WEBVTT 00:00:00.901 --> 00:00:04.832 Masoko ya Afrika yasiyo rasmi huwekewa kasumba kwa kuonekana 00:00:04.856 --> 00:00:06.703 vile yana kasheshe na goigoi. 00:00:07.234 --> 00:00:09.887 Ubaya wa kusikia neno "yasiyo rasmi" 00:00:09.911 --> 00:00:12.580 hutokana na jumuiya inayojiendesha ya misaada tuliyonayo, 00:00:12.604 --> 00:00:14.230 ambayo ina mitazamo hasi sana, 00:00:14.254 --> 00:00:18.763 na ilikuwa na madhara makubwa katika kuanguka kwa uchumi, 00:00:18.787 --> 00:00:24.273 kuongeza kirahisi -- au kupunguza -- asilimia 40 hadi 60 ya ukomo wa faida 00:00:24.297 --> 00:00:27.133 kwa masoko yasiyo rasmi pekee. 00:00:27.157 --> 00:00:31.459 Ikiwa moja ya jukumu la kuweka ramani ya mzunguko wa biashara zisizo rasmi, 00:00:31.483 --> 00:00:34.016 tumetengeneza machapisho kwa kina 00:00:34.040 --> 00:00:38.991 ya ripoti zote na tafiti kwenye biashara za mipakani katika ukanda wa Afrika Mashariki, 00:00:39.015 --> 00:00:40.826 tukirudi nyuma hadi miaka 20. 00:00:40.850 --> 00:00:45.184 Hii ilikuwa ni kwa ajili ya kutuandaa kwa ajili ya kazi ya kwenda kutathmini tatizo ni nini, 00:00:45.208 --> 00:00:49.370 kipi kilichokuwa kinarudisha nyuma biashara isiyo rasmi katika sekta isiyo rasmi. NOTE Paragraph 00:00:49.990 --> 00:00:53.494 Tulichogundua katika miaka 20 iliyopita ni kwamba, 00:00:53.518 --> 00:00:57.271 hakuna aliyeweza kutofautisha kati ya magendo -- 00:00:57.295 --> 00:01:01.740 ambayo ni sawa na upenyeshaji mali isiyo halali au iliyopigwa marufuku katika sekta isiyo rasmi -- 00:01:01.764 --> 00:01:04.104 na mali halali ambayo haikuwekwa katika kumbukumbu 00:01:04.128 --> 00:01:07.133 kama nyanya, machungwa, matunda. 00:01:07.697 --> 00:01:10.017 Uhalifu huu -- 00:01:10.041 --> 00:01:15.239 ambao kwa kiswahili unafahamika kama "biashara," ambao ni biashara, 00:01:15.263 --> 00:01:18.697 ukilinganisha na "magendo", ambayo upenyeshaji bidhaa usio halali -- 00:01:18.721 --> 00:01:22.242 uhalifu katika sekta isiyo rasmi, 00:01:22.266 --> 00:01:26.135 kwa Kiingereza, bila kutofautisha nyanja hizi, 00:01:26.159 --> 00:01:31.752 kwa urahisi inaweza kugharimu kila uchumi wa Afrika kati ya asilimia 60 hadi 80 ukiongezea 00:01:31.776 --> 00:01:34.544 katika ukuaji wa pato la taifa kwa mwaka, 00:01:34.568 --> 00:01:38.302 kwa sababu hatujambua injini 00:01:38.326 --> 00:01:40.900 inayofanya uchumi kuendelea. NOTE Paragraph 00:01:40.924 --> 00:01:44.401 Sekta isiyo rasmi inaongeza ajira mara nne katika kiasi 00:01:44.425 --> 00:01:46.367 cha uchumi ulio rasmi, 00:01:46.391 --> 00:01:48.948 au uchumi wa "kisasa", kama wengi wauitavyo. 00:01:48.972 --> 00:01:52.438 Hutoa nafasi za ajira na kuweza kujipatia kipato 00:01:52.462 --> 00:01:56.159 kwa wale wengi ambao hawana "ujuzi wa darasani" katika nyanja mbalimbali za taaluma. 00:01:56.183 --> 00:01:59.819 Lakini, je unaweza kutengeneza mashine ya kukaanga chipsi kutokana na gari bovu? NOTE Paragraph 00:02:00.403 --> 00:02:03.864 Kwa hiyo, hili, mabibi na mabwana, 00:02:03.888 --> 00:02:07.104 ni jambo ambalo linatakiwa kutambuliwa kwa shauku kubwa. 00:02:07.128 --> 00:02:11.386 Ambapo mtazamo wa sasa uliopo kuhusu sekta hii ni uhalifu, 00:02:11.410 --> 00:02:12.637 hiki ni kivuli, 00:02:12.661 --> 00:02:14.279 hii si halali, 00:02:14.303 --> 00:02:18.763 hakutakiwa na madhumuni ya kuunganisha mzunguko wa uchumi usio rasmi 00:02:18.787 --> 00:02:21.735 na ule ulio rasmi au hata ule wa kiulimwengu. NOTE Paragraph 00:02:22.968 --> 00:02:25.772 Nitawaeleza hadithi inayomuhusu Teresia, 00:02:25.796 --> 00:02:29.872 mfanyabiashara ambaye anapindua mitazamo yetu yote, 00:02:29.896 --> 00:02:33.246 anatufanya kuhoji kasumba zetu zote tulizokuwa nazo, 00:02:33.270 --> 00:02:36.176 ukihusisha na ripoti ya miaka 20 nyuma. 