Hujambo, Jina langu ni Suzan Song,
Mwelekezi wa Kitengo cha Tiba na Taaluma ya Ugonjwa wa Akili kwa Watoto, Vijana na Familia
cha Chuo Kikuu cha George Washington,
na Mshauri wa Kulinda Ubinadamu
kwa waathiriwa wa uhamishaji
wa lazima kote duniani na nchini.
Kumekuwa na ongezeko la kipekee
la idadi ya wakimbizi kote ulimwenguni,
wakiwemo wakimbizi, watafuta
makao, wahamiaji wasio halali
na watoto walio pweke.
Kote ulimwenguni, zaidi ya watu milioni 65
kwa sasa ni wakimbizi kutokana
na vita, mateso au mgogoro wa kivita.
Kufikia mwanzo mwa 2018, takribani watoto milioni 31 kote ulimwenguni
walifanywa wakimbizi kutokana na vurugu na migogoro.
Iwapo mitindo hii ya sasa itaendelea,
mtu mmoja kati ya watu mia moja
atakuwa mkimbizi hivi karibuni.
Kwa bahati mbaya, wakimbizi na
waathiriwa wengi wa uhamaji wa lazima
hawapokei huduma
inayohitajika ya afya ya akili.
kutokana na umakini wa huduma,
ukosefu wa kufikia huduma ya kitaalamu,
na shutuma dhidi ya matatizo ya akili.
Wakimbizi ni wale ambao
wametoroka katika nchi zao halisi
kutokana na wasiwasi wa
mateso yaliyopangwa
yanayolingana na mbari, dini,
uraia, maoni ya kisiasa
au uanachama katika
kikundi fulani cha jumuiya.
Ingawa wakimbizi huomba
ulinzi wakiwa ughaibuni
na wanapewa ruhusa ya kuingia Marekani,
Watu wanaotafuta
makao pia wana hofu ya mateso.
Lakini wanatafuta ulinzi wakiwa
ndani ya Marekani.
Wakimbizi na watu wengine
walioathiriwa na mzozo
waliripotiwa kuwa na
asilimia 15 hadi 30 ya
PTSD na mafadhaiko,
ikilinganishwa na asilimia 3.5 ya PTSD
miongoni mwa wasio wakimbizi.
Mambo thabiti
yanayoashiria afya mbovu ya akili
ni kupitia mateso na matukio
mengi yanayosababisha kiwewe.
Lakini mateso, kutenganishwa na familia, michakato ya kuchosha ya mahali pa hifadhi,
kutengwa na hali ngumu katika nchi unakoishi
zote huongeza ubaya wa afya ya akili.
Mazingira baada ya uhamiaji, hasa kipindi kirefu cha kuzuiliwa,
hali isiyo salama ya uhamiaji,
ufikiaji mbovu wa huduma
na vikwazo vya kazi na elimu
vinaweza kudhoofisha zaidi afya ya akili.
Haya hayatoi upeo kamili wa matatizo ya hisia
yanayokumbwa na watu walioathiriwa na mgogoro
ikiwa ni pamoja na huzuni isioelezeka, kiwewe kigumu,
kukata tamaa, kutengwa, hasira, na kutoamini.