0:00:06.025,0:00:10.042 Baada ya kuwafanyia usahili maelfu ya wakulima masikini 0:00:10.042,0:00:17.002 katika nchi kama Nepal, Bangladesh, China, Mexico, na Zambia 0:00:17.002,0:00:21.061 Nimejifunza kwamba utatuzi wa kivitendo katika umasikini uliokithiri 0:00:21.061,0:00:25.085 unaweza kupatikana kwa kuwasikiliza watu hao masikini 0:00:25.085,0:00:30.056 na sio toka kwa jeshi la wataalam wa umasikini duniani. 0:00:30.056,0:00:34.071 Nimetengeneza hatua 12 za kivitendo kwa ajili ya utatuzi wa matatizo 0:00:34.071,0:00:38.053 ambazo zimesaidia watu 17 milioni kuondokana na umasikini 0:00:38.053,0:00:42.060 na kuwepo katika tabaka la kati milele. 0:00:42.060,0:00:47.064 Hatua hizi 12 zinatumika vizuri pia katika kutafuta hatua za kivitendo za utatuzi 0:00:47.064,0:00:51.080 katika matatizo makubwa ya kijamii ambayo unaweza ukawa unayafanyia kazi. 0:00:51.080,0:00:57.067 Nimezielezea hatua hizi 12 katika kitabu changu cha, Out of Poverty. 0:00:57.067,0:00:59.077 Kwa miaka mitano iliyopita nimekuwa nikifanyia kazi kitabu 0:00:59.077,0:01:02.028 na hatimaye nimekimaliza. 0:01:02.028,0:01:07.077 Imenichukua miaka mitano kuandika kurasa 200 tu. 0:01:07.077,0:01:11.009 Kitabu kinaitwa Out of Poverty: 0:01:11.009,0:01:17.088 What works when traditional approaches fail. 0:01:17.088,0:01:21.040 Kwa kweli nimeandika kitabu hicho kuleta mapinduzi 0:01:21.040,0:01:26.035 katika tunavyofikiri juu ya umasikini na yale tunayofanya juu yake. 0:01:26.035,0:01:32.037 Hakitaweza kuleta mapinduzi chenyewe lakini nina imani kitasaidia. 0:01:32.037,0:01:39.074 Kwa miaka 25 iliyopita maswali mawili yamegandama udadisi wangu. 0:01:39.074,0:01:42.055 Nini kinawafanya watu masikini kuwa masikini? 0:01:42.055,0:01:47.081 Na kitu gani wanaweza kufanya juu ya hali hiyo? 0:01:47.081,0:01:51.007 Kwa sababu ya maswali haya mawili yanayokera, 0:01:51.007,0:01:58.058 Nimekuwa na mazungumzo marefu na wamiliki maelfu wa eka moja katika nchi zinazoendelea. 0:01:58.058,0:02:02.016 Nilichojifunza kimeleta uwezekano kwa IDE, 0:02:02.016,0:02:05.085 asasi ya kimaendeleo niliyoianzisha miaka 25 iliyopita, 0:02:05.085,0:02:13.009 kusaidia watu 17 milioni watu wa $1-kwa-siku kuondokana na umasikini milele. 0:02:13.009,0:02:17.013 Hatua tatu za kwanza za utatuzi wa kivitendo wa matatizo ni 0:02:17.013,0:02:23.006 yawezekana zilizo wazi zaidi, zilizo rahisi zaidi, na zinazofuatwa kwa kiwango kidogo zaidi. 0:02:23.006,0:02:29.004 Ya kwanza ni kwenda pale tendo liliko. 0:02:29.004,0:02:31.020 Uwezi ukakaa katika ofisi yako katika Benki ya Dunia 0:02:31.020,0:02:38.004 na ukagundua jinsi ya kutatua matatizo ya umasikini Myanmar. 0:02:38.004,0:02:41.091 Hatua ya 2, ongea na watu ambao wana hilo tatizo 0:02:41.091,0:02:45.069 na sikiliza yale watakayosema. 