00:02:37.675 --> 00:02:43.164 Teresia anauza nguo chini ya mti katika mji unaoitwa Malaba, 00:02:43.188 --> 00:02:45.284 katika mpaka wa Uganda na Kenya. 00:02:45.876 --> 00:02:48.045 Unadhani ni rahisi sana, au sivyo? 00:02:48.810 --> 00:02:51.467 Tutakwenda ning'iniza nguo mpya kwenye matawi, 00:02:51.491 --> 00:02:54.423 tutatandika turubai, kisha kuketi chini, kusubiri wateja, 00:02:54.447 --> 00:02:55.792 na hivyo ndivyo inakuwa. 00:02:55.816 --> 00:02:59.201 Alikuwa ni mtu ambaye tuliona anarandana na yale yaliyomo katika ripoti, 00:02:59.225 --> 00:03:00.493 katika tafiti, 00:03:00.517 --> 00:03:04.294 alikuwa ni mama mjane anayefanya biashara, 00:03:04.318 --> 00:03:05.806 akilea watoto wake. NOTE Paragraph 00:03:07.092 --> 00:03:09.702 Ni kipi kilibadili udhanifu wetu? 00:03:09.726 --> 00:03:11.245 Kipi kilitushangaza? 00:03:11.269 --> 00:03:14.991 Kwanza, Teresia analipia kodi ya serikali ya soko la mkoa 00:03:15.015 --> 00:03:16.846 kila siku anayofanya biashara 00:03:16.870 --> 00:03:20.123 kutokana na kuweka biashara chini ya mti wake. 00:03:20.147 --> 00:03:22.198 Amekuwa akifanya hivi kwa miaka saba, 00:03:22.222 --> 00:03:24.144 na amekuwa akipewa risiti. 00:03:24.560 --> 00:03:26.037 Anatunza kumbumkumbu. 00:03:26.061 --> 00:03:29.228 Tunamuona asiye hafifu, 00:03:29.252 --> 00:03:30.599 masikini, 00:03:30.623 --> 00:03:36.439 mwanamke asiye na uwezo anayefanya biashara pembezoni mwa barabara -- hapana. 00:03:36.463 --> 00:03:40.562 Tunamuona mfanyabiashara ambaye anatunza kumbukumbu za mauzo kwa miaka; 00:03:40.586 --> 00:03:46.907 mtu ambaye amekuwa na mzunguko wote wa biashara za rejareja zitokazo Uganda 00:03:46.931 --> 00:03:49.246 hadi orodha ya uchukuaji; 00:03:49.270 --> 00:03:53.132 aliye na mkokoteni unaoleta bidhaa, 00:03:53.156 --> 00:03:56.072 au wakala wa mfumo wa fedha wa simu anayekuja kuchukua pesa taslimu 00:03:56.096 --> 00:03:57.524 kila mwisho wa jioni. 00:03:57.548 --> 00:04:01.956 Unaweza kisia ni kiasi gani Teresia hutumia, kwa wastani, 00:04:01.980 --> 00:04:04.577 kila mwezi katika uorodheshaji bidhaa -- 00:04:04.601 --> 00:04:07.274 shehena ya nguo mpya ambazo anapata kutoka Nairobi? 00:04:07.819 --> 00:04:10.009 Dola za Kimarekani elfu moja na mia tano. 00:04:10.525 --> 00:04:15.965 Ambayo ni takribani dola za Kimarekani 20,000 zilizowekezwa kwenye katika bidhaa za biashara na huduma 00:04:15.989 --> 00:04:17.544 kila mwaka. 00:04:17.568 --> 00:04:19.018 Huyu ni Teresia, 00:04:19.042 --> 00:04:20.439 asiyeonekana, 00:04:20.463 --> 00:04:21.743 aliyefichwa katikati. NOTE Paragraph 00:04:22.442 --> 00:04:26.535 Na huyu ni mtu wa ngazi ya kwanza ya wajasiriamali wadogo, 00:04:26.559 --> 00:04:30.650 biashara ndogo ndogo zinazopatikana katika masoko ya ya miji hii. 00:04:30.674 --> 00:04:35.558 Angalau katika mpaka mkubwa wa Malaba, yupo katika ngazi ya kwanza. 00:04:36.523 --> 00:04:39.159 Watu wa mbele zaidi wanathamini mlolongo huu 00:04:39.183 --> 00:04:42.228 na kwa rahisi wanafanya biashara tatu, 00:04:42.252 --> 00:04:47.343 wakiwekeza dola za Kimarekani kati ya 2500 hadi 3000 kila mwezi. 