WEBVTT 00:00:06.025 --> 00:00:10.042 Baada ya kuwafanyia usahili maelfu ya wakulima masikini 00:00:10.042 --> 00:00:17.002 katika nchi kama Nepal, Bangladesh, China, Mexico, na Zambia 00:00:17.002 --> 00:00:21.061 Nimejifunza kwamba utatuzi wa kivitendo katika umasikini uliokithiri 00:00:21.061 --> 00:00:25.085 unaweza kupatikana kwa kuwasikiliza watu hao masikini 00:00:25.085 --> 00:00:30.056 na sio toka kwa jeshi la wataalam wa umasikini duniani. 00:00:30.056 --> 00:00:34.071 Nimetengeneza hatua 12 za kivitendo kwa ajili ya utatuzi wa matatizo 00:00:34.071 --> 00:00:38.053 ambazo zimesaidia watu 17 milioni kuondokana na umasikini 00:00:38.053 --> 00:00:42.060 na kuwepo katika tabaka la kati milele. 00:00:42.060 --> 00:00:47.064 Hatua hizi 12 zinatumika vizuri pia katika kutafuta hatua za kivitendo za utatuzi 00:00:47.064 --> 00:00:51.080 katika matatizo makubwa ya kijamii ambayo unaweza ukawa unayafanyia kazi. 00:00:51.080 --> 00:00:57.067 Nimezielezea hatua hizi 12 katika kitabu changu cha, Out of Poverty. 00:00:57.067 --> 00:00:59.077 Kwa miaka mitano iliyopita nimekuwa nikifanyia kazi kitabu 00:00:59.077 --> 00:01:02.028 na hatimaye nimekimaliza. 00:01:02.028 --> 00:01:07.077 Imenichukua miaka mitano kuandika kurasa 200 tu. 00:01:07.077 --> 00:01:11.009 Kitabu kinaitwa Out of Poverty: 00:01:11.009 --> 00:01:17.088 What works when traditional approaches fail. 00:01:17.088 --> 00:01:21.040 Kwa kweli nimeandika kitabu hicho kuleta mapinduzi 00:01:21.040 --> 00:01:26.035 katika tunavyofikiri juu ya umasikini na yale tunayofanya juu yake. 00:01:26.035 --> 00:01:32.037 Hakitaweza kuleta mapinduzi chenyewe lakini nina imani kitasaidia. 00:01:32.037 --> 00:01:39.074 Kwa miaka 25 iliyopita maswali mawili yamegandama udadisi wangu. 00:01:39.074 --> 00:01:42.055 Nini kinawafanya watu masikini kuwa masikini? 00:01:42.055 --> 00:01:47.081 Na kitu gani wanaweza kufanya juu ya hali hiyo? 00:01:47.081 --> 00:01:51.007 Kwa sababu ya maswali haya mawili yanayokera, 00:01:51.007 --> 00:01:58.058 Nimekuwa na mazungumzo marefu na wamiliki maelfu wa eka moja katika nchi zinazoendelea. 00:01:58.058 --> 00:02:02.016 Nilichojifunza kimeleta uwezekano kwa IDE, 00:02:02.016 --> 00:02:05.085 asasi ya kimaendeleo niliyoianzisha miaka 25 iliyopita, 00:02:05.085 --> 00:02:13.009 kusaidia watu 17 milioni watu wa $1-kwa-siku kuondokana na umasikini milele. 00:02:13.009 --> 00:02:17.013 Hatua tatu za kwanza za utatuzi wa kivitendo wa matatizo ni 00:02:17.013 --> 00:02:23.006 yawezekana zilizo wazi zaidi, zilizo rahisi zaidi, na zinazofuatwa kwa kiwango kidogo zaidi. 00:02:23.006 --> 00:02:29.004 Ya kwanza ni kwenda pale tendo liliko. 00:02:29.004 --> 00:02:31.020 Uwezi ukakaa katika ofisi yako katika Benki ya Dunia 00:02:31.020 --> 00:02:38.004 na ukagundua jinsi ya kutatua matatizo ya umasikini Myanmar. 00:02:38.004 --> 00:02:41.091 Hatua ya 2, ongea na watu ambao wana hilo tatizo 00:02:41.091 --> 00:02:45.069 na sikiliza yale watakayosema. 