0:02:45.069,0:02:51.021 Katika miaka ya 1990, wataalam wa kilimo wa Bangladesh walisikitishwa 0:02:51.021,0:02:58.053 na viwango finyu vya mbolea wakulima wa Bangladesh walivyotumia katika mazao yao ya mchele/mpunga (monsoon rice crops). 0:02:58.053,0:03:03.084 Wakaanzisha programu za mafunzo kwa wakulima lakini hakuna kilichofanya kazi. 0:03:03.084,0:03:08.084 Hatimaye, mtu mmoja akawauliza baadhi ya wakulima kwanini wanatumia kiwango kidogo sana cha mbolea. 0:03:08.084,0:03:10.024 “Hilo rahisi,” walisema. 0:03:10.024,0:03:15.056 “Kila baada ya miaka 10 hivi tunakuwa na mafuriko makubwa yanayosafisha kila kitu tulichopanda. ..." 0:03:15.056,0:03:22.035 "... Kwa hiyo tunatumia kiwango sawia cha mbolea tunachoweza kumudu katika mafuriko ya miaka 10.” 0:03:22.035,0:03:30.053 Punde wakulima hawa wakabadilishwa toka katika ujinga, woga, 0:03:30.053,0:03:35.037 na kuwa watu wanaoweza kuwafundisha wataalam wa kilimo kitu fulani. 0:03:35.037,0:03:41.064 Hatua ya 3, jifunze kila kitu kilichopo juu ya mazingira na hali halisi ya tatizo husika. 0:03:41.064,0:03:44.065 Mazingira halisi ya watu 800 milioni 0:03:44.065,0:03:48.078 kati ya watu 1.2 bilioni duniani wanaoishi kwa chini ya $2 kwa siku, 0:03:48.078,0:03:55.009 ni kashamba kadogo chenye udongo usio na rutuba na hakuna umwagiliaji. 0:03:55.009,0:03:57.003 Mashamba haya sanasana ni ya eka moja, 0:03:57.003,0:04:02.000 na yamegawanywa katika ploti 4 au 5. 0:04:02.000,0:04:03.091 Na hili ni wazo la nne, 0:04:03.091,0:04:09.042 kama utagundua utatuzi juu ya tatizo hakuna sababu ya kuwa wastani. 0:04:09.042,0:04:14.088 Baadhi ya matatizo makubwa sana duniani katika hali halisi yanahitaji utatuzi madhubuti/mkubwa 0:04:14.088,0:04:21.079 ambao katika hali halisi ni utatuzi mdogomdogo unaotekelezwa mara maelfu na maelfu. 0:04:21.079,0:04:24.088 Hatua ya 5, fikiri kama mtoto. 0:04:24.088,0:04:31.028 Inakinzana kidogo kwamba kufikiri makubwa na kufikiri kama mtoto vinaenda pamoja, lakini inakuwa hivyo. 0:04:31.028,0:04:38.098 Inabidi ufikiri kama mtoto ili kupata utatuzi ulio wazi juu ya tatizo kubwa ambalo watu wamelishindwa. 0:04:38.098,0:04:43.033 Hatua ya 6, angalia na fanya kilicho wazi. 0:04:43.033,0:04:48.020 Kama hatuwezi kuona upofu wetu ni vipi tutaona na kufanya kilicho wazi? 0:04:48.020,0:04:53.002 Kujiweka katika tatizo kunasaidia. 0:04:53.002,0:04:58.066 Hatua ya 7, kama tayari kuna mtu amekwisha buni hauhitajiki kufanya hivyo. 0:04:58.066,0:05:05.005 Ni rahisi siku hizi kufuatilia utatuzi ambao tayari watu wameshautoa. 0:05:05.005,0:05:15.063 Hatua ya 8, hakikisha mkabala wako una matokeo chanya yanayopimika na yanayoweza kukuzwa/kuwekwa katika skeli. 0:05:15.063,0:05:21.072 Hatua ya 9, sanifu ukilenga bei fulani. 