Nilikuwa na miaka 10 katika tukiwa safari ya kambi na baba yangu Katika milima ya Adirondack, eneo la nyika Kaskazini mwa jimbo la New York. Ilikuwa ni siku nzuri sana. Msitu ulikuwa unang'aa. Jua lilifanya majani yawake kama kioo, na kama si kwa njia tuliyofuata, tungejifanya kama wanadamu wa kwanza kupita eneo lile. tukafika katka eneo letu la kufanyia kambi. ilikuwa ni eneo linalotazama ziwa zuri sana, nilipogundua kitu kibaya. nyuma ya eneo hilo kulikuwa na dampo kama futi za mraba 40 likiwa na matufaa yaliyooza na makaratasi ya madini ya aluminium na vitu vilivyokufa, nilishangazwa sana, niliingiwa na hasira, na kuchanganyikiwa pia. Wapiga kambi wazembe walioshindwa kuchukua vile walivyokuja navyo, walifikiri ni nani atakayesafisha kama si wao? Swali hili lilikaa ndani yangu, lilirahisishwa kidogo. nani atakayesafisha baada yetu? vyovyote utakavyofanya au popote utakapotuweka, nani takayesafisha baada yetu Instanbul? nani takayesafisha baada yetu Rio? au Paris na London? Hapa New York, Idara ya Usafi wa mazingira inasafisha baada yetu, kiasi cha tani 11,000 za uchafu na tani 2000 za uchafu wa kuchakatwa kila siku. nilitaka niwajue kama watu binafsi. nilitaka kujua nani anyefanya kazi hii. inakuwaje kuvaa sare na kuchukua mzigo huo? kwa hiyo nikaazisha utafiti nao. nilipanda magari yao na nikaanza kuzunguka nao nikawahoji watu katika ofisi na maeneo mengine kila sehemu ya mji, nilijifunza mengi, lakini bado nilikuwa mtu wa nje tu. nilitaka kujua zaidi. kwa hiyo niomba kazi ya usafi wa mazingira. sikupanda tu magari tena. bali niliyaendesha. nikatumia mafagio ya kwenye magari na nikawa nakusanya barafu. ilikuwa ni neema ya ajabu na elimu moja ya ajabu sana. kila mtu anauliza juu ya harufu. ipo,lakini si kama kali unavyofikiri, na katika siku ambazo inakuwa kali sana, unaizoe mara moja. uzito unachukua muda kuuzoea. Niliwafahamu watu waliokuwa katika kazi miaka kadhaa ambao miili yao ilikuwa inaendelea kuzoea mzigo huo katika miili yao tani za uchafu kila wiki. halafu pia kuna hatari. Kulingana na idara ya takwimu za kazi, Kazi ya usafi wa mazingira ni moja kati ya kazi 10 za hatari sana Katika nchi, na nilijifunza kwa nini. Uko katika foleni kila siku, inakuzunguka wanataka kukupita, kwa hiyo madereva hawajali. hii ni mbaya sana kwa mfanyakazi. na uchafu wenyewe umejaa sumu nyingi ambao unaruka nje ya gari na kusababisha madhara. nikajifunza pia uking'ang'ani wa taka unapushuka na kuuangalia mji kutokea kwenye gari la taka, unaelewa kuwa taka ni kama nguvu ya asili. haiachi kuja. na pia ni kama aina ya upumuaji au mzunguko. lazima iwe katika mwendo wakati wote. halafu tena kuna unyanyapaa. unavaa sare , unakuwa kama hauonekani mpaka mtu anapokasirishwa na kwa sababu kama umezuia magari kwa kutumia gari lako, au umepumzika karibu sana na nyumba yake, au unakunywa kahawa katika sehemu yao ya kulia chakula, watakuja na kukushutumu, na kukwambia hawatak kukuona karibu yao. unyanyapaa huu naona unashangaza