumza! Wewe ni nani? Wewe ni nani? Zungumza sasa hivi! Umemfanya nini? Nimempa maumivu mgongoni mwake. Sawa, wewe ndiye uliyesababisha ugonjwa mgongoni mwake? Ndiyo, mimi ndiye. Wewe ni nani katika mwili huu uliyesababisha ugonjwa huu? Ninatoka upande wa baba. Sitaki afanikiwe. Kwa hivyo sasa hivi, wakati wako katika mwili huu umefika mwisho. Ulimuingizaje? Jinsi gani? Niliingia kwake kupitia ndoto. Kwa hivyo sasa hivi, wewe pepo mwovu, katika jina kuu la Yesu Kristo - toka! Toka, kwa jina la Yesu! Inuka dada yetu huko Zambia. Uko huru kutoka kwenye roho hiyo chafu. Inuka na ujiangalie mwenyewe kwa utukufu wa Mungu. Amina. Asante, Yesu. niko huru. Asante, Yesu. Dada yangu, unakaribishwa sana katika jina kuu la Bwana wetu Yesu Kristo. Tafadhali, unaweza kutuambia jina lako, unaishi wapi na utushirikishe ushuhuda wako? Jina langu ni Linda, ninatoka Zambia. Nilikuwa nikisumbuliwa na mgongo kwa karibu miaka miwili. Maumivu ya mgongo yaliendelea kuwa mabaya zaidi na zaidi. Niliamua kwenda hospitali mbalimbali kutafuta usaidizi. Nilipendekezwa kupitia mfululizo wa huduma ya tiba ya kimwili, ambayo nilifanya, lakini maumivu yaliendelea. Madaktari walipendekeza niendelee, lakini maumivu bado yaliendelea. Madaktari hatimaye walipendekeza nichukue skana ya MRI lakini sikukubaliana nao. Maumivu ya mgongo yalinizuia kufanya mambo mengi. Mimi ni mwalimu kwa taaluma, hivyo ualimu ukawa mgumu sana kwangu. Kwa sababu sikuweza kuinama au kukaa kwa muda mrefu. Sikuweza kusimama kwa muda mrefu. Sikuweza kufundisha kwa ufanisi kama nilivyokuwa kabla ya kuumwa na mgongo huu. Hata kuokota tu kitu kutoka sakafuni ilikuwa ngumu sana kwangu. Ningesikia uchungu mwingi. Nafasi pekee ambayo ningestarehe nayo, ilikuwa kulala chali tu. Sikuweza kuketi kama jinsi ninavyokaa sasa hivi. Ilikuwa ngumu sana kwangu. Nilihisi maumivu ndani ya kifua changu na sehemu ya kati ya mgongo wangu pia. Kwa kweli iliniathiri sana. Niliamua kuwasiliana na TV ya Moyo wa Mungu kwa sababu niliona jinsi watu katika hali kama zangu walivyoponywa. Baada ya kuwasiliana na TV ya Moyo wa Mungu, Nilialikwa kujiunga na Ibada Shirikishi ya Maombi pamoja na Ndugu Chris, tarehe 21 Oktoba 2023. Wakati wa Ibada Sihirikishi ya Maombi, Nilianza kuomba na kumwomba Mungu anirehemu. Mtu wa Mungu Ndugu Chris alipokuwa akihubiri Neno, Nilihisi joto kali mwili mzima. Alipotuomba tusimame tuombe, nilipoinuka, mwili wangu ulikuwa ukitetemeka. Sikuweza kujizuia. Sikujua kilichokuwa kikitendeka - nilijipata tu sakafuni. Nguvu za Mungu zilijaza chumba nilichokuwamo. Nilianguka chini kwa uwezo wa Mungu. Nilipoinuka, niligundua kwamba maumivu yote niliyokuwa nayo kwenye uti wa mgongo wangu upande wa kulia wa mgongo wangu yalikuwa yametoweka. Nilijaribu kujinyoosha chini ili kupata kitu kwenye sakafu. Niliweza kukichukua kwa urahisi bila maumivu yoyote. Wakati nilipokuwa nikipata maumivu ya mgongo, Sikuweza hata kuvaa visigino au kuhudhuria mikutano mirefu. Madaktari waliniambia kwamba nilipaswa kufanya kazi kwa saa chache tu kwa sababu nilihitaji muda zaidi wa kupumzika. Lakini baada ya Ibada Shirikishi ya Maombi, nimerejea kwenye majukumu yangu ya kawaida. Ninaweza kufanya kazi masaa ya kawaida. Ninaweza kunyoosha, kupinda na kufanya mambo yote ambayo sikuweza kufanya. Kwa hiyo namshukuru Mungu kwamba nilipokea uponyaji wangu. Ninaweza kuinama kwa uhuru na kurudi juu. Ninaweza kuegemea pande zote mbili na nyuma. Hakuna uchungu. Maumivu yameisha kabisa. Namshukuru Mungu! Tunamshukuru Mungu. Je, kuna ushauri wowote ambao ungependa kuwapa watazamaji wetu? Ushauri wangu ni kwamba wakati unakabiliwa na hali ngumu tofauti, Ninataka kukuhimiza kumewndea Mungu. Anaweza kufanya lolote. Kila kitu kwake kinawezekana. Hata unapojiunga na Huduma hii Shirikishi ya Maombi na Ndugu Chris, amini kwamba Mungu atagusa maisha yako - Mungu anakwenda kukuponya. Mungu anaweza kubadilisha hali yoyote kwa sababu Anaweza kulitenda hilo. Kwa hivyo ninataka kukuhimiza kuamini na kumtumaini Mungu. Mungu anaweza kukutendea. Amina!