Hebu tufanye maswali ya kugawanya. Tunachukua 280 na tunaigawanya kwa 5. Ninakushauri usimamishe video na ujaribu kutumia njia tulizojifunza mwanzo kujua 280 gawanya kwa 5 ni ngapi. Tuanze. Tunaweza kuandika tena. Tumeshaona ni 280 gawanya kwa 5. Swali la kwanza kujiuliza ni 5 inaingia kwa 2 mara ngapi? 5 haingii kwa 2. Inaingia mara 0. 0 mara 5 ni 0. Na kisha tunatoa. 2 kutoa 0 ni 2. Na sasa, tunaweza kushusha tarakimu inayofuata, ambayo katika mfano huu ni 8. Ni mara ngapi 5 inaingia kwa 28 bila kuzidi? Tunaweza kufikiria, 5 mara 5 ni 25. 5 mara 6 ni 330 5 mara 6 itazidi 28. Kwa hiyo tunarudi kwa 5 mara 5. Kwa hiyo 5 inaingia kwa 28 mara 5. 5 mara 5 ni 25 Na unatoa. 28 kutoa 25 ni 3 Na sasa, tushushe tarakimu inayofuata. Kwenye mfano huu, ni 0. Kwa hiyo mara ngapi tano inaingia kwa 30? Inaingia mara 6 Tulishafanya hii 6 mara 5 ni 30. Tunatoa. Na hatuna kilichobaki. Kwa hiyo tumepata 280 gawanya kwa 5 ni sawa na 56. Sasa, kwa nini njia hii imetupa jibu sahihi? Njia ya kwanza ya kufikiria hili, tuna 200 kwenye sehemu ya mamia Njia moja ya kufikiria hili ni, ni mara mia ngapi 5 inaingia kwa 200? Na haingii kwa 100. Na kama hii inachanganya, usiogope. Lakini unatakiwa kufikitia kuhusu nafasi. Lakini tumeweza kuongeza, badala ya 200 tuna 280. Hii ni 28 hapa, kama utafikiria hii 2 ipo nafasi ya mamia. Hii 8 ipo nafasi ya makumi. Kwa hiyo hii inawakilisha 280. Na tulisema ni mara kumi ngapi 5 inaingia kwa 280? Inaenda mara kumi 5, au inaenda mara 50. 50 mara 5 ni 250. Ukitoa 250 kutoka 280, unapata 30. Na hakuna chochote kwenye sehemu ya momoja Kwa hiyo tunatafuta ni mara ngapi 5 inaingia kwa 30. Natumaini, hii imekupa maana ya kianchoendelea kwenye tendo la kugawanya. Sio maajabu. Tunaangalia thamani za namba tu. Kitu kingine ninachotaka kukuonyesha ni kwamba haikuwa na ulazima wa kuiandika hii 0 hapa. Njia nyingine ya kufanya, tungesma 280 gawanya kwa 5 Na tungesema ni mara ngapi 5 inaingia kwa 2. Hapa haingii mara zozote. Kwa hiyo tunafikiria 5 inaingia kwa 28. 5 inaingia kwa 28 mara 5 5 mara 5 ni 25. Toa 28 toa 25 ni 3 Shusha 0 5 inaingia kwa 30 mara 6 6 mara 5 ni 30 Na hatuna kilichabaki. Na tena, tunasema 5 haingii kwa 200 mara mia zozote. Kama hii ingekuwa 500, ungesema inaingia mara 100. Lakini badala yake, tumesema 5 inaingia mara ngapi kwa 280? Inaingia mara 50 50 mara 5 ni 250. 280 mara 250 ni 30 5 inaingia kwa 30 mara sita. Natumaini, hii imeleta maana.