1 00:00:03,629 --> 00:00:05,273 Hujambo, Jina langu ni Suzan Song, 2 00:00:05,273 --> 00:00:09,095 Mwelekezi wa Idara cha Taaluma ya Ugonjwa wa Akili kwa Watoto, Vijana na Familia 3 00:00:09,115 --> 00:00:10,839 ya Chuo Kikuu cha George Washington, 4 00:00:10,849 --> 00:00:12,330 na Mshauri wa Kulinda Ubinadamu 5 00:00:12,330 --> 00:00:15,431 kwa waathiriwa wa uhamishaji wa lazima kote duniani na nchini. 6 00:00:15,431 --> 00:00:17,112 Kumekuwa na ongezeko la kipekee 7 00:00:17,112 --> 00:00:19,192 la idadi ya wakimbizi kote ulimwenguni, 8 00:00:19,402 --> 00:00:22,963 wakiwemo wakimbizi, watafuta makao, wahamiaji wasio halali 9 00:00:23,226 --> 00:00:24,738 na watoto walio pweke. 10 00:00:25,339 --> 00:00:28,074 Kote ulimwenguni, zaidi ya watu milioni 65 11 00:00:28,074 --> 00:00:31,757 kwa sasa ni wakimbizi kutokana na vita, mateso au mgogoro wa kivita. 12 00:00:32,059 --> 00:00:35,653 Kufikia mwanzo mwa 2018, takribani watoto milioni 31 kote ulimwenguni 13 00:00:35,733 --> 00:00:38,207 walifanywa wakimbizi kutokana na vurugu na migogoro. 14 00:00:38,207 --> 00:00:39,974 Iwapo mitindo hii ya sasa itaendelea, 15 00:00:40,014 --> 00:00:43,010 mtu mmoja kati ya watu mia moja atakuwa mkimbizi hivi karibuni. 16 00:00:43,010 --> 00:00:46,328 Kwa bahati mbaya, wakimbizi na waathiriwa wengi wa uhamaji wa lazima 17 00:00:46,328 --> 00:00:48,614 hawapokei huduma inayohitajika ya afya ya akili. 18 00:00:48,687 --> 00:00:52,138 kutokana na usiri wa huduma, ukosefu wa kufikia huduma ya kitaalamu, 19 00:00:52,547 --> 00:00:54,477 na shutuma dhidi ya matatizo ya akili. 20 00:00:54,740 --> 00:00:57,410 Wakimbizi ni wale ambao wametoroka katika nchi zao halisi 21 00:00:57,410 --> 00:00:59,503 kutokana na wasiwasi wa mateso yaliyokithiri 22 00:00:59,503 --> 00:01:03,310 yanayolingana na mbari, dini, uraia, maoni ya kisiasa 23 00:01:03,310 --> 00:01:05,572 au uanachama katika kikundi fulani cha jumuiya. 24 00:01:05,748 --> 00:01:08,437 Ingawa wakimbizi huomba ulinzi wakiwa ughaibuni 25 00:01:08,437 --> 00:01:10,557 na wanapewa ruhusa ya kuingia Marekani, 26 00:01:10,759 --> 00:01:13,972 Watu wanaotafuta makao pia wana hofu ya mateso. 27 00:01:14,319 --> 00:01:16,837 Lakini wanatafuta ulinzi wakiwa ndani ya Marekani. 28 00:01:17,005 --> 00:01:19,301 Wakimbizi na watu wengine walioathiriwa na mzozo 29 00:01:19,301 --> 00:01:22,001 waliripotiwa kuwa na asilimia 15 hadi 30 ya 30 00:01:22,001 --> 00:01:23,335 PTSD na mafadhaiko, 31 00:01:23,732 --> 00:01:28,897 ikilinganishwa na asilimia 3.5 ya PTSD miongoni mwa wasio wakimbizi. 32 00:01:29,160 --> 00:01:31,398 Mambo thabiti yanayoashiria afya mbovu ya akili 33 00:01:31,398 --> 00:01:34,588 ni kupitia mateso na matukio mengi yanayosababisha kiwewe. 