00:02:45.069 --> 00:02:51.021 Katika miaka ya 1990, wataalam wa kilimo wa Bangladesh walisikitishwa 00:02:51.021 --> 00:02:58.053 na viwango finyu vya mbolea wakulima wa Bangladesh walivyotumia katika mazao yao ya mchele/mpunga (monsoon rice crops). 00:02:58.053 --> 00:03:03.084 Wakaanzisha programu za mafunzo kwa wakulima lakini hakuna kilichofanya kazi. 00:03:03.084 --> 00:03:08.084 Hatimaye, mtu mmoja akawauliza baadhi ya wakulima kwanini wanatumia kiwango kidogo sana cha mbolea. 00:03:08.084 --> 00:03:10.024 “Hilo rahisi,” walisema. 00:03:10.024 --> 00:03:15.056 “Kila baada ya miaka 10 hivi tunakuwa na mafuriko makubwa yanayosafisha kila kitu tulichopanda. ..." 00:03:15.056 --> 00:03:22.035 "... Kwa hiyo tunatumia kiwango sawia cha mbolea tunachoweza kumudu katika mafuriko ya miaka 10.” 00:03:22.035 --> 00:03:30.053 Punde wakulima hawa wakabadilishwa toka katika ujinga, woga, 00:03:30.053 --> 00:03:35.037 na kuwa watu wanaoweza kuwafundisha wataalam wa kilimo kitu fulani. 00:03:35.037 --> 00:03:41.064 Hatua ya 3, jifunze kila kitu kilichopo juu ya mazingira na hali halisi ya tatizo husika. 00:03:41.064 --> 00:03:44.065 Mazingira halisi ya watu 800 milioni 00:03:44.065 --> 00:03:48.078 kati ya watu 1.2 bilioni duniani wanaoishi kwa chini ya $2 kwa siku, 00:03:48.078 --> 00:03:55.009 ni kashamba kadogo chenye udongo usio na rutuba na hakuna umwagiliaji. 00:03:55.009 --> 00:03:57.003 Mashamba haya sanasana ni ya eka moja, 00:03:57.003 --> 00:04:02.000 na yamegawanywa katika ploti 4 au 5. 00:04:02.000 --> 00:04:03.091 Na hili ni wazo la nne, 00:04:03.091 --> 00:04:09.042 kama utagundua utatuzi juu ya tatizo hakuna sababu ya kuwa wastani. 00:04:09.042 --> 00:04:14.088 Baadhi ya matatizo makubwa sana duniani katika hali halisi yanahitaji utatuzi madhubuti/mkubwa 00:04:14.088 --> 00:04:21.079 ambao katika hali halisi ni utatuzi mdogomdogo unaotekelezwa mara maelfu na maelfu. 00:04:21.079 --> 00:04:24.088 Hatua ya 5, fikiri kama mtoto. 00:04:24.088 --> 00:04:31.028 Inakinzana kidogo kwamba kufikiri makubwa na kufikiri kama mtoto vinaenda pamoja, lakini inakuwa hivyo. 00:04:31.028 --> 00:04:38.098 Inabidi ufikiri kama mtoto ili kupata utatuzi ulio wazi juu ya tatizo kubwa ambalo watu wamelishindwa. 00:04:38.098 --> 00:04:43.033 Hatua ya 6, angalia na fanya kilicho wazi. 00:04:43.033 --> 00:04:48.020 Kama hatuwezi kuona upofu wetu ni vipi tutaona na kufanya kilicho wazi? 00:04:48.020 --> 00:04:53.002 Kujiweka katika tatizo kunasaidia. 00:04:53.002 --> 00:04:58.066 Hatua ya 7, kama tayari kuna mtu amekwisha buni hauhitajiki kufanya hivyo. 00:04:58.066 --> 00:05:05.005 Ni rahisi siku hizi kufuatilia utatuzi ambao tayari watu wameshautoa. 00:05:05.005 --> 00:05:15.063 Hatua ya 8, hakikisha mkabala wako una matokeo chanya yanayopimika na yanayoweza kukuzwa/kuwekwa katika skeli. 00:05:15.063 --> 00:05:21.072 Hatua ya 9, sanifu ukilenga bei fulani. 