Mnamo Agosti 4, kulikuwa na mlipuko mkubwa
kwenye bandari ya Beirut, Lebanon.
(Milipuko)
Simu za rununu zilinasa mlipuko huo
kutoka karibu kila pembe.
Video zilisambaa
kupitia mitandao ya kijamii
na majukwaa ya ujumbe karibu mara moja.
Baadhi zilikuwa halisi,
baadhi ziliendeshwa.
Chache zilionekana kuonyesha kombora
kugonga kabla ya mlipuko huo.
(Milipuko)
Video hizi zilibadilishwa
Mwanahabari mchunguzi Emmanuelle Saliba
alipopokea moja ya video hizo
tokea chanzo Beirut,
alijua lazima aende kazini.
Kama mwanahabari mchunguzaji,
jukumu langu ni kujaribu kujua
nini kilichosababisha mlipuko kwenye kesi hii.
Kwa hivyo niliwasiliana na mtu
ambaye anafanya biashara
katika bandari la Beirut.
Familia yake imekuwa
ikifanya kazi huko kwa miaka 40.
Na katika mabadilishano haya alisema:
"Wacha nikutumie video."
"Nadhani kombora lilisababisha mlipuko huo."
Tayari nilikuwa na shauku sana
kwa sababu nilikuwa nimeona baadhi kwa urahisi
video zinazoweza kufichulika huko nje.
Kwa hivyo tunachoangalia hapa
ni video ya kwanza iliyotoka ambayo ilibadilishwa.
Kinachovutia katika kesi hii ni -
ni video halisi ya shahidi.
kwa hivyo kweli tunaliona tukio hilo,
lakini kile mtu huyo alifanya ni
kuongeza kombora.
Na nitawaonyesha video halisi, ambayo ni hii.
(Gari yapiga honi)
(Milipuko)
Kikubwa kizuri sasa kuhusu
kinacho endelea mtandaoni
ni kuwa punde tu video iliyo badilishwa inapotokea,
kuna waandishi wa habari wengi
ambao wamefunzwa kufanya hivi,
kuwa kwa kasi zinafichuliwa.
Kwa hivyo mwenzangu katika BBC
ambaye anaangazia
juu ya habari za uongo,
alifichua hili.
Na tupo sote, ingawaje tunafanyia kazi kampuni tofauti,
sote tunaangalia kazi za wenzetu na kusaidiana.
Kwa hiyo nilikuwa na hilo kichwani wakati
nilikuwa nazungumza na chanzo changu,
na nikafikiri, "Wajua, tumesha ifichua video hii.
Nina shaka sana kuhusu hili."
"Nitumie."
Alinitumia kwa njia ya WhatsApp
na yeye alisema aliipata kutoka kwa
marafiki na familia, unajua.
Fikiria biashara yake imeharibiwa, wanataka majibu.
Wanataka kujua ni nini kilisababisha mlipuko huo.
Niliangalia video na ni video ya infrared.
Nitakuonyesha toleo ambayo iko hapa,
ambayo bado inaishi kwenye Twitter.
Nitakuchezea ili uone.
(Milipuko)
Unaweza kuona kuwa hizi ni video mbili
ambazo zimehaririwa pamoja
kuifanya ionekane kama
ni shoti moja mfululizo.
Lakini kwa kuiangalia tu,
mtu yeyote angeweza kuona kuwa
zimechukuliwa kutoka pembe mbili tofauti.
Pia kuna safu hii ya picha ya joto
ambayo ni ya ajabu kidogo,
ukizingatia hiyo video
kamera huanguka kwenye sakafu
na unaweza kuona ilichukuliwa na mwanadamu.
Ni binadamu gani ana kamera ya infrared?
Hii gia ni ya kitaalamu.
Haki. Video inatetemeka.
Hakuna picha za usalama ambazo zingetoka hivyo haraka
kutokana na nguvu ya mlipuko huo.
Kwa hivyo unaanza tu, kama,
kuunganisha mambo haya pamoja.
Nilitambua shoti hii ya kwanza
na nilijua kuwa ilichukuliwa
na mhariri wa mitandao ya kijamii
ambaye kwa kweli alikuwa ardhini,
ambaye anafanya kazi CNN.
Na hii hapa video asili.
Unaona, haina kichujio hicho.
Na unapoicheza,
(Milipuko)
unaweza kuona kwamba hakuna kombora
ambayo inapita angani na kugonga.
Kwa hivyo hiyo iliongezwa.
Nilizungumza naye na akasema,
"Ndio, video yangu ilichukuliwa, ikabadilishwa.
Na niliendelea kupata barua pepe hizi zote
kuhusu kombora linalodhaniwa kwenye video yangu"
ambayo unaweza kuona haipo.
Na haraka baadaye, Twitter kweli iliweka tukio
ili kuonyesha kwamba
wachunguzi wa ukweli walikuwa wamehitimisha
kwamba video ya mlipuko wa Beirut
ilibadilishwa na ni pamoja na kombora bandia.
Na walionyesha tweet yangu
na thread yangu niliyoifanya
na pia waliunganisha waandishi wengine wachache
ambao pia wamekuwa wakifanya kazi sawa ya ufichuzi.
Kwa hivyo ni muhimu kwetu
kuwa wepesi kabisa kukataa haya
na kuyafichua haraka
nakuonyesha watu jinsi tunavyoifanya, sio?
Ni rahisi kusema ni halisi.
lakini tunahitaji watu kuelewa kwanini na ni vipi sio halisi.
Kwa hivyo kweli nilimwandikia
nikaziweka hatua zangu, nikasema,
"Hivi ndivyo ninavyojua sio halisi."
Na yeye akasema,
"Sawa, hiyo ni nzuri sana kujua.
Nitawaambia marafiki zangu
na familia yangu."
Na ni jambo linalosaidia sana,
nadhani kama wewe ni mtu binafsi,
kuunda orodha na waandishi wa habari hawa tofauti,
ili uweze kuwafuatilia wakati habari zinapochipuka.
Jenga jumuiya yako ndogo ya wataalam unaoamini,
ambao wamethibitishwa,
na kwa njia hiyo unaweza kuona kwamba
kile unachotaka kushiriki
kweli kilionekana hapa
kama kitu ambacho hupaswi kufanya.
Hasa.
Mlipuko wa Agosti 4 katika
Beirut
ulikuwa wenye kuangamiza.
Maisha yalipotea. Maelfu walijeruhiwa.
Mabilioni ya dola ya uharibifu yalifanyika.
Sote tulitaka kujua jinsi hii ilifanyika.
Tulipata maelezo mara moja.
Lakini habari za kuaminika huchukua muda.
Kwa hivyo tunafanya nini wakati habari
husafiri haraka kuliko ukweli?
Unda orodha kama Emmanuelle anavyo pendekeza.
Tafuta waandishi wa habari
unao waamini na kuwafuata.
Halafu habari kubwa inapochipuka -
na ikiwa 2020 imetufundisha chochote,
hakika itachipuka -
utajua tayari kwenda kwa nani.
Mpaka wakati ujao. Iweke kweli.
Usieneze habari za uwongo.
Mimi ni Hari Sreenivasan
na hii ni Take On Fake.
Asante kwa kutazama.
kwa uchunguzi wa kina kama huu,
fuata mgeni wetu Emmanuelle Saliba kwenye Twitter
Unaweza kupata kiungo katika maelezo
Tupe maoni yako kwenye maoni
na usisahau ku subscribe,
ili ujue lini kipindi kijacho cha TakeOnFake kitakapoanguka.