Baada ya kuwafanyia usahili maelfu ya wakulima masikini katika nchi kama Nepal, Bangladesh, China, Mexico, na Zambia Nimejifunza kwamba utatuzi wa kivitendo katika umasikini uliokithiri unaweza kupatikana kwa kuwasikiliza watu hao masikini na sio toka kwa jeshi la wataalam wa umasikini duniani. Nimetengeneza hatua 12 za kivitendo kwa ajili ya utatuzi wa matatizo ambazo zimesaidia watu 17 milioni kuondokana na umasikini na kuwepo katika tabaka la kati milele. Hatua hizi 12 zinatumika vizuri pia katika kutafuta hatua za kivitendo za utatuzi katika matatizo makubwa ya kijamii ambayo unaweza ukawa unayafanyia kazi. Nimezielezea hatua hizi 12 katika kitabu changu cha, Out of Poverty. Kwa miaka mitano iliyopita nimekuwa nikifanyia kazi kitabu na hatimaye nimekimaliza. Imenichukua miaka mitano kuandika kurasa 200 tu. Kitabu kinaitwa Out of Poverty: What works when traditional approaches fail. Kwa kweli nimeandika kitabu hicho kuleta mapinduzi katika tunavyofikiri juu ya umasikini na yale tunayofanya juu yake. Hakitaweza kuleta mapinduzi chenyewe lakini nina imani kitasaidia. Kwa miaka 25 iliyopita maswali mawili yamegandama udadisi wangu. Nini kinawafanya watu masikini kuwa masikini? Na kitu gani wanaweza kufanya juu ya hali hiyo? Kwa sababu ya maswali haya mawili yanayokera, Nimekuwa na mazungumzo marefu na wamiliki maelfu wa eka moja katika nchi zinazoendelea. Nilichojifunza kimeleta uwezekano kwa IDE, asasi ya kimaendeleo niliyoianzisha miaka 25 iliyopita, kusaidia watu 17 milioni watu wa $1-kwa-siku kuondokana na umasikini milele. Hatua tatu za kwanza za utatuzi wa kivitendo wa matatizo ni yawezekana zilizo wazi zaidi, zilizo rahisi zaidi, na zinazofuatwa kwa kiwango kidogo zaidi. Ya kwanza ni kwenda pale tendo liliko. Uwezi ukakaa katika ofisi yako katika Benki ya Dunia na ukagundua jinsi ya kutatua matatizo ya umasikini Myanmar. Hatua ya 2, ongea na watu ambao wana hilo tatizo na sikiliza yale watakayosema. Katika miaka ya 1990, wataalam wa kilimo wa Bangladesh walisikitishwa na viwango finyu vya mbolea wakulima wa Bangladesh walivyotumia katika mazao yao ya mchele/mpunga (monsoon rice crops). Wakaanzisha programu za mafunzo kwa wakulima lakini hakuna kilichofanya kazi. Hatimaye, mtu mmoja akawauliza baadhi ya wakulima kwanini wanatumia kiwango kidogo sana cha mbolea. “Hilo rahisi,” walisema. “Kila baada ya miaka 10 hivi tunakuwa na mafuriko makubwa yanayosafisha kila kitu tulichopanda. ..." "... Kwa hiyo tunatumia kiwango sawia cha mbolea tunachoweza kumudu katika mafuriko ya miaka 10.” Punde wakulima hawa wakabadilishwa toka katika ujinga, woga, na kuwa watu wanaoweza kuwafundisha wataalam wa kilimo kitu fulani. Hatua ya 3, jifunze kila kitu kilichopo juu ya mazingira na hali halisi ya tatizo husika. Mazingira halisi ya watu 800 milioni kati ya watu 1.2 bilioni duniani wanaoishi kwa chini ya $2 kwa siku, ni kashamba kadogo chenye udongo usio na rutuba na hakuna umwagiliaji. Mashamba haya sanasana ni ya eka moja, na yamegawanywa katika ploti 4 au 5. Na hili ni wazo la nne, kama utagundua utatuzi juu ya tatizo hakuna sababu ya kuwa wastani. Baadhi ya matatizo makubwa sana duniani katika hali halisi yanahitaji utatuzi madhubuti/mkubwa ambao katika hali halisi ni utatuzi mdogomdogo unaotekelezwa mara maelfu na maelfu. Hatua ya 5, fikiri kama mtoto. Inakinzana kidogo kwamba kufikiri makubwa na kufikiri kama mtoto vinaenda pamoja, lakini inakuwa hivyo. Inabidi ufikiri kama mtoto ili kupata utatuzi ulio wazi juu ya tatizo kubwa ambalo watu wamelishindwa. Hatua ya 6, angalia na fanya kilicho wazi. Kama hatuwezi kuona upofu wetu ni vipi tutaona na kufanya kilicho wazi? Kujiweka katika tatizo kunasaidia. Hatua ya 7, kama tayari kuna mtu amekwisha buni hauhitajiki kufanya hivyo. Ni rahisi siku hizi kufuatilia utatuzi ambao tayari watu wameshautoa. Hatua ya 8, hakikisha mkabala wako una matokeo chanya yanayopimika na yanayoweza kukuzwa/kuwekwa katika skeli. Hatua ya 9, sanifu ukilenga bei fulani. Kumudu bei kunatawala mchakato wa usanifu kwa wateja masikini. Namba 10, fuata mipango ya kivitendo ya miaka 3. Bila kujali kiwango cha nguvu na ubadilishaji wa dunia katika dira yako juu ya mambo ya mbele, kama hautaweza kutafsiri katika mpango madhubuti ndani ya miaka mitatu ya mwanzo, hautaweza kufikia lengo. Hatua ya 11, endelea kujifunza toka kwa wateja wako. Nilipoanzisha IDE niliamua kwamba nitahudumu angalau wateja 100 kwa mwaka na nimefanya hivyo. Mpaka sasa nimehoji zaidi ya familia masikini za wakulima 3000, na nimetembea nao katika mashamba yao. Waliponiambia kwamba wamewekeza vipato vyao vipya toka kwenye treadle pump kwenye elimu ya watoto wao, tulisanifu taa ya umeme jua ya $12 ili watoto wao waweze kusoma usiku. Waliposema wamewekeza sehemu ya fedha zao toka kwenye mifumo ya umwagiliaji ya dripu katika nyati wa maziwa ama katika idadi ya mbuzi, tulijifunza kila kitu kilichohitajika juu ya ufugaji mdogo na tukaanza kusaidia wakulima walio na miradi midogo ya ufugaji. Namba 12, usiyumbishwe na yale yanayosemwa na watu wengine. Katika kila kitu ambacho nimefanyia kazi na kugeuka kuwa mafanikio makubwa, Nimesikia watu wengi wakiniambia kwamba napoteza muda. Milioni moja na nusu ya treadle pumps baadae, tuna ekari mpya elfu 750 chini ya umwagiliaji. Kama ningewasikiliza watu waliosema ni kupoteza muda, tusingefika hapo. Kama una nia ya kuwa sehemu ya kitu haswa, tembelea watu katika mazingira yao halisi na sikiliza wanachosema, na muhimu sana, kuwa na nia ya kujifunza mambo mapya, hapo mkabala huu utakuwa kwa ajili yako. Kama wewe na kundi lako mtaamua kwamba kitu bora mtakachofanya nia kutoa msaada wa fedha, hakikisha unachagua asasi zilizo na matokeo yanayopimika, kama asasi za umasikini zinazoongeza kipato cha watu wanaoishi kwa chini ya dola moja kwa siku.