00:04:47.772 --> 00:04:51.752 Kwa hiyo tatizo lilikuja gundulika kwamba halikuwa uhalifu; 00:04:51.776 --> 00:04:56.421 huwezi kumtuhumu mtu ambaye unamtoza na kumpa risiti. 00:04:56.957 --> 00:05:02.347 Ni ukosefu wa kutambua ujuzi wa kazi zao. 00:05:03.048 --> 00:05:07.044 Mifumo ya kibenki haina njia ya kuwatambua 00:05:07.068 --> 00:05:08.556 kama wafanyabiashara ndogo ndogo. 00:05:08.580 --> 00:05:11.158 pasipo kukataa ukweli, unajua, 00:05:11.182 --> 00:05:13.390 mti wake hauna anuani. NOTE Paragraph 00:05:13.912 --> 00:05:16.238 Kwa hiyo amebanwa katikati. 00:05:16.262 --> 00:05:18.693 Anaangukia katika mpasuko wa dhana zetu. 00:05:18.717 --> 00:05:22.256 Unaijua ile mikopo midogo midogo ya kusaidia wanawake wa Kiafrika ambao ni wafanyabiashara? 00:05:22.646 --> 00:05:25.476 Watampa mkopo wa dola za Kimarekani 50 au 100. 00:05:25.500 --> 00:05:27.106 Atafanyia nini kiasi hiki? 00:05:27.130 --> 00:05:29.472 Anatumia mara 10 ya kiasi hicho kila mwezi 00:05:29.496 --> 00:05:31.098 katika uorodheshaji tu. 00:05:31.122 --> 00:05:33.409 hatuongelei huduma nyingine za ziada 00:05:33.433 --> 00:05:35.267 au mzunguko wote. 00:05:35.864 --> 00:05:39.452 Hawa ni wale ambao hawastahili kuwepo katika kasumba ya sera 00:05:39.476 --> 00:05:41.880 ya walio na ujuzi mdogo au wale duni, 00:05:41.904 --> 00:05:44.775 wala si mwajiriwa, ofisa anayelipwa mshahara 00:05:44.799 --> 00:05:46.660 au mtumishi aliye na pensheni 00:05:46.684 --> 00:05:50.056 ambapo ndipo watu wa kipato cha kati walipo. NOTE Paragraph 00:05:50.080 --> 00:05:54.632 Badala yake, tulichonacho hapa ni mifano ya viwanda vidogo na vya kati 00:05:54.656 --> 00:05:58.451 hizi ni mbegu zilizo na rutuba za biashara na viwanda 00:05:58.475 --> 00:06:00.418 ambazo zinafanya injini iendelee kutembea. 00:06:00.442 --> 00:06:02.177 Vinaleta chakula mezani. 00:06:02.201 --> 00:06:05.274 Hata hapa katika hotel hii, wasioonekana -- 00:06:05.298 --> 00:06:08.750 wachinjaji nyama, watengeneza mikate na watengeneza mishumaa -- 00:06:08.774 --> 00:06:11.167 wanatengeneza mashine ambazo zinatengeneza chipsi 00:06:11.191 --> 00:06:12.417 na wanatengeneza vitanda vyako, 00:06:12.441 --> 00:06:15.846 Hawa ni wanawake ambao hawaonekani wanaofanya biashara mipakani, 00:06:17.037 --> 00:06:19.406 pembezoni mwa barabara, 00:06:19.430 --> 00:06:22.348 hawaonekani kwa watu wanaokusanya taarifa. 00:06:22.704 --> 00:06:26.360 Na wanawekwa pamoja katika sekta kubwa isiyo rasmi 00:06:26.384 --> 00:06:31.457 ambayo haihangaiki kutofautisha watu wanaopenyesha bidhaa na wakwepa kodi 00:06:31.481 --> 00:06:34.089 na wale wanaofanya biashara za magendo, 00:06:34.113 --> 00:06:36.144 na wanawake wanaofanya bashara, 00:06:36.168 --> 00:06:40.313 na wale wanaoleta chakula mezani na kuwasomesha watoto zao hadi chuo kikuu NOTE Paragraph 00:06:40.337 --> 00:06:43.562 Kwa hiyo hili ndilo ninalouliza hapa. 00:06:43.586 --> 00:06:46.421 Hayo ndiyo tunatakiwa kuanza kufanya. 00:06:46.868 --> 00:06:51.477 Je tunaweza kuanza kwa kutambua ujuzi, kazi? 00:06:51.501 --> 00:06:56.125 Tunaweza kubadili uchumi wa sekta isiyo rasmi kwa kuanza na utambuzi huu 00:06:56.149 --> 00:07:00.830 na kisha kutengeneza milango ya wao kupita 00:07:00.854 --> 00:07:03.063 na kushirikiana na sekta iliyo rasmi, 00:07:03.087 --> 00:07:04.391 na ulimwengu, 00:07:04.415 --> 00:07:06.126 na mfumo mzima. NOTE Paragraph 00:07:06.150 --> 00:07:07.714 Asante, mabibi na mabwana. NOTE Paragraph 00:07:07.738 --> 00:07:11.459 (Makofi)