1 00:00:06,025 --> 00:00:10,042 Baada ya kuwafanyia usahili maelfu ya wakulima masikini 2 00:00:10,042 --> 00:00:17,002 katika nchi kama Nepal, Bangladesh, China, Mexico, na Zambia 3 00:00:17,002 --> 00:00:21,061 Nimejifunza kwamba utatuzi wa kivitendo katika umasikini uliokithiri 4 00:00:21,061 --> 00:00:25,085 unaweza kupatikana kwa kuwasikiliza watu hao masikini 5 00:00:25,085 --> 00:00:30,056 na sio toka kwa jeshi la wataalam wa umasikini duniani. 6 00:00:30,056 --> 00:00:34,071 Nimetengeneza hatua 12 za kivitendo kwa ajili ya utatuzi wa matatizo 7 00:00:34,071 --> 00:00:38,053 ambazo zimesaidia watu 17 milioni kuondokana na umasikini 8 00:00:38,053 --> 00:00:42,060 na kuwepo katika tabaka la kati milele. 9 00:00:42,060 --> 00:00:47,064 Hatua hizi 12 zinatumika vizuri pia katika kutafuta hatua za kivitendo za utatuzi 10 00:00:47,064 --> 00:00:51,080 katika matatizo makubwa ya kijamii ambayo unaweza ukawa unayafanyia kazi. 11 00:00:51,080 --> 00:00:57,067 Nimezielezea hatua hizi 12 katika kitabu changu cha, Out of Poverty. 12 00:00:57,067 --> 00:00:59,077 Kwa miaka mitano iliyopita nimekuwa nikifanyia kazi kitabu 13 00:00:59,077 --> 00:01:02,028 na hatimaye nimekimaliza. 14 00:01:02,028 --> 00:01:07,077 Imenichukua miaka mitano kuandika kurasa 200 tu. 15 00:01:07,077 --> 00:01:11,009 Kitabu kinaitwa Out of Poverty: 16 00:01:11,009 --> 00:01:17,088 What works when traditional approaches fail. 17 00:01:17,088 --> 00:01:21,040 Kwa kweli nimeandika kitabu hicho kuleta mapinduzi 18 00:01:21,040 --> 00:01:26,035 katika tunavyofikiri juu ya umasikini na yale tunayofanya juu yake. 19 00:01:26,035 --> 00:01:32,037 Hakitaweza kuleta mapinduzi chenyewe lakini nina imani kitasaidia. 20 00:01:32,037 --> 00:01:39,074 Kwa miaka 25 iliyopita maswali mawili yamegandama udadisi wangu. 21 00:01:39,074 --> 00:01:42,055 Nini kinawafanya watu masikini kuwa masikini? 22 00:01:42,055 --> 00:01:47,081 Na kitu gani wanaweza kufanya juu ya hali hiyo? 23 00:01:47,081 --> 00:01:51,007 Kwa sababu ya maswali haya mawili yanayokera, 24 00:01:51,007 --> 00:01:58,058 Nimekuwa na mazungumzo marefu na wamiliki maelfu wa eka moja katika nchi zinazoendelea. 25 00:01:58,058 --> 00:02:02,016 Nilichojifunza kimeleta uwezekano kwa IDE, 26 00:02:02,016 --> 00:02:05,085 asasi ya kimaendeleo niliyoianzisha miaka 25 iliyopita, 27 00:02:05,085 --> 00:02:13,009 kusaidia watu 17 milioni watu wa $1-kwa-siku kuondokana na umasikini milele. 28 00:02:13,009 --> 00:02:17,013 Hatua tatu za kwanza za utatuzi wa kivitendo wa matatizo ni 29 00:02:17,013 --> 00:02:23,006 yawezekana zilizo wazi zaidi, zilizo rahisi zaidi, na zinazofuatwa kwa kiwango kidogo zaidi. 30 00:02:23,006 --> 00:02:29,004 Ya kwanza ni kwenda pale tendo liliko. 31 00:02:29,004 --> 00:02:31,020 Uwezi ukakaa katika ofisi yako katika Benki ya Dunia 32 00:02:31,020 --> 00:02:38,004 na ukagundua jinsi ya kutatua matatizo ya umasikini Myanmar. 33 00:02:38,004 --> 00:02:41,091 Hatua ya 2, ongea na watu ambao wana hilo tatizo 34 00:02:41,091 --> 00:02:45,069 na sikiliza yale watakayosema. 