1 00:00:00,490 --> 00:00:03,340 Polio ni ugonjwa unaosababisha kupooza ya kudumu. 2 00:00:05,414 --> 00:00:07,908 Hatuwezi kuiponya lakini tunaweza kuizuia. 3 00:00:08,520 --> 00:00:10,800 Taratibu mbili zinasaidia kuzuia polio. 4 00:00:11,352 --> 00:00:13,242 Chanjo mbili salama na fanisi 5 00:00:15,069 --> 00:00:17,919 Mojawapo ya chanjo hizi hupeanwa na matone mawili tu 6 00:00:17,919 --> 00:00:19,660 ndani ya kinywa cha mtoto, 7 00:00:19,660 --> 00:00:21,594 hii huitwa chanjo ya polio ya kinywani. 8 00:00:22,529 --> 00:00:24,499 nyingine hupeanwa kama shindano, 9 00:00:24,499 --> 00:00:27,959 hii huitwa chanjo ya virusi vya polio visivyoamilishwa. 10 00:00:28,012 --> 00:00:31,692 Zote zinafunza miili ya watoto kupambana na virusi vya Polio. 11 00:00:32,093 --> 00:00:34,253 Lakini vinafanya hivi kwa njia mbalimbali. 12 00:00:34,765 --> 00:00:38,755 Chanjo ya polio ya kinywani hujenga ulinzi ndani ya matumbo ya mtoto 13 00:00:39,097 --> 00:00:41,947 Chanjo hii hailindi tu mtoto anayeipokea, 14 00:00:42,321 --> 00:00:45,221 bali pia na wale walio karibu na mtoto aliyechanjwa 15 00:00:45,600 --> 00:00:50,200 Dozi kadhaa ya chanjo ya polio ya kinywani inafaa kupewa kila mtoto 16 00:00:50,200 --> 00:00:52,503 katika eneo ambayo polio ni tishio. 17 00:00:53,323 --> 00:00:57,506 Chanjo ya shindano inajenga kinga damuni badala ya mfereji wa chakula. 18 00:00:57,712 --> 00:01:01,782 Inasaidia kuongeza kinga na kufanya nchi ziwe bila polio. 19 00:01:02,497 --> 00:01:05,077 Lakini haikomeshi kusambaa kwa polio kati ya watoto, 20 00:01:05,471 --> 00:01:09,331 kwa hivyo si muhimu sana katika maeneo ambayo polio bado inasambaa. 21 00:01:09,767 --> 00:01:14,187 Tunahitaji chanjo ya kinywani kukomesha virusi popote ipatikanapo. 22 00:01:14,778 --> 00:01:17,258 Pindi polio inapokomeshwa kila pahali, 23 00:01:17,258 --> 00:01:20,391 chanjo ya virusi vya polio visiyoamilishwa vitatumiwa pekee yao 24 00:01:20,391 --> 00:01:22,764 kuhakikisha umma imekingwa. 25 00:01:23,578 --> 00:01:27,308 Chanjo hizi zote zimeidhinishwa kuwa salama na fanisi 26 00:01:27,308 --> 00:01:29,258 na Shirika la Afya Ulimwenguni. 27 00:01:29,565 --> 00:01:33,232 Kuhakikisha utendakazi bora, zinaafaa kupewa watoto wote 28 00:01:33,232 --> 00:01:35,142 bila kujali wanapoishi. 29 00:01:35,970 --> 00:01:37,710 Kwa sababu ya hizi chanjo 30 00:01:37,710 --> 00:01:42,056 visa vya polio vimepungua kwa asilimia 99 kote duniani. 31 00:01:44,820 --> 00:01:47,520 Tuchanje kila mtoto! 32 00:01:47,940 --> 00:01:49,770 Tuangamimize polio damia!