Polio ni ugonjwa unaosababisha kupooza ya kudumu. Hatuwezi kuiponya lakini tunaweza kuizuia. Taratibu mbili zinasaidia kuzuia polio. Chanjo mbili salama na fanisi Mojawapo ya chanjo hizi hupeanwa na matone mawili tu ndani ya kinywa cha mtoto, hii huitwa chanjo ya polio ya kinywani. nyingine hupeanwa kama shindano, hii huitwa chanjo ya virusi vya polio visivyoamilishwa. Zote zinafunza miili ya watoto kupambana na virusi vya Polio. Lakini vinafanya hivi kwa njia mbalimbali. Chanjo ya polio ya kinywani hujenga ulinzi ndani ya matumbo ya mtoto Chanjo hii hailindi tu mtoto anayeipokea, bali pia na wale walio karibu na mtoto aliyechanjwa Dozi kadhaa ya chanjo ya polio ya kinywani inafaa kupewa kila mtoto katika eneo ambayo polio ni tishio. Chanjo ya shindano inajenga kinga damuni badala ya mfereji wa chakula. Inasaidia kuongeza kinga na kufanya nchi ziwe bila polio. Lakini haikomeshi kusambaa kwa polio kati ya watoto, kwa hivyo si muhimu sana katika maeneo ambayo polio bado inasambaa. Tunahitaji chanjo ya kinywani kukomesha virusi popote ipatikanapo. Pindi polio inapokomeshwa kila pahali, chanjo ya virusi vya polio visiyoamilishwa vitatumiwa pekee yao kuhakikisha umma imekingwa. Chanjo hizi zote zimeidhinishwa kuwa salama na fanisi na Shirika la Afya Ulimwenguni. Kuhakikisha utendakazi bora, zinaafaa kupewa watoto wote bila kujali wanapoishi. Kwa sababu ya hizi chanjo visa vya polio vimepungua kwa asilimia 99 kote duniani. Tuchanje kila mtoto! Tuangamimize polio damia!