Hujambo, Jina langu ni Suzan Song,
Mwelekezi wa Kitengo cha Tiba na Taaluma ya Ugonjwa wa Akili kwa Watoto, Vijana na Familia
cha Chuo Kikuu cha George Washington,
na Mshauri wa Kulinda Ubinadamu
kwa waathiriwa wa uhamishaji
wa lazima kote duniani na nchini.
Kumekuwa na ongezeko la kipekee
la idadi ya wakimbizi kote ulimwenguni,
wakiwemo wakimbizi, watafuta
makao, wahamiaji wasio halali
na watoto walio pweke.
Kote ulimwenguni, zaidi ya watu milioni 65
kwa sasa ni wakimbizi kutokana
na vita, mateso au mgogoro wa kivita.
Kufikia mwanzo mwa 2018, takribani watoto milioni 31 kote ulimwenguni
walifanywa wakimbizi kutokana na vurugu na migogoro.
Iwapo mitindo hii ya sasa itaendelea,
mtu mmoja kati ya watu mia moja
atakuwa mkimbizi hivi karibuni.
Kwa bahati mbaya, wakimbizi na
waathiriwa wengi wa uhamaji wa lazima
hawapokei huduma
inayohitajika ya afya ya akili.
kutokana na umakini wa huduma,
ukosefu wa kufikia huduma ya kitaalamu,
na shutuma dhidi ya matatizo ya akili.