sana, kwa sababu naamini kuwa wafanyakazi wa usafi wa mazingira ni wafanyakazi muhimu sana katika mitaa ya mji, kwa sababu tatu. wao ndio walinzi wa kwanza wa afya ya jamii. kama hawakusanyi taka kwa ufanisi na usahihi kila siku, zinaanza kutoka katika sehemu zilizotunzwa na madhara yake yanatutishia wote katika ya halisi kabisa. magonjwa tuliyoyadhibiti kwa miaka mingi yanaibuka tena na kutudhuru. Uchumi unahitaji wanyakazi hawa. Kama hatuwezi kutupa vitu vya zamani, hakuwezi kukawa na nafasi ya vitu vipya, kwa hiyo injini za uchumi zinashindwa kuendelea kwa kuwa hakuna matumizi Sipigii debe ubepari,lakini najaribu kuonyesha uhusiano uliopo. Lakini pia kuna kile nachoita na mwendo wa wastani wetu Na hii namaanisha ni haraka kiasi gani tumezoea kwenda katika siku hizi za sasa. Hatujali ,marekebisho,safi tulichochukua katika kikombe cha kahawa, chupa yetu ya maji. Tunatumia,tunatupa,tunazisahau, Kwa sababu tunajua kuna wafanyakazi upande wa pili wataochukua wote. Sasa nataka nitoe mapendekezo ya kufikiria kuhusu usafi ambayo yatapunguza unyanyapaa na kuwaingiza katika mazungumzo haya ya jinsi ya kuwa na mji unaokua kistaarabu. Kazi yao ni ile inayojirudia rudia. wako mitaani kila siku, Wakiwa na sare zao katika miji mingi Unajua wakati gani wa kuwategemea. Kazi yao inasabisha sisi pia tufanye kazi. Ni kama uhakikisho Ambao unaendelea kutufanya tuwe salama, mbali na uchafu wetu wenyewe na hali lazima iendelezwe kila wakati bila kujali chochote. Siku ya Septemba 11, 2001, Na nilisikia muungurumo wa gari la usafi mtaani, nikamchukua mwanangu mchanga na kukimbilia chini kulikuwa na mtu ambaye alikuwa anachakata karatasi kama afanyavyo kila Jumatano. Na nikawa najaribu kumshukuru kwa kazi yake katika siku hii, lakini nikaanza kulia. akaniangalia, akatingisha kichwa,akisema, "Tutakuwa salama. "Tutakuwa salama." Ilikuwa ni baadae nilipoanza utafiti wangu wa usafi wa mazingira, nikakutana na mtu yule tena. Jina lake ni Paulie,tulifanya kazi pamoja mara nyingi, tulikuwa marafiki wazuri. Nataka kuamini Paulie alikuwa sahihi. Kwamba tutakuwa salama. lakini katika jitahidi zetu za kutengeneza jinsi kama viumbe tutakavyoendelea kuishi katika dunia hii, lazima tuunganishe na kuangalia gharama zote, ikiwemo gharama za kazi. pia tutakuwa na taarifa za kuwafikia watu wanaofanya kazi hizo na kupata utaalam wao jinsi tunavyofikiri kuhusu, kutengeneza mifumo endelevu ambayo inatuchukua kutoka katika uchakataji, ambao ni mafanikio makubwa katika miaka 40, Katika nchi yote ya Marekani, na nchi mbalimbali duniani kote, na kutupeleka juu zaidi ambako tutaangalia aina nyingine za uchafu ambazo zinaweza zikapunguzwa kutoka viwandani. uchafu katika miji, jinsi tunavyofikiri tunapoongelea uchafu, unakaribia asilimia tatu ya uchafu wote katika taifa ni takwimu za kushangaza. katika siku zako, katika maisha yako, utakapomwona mtu ambaye kazi yake ni kufanya usafi, chukua muda kuwatambua. chukua muda wako kuwashukuru. (Makofi)