Hebu tufanye baadhi ya maswali
kwenye mazoezi ya shule ya Khan ambayo yatatufanya
tuandike upya hesabu za kujumlisha ili
tuweze kufanya ziwe kwenye namba za kukaribisha.
Namba ambazo zinaweza kuwa vigawe vya 10 au vigawe vya 100
Ngoja tuone, nina 63 jumlisha 427,
na hii inaonekana kama ngumu, unajua,
nahisi kama natakiwa kuandika ili kueleweka,
lakini labda natakiwa kuchukua kutoka kwenye namba moja,
na kuipa namba nyingine ili zote
ziwe namba zilizokaribishwa, ni wazi
kwamba 63, nikitoa tatu nitapata 60,
na kama nitaipeleka hiyo tatu kwenye 427,
itakuwa 430, na 60 jumlisha 430
ni hesabu rahisi zaidi.
Hebu tuone swali linauliza nini.
Hebu tufuatilie hatua kwa hatua jinsi ya kulifanya.
Swali linauliza 63 jumlisha 427 ni sawa
na 60 jumlisha ngapi jumlisha 427.
Kwa hiyo 60 jumlisha ngapi, hii ni
sawa na 63, kwa sababu tuna
427 sehemu zote, kwa hiyo 63 ni 60 jumlisha tatu.
Hiyo inaleta maana.
Katika hatua inayofuata, wamebadilisha mpangilio
60 jumlisha tatu, na halafu ongeza 427
ni sawa na kufanya 60 jumlisha
na halafu ujumlishe tatu kwa 427 kwanza.
Kwa hiyo tunaichukua hii tatu
na kuihamisha kutoka kwa 63 kwenda kwa 427.
Tatu jumlisha 427, hiyo ni sawa na 430.
Na sasa hii hesabu ya kujumlisha imekuwa rahisi zaidi.
60 jumlisha 430, tunaweza kufanya kwenye vichwa vyetu.
Tanaongeza makumi sita kweye hii,
kwa hiyo itakuwa 490, na tumemaliza.
Hebu tufanye mifano zaidi ya hii.
Kwa hiyo, hapa, tunataka
kujumlisha hizi namba mbili,
na ngoja tuone kama
tunaweza kuzikaribisha.
Kwa hiyo hapa, tunazivunja
275 kwenye 270 na ziada.
Hii itakuwa 270 jumlisha tano.
Angalia namba nyingine bado iko vile vile,
jumlisha 297.
Sasa, kwa nini tunafanya hivyo?
Tukichukua 5 kutoka kwenye 275 na kuipeleka kwenye 595,
ambacho ndicho tunachokifanya hapa,
595 itakuwa 600.
Itafanya swali liwe rahisi
Kwa hiyo, kwa mara nyingine, hapa tunajumlisha
270 na tano kwanza, na halafu tunaongeza 595,
lakini tunaweza kubadilisha mpangilio wa tunavyofanya.
Tunaweza kujumlisha tano kwa 595 kwanza,
na halafu tujumlishe 270.
Hii ni sawa na 270 jumlisha,
tano jumlisha 595 ni 600, na sababu
kwa nini tumechukua tano kutoka kwenye 270 ni ili
tuweze kuijumlisha kwenye 595 na kupata 600,
na sasa tunaweza kufanya hili kwenye vichwa vyetu.
270 jumlisha mamia 6, tutakwenda kuongeza
mamia yetu kwa sita, kwa hiyo itakuwa 870.
Ngoja tufanye mifano zaidi hapa.
Jaza nafasi iliyoachwa wazi.
51 jumlisha 83 ni sawa na nafasi iliyoachwa wazi jumlisha 84.
Naam, wameongeza 83 kwa moja kupata 84,
kwa hiyo tunatakiwa kupunguza 51 kwa moja.
Hivyo, hii itakuwa sawa na 50 jumlisha 84.
Sasa kwa nini mnatakiwa kujali hili?
Kwa nini mjali?
Kwa sababu sasa ni rahisi kufanya,
kwa sababu sasa natakiwa niseme
makumi nane jumlisha mamoja manne, jumlisha, jumlisha makumi mengine matano
Hiyo itakuwa makumi 13 na mamoja manne, au 134.
Kwa hiyo, hii naiona hii rahisi zaidi,
lakini kitu cha muhimu ni kama tukiongeza moja kwenye namba
tunatakiwa tutoe kiasi hicho hicho kwenye namba nyingine.
ili kutokubadilisha thamani
ya hesabu hii ya kujumlisha, kwenye swali hili.
Hebu tufanye maswali zaidi.
138 jumlisha 710 ni sawa na sehemu iliyoachwa wazi jumlisha 700
Kwa hiyo tulikuw na 710, na sasa ni 700.
Kwa hiyo tumetoa kumi kutoka kwenye hiyo namba,
hivyo tunatakiwa tuipe namba nyingine.
Hivyo tunatakiwa kuongeza 10 kwenye 138,
kwa hiyo itakuwa 148.
Sasa, kwa nini hiyo ilikuwa muhimu?
Naam 148 jumlisha 700, unaweza kufanya hilo kichwani mwako.
Itakuwa 848, na hiyo ni rahisi kufanya
zaidi ya hichi tulichokuwa nacho hapa.