Hujambo, Jina langu ni Suzan Song, Mwelekezi wa Idara cha Taaluma ya Ugonjwa wa Akili kwa Watoto, Vijana na Familia ya Chuo Kikuu cha George Washington, na Mshauri wa Kulinda Ubinadamu kwa waathiriwa wa uhamishaji wa lazima kote duniani na nchini. Kumekuwa na ongezeko la kipekee la idadi ya wakimbizi kote ulimwenguni, wakiwemo wakimbizi, watafuta makao, wahamiaji wasio halali na watoto walio pweke. Kote ulimwenguni, zaidi ya watu milioni 65 kwa sasa ni wakimbizi kutokana na vita, mateso au mgogoro wa kivita. Kufikia mwanzo mwa 2018, takribani watoto milioni 31 kote ulimwenguni walifanywa wakimbizi kutokana na vurugu na migogoro. Iwapo mitindo hii ya sasa itaendelea, mtu mmoja kati ya watu mia moja atakuwa mkimbizi hivi karibuni. Kwa bahati mbaya, wakimbizi na waathiriwa wengi wa uhamaji wa lazima hawapokei huduma inayohitajika ya afya ya akili. kutokana na usiri wa huduma, ukosefu wa kufikia huduma ya kitaalamu, na shutuma dhidi ya matatizo ya akili. Wakimbizi ni wale ambao wametoroka katika nchi zao halisi kutokana na wasiwasi wa mateso yaliyokithiri yanayolingana na mbari, dini, uraia, maoni ya kisiasa au uanachama katika kikundi fulani cha jumuiya. Ingawa wakimbizi huomba ulinzi wakiwa ughaibuni na wanapewa ruhusa ya kuingia Marekani, Watu wanaotafuta makao pia wana hofu ya mateso. Lakini wanatafuta ulinzi wakiwa ndani ya Marekani. Wakimbizi na watu wengine walioathiriwa na mzozo waliripotiwa kuwa na asilimia 15 hadi 30 ya PTSD na mafadhaiko, ikilinganishwa na asilimia 3.5 ya PTSD miongoni mwa wasio wakimbizi. Mambo thabiti yanayoashiria afya mbovu ya akili ni kupitia mateso na matukio mengi yanayosababisha kiwewe. Lakini mateso, kutenganishwa na familia, michakato ya kuchosha ya kupata makao, kutengwa na hali ngumu katika nchi mpya zote huongeza ubaya wa afya ya akili. Mazingira baada ya kuhama, hasa kipindi kirefu cha kuzuiliwa, hali isiyo salama ya uhamiaji, ufikiaji mbovu wa huduma na vikwazo vya kazi na elimu vinaweza kudhoofisha zaidi afya ya akili. Haya hayatoi upeo kamili wa matatizo ya hisia yanayokumbwa na watu wengi walioathiriwa na mgogoro ikiwa ni pamoja na huzuni isioelezeka, kiwewe kigumu, kukata tamaa, kutengwa, hasira, na kutoamini. Watu wengi wanakumbana na hatua za kawaida kwa matukio yasiyo ya kawaida kabisa. Baada ya muda, wakimbizi wengi huonyesha dalili chache au hawaonyeshi kabisa. Idadi ndogo huonyesha mtindo wa kupona polepole na idadi ndogo ingine huendelea kutatizika. Kwa hivyo tunahitaji kutathmini tofauti kati ya hali za tukio za dhiki na hali dhahiri za ugonjwa wa akili kwa wakimbizi. Tunafanya hili kwa kulenga kushirikisha hali za awali za kiwewe, mambo ya kila siku ya kusababisha mzongo, na mifumo mikuu ya ushirikiano wa kijamii ambayo mtu anahusika. Wataalamu wa akili wanaweza kusaidia watu hawa kupitia shughuli za kliniki zinazofaa kwa wakimbizi na wanaotafuta makao. Kwa kiwango cha sera kwa kufanya tathmini za makao na kwa kiwango cha utetezi kwa kuhimiza usawa wa kufikia, uwezo wa huduma kuwahifadhi wakimbizi na watu waliohamishwa kwa lazima, na kwa kushirikiana na wanachama wa jumuiya ya masomo mbalimbali kama vile mawakili, walimu na watengenezaji wa sera kutoa mfumo salama ambao wakimbizi na walionusurika kuhamishwa lazima wanaweza kutegemea.