35 00:02:45,069 --> 00:02:51,021 Katika miaka ya 1990, wataalam wa kilimo wa Bangladesh walisikitishwa 36 00:02:51,021 --> 00:02:58,053 na viwango finyu vya mbolea wakulima wa Bangladesh walivyotumia katika mazao yao ya mchele/mpunga (monsoon rice crops). 37 00:02:58,053 --> 00:03:03,084 Wakaanzisha programu za mafunzo kwa wakulima lakini hakuna kilichofanya kazi. 38 00:03:03,084 --> 00:03:08,084 Hatimaye, mtu mmoja akawauliza baadhi ya wakulima kwanini wanatumia kiwango kidogo sana cha mbolea. 39 00:03:08,084 --> 00:03:10,024 “Hilo rahisi,” walisema. 40 00:03:10,024 --> 00:03:15,056 “Kila baada ya miaka 10 hivi tunakuwa na mafuriko makubwa yanayosafisha kila kitu tulichopanda. ..." 41 00:03:15,056 --> 00:03:22,035 "... Kwa hiyo tunatumia kiwango sawia cha mbolea tunachoweza kumudu katika mafuriko ya miaka 10.” 42 00:03:22,035 --> 00:03:30,053 Punde wakulima hawa wakabadilishwa toka katika ujinga, woga, 43 00:03:30,053 --> 00:03:35,037 na kuwa watu wanaoweza kuwafundisha wataalam wa kilimo kitu fulani. 44 00:03:35,037 --> 00:03:41,064 Hatua ya 3, jifunze kila kitu kilichopo juu ya mazingira na hali halisi ya tatizo husika. 45 00:03:41,064 --> 00:03:44,065 Mazingira halisi ya watu 800 milioni 46 00:03:44,065 --> 00:03:48,078 kati ya watu 1.2 bilioni duniani wanaoishi kwa chini ya $2 kwa siku, 47 00:03:48,078 --> 00:03:55,009 ni kashamba kadogo chenye udongo usio na rutuba na hakuna umwagiliaji. 48 00:03:55,009 --> 00:03:57,003 Mashamba haya sanasana ni ya eka moja, 49 00:03:57,003 --> 00:04:02,000 na yamegawanywa katika ploti 4 au 5. 50 00:04:02,000 --> 00:04:03,091 Na hili ni wazo la nne, 51 00:04:03,091 --> 00:04:09,042 kama utagundua utatuzi juu ya tatizo hakuna sababu ya kuwa wastani. 52 00:04:09,042 --> 00:04:14,088 Baadhi ya matatizo makubwa sana duniani katika hali halisi yanahitaji utatuzi madhubuti/mkubwa 53 00:04:14,088 --> 00:04:21,079 ambao katika hali halisi ni utatuzi mdogomdogo unaotekelezwa mara maelfu na maelfu. 54 00:04:21,079 --> 00:04:24,088 Hatua ya 5, fikiri kama mtoto. 55 00:04:24,088 --> 00:04:31,028 Inakinzana kidogo kwamba kufikiri makubwa na kufikiri kama mtoto vinaenda pamoja, lakini inakuwa hivyo. 56 00:04:31,028 --> 00:04:38,098 Inabidi ufikiri kama mtoto ili kupata utatuzi ulio wazi juu ya tatizo kubwa ambalo watu wamelishindwa. 57 00:04:38,098 --> 00:04:43,033 Hatua ya 6, angalia na fanya kilicho wazi. 58 00:04:43,033 --> 00:04:48,020 Kama hatuwezi kuona upofu wetu ni vipi tutaona na kufanya kilicho wazi? 59 00:04:48,020 --> 00:04:53,002 Kujiweka katika tatizo kunasaidia. 60 00:04:53,002 --> 00:04:58,066 Hatua ya 7, kama tayari kuna mtu amekwisha buni hauhitajiki kufanya hivyo. 61 00:04:58,066 --> 00:05:05,005 Ni rahisi siku hizi kufuatilia utatuzi ambao tayari watu wameshautoa. 62 00:05:05,005 --> 00:05:15,063 Hatua ya 8, hakikisha mkabala wako una matokeo chanya yanayopimika na yanayoweza kukuzwa/kuwekwa katika skeli. 63 00:05:15,063 --> 00:05:21,072 Hatua ya 9, sanifu ukilenga bei fulani. 