0:05:21.072,0:05:27.014 Kumudu bei kunatawala mchakato wa usanifu kwa wateja masikini. 0:05:27.014,0:05:31.001 Namba 10, fuata mipango ya kivitendo ya miaka 3. 0:05:31.001,0:05:36.038 Bila kujali kiwango cha nguvu na ubadilishaji wa dunia katika dira yako juu ya mambo ya mbele, 0:05:36.038,0:05:42.024 kama hautaweza kutafsiri katika mpango madhubuti ndani ya miaka mitatu ya mwanzo, 0:05:42.024,0:05:46.003 hautaweza kufikia lengo. 0:05:46.003,0:05:52.067 Hatua ya 11, endelea kujifunza toka kwa wateja wako. 0:05:52.067,0:05:58.079 Nilipoanzisha IDE niliamua kwamba nitahudumu angalau wateja 100 kwa mwaka 0:05:58.079,0:06:00.037 na nimefanya hivyo. 0:06:00.037,0:06:07.075 Mpaka sasa nimehoji zaidi ya familia masikini za wakulima 3000, 0:06:07.075,0:06:12.019 na nimetembea nao katika mashamba yao. 0:06:12.019,0:06:15.006 Waliponiambia kwamba wamewekeza 0:06:15.006,0:06:16.084 vipato vyao vipya toka kwenye treadle pump 0:06:16.084,0:06:19.080 kwenye elimu ya watoto wao, 0:06:19.080,0:06:22.010 tulisanifu taa ya umeme jua ya $12 0:06:22.010,0:06:26.012 ili watoto wao waweze kusoma usiku. 0:06:26.012,0:06:27.045 Waliposema wamewekeza 0:06:27.045,0:06:30.077 sehemu ya fedha zao toka kwenye mifumo ya umwagiliaji ya dripu 0:06:30.077,0:06:34.041 katika nyati wa maziwa ama katika idadi ya mbuzi, 0:06:34.041,0:06:37.090 tulijifunza kila kitu kilichohitajika juu ya ufugaji mdogo 0:06:37.090,0:06:44.089 na tukaanza kusaidia wakulima walio na miradi midogo ya ufugaji. 0:06:44.089,0:06:49.038 Namba 12, usiyumbishwe na yale yanayosemwa na watu wengine. 0:06:49.038,0:06:52.024 Katika kila kitu ambacho nimefanyia kazi 0:06:52.024,0:06:55.030 na kugeuka kuwa mafanikio makubwa, 0:06:55.030,0:07:00.058 Nimesikia watu wengi wakiniambia kwamba napoteza muda. 0:07:00.058,0:07:03.045 Milioni moja na nusu ya treadle pumps baadae, 0:07:03.045,0:07:10.035 tuna ekari mpya elfu 750 chini ya umwagiliaji. 0:07:10.035,0:07:14.089 Kama ningewasikiliza watu waliosema ni kupoteza muda, 0:07:14.089,0:07:17.045 tusingefika hapo. 0:07:17.045,0:07:20.068 Kama una nia ya kuwa sehemu ya kitu haswa, 0:07:20.068,0:07:25.058 tembelea watu katika mazingira yao halisi 0:07:25.058,0:07:30.018 na sikiliza wanachosema, 0:07:30.018,0:07:31.038 na muhimu sana, 0:07:31.038,0:07:34.041 kuwa na nia ya kujifunza mambo mapya, 0:07:34.041,0:07:36.073 hapo mkabala huu utakuwa kwa ajili yako. 0:07:36.073,0:07:39.099 Kama wewe na kundi lako mtaamua kwamba kitu bora mtakachofanya nia kutoa msaada wa fedha, 0:07:39.099,0:07:43.076 hakikisha unachagua asasi zilizo na matokeo yanayopimika, 0:07:43.076,0:07:47.035 kama asasi za umasikini zinazoongeza kipato 0:07:47.035,0:08:25.073 cha watu wanaoishi kwa chini ya dola moja kwa siku.