Nachotaka kuongea kwenye video hii.
ni maumbo yenye pande nne,
na jina la kihisabati la maumbo hayo
ni pembenne.
pembenne.
Kila unapoona neno pande nne,
ni vema ukajua
zinahusu namba nne.
Kwa hiyo pembenne ina pande nne.
hiyo ni pembenne,
hii ni pembenne,
hii ni pembenne
Yote yana pande nne.
Hii ni pembenne.
hata hii ni,
ngoja niiongezee upana kidogo,
hii nayo ni pembenne.
Je ipi sio pembenne?
Pembetatu sio pembenne.
Ina pande tatu,
1, 2, 3.
Hivyo tuiondoe.
Pembetano ina pande tano,
hii sio pembenne.
Ina pande 1, 2, 3, 4, 5.
Duara tunasema halina pande,
ni mduara tu.
Hii sio pembenne.
Kama una pande sita, pande saba, pande miamoja,
zote hizo sio pembe nne.
Hebu tuangalie
aina mbalimbali za pembenne,
au makundi tofauti ya pembenne.
Ya kwanza ni msambamaba.
Kwahiyo msambamba ni pembenne,
na tunavyozidi kujifunza,
tunagundua njia nyingine za kuyafanya haya,
Ni pembenne ambapo pande zinazoelekeana ni sambamba.
Na sambamba ni njia nyingine ya kusema
zina muelekeo mmoja.
Nina maana gani hapo?
Kitu kama hiki,
ninachora,
ni msambamba.
kwanini?
Kwasababu upande huu unaangaliana na huu.
na zina uelekeo mmoja.
Zinakwenda,
kama nikichora mshale
nikichora mshale hapa,
hii mishale ina uelekeo mmoja,
kwahiyo hizo pande mbili
zinaelekeana.
Na hizi pande mbili,
pande mbili hapa zinaelekeana.
Hivyo huu ni msambamba.
Mfano mwingine wa msambamba ni upi?
Hata mraba ni msambamba,
mraba,
ni msambamba.
Na tutaonesha nini kinafanya mraba kuwa msambamba.
ni msambamba maalumu
kwasababu upande huu
unaelekeana na upande huu,
na upande huu hivyo hivyo na upande huu hivyo hivyo,
nitachora kwa rangi ya njano,
na upande huu ni sambamba na huo,
Je umbo lipi si msambamba?
Kitu kama hiki,
huu mchoro
hatusemi ni msambamba.
Unaweza sema "subiri,
"ninaona pande zinazoelekeana ni sambamba".
Unaweza sema, tazama huu ni sambamba na huu
lakini huu si sambamba na huu.
Njia ingine ya kutambua kuwa huu si msambamba ni
kama mistari inaendelea,
ikakutana mahali fulani,
wakati hii mistari,
hapa,
haiwezi kukutana.
Hivyo huu hapa
sio msambamba.
Ina mistari sambamba inayoelekeana,
ila sio mingine.
Mfano mwingine wa umbo ambalo si msambamba
utakuwa huu hapa,
kwasababu pande zinazoshabihiana si sambamba.
Hivyo msambamba, pande zinazoshabihiana ni sambamba.
Sasa tuzungumzie,
aina nyingine za pembe zenye pande nne,
au pembenne.
Nyingine ni msambamba sawa.
Hivyo msambamba sawa ni aina ya msambamba.
Pande mbili zinashabihiana,
Yenyewe kama yenyewe si msambamba
Pande zinazoshabihiana zinatakiwa ziwe sambamba,
na pande zote ziwe sawa.
Kwa mfano,
Nachora,
huu ni msambamba, ila si msambamba sawa.
Ni msambamba kwasababu upande ule,
hizi pande zinazoshabihiana ni sambamba.
Na zikiendelea hazikutani.
Na pande hizi ni sambamba.
Hivyo ni msambamba ila si msambamba sawa
kwasababu pande za bluu ni ndefu kuliko za njano.
hivyo huu si msambamba sawa.
Msambamba sawa unaonekana hivi.
Utaonekana hivi.
Hivyo pande zinazoshabihiana ni sambamba
na pande zote zina urefu sawa.
Na unaweza sema "mraba ni msambamba,"
na unataka kujua.
Je mraba ni msambamba?
Je pande zote zina urefu sawa,
na zinashabihiana?
Tumeshasema pande
za mraba ni sambamba.
Mraba ni msambamba.
Na pande zote za mraba zinalingana.
Hivyo mraba ni msambamba sawa.
Hivyo namna nyingine ya kuujua msambamba sawa
una mraba,
na unaweza sema ni
aina ya mraba uliominywa,
wakati ukitembea
haraka haraka kama kwenye katuni,
ndivyo huwa ninaifananisha hivyo kila nikiufikiria msambamba sawa
Sasa tuangalie mstatili.
na umeshalisikia neno mstatili nyuma,
tuutazame zaidi
nini kinatengeneza mstatili,
Hivyo mstatili utakuwa ni msambamba,
pekeyake hausemi mstatili.
Kwamfano, huu hapa ni mstatili.
kwanini?
Ni msambamba
upande huu na upande huu ni sambamba.
Haiwezi kukutana.
Na upande huu na huu unashabihiana.
Na haziwezi kukutana.
ukiendelea na kuendelea
haziwezi kukutana.
Je nini inafanya mstatili?
Hivyo huu ni msambamba,
lakini kwanini tunatumia neno mstatili?
Chakufanya ni kuangalia
namna mistari inavyokutana kwenye kona.
Hivyo kwenye mstatili,
pale mistari inapokutana,
inaitwa pembemraba.
Hii hapa ni pembemraba.
hii ndio ndio inafanya mstatili.
Ni msambamba ambapo pembe zote ni mraba.
Unaweka kimraba kidogo pale.
kama unataka kuifanya hivyo.
Kwamfano hapa
huu sio mstatili.
Kwanini?
Kwasababu ukiweka mraba hapa
hautoshi
kama ulivyotosha hapa.
Una mraba usiotosha kukaa hapa
Huu ni msambamba, ila sio mstatili.
Mstatili ni msambamba wenye mraba.
Je vipi kuhusu mraba?
Je mraba ni mstatili?
Tuchore.
hebu tutazame.
Mraba pembe zinazoshabihiana ni sambamba.
Tulishasema ni msambamba.
Na mraba una,
pembemraba.
Hapa ndio tunasema tengeneza pembemraba,
hivi ndio unavyopatikana.
Pembe ni mraba.
Ni pembe mraba
Hivyo mraba ni mstatili.
Hivyo mraba ni msambamba wa kuvutia,
kwasababu mraba unaingia kwenye makundi yote.
Mraba, ni mraba,
ni msambambasawa
ni aina ya msambamba sawa
ambapo pande zake ni pembemraba
au unaweza sema pembemraba.
Hii hapa sio mraba,
hii hapa ni mraba.
Zote ni msambambasawa
Mraba pia ni mstatili.
Ni msambamba ambapo pande zake ni pembemraba,
mraba
Hivyo mraba ni msambamba,
na yote tulivyozungumza ni msambamba