Nina piza nzima hapa, na tuchukulie
kwamba ninatakiwa niikate kwenye vipande viwili vilivyo sawa.
Naikata hapa vipande viwili vilivyo sawa.
Na tuseme nimekula moja ya vipande 2 sawa.
Tuchukulie nimekula sehemu hii hapa.
Je, ni sehemu gani ya piza niliyokula?
Nimechukua nzima na kuigawanya
vipande viwili vilivyo sawa, kisha nikala moja ya vipande hivyo.
Hivyo nilikula nusu ya piza.
Hebu tuchukulie kwamba, badala ya kukata piza kwenye
vipande 2 sawa, tuchukulie
kwamba tumeikata kwenye vipande 4 vilivyosawa.
Hebu tuchore.
Kwa hiyo vipande 4 vilivyo sawa.
Kwa hiyo nitakata mara moja namna hii na kisha,
nitakata mara moja kama hivi.
Hivyo nina vipande 4 vilivyo sawa.
Lakini ninataka kula kiasi kilekile cha piza.
Je, nitakula vipande vingapi kati ya hivi vipande 4 sawa?
Ninakushauri usimamishe video na kufikiria.
Nitakula kula kipande hiki.
Chukulia nitakula kipande hiki na kipande hiki
hapa.
Nimekula sehemu ileile ya piza.
Kila moja ya vipande hivi imekatwa katika sehemu mbili
nilipokata piza namna hii.
Hivyo natakiwa nile vipande 2 kati ya 4,
tofauti na kipande 1 kati ya 2.
Kwa hiyo nimekula vipande 2 kati ya 4
Natumia namba tofauti hapa.
Hapa natumia 1 kwenye kiasi
na 2 kwenye asili.
Hapa, natumia 2 kwenye kiasi
na 4 kwenye asili.
Hizi sehemu mbili zinawakilisha kitu kile kile.
Nimekula kiasi kilekile cha piza.
Kama nimekula 2/4 ya piza, kama nimekula vipande 2 kati ya 4,
hiyo ni sehemu ileile ya piza
kama nimekula kipande 1 kati ya 2.
Kwa hiyo tunaweza kusema hizi mbili
ni sehemu sawa.
Hebu tufanye mfano mwingine.
Badala ya kugawanya katika vipande 4 vilivyo sawa,
hebu nigawanye katika vipande 8 vilivyo sawa.
Kwa hiyo sasa tutakata mara moja kama hivi.
Sasa tuna vipande viwili vilivyo sawa.
Kata mara moja kama hivi.
Sasa tuna vipande vinne vilivyo sawa.
Halafu gawanya kila moja ya hivyo vipande 4 kuwa vipande 2.
Kwa hiyo kata--
Nataka kupata vipande sawa.
Hivyo havionekani sawa kama ninavyotaka
Hivyo vinaonekana sawa.
Hivyo nina vipande vingapi vilivyosawa?
Nina vipande 8 sawa.
Tuchukulie ninataka kula sehemu ileile ya piza.
Kwa hiyo nitakula vipande vyote hivi hapa.
Vipande vingapi kati ya hivyo vipande sawa 8 nimekula?
Nimekula 1, 2, 3, 4 ya vipande sawa 8.
Kwa mara nyingine, sehemu hii, 4 ya 8 au 4/8,
ni sawa 2/4, ambayo ni sawa na 1/2.
Na unaweza kuona mpangilio hapa.
Kutoka kwenye umbo hili kwenda kwenye umbo hili,
ninapata mara mbili ya vipande sawa.
Kwa sababu nina mara mbili ya vipande sawa
Ninatakiwa kula mara mbili ya idadi ya viapnde.
Kwa hiyo nazidisha asili kwa 2,
na nazidisha kiasi kwa mbili
Kama nikizidisha kiasi na asili
kawa namba ileile, sibadilishi
kinachowakiliswa na sehemu.
Na unaweza kuona hapa.
Kutoka vipande 4 kwenda vipande 8, nimekata kila kipande,
nimebadilisha kila kipande kuwa vipande viwili
kwa hiyo nina mara mbili ya vipande.
Na nikitaka kula kiasi kile kile,
ninatakiwa kula mara mbili ya vipande.
Kwa hiyo zote hizi 1/2, 2/4, 4/8 na ninaweza kuendelea.
Ninaweza kufanya 8/16.
Ninaweza kufanya 16/32.
Zote hizi zitakuwa sehemu sawa.