34 00:01:34,588 --> 00:01:38,586 Lakini mateso, kutenganishwa na familia, michakato ya kuchosha ya kupata makao, 35 00:01:38,756 --> 00:01:41,356 kutengwa na hali ngumu katika nchi mpya 36 00:01:41,466 --> 00:01:43,277 zote huongeza ubaya wa afya ya akili. 37 00:01:43,491 --> 00:01:46,516 Mazingira baada ya kuhama, hasa kipindi kirefu cha kuzuiliwa, 38 00:01:46,643 --> 00:01:48,523 hali isiyo salama ya uhamiaji, 39 00:01:48,860 --> 00:01:52,712 ufikiaji mbovu wa huduma na vikwazo vya kazi na elimu 40 00:01:52,772 --> 00:01:54,736 vinaweza kudhoofisha zaidi afya ya akili. 41 00:01:54,736 --> 00:01:57,533 Haya hayatoi upeo kamili wa matatizo ya hisia 42 00:01:57,533 --> 00:01:59,960 yanayokumbwa na watu wengi walioathiriwa na mgogoro 43 00:01:59,960 --> 00:02:02,944 ikiwa ni pamoja na huzuni isioelezeka, kiwewe kigumu, 44 00:02:03,232 --> 00:02:07,007 kukata tamaa, kutengwa, hasira, na kutoamini. 45 00:02:07,173 --> 00:02:09,750 Watu wengi wanakumbana na hatua za kawaida 46 00:02:09,875 --> 00:02:11,900 kwa matukio yasiyo ya kawaida kabisa. 47 00:02:11,910 --> 00:02:15,580 Baada ya muda, wakimbizi wengi huonyesha dalili chache au hawaonyeshi kabisa. 48 00:02:15,592 --> 00:02:18,056 Idadi ndogo huonyesha mtindo wa kupona polepole 49 00:02:18,350 --> 00:02:20,400 na idadi ndogo ingine huendelea kutatizika. 50 00:02:20,954 --> 00:02:24,714 Kwa hivyo tunahitaji kutathmini tofauti kati ya hali za tukio za dhiki 51 00:02:24,863 --> 00:02:27,243 na hali dhahiri za ugonjwa wa akili kwa wakimbizi. 52 00:02:27,350 --> 00:02:30,449 Tunafanya hili kwa kulenga kushirikisha 53 00:02:30,449 --> 00:02:32,318 hali za awali za kiwewe, 54 00:02:32,602 --> 00:02:34,086 mambo ya kila siku ya kusababisha mzongo, 55 00:02:34,336 --> 00:02:37,303 na mifumo mikuu ya ushirikiano wa kijamii ambayo mtu anahusika. 56 00:02:37,581 --> 00:02:39,561 Wataalamu wa akili wanaweza kusaidia watu hawa 57 00:02:39,561 --> 00:02:43,437 kupitia shughuli za kliniki zinazofaa kwa wakimbizi na wanaotafuta makao. 58 00:02:43,749 --> 00:02:46,715 Kwa kiwango cha sera kwa kufanya tathmini za makao 59 00:02:46,715 --> 00:02:50,185 na kwa kiwango cha utetezi kwa kuhimiza usawa wa kufikia, 60 00:02:50,425 --> 00:02:54,119 uwezo wa huduma kuwahifadhi wakimbizi na watu waliohamishwa kwa lazima, 61 00:02:54,119 --> 00:02:56,907 na kwa kushirikiana na wanachama wa jumuiya ya masomo mbalimbali 62 00:02:56,907 --> 00:02:59,478 kama vile mawakili, walimu na watengenezaji wa sera 63 00:02:59,660 --> 00:03:02,141 kutoa mfumo salama ambao wakimbizi 64 00:03:02,141 --> 00:03:04,539 na walionusurika kuhamishwa lazima wanaweza kutegemea.