Tunatakiwa kuziandika tena sehemu zifuatazo kama zenye asili ndogo ya shirika. Hivyo asili ndogo ya shirika ya sehemu hizi mbili itakuwa ni kigawe kidogo cha shirika cha hizi asili. Na thamani ya kufanya hivyo itakuwa kama unaweza kuzifanya hizi kuwa na asili zinazofanana, basi unaweza kuzijumlisha hizi sehemu mbili. Na tutaiona hii kwenye video nyingine. Lakini kwanza, tutafute kigawe kidogo cha shirika. Nitaiandika kwa sababu wakati mwingine KDS inaweza maanisha kitu kingine. Hivyo asili ndogo ya shirika ya sehemu hizi itakuwa kitu kile kile kama kigawe kidogo cha shirika cha hizi asili mbili hapa. Kigawe cha kidogo cha shirika cha 8 na 6. Kuna njia nyingi za kutafuta kigawe cha shirika-- unaweza kuchukua vigawe vya 8 na 6 na kuangalia kigawe kidogo kabisa ni kipi. Tuanze na njia hii sasa. Hivyo vigawe vya 6 ni, 12, 18, 24, 30. Na tungeendelea kama bado tusingepata kigawo kidogo katika kundi hili . Hivi ni vigawe vya 8. Navyo ni 8, 16, 24, na inaonekana tumeshamaliza. Na tungeendelea mpaka 32, na kuendelea. Ila nimekwishapata kigawe ambacho ndio kigodo kabisa. Kuna vigawe vingine vya shirika kama --48 na 72, na tunaweza endelea kuongeza zaidi na zaidi. Ila hiki ndicho kigawe kidogo kabisa cha shirika, kigawe kidogo kabisa. Ni 24. Njia nyingine ya kutafuta kigawe kidogo cha shirika kama ukichukua vigawo tasa vya 6 na ukasema hivi ni 2 na 3. Hivyo kigawe kidogo kabisa kitakuwa 1, 2, na 1, 3 kwenye vigawo tasa ili viweze kugawanyika kwa 6. Na ungejiuliza, vigawe tasa vya 8 ni vipi? ni 2 mara 4, na vya 4 ni 2 mara 2. Hivyo ili viweze kugawanyika kwa 8, angalau uwe na 2 mbili kwenye vigawo tasa. Ili vigawanyike kwa 6, inabidi uwe na 2 mara 3. Halafu ili vigawanyike kwa 8, inabidi uwe na 2 mbili. Unatakliwa uwe na mbili uizidishe kwa yenyewe mara 3 naweza kusema hivyo. Haya tuna mbili ya kwanza hapa. Kisha tuna 2 nyingine na 2 nyingine. Hivyo sehemu hii hapa inagawanyika kwa 8. Na hii sehemu hapa inaifanya igawanyike kwa 6. Nikichukua 2 mara 2 mara 2 mara 3, itanipa jibu 24. Hivyo kigawe kidogo cha shirika cha 8 na 6, ambacho pia kina asili sawa cha hizi sehemu mbili kitakuwa 24. Tunachotaka kufanya ni kuziandika upya sehemu zifuatazo na 24 kama asili. Nitaanza na 2 juu ya 8. Na ninataka kuiandika kama kitu juu ya 24. Kupata asili iwe 24, inabidi kuizidisha kwa 3. 8 mara 3 ni 24. Na kama hatutaki kubadili thamani ya sehemu, tunazidisha asili na kiasi kwa namba ile ile. Sasa tuzidishe kiasi kwa 3 pia. 2 mara 3 ni 6. Hivyo 2/8 ni sawa na 6/24. Ili kuielewa vizuri, unaweza kusema, kama nina 2/8 na nikiizidisha mara 3 juu ya 3, itanipa 6/24. Na hizi ni sehemu sawa kwa sababu 3 juu ya 3 maana yake ni 1. Moja nzima.. Hivyo 2/8 ni 6/24, hebu tufanye hivi kwa 5/6. Hivyo 5 juu ya 6 ni sawa na kitu juu ya 24. Nitaifanya kwa kutumia rangi nyingine. Rangi ya bluu. Kitu fulani juu ya 24. Kupata asili toka kwenye 6 mpaka 24, tunazidisha kwa 4. Hivyo kama hatutaki kubadili thamani ya 5/6, tunazidisha kiasi na asili kuwa namba ile ile.. Hebu tuzidishe kiasi mara 4. 5 mara 4 ni 20. 5/6 ni sawa na 20/24. Tumemaliza. Tumeandika 2/8 kama 6/24 na tumeandika 5/6 kama 20/24. Kama tukitaka kuzijumlisha, tunajumlisha 6/24 na 20/24. Nitaishia hapa kwa sababu hatujaambiwa kufanya hivyo.