00:05:21.072 --> 00:05:27.014 Kumudu bei kunatawala mchakato wa usanifu kwa wateja masikini. 00:05:27.014 --> 00:05:31.001 Namba 10, fuata mipango ya kivitendo ya miaka 3. 00:05:31.001 --> 00:05:36.038 Bila kujali kiwango cha nguvu na ubadilishaji wa dunia katika dira yako juu ya mambo ya mbele, 00:05:36.038 --> 00:05:42.024 kama hautaweza kutafsiri katika mpango madhubuti ndani ya miaka mitatu ya mwanzo, 00:05:42.024 --> 00:05:46.003 hautaweza kufikia lengo. 00:05:46.003 --> 00:05:52.067 Hatua ya 11, endelea kujifunza toka kwa wateja wako. 00:05:52.067 --> 00:05:58.079 Nilipoanzisha IDE niliamua kwamba nitahudumu angalau wateja 100 kwa mwaka 00:05:58.079 --> 00:06:00.037 na nimefanya hivyo. 00:06:00.037 --> 00:06:07.075 Mpaka sasa nimehoji zaidi ya familia masikini za wakulima 3000, 00:06:07.075 --> 00:06:12.019 na nimetembea nao katika mashamba yao. 00:06:12.019 --> 00:06:15.006 Waliponiambia kwamba wamewekeza 00:06:15.006 --> 00:06:16.084 vipato vyao vipya toka kwenye treadle pump 00:06:16.084 --> 00:06:19.080 kwenye elimu ya watoto wao, 00:06:19.080 --> 00:06:22.010 tulisanifu taa ya umeme jua ya $12 00:06:22.010 --> 00:06:26.012 ili watoto wao waweze kusoma usiku. 00:06:26.012 --> 00:06:27.045 Waliposema wamewekeza 00:06:27.045 --> 00:06:30.077 sehemu ya fedha zao toka kwenye mifumo ya umwagiliaji ya dripu 00:06:30.077 --> 00:06:34.041 katika nyati wa maziwa ama katika idadi ya mbuzi, 00:06:34.041 --> 00:06:37.090 tulijifunza kila kitu kilichohitajika juu ya ufugaji mdogo 00:06:37.090 --> 00:06:44.089 na tukaanza kusaidia wakulima walio na miradi midogo ya ufugaji. 00:06:44.089 --> 00:06:49.038 Namba 12, usiyumbishwe na yale yanayosemwa na watu wengine. 00:06:49.038 --> 00:06:52.024 Katika kila kitu ambacho nimefanyia kazi 00:06:52.024 --> 00:06:55.030 na kugeuka kuwa mafanikio makubwa, 00:06:55.030 --> 00:07:00.058 Nimesikia watu wengi wakiniambia kwamba napoteza muda. 00:07:00.058 --> 00:07:03.045 Milioni moja na nusu ya treadle pumps baadae, 00:07:03.045 --> 00:07:10.035 tuna ekari mpya elfu 750 chini ya umwagiliaji. 00:07:10.035 --> 00:07:14.089 Kama ningewasikiliza watu waliosema ni kupoteza muda, 00:07:14.089 --> 00:07:17.045 tusingefika hapo. 00:07:17.045 --> 00:07:20.068 Kama una nia ya kuwa sehemu ya kitu haswa, 00:07:20.068 --> 00:07:25.058 tembelea watu katika mazingira yao halisi 00:07:25.058 --> 00:07:30.018 na sikiliza wanachosema, 00:07:30.018 --> 00:07:31.038 na muhimu sana, 00:07:31.038 --> 00:07:34.041 kuwa na nia ya kujifunza mambo mapya, 00:07:34.041 --> 00:07:36.073 hapo mkabala huu utakuwa kwa ajili yako. 00:07:36.073 --> 00:07:39.099 Kama wewe na kundi lako mtaamua kwamba kitu bora mtakachofanya nia kutoa msaada wa fedha, 00:07:39.099 --> 00:07:43.076 hakikisha unachagua asasi zilizo na matokeo yanayopimika, 00:07:43.076 --> 00:07:47.035 kama asasi za umasikini zinazoongeza kipato 00:07:47.035 --> 00:08:25.073 cha watu wanaoishi kwa chini ya dola moja kwa siku.