64 00:05:21,072 --> 00:05:27,014 Kumudu bei kunatawala mchakato wa usanifu kwa wateja masikini. 65 00:05:27,014 --> 00:05:31,001 Namba 10, fuata mipango ya kivitendo ya miaka 3. 66 00:05:31,001 --> 00:05:36,038 Bila kujali kiwango cha nguvu na ubadilishaji wa dunia katika dira yako juu ya mambo ya mbele, 67 00:05:36,038 --> 00:05:42,024 kama hautaweza kutafsiri katika mpango madhubuti ndani ya miaka mitatu ya mwanzo, 68 00:05:42,024 --> 00:05:46,003 hautaweza kufikia lengo. 69 00:05:46,003 --> 00:05:52,067 Hatua ya 11, endelea kujifunza toka kwa wateja wako. 70 00:05:52,067 --> 00:05:58,079 Nilipoanzisha IDE niliamua kwamba nitahudumu angalau wateja 100 kwa mwaka 71 00:05:58,079 --> 00:06:00,037 na nimefanya hivyo. 72 00:06:00,037 --> 00:06:07,075 Mpaka sasa nimehoji zaidi ya familia masikini za wakulima 3000, 73 00:06:07,075 --> 00:06:12,019 na nimetembea nao katika mashamba yao. 74 00:06:12,019 --> 00:06:15,006 Waliponiambia kwamba wamewekeza 75 00:06:15,006 --> 00:06:16,084 vipato vyao vipya toka kwenye treadle pump 76 00:06:16,084 --> 00:06:19,080 kwenye elimu ya watoto wao, 77 00:06:19,080 --> 00:06:22,010 tulisanifu taa ya umeme jua ya $12 78 00:06:22,010 --> 00:06:26,012 ili watoto wao waweze kusoma usiku. 79 00:06:26,012 --> 00:06:27,045 Waliposema wamewekeza 80 00:06:27,045 --> 00:06:30,077 sehemu ya fedha zao toka kwenye mifumo ya umwagiliaji ya dripu 81 00:06:30,077 --> 00:06:34,041 katika nyati wa maziwa ama katika idadi ya mbuzi, 82 00:06:34,041 --> 00:06:37,090 tulijifunza kila kitu kilichohitajika juu ya ufugaji mdogo 83 00:06:37,090 --> 00:06:44,089 na tukaanza kusaidia wakulima walio na miradi midogo ya ufugaji. 84 00:06:44,089 --> 00:06:49,038 Namba 12, usiyumbishwe na yale yanayosemwa na watu wengine. 85 00:06:49,038 --> 00:06:52,024 Katika kila kitu ambacho nimefanyia kazi 86 00:06:52,024 --> 00:06:55,030 na kugeuka kuwa mafanikio makubwa, 87 00:06:55,030 --> 00:07:00,058 Nimesikia watu wengi wakiniambia kwamba napoteza muda. 88 00:07:00,058 --> 00:07:03,045 Milioni moja na nusu ya treadle pumps baadae, 89 00:07:03,045 --> 00:07:10,035 tuna ekari mpya elfu 750 chini ya umwagiliaji. 90 00:07:10,035 --> 00:07:14,089 Kama ningewasikiliza watu waliosema ni kupoteza muda, 91 00:07:14,089 --> 00:07:17,045 tusingefika hapo. 92 00:07:17,045 --> 00:07:20,068 Kama una nia ya kuwa sehemu ya kitu haswa, 93 00:07:20,068 --> 00:07:25,058 tembelea watu katika mazingira yao halisi 94 00:07:25,058 --> 00:07:30,018 na sikiliza wanachosema, 95 00:07:30,018 --> 00:07:31,038 na muhimu sana, 96 00:07:31,038 --> 00:07:34,041 kuwa na nia ya kujifunza mambo mapya, 97 00:07:34,041 --> 00:07:36,073 hapo mkabala huu utakuwa kwa ajili yako. 98 00:07:36,073 --> 00:07:39,099 Kama wewe na kundi lako mtaamua kwamba kitu bora mtakachofanya nia kutoa msaada wa fedha, 99 00:07:39,099 --> 00:07:43,076 hakikisha unachagua asasi zilizo na matokeo yanayopimika, 100 00:07:43,076 --> 00:07:47,035 kama asasi za umasikini zinazoongeza kipato 101 00:07:47,035 --> 00:08:25,073 cha watu wanaoishi kwa chini ya dola moja kwa siku.